Kwanini Trafiki akisimamisha Daladala, anayeshuka ni Kondakta?

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,372
8,108
Wakuu, kuna jambo nataka kujifunza leo, hivi ni utaratibu kwenye Madaladala (Hasa ya Dar) kwamba Trafiki akipiga mkono anayetakiwa kwenda kuongea naye ni Kondakta?

Kwa ninavyofahamu ukisamishwa na Trafiki hautakiwi kushuka kwenye gari mpaka Trafiki aje akague anachokitaka bila wahusika wa gari kushuka, kama itatokea shida ndio unatakiwa kushuka kwaajili ya maelezo.

Sasa kwenye Daladala Kondakta anashuka kwenda mbele ya Gari au nyuma kufanya nini? Wasikilize wazee wa minyama hapa.

Wakuu, kuna jambo nataka kujifunza leo, hivi ni utaratibu kwenye Madaladala (Hasa ya Dar) kwamba Trafiki akipiga mkono anayetakiwa kwenda kuongea naye ni Kondakta? Kwa ninavyofahamu ukisamishwa na Trafiki hautakiwi kushuka kwenye gari mpaka Trafiki aje akague anachokitaka bila wahusika wa gari kushuka, kama itatokea shida ndio unatakiwa kushuka kwaajili ya maelezo.

Sasa kwenye Daladala Kondakta anashuka kwenda mbele ya Gari au nyuma kufanya nini? Wasikilize wazee wa minyama hapa.
View attachment 2641029
Konda ndo mmiliki kisha kamuajiri.dereva😀
 
Kondakta si ndiye anaenda kuhonga pesa.

Jeshi la polisi Tanzania ni "organised crime" kabisa.

Umafia tu. Hakuna siri.
 
Vehicle inspector ndio wanamuita traffic wakati traffic ndio chombo chenyewe. Kweli bongo nyoso

Hawa hawa ndio wale wa FLAMPENI badala ya FRYING PAN
Vehicle police ndio Nini, Ni Traffic Police ndio tinafupisha kumwita Traffic tu, tunafanya hivi kwenye vitu mbalimbali hakuna asiyejua neno traffic inamaana ya chombo umeamua kukaza fuvu tu
 
Gari ikisimama tuu konda chap na 2000 mkononi , ni kwenda kama anamsalimia ndo imeisha hyo , Kwa sku akidaka dalala 30 , hapo ni Kati ya 60000-100000 , hata mshahara hawazi....!! Hakuna gari ambayo haina makosa haipo , ukishusha Tu bandarini gari inakuwa na makosa 100
 
Vehicle police ndio Nini, Ni Traffic Police ndio tinafupisha kumwita Traffic tu, tunafanya hivi kwenye vitu mbalimbali hakuna asiyejua neno traffic inamaana ya chombo umeamua kukaza fuvu tu
Umekuwa race halafu hujaelewa. Soma upya, Kisha nionyeshe wapi nimeandika police kwenye comment yangu.

tinafupisha ndio nini kwanza we mmang'ati?
 
Back
Top Bottom