Kwanini tunawachukulia poa watoto waliorithi utajiri toka kwa wazazi wao

Wivu, chuki, husda nk hakuna zaidi. Tunapambania vizazi vyetu lakini tukiona wenzetu wanafaidi toka kwa wazazi wao tunakunja.
 
Tatizo watu wakishaona mtu amezaliwa mahali flani ambapo kwa mtazamo wao wanaona ni pazuri, wanahisi labda kila kitu ni mserereko.. Hawaelewi kama kuna hustling behind the scenes wanazifanya ambazo wao wanaweza wasiweze kufanya au wakaogopa kufanya kwasababu ni ngumu mno
Asante sana.
Nakuunga mkono.
Kuendeleza mali ya urithi si jambo dogo.
Una uwezo wa kufuja mali hiyo ikachakaa na kupotea ndani ya muda mfupi.
Lakini ukiwa na maono utadumu nayo kwa muda mrefu na kuiongeza maradufu
 
Habari

Kumekuwa na kasumba ya kuwachukulia poa wale watoto ambao wamezaliwa kwenye familia za kitajiri, na kukuta kila kitu kisha kurithi utajiri au mali toka kwa wazazi wao, hasa sisi masikini ngozi nyeusi

Huwa nashindwa kuelewa kwanini inakuwa hivyo, wakati kila siku watu wanasisitiza kutafuta pesa kwa ajili ya kuwarithisha watoto, wajukuu pamoja na vizazi vingine vitakavyofuata ili wasije kuteseka

Lakini cha ajabu hao watoto wanaorithi hizo pesa au mali za wazazi wao hasa wale matajiri, kuna namna jamii hasa masikini inawachukulia, yani inawaona kama some spoiled and inexperienced brats tu

Kwamba we utatuambia nini hujui hustle za kitaa, mtu mwenyewe mtoto wa mama tu mara sijui geti kali mara wa kishua mboga saba, huna cha kutushauri hivyo huwezi kutuinspire kwa utajiri wa kurithi tu

Huwa sielewi ni kwamba tunawaonea wivu plus chuki na husda, sababu labda wazazi wetu walishindwa kutuachia mali au huwa ni njia ya kujifariji na umasikini wetu tu, kwanini huwa tunaona kama kuanzia kwenye umasikini na kuhustle ndio sifa

Je ni lazima kila mtu mafanikio yake yawe yametokea kwenye umasikini na kuhustle ndio awe na story to tell, kama ni hivyo sasa tunawasisitiza watu watafute utajiri kwa ajili ya vizazi vyao ili iweje, kama bado tuna hiyo mentality ya kwamba mtu aliyehustle from the scratch ndio legend

Na wengi tuna ile imani ya kwamba watoto wa kishua wakirithi utajiri toka kwa wazazi wao, huwa haudumu wanaishia kutapanya mali na kuingia kwenye umasikini, sababu walizoea kudekezwa na kupewa kila kitu but in reality that's not always the case

Tuchukulie mfano wa hapa kwetu watu wengi husema matajiri wa kweli ni Said Bakhresa, Reginald Mengi et al, ila Mo Dewji na ndugu zake wamerithi tu utajiri kwa baba yao na siyo self made, mind you hapa siongelei urithi baada ya mzazi kufa, bali utajiri ambao wamepewa waendeleze wakati wazazi wao bado wapo

Kwanza kabisa tunakosea kuwalinganisha hao wazee na Mo Dewji sababu siyo rika moja, pili speaking of kurithi hata Said Bakhresa ana watoto waliorithi utajiri wake, na ndio kwa asilimia kubwa wanasimamia na kuendesha biashara zake sasa hivi wakiongozwa na Yusuf Bakhresa

Na ukiangalia Mo Dewji na Yusuf Bakhresa ndio wako rika moja hivyo wanatakiwa walinganishwe wao, Mzee Said Bakhresa na hao kina Reginald Mengi wanatakiwa walinganishwe na baba yake Mo Dewji Mzee Gulam Dewji, ambaye naye ni self made kama hao wazee wenzie

Lakini bado hatutakiwi kuwachukulia poa kina Mo Dewji na Yusuf Bakhresa eti kisa tu utajiri wao wameurithi, nao wanatakiwa wapongezwe kwa kuuendeleza since the goal is to become rich haijalishi umefanyaje, ukizingatia kurithi utajiri wa mzazi si dhambi wala si kosa kisheria

Well mifano ni mingi ila nimewatolea hao sababu ndio maarufu, lakini wapo watoto wengi ambao wamerithi utajiri toka kwa wazazi wao na wakafanikiwa kuuendeleza vizuri tu bila kufilisika, na si kwamba eti kila mtoto anayeachiwa urithi wa mali basi zitamshinda kisa anaonekana ni mzembe

Na pia haijaandikwa kwamba kila mtoto ambaye hakuachiwa urithi basi akihustle kitaa ndio atakuwa tajiri, wengine huishia kuwa middle class na wengine huishia kuwa masikini kabisa, kuna watu wamehustle from the scratch ila mpaka wanazeeka wameishia kuwa na nyumba, gari, duka Kariakoo au Makumbusho

Na wakati huo huo kuna watu wamezaliwa wamekuta kila kitu kwao, wakarithi utajiri wa wazazi wao na kufanikiwa kuendeleza na mpaka wanazeeka wanamiliki mijumba, magari, makampuni, viwanda et al

So mimi sioni mantiki ya kuwachukulia poa watoto waliozaliwa kwenye utajiri, ikiwa malengo ya watu wengi ni kutafuta utajiri kwa ajili ya watoto wao na vizazi vyao, hakuna na hakutawahi kuwa na tuzo ya kuzaliwa kwenye umasikini na kuhustle from the scratch na wala siyo sifa
Ulaani umasikini mdau
 
Back
Top Bottom