Kwanini Uganda na Egypt hawana mgao wa umeme na wanategemea maji kuzalisha umeme?

Nafikiri kama huu mgao wa umeme ni kweli unasababishwa na vyanzo vya maji kukauka na kupunguza uwezo wa uzalishaji umeme, inabidi kwenda kujifunza kwa wenzetu wanawezaje.

Uganda na Egypt ni nchi ambazo zinategemea kuzalisha umeme kwa hydropower.

Wao wanawezaje pamoja na mabadiliko ya tabia nchi kuendelea kuzalisha umeme wa kutosha.

Tukajifunze.
Shida kubwa katika nchi hii mawaziri kuingia mikataba bila kufika kwa wananchi yaani bungeni ili kujadiliwa kujua manufaa yake. Ndio maana akiingia kiongozi fulani anaona mwenzeka kaharibu alitakiwa kufanya hivi na hii yote ni kutaka kupata tenda mpya ambayo na yeye atapata maslahi

Hii ndio inasababisha miradi kuishia njiana huku pesa imetumika bila kutoa matoke chanya
 
Ziwa victoria huku tz halipo?
Ukame upo tangu Enzi za akina Ibrahimu , Isaka na Yakobo , upo tangu Enzi za nabii Eliya , Leo hii mtu anakuja na visababu et mabadriko ya tabia ya nchi aisee hii inchi ina viongozi vilaza Sana , Enzi za kikwete bwawa la mtera halikutumika Enzi za jiwe likatumika , few months baada ya kifo cha jiwe tunaambiwa Bwawa lipo out of range , mara crane ,mara mitambo yaan bla bla kibao, ili watu wafanye biashara huu uongozi Mungu anatakiwa auondoe madarakani mara moja pamoja na Wazir husika...sometime tuombeane Vifo tu
 
Hata sisi Mambo ya mgao tulishayamaliza,Ila Sasa ndo tunshangaa haka kajamaa kanatulazimisha mgao.
 
Hamna swali la Kijinga Isipokuwa muulizwaji anaweza kuona la Kijinga kwasababu ya ujinga wake.
Kwani ujinga ni shida mkuu, mbona hapa umetambua jibu wewe mwenyewe na ujinga ukakutoka hapohapo kuhusu swala hilo la mafuriko yanayoweza kusababishwa Kisumu kwa matendo yanayofanyika Uganda, hata kama Kisumu yenyewe haipo Uganda?

Wakati mwingine inafaa kujiongeza tu na kuona jinsi ulivyokuwa na ujinga hapo mwanzo ulipohoji jambo ambalo hukuwa na ufahamu nalo..
Sioni ni kwa vipi anayekutoa ujinga ndiye awe mjinga, labda kama unataka tu kuendeleza mambo mengine baada ya kufundishwa kitu ambacho hukukijua.
 
Kwani ujinga ni shida mkuu, mbona hapa umetambua jibu wewe mwenyewe na ujinga ukakutoka hapohapo kuhusu swala hilo la mafuriko yanayoweza kusababishwa Kisumu kwa matendo yanayofanyika Uganda, hata kama Kisumu yenyewe haipo Uganda?

Wakati mwingine inafaa kujiongeza tu na kuona jinsi ulivyokuwa na ujinga hapo mwanzo ulipohoji jambo ambalo hukuwa na ufahamu nalo..
Sioni ni kwa vipi anayekutoa ujinga ndiye awe mjinga, labda kama unataka tu kuendeleza mambo mengine baada ya kufundishwa kitu ambacho hukukijua.
Kukubali kuwa umekosea ni busara, Mkuu kubali tu kuwa Kisumu haipo Uganda Bali ipo Kenya, Hilo tu.
 
Hivi Nchi ilipofikia kuikomboa ni apatikane mtu aliye nje ya mfumo wa siasa za Tanzania aweke mifumo sawa
Huyo mtu ataingilia wapi na atatoboa vipi? Maana kama kupitia sanduku la kura hawezi kupewa chochote kinachoitwa ushindi😅!

Labda CCM yote iuawe asibakie mtu
 
Niwaambieni jambo,

Moja ya issue iliomtesa JPM ni mkataba wa Dowans na Symbion ambao JK alikuwa ameingia wakati wake,

Mkataba ile ulisainiwa kww vipengele vya kuifunga Tanesco isichomoke,
1: Mkataba ulikuwa inaitaka Tanesco itumie umeme wa Dowans/Symbion kwa Miaka yote,

2: Mkataba ulikuwa umeandika Tanesco watumie au wasitumie Umeme wa Dowans / Symbion wanapaswa kumlipa kila siku ,Kila Mwezi,maisha yote...

