Kwanini Sumaye asishitakiwe kwa mauaji ya Mwembe Chai na Pemba?

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
15,136
10,112
Wakati Sumaye akiwa Waziri mkuu watu wengi waliuliwa kwa kupigwa risasi kinyama kama tembo wauliwavyo na wawindaji haramu.

Matukio ya kutisha ni kuuliwa kwa ndugu zetu waliokuwa wakitokea msikitini pale mwembe chai waliuliwa kwa kushambuliwa kwa risasi za moto. Unyama huu ulifanyika wakati bwana Sumaye alikuwa kiongozi mkuu wa serikali hivyo anastahili kushitakiwa kwa mauaji yale.

Hiyo haikutosha wapemba waliuliwa kwa kushambuliwa kwa risasi za moto hadi wengine walishakimbilia Somalia na shimoni kule Mombasa. Huu ulikuwa ni utawala wa huyu bwana mkubwa.

Kwanini huyu jamaa atembee huru huku mikono yake imetapakaa damu? kwanini asishitakiwe kwa hayo mauaji wakati yeye ndo alikuwa kiongozi mkuu wa serikali?
 
Kweli kiongozi,lakini kumbuka mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri lilloidhinisha kuuliwa kwa hao wapendwa wetu ikiwa ni pamoja na kuidhinisha manunuzi ya silaha zilizowauwa alikuwa ni BWM-Rais wa awamu III,bado yu hai anaendelea kudunda na kututukana WaTz.Vipi naye hastahili hayo mashitaka?

Awamu iliyomaliza muda wake yalitokea mauwaji ya kinyama,kwa Mara ya kwanza tulishuhudia mauwaji yaliyofanywa na makombora yaliyotengenezwa China yakivurumishwa kwenye mkutano na kuuwa watu.Serikali kupitia wataalamu wake,waliuthibitishia Umma kuwa mabomu hayo yalitengenezwa China,lakini cha kustaajabisha hakuna hatua zozote za uchunguzi zilizofanyika kubaini nani alisafiri hadi Uchina na kuingiza nchini silaha za kivita.Unaonaje waziri MKUU na Rais wa kipindi hicho wasinyongwe?Au ni Sumaye tu uliyemkuta na hatia ya mauwaji?Kweli kuishabikia fisiemu kunahitaji uwendawazimu fulani,Fisiemu hoyeee!!!
 
Umenena kweli ndugu yangu. Kuna watu wengine wanafikiria kwa kutumia Miguu, mtoa maada huyu ni mmoja ya watu hao. Huwezi kuongelea habari ya kuteketeza tumbili kama mhalibifu wa mahindi shambani kwako huku ukiwa unajua kazi iliyofanywa na inaendelea kufanywa na nyani mara aingiapo shambani kwako.. Hakuna shaka kuwa kuwa Wakuu wa nchi katika Awamu ya III na ya IV wametudhihirishia kuwa Tanzania ni nchi ya kidikiteta na si ya Kidemokrasia. Ukisema ukweli basi wewe lazima uwindwe kama digidigi. CCM Hoyee, ama kweli wa TZ tunaisoma namba ya
 
Kama tunakumbukumbu nzuri basi ni Mkapa ndie alieamrisha mauaji yote haya maana pamoja ya kuwa alikuwa nje ya nchi lakini kauli zake alizoziacha wakati anasafiri ndizo zilizofanya kazi.

Na kulithibitisha hilo kuwa mkapa ndio mhusika mkuu ni pale aliporudi safari yake na kuwapa vyeo akina venasi toss.

Kama sikosei mauaji ya muembe chai yalikuwa wakati wa mzee ruksa mh Mwinyi na serikali yake.
 
Unayo fulsa ya kwenda mahakamani kumshitaki japo mimi napenda anyongwe kabisa hili ntalisimamia mwenyewe.
 
Magufuli shugulikia kikamilifu suala la elimu, mleta mada ni zao la ukosefu wa elimu hajui nani ni amiri jeshi mkuu. Mbaya zaidi wengine wanadhani rais akisafiri nchi inakuwa haina kiongozi, which means wakati wa Kikwete siku 2000 nchi ilikosa uongozi
 
Mauaji ya mwembechai aliyesababisha ni mkuu wa mko wakati ule bwana makamba aliposema " atakamata wadhamini wa msikiti wa mwembechai" ndiye aliyesababisha hayo. Uzuri mashahidi wengi wapo hai kama sheikh ponda issa ponda, ingawa sheikh wetu omari bashir mungu amrehemu ameshatangulia mbele ya haki. Sumaye hahusiki na mwembe chai.
 
Wakati sumaye akiwa waziri mkuu watu wengi waliuliwa kwa kupigwa risasi kinyama kama tembo wauliwavyo na wawindaji haramu.

Matukio ya kutisha ni kuuliwa kwa ndugu zetu waliokuwa wakitokea msikitini pale mwembe chai waliuliwa kwa kushambuliwa kwa risasi za moto. Unyama huu ulifanyika wakati bwana sumaye alikuwa kiongozi mkuu wa serikali hivyo anastahili kushitakiwa kwa mauaji yale.

