Kwanini Sumaye asishitakiwe kwa mauaji ya Mwembe Chai na Pemba?

Kwa mara ya kwanza nasikia basi limepinduka na kuuwa abiria wote kisha utingo ndiye anashitakiwa. Dereva akiwa upande wa mwendesha mashaitaka! Na utingo anaulizwa kama ana leseni ya udereva!!
 
Wakati Sumaye akiwa Waziri mkuu watu wengi waliuliwa kwa kupigwa risasi kinyama kama tembo wauliwavyo na wawindaji haramu.

Matukio ya kutisha ni kuuliwa kwa ndugu zetu waliokuwa wakitokea msikitini pale mwembe chai waliuliwa kwa kushambuliwa kwa risasi za moto. Unyama huu ulifanyika wakati bwana Sumaye alikuwa kiongozi mkuu wa serikali hivyo anastahili kushitakiwa kwa mauaji yale.

Hiyo haikutosha wapemba waliuliwa kwa kushambuliwa kwa risasi za moto hadi wengine walishakimbilia Somalia na shimoni kule Mombasa. Huu ulikuwa ni utawala wa huyu bwana mkubwa.

Kwanini huyu jamaa atembee huru huku mikono yake imetapakaa damu? kwanini asishitakiwe kwa hayo mauaji wakati yeye ndo alikuwa kiongozi mkuu wa serikali?
Watoto wa siku hizi bana!!
Waombe Mods tu wakusaidie kuuondoa huo uzi, maana umeshaharibu!
 
Hata kama unamchukia Sumaye. Lakini mauaji ya mwembechai ni mwinyi na malecela mkapa na sumaye ni yale ya pemba. Uwe na kumbukumbu kidogo au ukiwa chama cha majipu huwa hamkumbuki vitu
Kweli wewe ndiye usiye na kumbukumbu ndio mbna mnaitwa malofa kwa kuwa hata vichwa vimefilisika na kupoteza kumbukumbu.

Mwinyi katoka madarakani mwaka 1995 mauji ya mwembechai yametokea mwaka 1998 haya tuambia wapi na wapi, sumaye hachomoki katika sakata la mwembechai hata kidogo.
 
Mbona Waziri Mkuu Mstaafu hakushtakiwa Kwa Mauaji ya Mwangosi pale Iringa wakati in yeye aliyesema Polisi wapige tu?
 
Ukiwa nchi unafurahi viongozi mazingaombwe wafuasi mazingaombwe,unaweza kuona mtu anamyoshea kidole mwenzake kuwa ana uvundo ili hali na yeye uvundo umemzunguuka!
 
Kweli wewe ndiye usiye na kumbukumbu ndio mbna mnaitwa malofa kwa kuwa hata vichwa vimefilisika na kupoteza kumbukumbu.

Mwinyi katoka madarakani mwaka 1995 mauji ya mwembechai yametokea mwaka 1998 haya tuambia wapi na wapi, sumaye hachomoki katika sakata la mwembechai hata kidogo.
Upuuzi mwingine bhana! We wa wapi wewe? Unajua kazi ya Amiri jeshi mkuu? Waziri mkuu hana mamlaka ya kikatiba kutoa maamuzi hayo. Kazi hiyo hufanywa na Rais ambaye ni amri jeshi mkuu.Huu mzigo wote ni wa Mkapa.
 
Hatutaisahau kamwe damu ya Waislam iliyomwagwa bila huruma. Daima tunawalaani wote waliohusika.
Waislamu waliyokuwa wanafanya yalikuwa sahihi waliambiwa wafungue barabara wakafungua bado wanapigwa risasi?
 
Mauaji ya mwembechai aliyesababisha ni mkuu wa mko wakati ule bwana makamba aliposema " atakamata wadhamini wa msikiti wa mwembechai" ndiye aliyesababisha hayo. Uzuri mashahidi wengi wapo hai kama sheikh ponda issa ponda, ingawa sheikh wetu omari bashir mungu amrehemu ameshatangulia mbele ya haki. Sumaye hahusiki na mwembe chai.
.......acha kumtetea sumaye anahusika a-z
 
Mhe Sumaye hajawahi kuwa amiri jeshi mkuu kwahiyo hausiki na mauaji ya Pemba na mwembechai hata kama rais kipindi hicho alikuwa nje ya nchi kwa nafasi yake hakuwa amiri jeshi(ni mawazo yangu)na niseme sio mfuasi wa mhe sumaye.
 