JPM alipouona akamteua Mkurugenzi DR Mwinuka Clean , Procurement clean man na wanasheria kadhaa ili wachambue waangalie weakness ilipo ili wauvunje,

Walipokaa walifanikiwa kupata vipengele vya kuwakamata Dowans/Symbion

1: Walipata Kuwa Dowans /Symbion hawakuwahi kulipa Kodi Miaka yote walikuwa wanadaiwa Trillion zaidi 40 ukwepaji kodi

2: Dowans/Symbion hawakuwa na Mitambo ya kuzalishia ,Kumbe walikuwa wanatumia Mitambo ya serikali kww Hiyo ikawa point Muhimu kuwa hawakuleta Mitambo mipya kama mkataba unavyo sema.

Matokeo yake:
JPM akawa amwakamata pabaya Dowans na Symbion ya JK Kikwete na Obama....
Wakaingia kwenye mazungumzo Symbion wakaona kwa vigezo hivyo hawachomoki

Bahati Mbaya Jpm akafariki wakiwa katikati kutaka kukimbia na kuachana kudai Serikali

Baadae Team Msoga ,Akiwemo Rostam na wenzake wakabuni mkakati wa namna ya kurudisha fedha ile
Wakajifanya kumzunguka Mama na kudanganya kuwa amteue Makamba,Mama bila kujua akamteua,

Makamba alipofika ili utekelezaji wa malipo Symbion ufanyinikiwe Makamba akaivunja Team yote ya Tanesco, akamtimua DR Mwinuka na team yake yote akamteua jamaa aliekuwepo DStv ambae hata calculation ya umeme hana uzoefu,

Akateua board ya Tanesco mpya wote wakiwemo wamiliki / CEO wa Dowans na Symbion na kubadilisha baadhi ya watalaamu ambao wamekutanishwa na wamiliki wa Dowans na Symbion Kule Dubai,JK Kikwete nadhani mmeona picha zile Kule Dubai wako pamoja linalojadiliwa hata Mama Samia hajui hata sisi wananchi hatujui

3: Lakini kubwa ni kuhakikisha Umeme wa Rufiji wanaletwa watu nyuma ya Pazia kununua Share na watajifanya wanaleta mitaji,watajifanya wanakuja kiwekeza lengo ni kuwa mradi Dowans na Symbion wapate cha kufanya

4: Mkakati mzima iliopo wametengeneza kumhujumu mama Samia 2025 watahakikisha hagombei na plan zao wanazopanga sasa hivi hatari lengo ili Makamba apate nafasi waendelee na Upigaji na utekelezaji

4 : Jambo mbaya mkakati mbaya uliopo ni Kuihujumu serikali ya Mama Samia

Nini kifanyike,

1: Mama Ondoa Makamba na team yote Nishati,

2: Mama asiruhusu uwekezaji wowote kwenye umeme ni bora tujenge Taratibu tutamaliza mradi umeme itarudi tena kawaida

3: Mama aangalie vizuri team yake ndani ya ofisi yake na Chama kww sababu JK anazidi kupandia mizizi

4: Mama asikubali kupangiwa na mtu yeyote na mama aache ushauri nje ya Idara ya Tiss ingawa na kwenye kunahitaji reshafle

5: Mama arudishe zile taskforce zilizowekwa na JPM kudhibiti maovu ikiwemo ukwepaji wa kodi na utoroshaji wa mizigo Bandarini

6: Kuna watu wanauza Risiti za EFD kariakoo imepelekea kushuka kwa mapato,
7: Mama Ahakikishe vituo vya Mizani iwe ni sehemu ya kukagulia Kodi na Risiti za EFD atabaini mengi.

8: Symbion /Dowans wapelekwe Mahakamani kwa kukwepa kodi na uhujumu Uchumi.

9: JK Kikwete apunguziwe safari za nje maana wananchi wanahoji why mkwere kila siku safari budget anatoa wapi?

10: Mama atengue mkuu wa Mkoa Dar essalaam halafu Ras wa Dar awe mkuu wa Mkoa

11: Maeneo ya wazo wapewe Machinga na Mama Ntilie kwa muda wakati huo yanajengwa Majengo kwa ajili ya wamachinga...zoezi hili ni kwa Dar es salaam Kariakoo na Posts,

Walioko mbezi waachwe waendelee

12: Mama aende kwenye Mafuta kuna hujuma huko nyingi sana ....

13: Mama aachwe afanye kazi kww uhuru bila kuingiliwa na JK maana hamtakii mema.

