Kwanini Tanzania haijavunja Uhusiano na Gadaffi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Tanzania haijavunja Uhusiano na Gadaffi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 19, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  Wakati wa Nyerere Tanzania haikuwa na utata katika masuala ya siasa za Kimataifa; tulitambua POLISARIO na PLO kama vyama vilivyokuwa vinawakilisha maslahi ya watu wa Western Sahara na Palestina. Hatukuona shida kutambua na kutoa ushirikiano kwa vyama vya ANC na vingine vya haarakati za ukombozi wa Kusini mwa Afrika. Tulitambua dhana ya utu wa mtu na kukataa kuhusiana na tawala dhalimu. Ndio sababu ya kuwa tayari kujitoa Commonwealth kama RSA ingeruhusiwa kuingizwa ndani.

  Wakati huo Tanzania ilikuwa kiongozi katika masuala ya haki za watu na kukataa ukandamizaji wa watawala dhidi ya watu wao. Watanzania wenyewe walitembea kifua mbali kwani kuitwa Mtanzania ilikuwa inaendana kabisa na kuwa "mpigania haki za wanyonge". Ukisema "Tanzania" ulikuwa unazungumzia sauti ya Afrika katika masuala ya Kimataifa. Hakutukuwa na ukaribu sana na nchi za Kimagharibi kiasi cha kushindwa kuwambia ukweli. (kesho inshallah, nitawawekea barua ya Nyerere kwa JFK kuhusu Angola/Mozambique na RSA).

  Leo hii Tanzania hii ya Mwalimu imekatwa mkia na haina tena uwezo wa kusimama na kunyoshea kidole mtu yeyote. Haiwezi kuwanyoshea kidole Wamarekani wala Waingereza (Nyerere alivunja hata uhusiano na Waingereza! huku akimtimua Padre mmoja kutoka nchini!). Tanzania hii ya sasa haina uwezo hata wa kujenga hoja ya kimaadili dhidi ya tawala dhalimu. Matokeo yake ni kuwa Tanzania ndugu zangu sasa inafuata. Ndugu zangu, Tanzania inafuata nchi za Senegal, Liberia, Qatar, n.k linapokuja suala la Libya.

  Tanzania ambayo ilikuwa na sauti ya kukataa viongozi wake wamepewa misaada ya magari kiasi kwamba hawawezi tena kuzungumza na wanabakia kumung'unya maneno. Maskini Tanzania hii. Najiuliza mpaka nani atambue Baraza la Mpito la Waasi kule Libya ndio Tanzania ifuate? Kwanini nchi kama Liberia, Botswana na Senegal zimeweza kuvunja mahusiano na Gaddafi lakini nchi kongwe kama Tanzania imeshindwa hata kuonesha kuwatambua uwepo wao?

  Yawezekana kweli viongozi wetu wamekuwa so compromised kiasi kwamba wema umekuwa uovu na uovu umekuwa wema? Ni kweli Taifa letu limenunuliwa hadi sauti yake - ukiondolewa kununuliwa kwa wanyama na raslimali zake? Kwanini sauti za Upinzani nchini zinashindwa kupiga kelele kutaka serikali ivunje uhusiano na serikali ya LIbya? Rais wa Senegal ambaye alikuwa ni mpinzani kwa muda mrefu alielewa hili na hakuonesha utata tena yeye alienda kutangazia msimamo wake ndani ya Libya yenyewe (kule Benghazi), kina Kikwete wanashindwa nini? Wanaogopa nini? Tanzania haina tena ile moral standing ya kukemea udhalimu?
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Thubutu... Just a week ago The Libyan Ambassador visited The President @ the State House...

  Tulichukua Pesa za Mikopo ya Kujenga Misikiti we need to pay them back first...
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Huwezi kuukata mkono unaokulisha! U-matonya wetu kama taifa hauna mipaka wala miko. As a result we've sold our souls ili mradi ni muda wetu wa kula. tragedy!
   
 4. G

  GJ Mwanakatwe JF-Expert Member

  #4
  Jun 20, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 241
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mi nafikiri wewe ndo wa kulaumiwa sio Tanzania, wewe mwenyewe umesema wale ni" waasi wa libya" na huo ndio ukweli, sasa ni vipi tz na heshima zake zote hizi ilizonazo iwatambue waasi? hilo haliwezekani ndugu yangu. Wale ni waasi wa libya, na nchi zote zilizowatambua ni nchi ambazo zimefuata karoti kujipendekeza kwa marekani na nchi za magharibi, hamna lolote zaidi ya hapo. Hatuwezi kuwatambua waasi, kwa kuwa kwa kufanya hivyo ni kukaribisha uasi nchini kwetu, ile ni njia haramu na ni vibaraka tu hawana lolote wale.
   