Kweli ujinga mzigo! Mleta uzi unapenda sana kufukua makaburi sina uhakika na unachokitafuta. Mauaji yaliyonasa kwenye makamasi yako ni ya mwembechai tu hujayaona ya Mwangosi, Olasit, diwani Matata wala ya kule Pemba? Wakati wa Sumaye ulikuwa na umri gani? Ni kwanini hukuitendea haki katiba ukamshtaki wewe binafsi kwa kuwa ushahidi ulikuwa nao wa kutosha? Haya slishastaafu mfungulie mashtaka basi ili akikushinda ulipe hizo gharama.
Unashtaki jf kwani ndio mahakama? Mtafute mzee Sitta akupe falsafa ya siasa za majitaka ndio uje na huo ukilaz.a wako humu. Ccm mkizidiwa maujanja libido zenu zinashuka to the minimum. Tulieni na jifunzeni kuheshimu maamuzi ya wengine kwani waliamua wakiwa na akili timamu kuihama ccm. Tafuta kisa kingine hiki kilishashindwa.
 
Nimepata ukakasi na kumshangaa Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye anaposema kuwa polisi wametumia nguvu kubwa sana Dodoma katika mkutańo wa CHASO mjini humo.

Lakini napenda kumkumbusha Sumaye kuwa wakati akiwa Waziri Mkuu ndipo kwa mara ya kwanza tulishuhudia nguvu kubwa ya polisi dhidi ya raia ikiwemo mauaji ya Mwembechai. Ikiwa Sumaye amelisahau hilo anapaswa kuangalia ile video ya Mwembechai ambapo afisa wa polisi akitoa maelekezo kwa askari wake "piga huyo piga yule".

Vile vile wakati akiwa Waziri Mkuu tulishuhudia mauaji ya Pemba ambayo yalichafua historia ya Tanzania kwa kutoa wakimbizi kwa mara ya kwanza ambao walikuwa nchini kenya.

Sumaye anapaswa kufahamu kuwa watanzania hawajasahau alipokuwa akitumia nafasi yake ya uwaziri mkuu ndani ya bunge kuzima mijadala ya Mwembechai ndani ya bunge ilipokuwa inapelekwa na mbunge wa Kigamboni wakati huo, Kitwana Kondo.

Swali langu la Sumaye ikiwa anasema Dodoma ilitumika nguvu kubwa na polisi wanafata amri za wanasiasa na si taaluma, je Mwembechai na Pemba anatuambiaje?
Ooohoo hivi sumaye alikuwa...waziri wa mambo ya ndani enzi zile.......
 
ishi! Amiri jeshi anaingiaje? Kwani walitokea kongo hao waliouliwa? Isitoshe mkapa alikuwa nje ya nchi na yeye sumaye ndiyo alikuwa msimamizi mkuu wa serikali.

Rudi shule kidato cha 1 na 2 ukajifunze somo la Uraia.

Elimu, elimu, elimu ni muhimu sana!!
 
Kweli wewe ndiye usiye na kumbukumbu ndio mbna mnaitwa malofa kwa kuwa hata vichwa vimefilisika na kupoteza kumbukumbu.

Mwinyi katoka madarakani mwaka 1995 mauji ya mwembechai yametokea mwaka 1998 haya tuambia wapi na wapi, sumaye hachomoki katika sakata la mwembechai hata kidogo.

Weka kumbukumbu vizuri, Mzee ruksa baada ya mauaji ya mwembechai ndipo alipokuja na msemo wa 'RUKSA', anaetaka kula nguruwe ruksa, anaetaka kula nguchiro ruksa n.k.
 
Mkuu mwambie huyo nguchiro asiyejua chochote. Maana shida ilianzia kwenye mabucha ya nguruwe waislam walikua wanayavunja. Sasa ndio Rais Mwinyi akatoa kauli ya ruksa kila mtu ale ruksa hata ukila fisi poa tu.
 
Back
Top Bottom