Kwanini udikteta umeshindwa kuleta maendeleo Africa?

Kwanini udikteta umeshindwa kuleta maendeleo Africa?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,554
Reaction score
110,101
Kwa nini Africa udikteta umeshindwa vibaya sana kuleta maendeleo endelevu na utulivu?

Screenshot_20251028_095406_X.jpg


20251028_095413.jpg

20251028_095911.jpg


20251028_095805.jpg


20251028_094314.jpg


20251028_095506.jpg

​
 
Domokrasia imeshindwa kuleta maendeleo Africa

Udikteta wa libya, Rwanda etc umesogeza maendeleo mbele

Udiktesa nsio tatizo
 
Maisha bora kwa raia.
Maisha bora ni nini?

Maisha bora ni vitu tofauti kwa watu tofauti.

Maisha bora ni kitu tofauti hata kwa ntu yuleyule kwa muda tofauti.

Tatizo la udikteta ni kwamba, unawanyima watu nafasi ya kusema, kuamua wanataka nini, na hivyo unawanyima nafasi ya kuamua maisha bora gani wanayataka.

Na mtu ukishanyimwa nafasi hii tu, hupati maisha bora. Kwa sababu chochote utakachopata unapewa kwa hisani ya dikteta, si kwa matakwa yako mwenyewe.

Dikteta anaweza kuona maisha bora ni kuwajengea watu maghorofa na barabara, wakati dikteta anawateka watu.

Wakati watu wanatekwa. Hawataki kutekwa. Ukiwaletea chochote unachokiita maendeleo bila kuwapa uhuru, kinakuwa hakina maana sana.

Basi kwa definition hii udikteta hauwezi kuleta maisha bora kwa raia.

Kwa sababu ili kuleta maisha bora kwa raia, ni lazima raia wawe na input.

Na udikteta hauruhusu raia kuwa na input utafanya mambo kwa maoni ya dikteta tu.
 
Nini kimeweza na maendeleo yapi ? Kama ni Miundombinu ni mangapi Gadafi alijenga na kuwezesha Mafuta kutumika kwa ajili ya nchi yake na sio Mabeberu ?!!!

Black Cat, White Cat it does not Matter, So long as it Catches Mice.....
 
Domokrasia imeshindwa kuleta maendeleo Africa

Udikteta wa libya, Rwanda etc umesogeza maendeleo mbele

Udiktesa nsio tatizo
Mfano wa nchi gani Africa ambayo imeweza kuwa na demokrasia kwa miaka 40 mfululizo bila kuwa na maendeleo??
 
Maisha bora ni nini?

Maisha bora ni vitu tofauti kwa watu tofauti.

Maisha bora ni kitu tofauti hata kwa ntu yuleyule kwa muda tofauti.

Tatizo la udikteta ni kwamba, unawanyima watu nafasi ya kusema, kuamua wanataka nini, na hivyo unawanyima nafasi ya kuamua maisha bora gani wanayataka.

Na mtu ukishanyimwa nafasi hii tu, hupati maisha bora. Kwa sababu chochote utakachopata unapewa kwa hisani ya dikteta, si kwa matakwa yako mwenyewe.

Dikteta anaweza kuona maisha bora ni kuwajengea watu maghorofa na barabara, wakati dikteta anawateka watu.

Wakati watu wanatekwa. Hawataki kutekwa. Ukiwaletea chochote unachokiita maendeleo bila kuwapa uhuru, kinakuwa hakina maana sana.

Basi kwa definition hii udikteta hauwezi kuleta maisha bora kwa raia.

Kwa sababu ili kuleta maisha bora kwa raia, ni lazima raia wawe na input.

Na udikteta hauruhusu raia kuwa na input utafanya mambo kwa maoni ya dikteta tu.
Mkuu wewe kwako maisha bora ni yapi ukihusihanisha na wajibu wa serikali?
 
Madikteta ya Afrika yangejiita tu wafalme/malkia ijulikane, maana hata chaguzi zikifanyika huwa ni bandia tu
 
Mkuu wewe kwako maisha bora ni yapi ukihusihanisha na wajibu wa serikali?

