Kwanini Tundu Lissu na CHADEMA wanachukia maendeleo Kanda ya Ziwa?

Endeleeni tu na propaganda zenu uchwara!! Mnafikiri watanzania ni wajinga sana!!!

Hakuna mahala Lissu amepinga maendeleo ya kanda ya ziwa. Hoja ya Lissu ni upendeleo kwa chato ambako ni kijiji cha magufuli. Lissu amesema wazi Kwa nini Uwanja wa kimataifa haukujengwa Geita au Bukombe ukajengwa kijijini kwa Raisi Chato??? Sasa Geita na Bukombe ni wapi we kilaza wa Lumumba?????

Tunajua mnajaribu kuleta propaganda kupotosha ila tunawaambia tu mmeshafeli kabla hamjaanza
 
Watu hawali Madaraja, hivi CCM mmeshindwa kabisa namna ya kufikiria nje ya Madaraja na Mabarabara!?
Ndo maana chadema mnasema badala ya kujenga daraja la busisi watumie hizo fedha kuwanunulia hao watu chai na maandazi wale Hadi waache.
 
Sasa meli ziwa Victoria mbona mnachukia?
..Unakumbuka Ofisi ya Spika iliyojengwa Urambo?

..CCM walikuwa wakiitetea kama wanavyotetea uwanja wa ndege wa Chato.

..Chato International Airport haitumiki sasa hivi, ni afadhali fedha hizo zingeelekezwa kwenye miradi inayowagusa wananchi.
 
Unapomwacha mwanao avae suruali iliyotoboka huku unanunua iPhone ya M.2 huo ni upumbavu.
Tundu Lissu anapinga ule ujenzi wa Chato Airstrip uliogharimu mabilioni bila sababu maalumu
Kwani mmezuiliwa akufanya kazi wehu nyie. Fanyeni kazi mpate pesa
 
Ndo maana chadema mnasema badala ya kujenga daraja la busisi watumie hizo fedha kuwanunulia hao watu chai na maandazi wale Hadi waache.

Ha haaaa ,Mkuu mbona unatulisha maneno !?.Ilisemwa lini na wapi hiyo ,yani Watu walishwe Maandazi hadi waache ?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…