 5. nyengo

  nyengo JF-Expert Member

  #5
  Jun 20, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 433
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kuna" faida" ambazo haziko wazi ambazoTanzania imefaidika kutoka kwa Gadafi, "faida" hizo ndizo zinatufanya tuone "aibu" kukata uhusiano na Gadafi ijapo Watanzania wengi wameshasahau jinsi gani Gadafi alikuwa adui wetu wa vita vya Kagerai.
  Nafikiri viongozi wengi wa Afrika wanaamini kuwa Gadafi atashinda tu vita hivyo, na kwa sababu hiyo, mataifa mengi ya Afrika yanaogopa huenda endapo Gadafi atashinda basi Gadafi anaweza aka wasapoti waasi na kuweza kupindua serikalihusika na huenda serikali yetu ikawa ktk woga huo. Gadafi alikuwa ni tishio, ka sponser waasi wengi sana
   
 6. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #6
  Jun 20, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,280
  Trophy Points: 280
  Hawa ndio wanaonufaika na ujenzi wa misikiti alioufanya Gaddafi hapa Tanzania badala ya kuwajengea shule na hospital. Kiwete ni rais mdini kwahiyo hawezi kumtosa mwislamu mwenzake Gaddafi. huu ndio ukweli wenyewe.
   
 7. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #7
  Jun 20, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,150
  Likes Received: 2,472
  Trophy Points: 280
  hatuendeshwi na matukio
   
 8. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #8
  Jun 20, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,859
  Likes Received: 4,544
  Trophy Points: 280
  Mwalimu alisema, nchi ikiendeshwa kwa kutegemea misaada toka nchi za nje, itakosa pia uhuru wa kuamua mambo yake. Na mwishowe itakua inaamuliwa mambo yake na nchi za nje.

  That's what is happening katika TZ yetu sasa. Tumekua matonya kiasa kwamba hadi wabunge walishawahi kusema (wakati wa ujio wa Kichaka Jr.) "kua maandamano ya kupinga ujio wake yataonyesha picha mbaya, ivyo wajerumani, waingereza n.k. wataogopa kutuletea misaada!!!" Haya ni mawazo ya wabunge!!! Yaani kupenda misaada kunawafanya wasiwe huru katika kutoa mawazo na maoni yao!!
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Jun 20, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  Kwanini tulitambua POlisario na ANC?
   
 10. F

  FJM JF-Expert Member

  #10
  Jun 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Sijui kama status imebadilika, ila Nelson Mandela alichukuwa kiti cha urais kama a' convicted criminal' na ANC was branded a terrorist organisation. Na kama status haijabilika basi Mzee Mandela atakuwa a 'retired-convicted crimanal? mental!
   
 11. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #11
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,222
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Na kwanini hatukuitambua RENAMO na kuvunja uhusiano na Samora Machel?
   
 12. P

  PakavuNateleza JF-Expert Member

  #12
  Jun 20, 2011
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 957
  Likes Received: 513
  Trophy Points: 180
  kuwatammbua waasi ni insane.
   
 13. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #13
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kulikuwa na thread kama hii wiki iliyopita (https://www.jamiiforums.com/international-forum/145274-will-tanzania-soon-recognize-libyan-rebels.html) ambapo nilisema tatizo letu kubwa hatujui hata Tanzania's foreign policy ni ipi. Membe alipoulizwa juu ya hili anajichanganya sana. Hata kama tunayo foreign policy itakuwa inafuata upepo. That's why I am not surprised what Kikwete and his Co did in South Africa in his recent visit. Msikilize kwenye hii video kuanzia dakika ya 4.5 mpaka ya 8. Anaongelea sera ya defense of freedom, human rights, equality and democracy. Sasa compare na Kikwete kwenda South Africa juzi ku-abolish SADC's Tribunal for human rights. How come one hand you say that one of the pillars of our foreign policy ni protection of human rights, whilst on the hand you goes on to abolish a human rights tribunal? Kwa issue ya Libya sidhani kama tukp bold enough. If we were bold enough we should have expressed our position from the beginning badala ya kusubiri mpaka sasa.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #14
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji, kweli unachekesha sana unataka Tanzania wavunje uhusiano na Libra iwatambue waasi wa Libra Kwani Gaddaf kafanyaje mpaka uvunje uhusiano nae, yaani nchi yoyote Marekani akiichukia basi tuvunje uhusiano nao
   
 15. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #15
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Kumbe waasi wa Libya ni wakristo tulikuwa atufahamu
   
 16. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #16
  Jun 20, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  kifupi nio wanafiki na hatuna msimamo,hatujiamini ndio maana tunalala kotekote
   
 17. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #17
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  sera zetu za mabo ya nje ni "ECCONOMIC DIPLOMACY"
   
 18. Sijali

  Sijali JF-Expert Member

  #18
  Jun 20, 2011
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 2,062
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Duh, mkulima kule kiembeni hawezi kamwe kumfahamu mheshimiwa Waziri Membe, concensus, investors, disadvantage, handle at a time, accomodate n.k. kweli haya maneno hayana mukabala wake katika kiswahili? Jamani, huu utumwa wa kiakili utakwisha lini?
   
 19. n

  nitasemaukweli Member

  #19
  Jun 20, 2011
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sina la kusema zaidi!

  [​IMG]

   
 20. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #20
  Jun 20, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Kama sijakosea wakati wa Mwalimu tulikuwa upande wa Arafat dhidi ya Israel!? Maajabu sana na pia tulisimamia vita vya Kabila mpaka akamuondoa Mubutu wakati wa Mkapa hivi Kabila hakuwa muhasi kwa mubutu?!

  Anyway swala la qadhaffi ni la UN nashangaa sisi kama wanachama wa UN bado hatujamkana Qadhaffi adharani!
   
Loading...