Heshima kwenu wakuu.
Mataifa kadhaa duniani wamechagua baadhi wa wanyama kuwa nembo za nchi zao. Mfano Bald eagle (tai) ni nembo ya Marekani. Tai ni ndege anayepaa katika anga za juu sana kuliko ndege wote. Akiwa huko jicho lake linaweza kuona mbali hata mzoga wa sungura uliopo ardhini. Waamerika wanadai kwao tai anawakilisha nguvu, uhuru, akili na ujasiri wa kuona mbali.
Turudi hapa Tanzania. Mnyama wetu wa Taifa ni Twiga. (Giraffe). Neno giraffe limetokana na neno la kiarabu (xirefa) lenye maana ya anayetembea kwa maringo.
Je, kwanini wazee wetu waliamua kumchagua twiga?
Je, mchakato wa kuamua mnyama yupi atumike ulichukua miaka mingapi?
Je, kulikuwa na wanyama wengine au ndege waliopendekezwa zaidi ya twiga?
Je, watoto na wajukuu wetu wakitaka kujua habari kama hizi watazipata wapi? watazisoma wapi?
Nawasilisha.