Hiyo haikutosha wapemba waliuliwa kwa kushambuliwa kwa risasi za moto hadi wengine walishakimbilia somalia na shimoni kule mombasa. Huu ulikuwa ni utawala wa huyu bwana mkubwa.

Kwanini huyu jamaa atembee huru huku mikono yake imetapakaa damu? kwanini asishitakiwe kwa hayo mauaji wakati yeye ndo alikuwa kiongozi mkuu wa serikali?
Hivi Sumaye alishawahi kuwa Amiri Jeshi huko Tanzania?
 
Kama tunakumbukumbu nzuri basi ni Mkapa ndie alieamrisha mauaji yote haya maana pamoja ya kuwa alikuwa nje ya nchi lakini kauli zake alizoziacha wakati anasafiri ndizo zilizofanya kazi.

Na kulithibitisha hilo kuwa mkapa ndio mhusika mkuu ni pale aliporudi safari yake na kuwapa vyeo akina venasi toss.

Kama sikosei mauaji ya muembe chai yalikuwa wakati wa mzee ruksa mh Mwinyi na serikali yake.
Mauaji ya Mwembechai yalikuwa mwaka 1998 rais alikuwa Benjamin Mkapa.
 
Magufuli shugulikia kikamilifu suala la elimu, mleta mada ni zao la ukosefu wa elimu hajui nani ni amiri jeshi mkuu. Mbaya zaidi wengine wanadhani rais akisafiri nchi inakuwa haina kiongozi, which means wakati wa Kikwete siku 2000 nchi ilikosa uongozi

ishi! Amiri jeshi anaingiaje? Kwani walitokea kongo hao waliouliwa? Isitoshe mkapa alikuwa nje ya nchi na yeye sumaye ndiyo alikuwa msimamizi mkuu wa serikali.
 
Nimepata ukakasi na kumshangaa Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye anaposema kuwa polisi wametumia nguvu kubwa sana Dodoma katika mkutańo wa CHASO mjini humo.

Lakini napenda kumkumbusha Sumaye kuwa wakati akiwa Waziri Mkuu ndipo kwa mara ya kwanza tulishuhudia nguvu kubwa ya polisi dhidi ya raia ikiwemo mauaji ya Mwembechai. Ikiwa Sumaye amelisahau hilo anapaswa kuangalia ile video ya Mwembechai ambapo afisa wa polisi akitoa maelekezo kwa askari wake "piga huyo piga yule".

Vile vile wakati akiwa Waziri Mkuu tulishuhudia mauaji ya Pemba ambayo yalichafua historia ya Tanzania kwa kutoa wakimbizi kwa mara ya kwanza ambao walikuwa nchini kenya.

Sumaye anapaswa kufahamu kuwa watanzania hawajasahau alipokuwa akitumia nafasi yake ya uwaziri mkuu ndani ya bunge kuzima mijadala ya Mwembechai ndani ya bunge ilipokuwa inapelekwa na mbunge wa Kigamboni wakati huo, Kitwana Kondo.

Swali langu la Sumaye ikiwa anasema Dodoma ilitumika nguvu kubwa na polisi wanafata amri za wanasiasa na si taaluma, je Mwembechai na Pemba anatuambiaje?
 
Sijakuelewa unataka kujustify kinachotokea sasa kwa mambo ya kale ? People change ,sumaye kachange , ccm ndio ileile...
 
nimepata ukakasi na kumshangaa waziri mkuu mstaafu Fredirick Sumaye anaposema kuwa polisi wametumia nguvu kubwa sana dodoma katika mkutańo wa chaso mjini humo.

Lakini napenda kumkumbusha Sumaye kuwa wakati akiwa waziri mkuu ndipo kwa mara ya kwanza tulishuhudi nguvu kubwa ya polisi dhidi ya raia ikiwemo mauaji ya mwembechai, ikiwa sumaye amelisahau hilo anapaswa kuangalia ile video ya mwembechai ambapo afisa wa polisi akitoa maelekezo kwa askari wake "piga huyo piga yule".

Vile vile wakati akiwa waziri mkuu tulishuhudia mauaji ya pemba ambayo yalichafua historia ya Tanzania kwa kutoa wakimbizi kwa mara ya kwanza ambao walikuwa nchini kenya.

Sumaye anapaswa kufahamu kuwa watanzania hawajasahau alipokuwa akitumia nafasi yake ya uwaziri mkuu ndani ya bunge kuzima mijadala ya mwembechai ndani bunge ilipokuwa inapelekwa na mbunge wa kigamboni wakati huo Kitwana Kondo.

Swali langu la Sumaye ikiwa anasema Dodoma ilitumika nguvu kubwa na polisi wanafata amri za wanasiasa na si taaluma je mwembe cha na pemba anatuambiaje?
Kwa hiyo tafsiri yako ya nguvu kubwa ni hadi afe mtu. Acha hayo mawazo mgando.
 
Back
Top Bottom