Getrude Mollel
JF-Expert Member
- Apr 26, 2022
- 308
- 424
Afrika imekuwa ikishuhudia misururu ya mapinduzi ya kijeshi tangu enzi za Vita Baridi hadi karne ya 21. Nchi nyingi zilikumbwa na hali hii kutokana na migawanyiko ya kisiasa, kikabila na kiuchumi.
Ghana ilipitia mapinduzi yake ya kwanza mwaka 1966, Nigeria ikashuhudia mapinduzi mara kwa mara kuanzia miaka ya 1960 hadi mwishoni mwa karne ya 20, na Uganda ikapinduliwa mwaka 1971 chini ya Idi Amin.
Katika miaka ya hivi karibuni, hali hiyo imejirudia katika mataifa ya Sahel kama Mali mwaka 2020, Guinea 2021 na Niger 2023. Sababu kuu katika visa hivi imekuwa ni uchumi dhaifu, ukosefu wa mshikamano wa kitaifa, ukosefu wa usawa katika rasilimali na mara nyingine kuingilia kati kwa mataifa ya nje.
Tanzania ni nchi ya pekee barani Afrika ambayo haijawahi kushuhudia mapinduzi ya kijeshi, jambo linaloibua swali la msingi: kwanini hali hii haiwezekani?
Kwanza, Tanzania imejengeka juu ya msingi wa mshikamano wa kitaifa ulioasisiwa na Mwalimu Julius Nyerere. Kupitia sera ya Ujamaa na lugha ya Kiswahili, Watanzania waliunganishwa kwa utambulisho wa pamoja. Tofauti na nchi nyingi za Afrika zilizoathirika na mapinduzi kwa sababu ya migawanyiko ya kikabila na kidini, Tanzania haina kabila linalotawala au kudharaulika zaidi ya jingine. Lugha ya Kiswahili imekuwa daraja la mshikamano na taifa limekua na utambulisho mmoja, hali inayopunguza uwezekano wa machafuko ya kisiasa yanayotokana na ukabila.
Sababu ya pili ni nafasi ya jeshi na uhusiano wake na siasa. Katika nchi nyingi za Afrika, mapinduzi ya kijeshi hutokea pale ambapo jeshi linajiona kama taasisi iliyotengwa na siasa, na hivyo kuona lina haki ya kuingilia. Tanzania ni tofauti. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limeunganishwa moja kwa moja na chama tawala CCM na serikali.
Ni jambo la kawaida kuona maafisa wa JWTZ wakiteuliwa kuwa wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya au hata mabalozi. Hii inamaanisha jeshi halina nafasi ya kuona linabaki pembeni au kutengwa, bali linajiona sehemu ya moja kwa moja ya mfumo wa kiserikali. Hali hii hupunguza uwezekano wa maafisa wa kijeshi kuunda mapinduzi kwa sababu wanajua wanashiriki katika utawala.
Kwa upande wa uchumi, imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza 'income inequality' miongoni mwa watu wake hali ambayo inafanya Tanzania kusiwe na machafuko au vurugu kama ilivyo Kenya. Kenya ni mfano wa nchi yenye tofauti kubwa ya kipato na migogoro ya ardhi. Ni takribani asilimia 20 tu ya ardhi nchini Kenya inafaa kwa kilimo, na sehemu hiyo inamilikiwa na wachache matajiri. Wengi wa wananchi hukosa nafasi ya uzalishaji, jambo linalosababisha maandamano na vurugu mara kwa mara. Vilevile, nchi kama Afrika Kusini ina tofauti kubwa za kipato kati ya wazungu wachache (minority) na wananchi wengi raia wa Afrika Kusini, jambo ambalo limekuwa chanzo cha migomo na ghasia.
Tanzania inatofautiana kwa sababu ardhi ni mali ya umma kwa mujibu wa sheria, na hata maskini wanaweza kumiliki kipande cha shamba cha kulima. Zaidi ya asilimia kubwa ya Watanzania wanalima, na huzalisha chakula kwa wingi ikilinganishwa na majirani.
Hali hii inafanya Tanzania isiwe tegemezi kwa uagizaji wa chakula kutoka nje, na vijana wengi wanapata fursa ya kushiriki katika kilimo, biashara na ufugaji. Hivyo, vijana wa Tanzania hawana hasira/ghahabu kubwa za kiuchumi zinazowasukuma wenzao katika nchi kama Kenya au Afrika Kusini kuingia mitaani kwa maandamano.
Kwa mfano, Kenya inalazimika kuagiza chakula kutoka nje kutokana na kilimo chao kuuza sana mazao ya biashara kuliko mazao ya chakula, hali inayosababisha wananchi kukosa chakula cha kutosha. Hali hii huleta migongano ya kijamii na maandamano makubwa ya kupinga gharama za maisha. Tanzania kinyume chake huzalisha mazao ya chakula kwa wingi, jambo linalohakikisha usalama wa chakula na kupunguza hatari ya vurugu.
Hata hivyo, Niger na Mali zilishuhudia mapinduzi kutokana na ukosefu wa fursa za kiuchumi na migawanyiko ya kikabila. Afrika Kusini mara kwa mara hushuhudia vurugu kutokana na ukosefu mkubwa wa usawa wa kipato. Kenya imekumbwa na maandamano ya gharama za maisha na sera za kodi.
Tanzania haina mchanganyiko huu wa migogoro, ardhi inamilikiwa na umma, chakula kinapatikana kwa wingi, vijana wana fursa za uzalishaji, na mshikamano wa kijamii umejengwa kwa Kiswahili na utamaduni wa mshikamano.
Kwa kuzingatia historia hii, Tanzania imeweza kujiepusha na misururu ya mapinduzi na machafuko ambayo yamekumba mataifa mengine ya Afrika.
Uongozi ulioimarisha mshikamano, jeshi lililounganishwa na serikali, sheria za ardhi zinazoweka usawa, na uchumi unaozalisha chakula na fursa vimejenga mazingira yasiyofaa kwa mapinduzi au maandamano makubwa.
Tanzania ni mfano wa kipekee barani Afrika kwamba mshikamano wa kijamii na usawa wa fursa unaweza kuzuia migawanyiko na kulinda uthabiti wa taifa.