Umeandika kama kokolo, childish advises, hujui unaloandika, ni story za vijiweni
 
Shida kubwa katika nchi hii mawaziri kuingia mikataba bila kufika kwa wananchi yaani bungeni ili kujadiliwa kujua manufaa yake. Ndio maana akiingia kiongozi fulani anaona mwenzeka kaharibu alitakiwa kufanya hivi na hii yote ni kutaka kupata tenda mpya ambayo na yeye atapata maslahi

Hii ndio inasababisha miradi kuishia njiana huku pesa imetumika bila kutoa matoke chanya
Miongoni mwa kinachotakiwa kurekebishwa na kuwekwa sawa ni sheria za mikataba lazma iweke wazi kila mtu aweze ku access na kuusoma ama ziwekwe parameters za mikataba ya wawekezaji juu ya kile ambacho tunatakiwa kukipata kama taifa tokana na kila mkataba wa aina hio!

Kwanza muwekezaji asimiliki hio rasilimali by 100% nje ya kiwanda bali tukutane upande wa faida tu ikiwa ni 60/40kama hataki basi hamna waziri kusaini. Sio unamkabidhi mtu kitalu kinakuwa chake halafu mnaanza kulia lia anaipa serikali 5% na wizara iko kimya huku yeye anakunja 95% kumbe kuna waziri kwa baraka za raisi katengeneza 15% yake kimya kimya wanakula na raisi.

Mikataba iwe renewable and revised kila baada ya miaka 10 sio mtu anasinishwa mkataba wa milele! Ukiwa wa kipuuzi unatesa vizazi na vizazi! Kama hauna tija basi ku cancel iwepo.

Adhabu ya kunyongwa ama kupopolewa mawe hadharani na wananchi wenye hasira kali iwe kwa viongozi wote wala rushwa na mafisadi! Ikidhibitika tu mtu amefanya ucengerema iwe hakimu, speaker au raisi ni kipigo cha mbwa koko tu! Demokrasia iwepo sio kisiasa bali kwa utendaji. Bila kuwa na adhabu kali dhidi ya hawa washenzi wa CCM wataendelea kugombania madaraka na kujineemesha milele na milele huku wananchi tukipitia magumu miaka yote.
 
Kukubali kuwa umekosea ni busara, Mkuu kubali tu kuwa Kisumu haipo Uganda Bali ipo Kenya, Hilo tu.
Usitafute kunishangaza. Hivi nimeandika mahali popote kwamba Kisumu ipo Uganda, mbona unakuwa mtu usiyetaka kuelewa licha ya kukueleza kwa kurudia mara kadhaa!

Hivi jambo likifanyika Uganda, la kuzuia maji ya mto naili, tukio hilo haliwezi kusababisha mafuriko Kisumu, hata kama Kisumu haipo Uganda?

Hivi bado huelewi tu, wewe ni mtu mwenye akili za namna gani!
 
Usitafute kunishangaza. Hivi nimeandika mahali popote kwamba Kisumu ipo Uganda, mbona unakuwa mtu usiyetaka kuelewa licha ya kukueleza kwa kurudia mara kadhaa!

Hivi jambo likifanyika Uganda, la kuzuia maji ya mto naili, tukio hilo haliwezi kusababisha mafuriko Kisumu, hata kama Kisumu haipo Uganda?

Hivi bado huelewi tu, wewe ni mtu mwenye akili za namna gani!
Mimi ni great thinker,unapoleta hoja hapa jukwaani lazima ujipange.
 
Mkuu 'comte', naona umetoa viambatanisho kadhaa hapa kuonyesha kwamba Egypt na wao tatizo la umeme linawakabili kama ilivyo huku kwetu.
Lakini kwao naona wananchi hawataki mchezo kabisa, hadi kuiangusha serikali. Kwa hilo wao na sisi tupo tofauti sana.

Utofauti wao na sisi pia upo kwenye kiasi cha umeme wanachozalisha na wingi wa watu wanaofaidika na umeme huo.

Egypt ni nchi mojawapo yenye umeme wa bei ya cheee barani Afrika, kiasi kwamba gharama za uzalishaji bidhaa viwandani kama simenti/clinker ni nafuu zaidi na ndio maana hata wanawauzia wenzao kwenye soko lao la COMESA bidhaa nyingi, kwa vile uzalishaji wao ni 'competitive' kulinganisha na nchi zingine kwenye umoja huo.

Kwa hiyo, nadhanipamoja na matukio hayo uliyoyaweka hapa kama ushahidi mlinganisho wa Egypt na sisi haviendani sana. Sisi tupo chini sana.

Lakini inashangaza pia kuhusu hiyo "corruption" wanayokumbana nayo. Katika hili naona wao na sisi hatuchekani.
 
Back
Top Bottom