Maisha bora yanaanza na uhuru wa watu kuamua maisha bora kwao ni nini.

Na uhuru huu haupo katika mfumo wa udikteta.

Bila huu uhuru, maisha bora ya kulazimishana hayana ownership ya watu, hayana authenticity kwamba ni bora kweli au ni bora kwa kulazimishwa.

Kitu cha kwanza kabisa hapo umeniuliza mimi maisha bora kwangu ni yapi.

Hujamuuliza dikteta maisha bora ni yapi kwangu.

Hujajiuliza dikteta anataka maisha bora gani kwangu.

Kwa kuniuliza hivyo, umekubali kuwa sauti yangu ina umuhimu katika kuamua maisha bora ni yapi.

Na katika kukubali hilo, umekubali point yangu kwamba, kabla hatujafika kwenye maisha bora ni yapi, kitu cha muhimu kabisa ni watu kuwa na uhuru wa kuamua maisha bora wanayoyataka wao ni yapi.

This is a meta point. Si kwamba najaribu kukwepa kujibu swali lako la maisha bora ni yapi, nakwambia kabla ya kujibu hilo swali, kila mtu ana haki ya kujijibia mwenyewe, na udikteta unapora haki hiyo, na hivyo unaweka zoezi zima la kupata maisha bora mashakani. Kwa sababu dikteta ataleta mambo anavyojua yeye, si kwa kupata input ya wananchi.

Bila ya watu kuwa na sauti ya kuamua maisha bora ni yapi, dikteta anaweza kuwaletea watu kitu anachofikiri yeye ni maisha bora, wakati watu hawakitaki hicho kitu.

Ndoyo hizo habari za kulazimishana kwenda kwenye Vijiji vya Ujamaa kupata maisha bora, wakati watu hawataki kuhama kuacha makaburi ya babu na bibi zao.

Kuna balozi mmoja wa Marekani alikwenda Pemba. Kwenye hivi visiwa vidogo vinavyozunguka kisiwa cha Pemba. Balozi yule alikipenda sana kile kisiwa. Akawauliza watu wa pale, hapa pazuri sana, mngependa mradi gani wa maendeleo niwasaidie? Mimi naona hapa mngepata daraja la kuwaunganisha na kisiwa kikubwa cha Pemba ingekuwa vizuri sana.

Wale watu wa kisiwani wakamwambia balozi chonde chonde usijenge daraja hapa. Ukijenga daraja ndo utakuwa umetumaliza. Ujue sisi ni CUF, tunaandamwa na Polisi kila mara. Na salama yetu huwa tunakimbilia huku kisiwani Polisi hawawezi kutufuata. Ukijenga daraja maana yake Polisi wataweza kutufuata na kutuua huku. Chonde chonde usijenge daraja.

Habari hii inatufundisha nini? Habari hii inatufundisha kuwa maendeleo yanahitaji mazungumzo na watu, yanahitaji watu wawe na input. Watu waamue wanataka nini. Jambo alilofanya yule balozi wa Marekani kuuliza lilikuwa muhimu sana. Kwa sababu kapata feedback ya watu, kapata input yao.

Angesema ajenge daraja tu, angeweza kutumia pesa nyingi kujenga kitu ambacho yeye aliona ni maendeleo, lakini wananchi hawakukitaka. Angeweza kutumia pesa nyingi kujenga daraja, halafu akashangaa kukuta daraja limevunjwa.

Na hapo ndipo udikteta unaposhindwa. Kwa sababu udikteta utataka kuweka mambo bila kuwapa watu nafasi ya kuamua wanataka nini.

Utajenga daraja sehemu ambayo wananchi hawataki daraja, labda wanataka maji.

Muda mchache baadaye utakuta daraja limevunjwa.
 
Libya, Sheli Sheli na Misri ni mifano ya nchi zilizofanya vizuri kimaendeleo chini ya "Udikteta." Hata Uganda kwa M7 wametupita kwa pato la mwananchi mmoja mmoja.
 
Back
Top Bottom