Kwanini Twiga awe nembo ya Tanzania?

Kwanini Twiga awe nembo ya Tanzania?

Nani kakwambia twiga ndo nembo ya Taifa?

Unajua hata nembo ya Tanzania ni ipi.
mnyama wa taifa.. kiswahili kigumu.. 'national animal'
au wewe unamaanisha nembo ya bibi na bwana(coat of arms)?
 
...kwani marekani ilichukua muda gani??..ivi si kuna hii nchi inatumia kuku
 
Anawakilisha upole,ukarimu na ustaharabu wetu. Ila mi ningependekeza waweke 'MBUZI' nadhani ndo ingetuelezea vizuri.
 
...kwani marekani ilichukua muda gani??..ivi si kuna hii nchi inatumia kuku
wenzetu vitu vingi vipo kwenye maandishi. Wanadai majadiliano ilichukua miaka 6. Wengine walitaka awekwe njiwa, wengine kunguru. Baadaye wengine wakasema kimaadili tai sio mzuri bora bata mzinga.. n.k. mwishoni wakaafiki TAI kwamba akiwa katika anga za juu anaweza kuona dhahabu iliyopo geita au gesi iliyopo mtwara hata kabla wenyeji hawajavitambua.
 
Anawakilisha upole,ukarimu na ustaharabu wetu. Ila mi ningependekeza waweke 'MBUZI' nadhani ndo ingetuelezea vizuri.
aaaaa.. mbuzi mwizi sana, akiona mahindi shambani hatulii mpaka akazitafune. Ila hata mbuzi poa tu, ananoga kwenye mchuzi
 
nadhani huyo kwa mwendo wake anaacha dhahabu zinachukuliwa
wenzetu vitu vingi vipo kwenye maandishi. Wanadai majadiliano ilichukua miaka 6. Wengine walitaka awekwe njiwa, wengine kunguru. Baadaye wengine wakasema kimaadili tai sio mzuri bora bata mzinga.. n.k. mwishoni wakaafiki TAI kwamba akiwa katika anga za juu anaweza kuona dhahabu iliyopo geita au gesi iliyopo mtwara hata kabla wenyeji hawajavitambua.
 
Kichwa cha uzi kimesemaje?
Hicho kichwa ni namna ya kumteka msomaji. Ungeandika mnyama wa nchi.. ingekaa kimazingira zaidi wakati hapa TWIGA anawakilisha kitu fulani katika taifa
 
Twiga yuko juu,kwanza ndo mnyama pekee tz ambae ameshapanda ndege
Kweli kabisa. Anaheshimika sana. na ndo maana alipopanda ndege ilileta mushkeli maana mnyama wa taifa ana taratibu zake maalum za kuwindwa. Nadhani kibali kinatoka kwa rais pekee.
 
nadhani huyo kwa mwendo wake anaacha dhahabu zinachukuliwa
Tena akifika mgodini anabaki anashangaa.. wakati tai anaparangana mara aruke na dhahabu...daah kweli twiga anafaa kuwakilisha wabongo.
 
Heshima kwenu wakuu.

Mataifa kadhaa duniani wamechagua baadhi wa wanyama kuwa nembo za nchi zao. Mfano Bald eagle (tai) ni nembo ya Marekani. Tai ni ndege anayepaa katika anga za juu sana kuliko ndege wote. Akiwa huko jicho lake linaweza kuona mbali hata mzoga wa sungura uliopo ardhini. Waamerika wanadai kwao tai anawakilisha nguvu, uhuru, akili na ujasiri wa kuona mbali.

View attachment 407552

Turudi hapa Tanzania. Mnyama wetu wa Taifa ni Twiga. (Giraffe). Neno giraffe limetokana na neno la kiarabu (xirefa) lenye maana ya anayetembea kwa maringo.

View attachment 407553

Je, kwanini wazee wetu waliamua kumchagua twiga?
Je, mchakato wa kuamua mnyama yupi atumike ulichukua miaka mingapi?
Je, kulikuwa na wanyama wengine au ndege waliopendekezwa zaidi ya twiga?
Je, watoto na wajukuu wetu wakitaka kujua habari kama hizi watazipata wapi? watazisoma wapi?

Nawasilisha.
ukija kwenye masuala ya elimu za wanyama,Twiga ni mnyama mwenye sifa nyingi zilizoivutia nchi yetu kumtumia kama kilinganishi katika masuala mbalimbali,hasa ya kidiplomasia,Twiga huwa ni mnyama mpole,mtulivu,pia huwa ana tabia yakuangalia usalama wake na wa wanyama wengine,ndio maana porini ni kawaida kumuona kumuona twiga akiambatanana wanyama wengine kwa ajili ya usalama,ni mnyama ambae anaona mbali sana,hivyo nirahisi kum spot adui hata akiwa mbali,adui ambaye hawez kuonekanana mnyama wa kawaida kama swala nk,SASA ukija hali halisi Twiga ni mnyama anaewakilisha Tanzania,nchi ambayo ina amani,upole nakujali mataifa mengine,tulipo pata uhuru hatukuridhika tuu sisikua huru,tuliwasaidia pia nchi zingine kujikomboa,ndio maana mpaka leo maraisi wastaafu karibia wote,niwasuluhishiwa migogoro yanchi mbalimbali,Pia tunatumia picha ya twiga kama kuitangaza Tanzania kiutalii kama Australia wanavyotumia kangaroo
 
Back
Top Bottom