Kwanini sisi waafrika pekee tuna rangi nyeusi tii, tofauti kabisa na binadamu wa mabara mengine?

Wakuu marry chrismass.

Nimekaa nimewaza na kufikiri naona kama kuna kitu hakiko sawa kuhusu sisi waafrica.

kitu cha kwanza ni kwanini sisi waafrika pekee tuna rangi nyeusi tii,
tofauti kabisa na binadamu wa mabara mengine, mfano ulaya ni weupe,asia ni weupe,australia ni weupe,america kaskazini na kusini ni weupe (isipokuwa black americans tu ambao nao pia wanatokana na mababu zetu waliopelekwa utumwani kule).
so najiuliza kwanini only africans are the black people ? Kwa majujibu wa takwimu za population, dunia mpaka sasa ina watu bilion 7.8, na africa pekee ina watu bilion 1.3 tukijumlisha na yale masalia ya america na carribean labda tunakuwa 1.4 au 1.5 billion ndo watu pekee weusi duniani, maana ake kati ya watu bilion 7.8 weusi ni 1.5 bilion pekee,wengine wote wanaobaki ni weupe, kwanini yani weupe mbona wengi sana, je imekuwaje weusi wakawa wachache alafu wametengewa bara lao, maana mabara yote 6 yenye watu matano ni weupe isipokuwa bara moja tu la africa ndo weusi tii why mbona sipati majibu sahihi ? Sijichukii kwa sababu mimi mweusi ila najiuliza tu kwanini waafrica pekee ndo weusi ? Alafu pia wakawa wachache kuliko weupe ? Kuna laana gani ilipita hapa ebu nambieni wadau.

Kitu cha pili, kwanini sisi watu weusi tunaonekana tuko nyuma kwa karibu kila kitu, kuanzia ustaarabu watuletea watu weupe, teknolojia nyingi zimetoka kwao (asilimia karibu 90 ya kila tunachotumia waafrica kilianza kwanza kugunduliwa na mweupe), kwanini mweusi akawa nyuma sana ? Kuna laana gani hapa ? Kwanini sifa ya mwafrica ni ya umaskini na ujinga tu why this ? Walitutawala kwa karne karibu 4, wakatutumikisha kwenye ardhi yetu wenyewe na kutufanya watumwa na sisi tukakubaliana na hali, why only africans we became very stupid ? Mbona sisi hatukuanza kuwatawala ila wao weupe wakaanza ? Tuna rasimali kibao ila tumeshindwa kuzitumia zituboreshee maisha badala yake bado tumkabidhi mtu mweupe, kwanini sisi watu weusi tuna nini ebu nipeni majibu !

Cha mwisho, kwanini ngozi nyeusi inabaguliwa (racisim) na kuonekana duni, nadhani tunashuhudia wenzetu walioko ng'ambo jinsi wanavyobaguliwa na kuitwa nyani, ina maana sisi weusi duniani tulikuja bahati mbaya au ni vipi yani !...niki mnukuu mwarabu moja mweupe pale libya ambaye aliwateka waafrica wakiwa wanatorokea ulaya kupitia mediterania aliwaambia hivi "mnaenda wapi nyie watu weusi kutoka kuzimu watumwa mliolaaniwa ninyi"....unaweza kuona ni jinsi gani sisi watu weusi tunavyochukuliwa na watu weupe, sasa kwanini sisi waafrica tukaumbwa weusi (rangi ya kudharaulika,duni) alafu tukawa wachache na bado haitoshi tukapewa bara la peke yetu weusi (bara la africa) wakati weupe wao wakaumbwa wengi alafu wakasambazwa kwenye mabara matano tofauti na pia wakapewa upeo wa uelewa kuliko sisi ? Au ni kweli mungu alitulaani nini sisi weusi ? Au sisi weusi ni uzao wa shetani kama wanavoamini baadhi ya weupe ?

Nb : sijaudharau uafrica wangu ila najiuliza tu kwanini mweusi anadharauliwa na kudunishwa wakati mweupe yupo mbele yetu kwa karibu kila kitu ?
Ndugu yangu hii ni Melanin colour ni rangi iliyo kuwa bora kabisa na ndio watu walio kuwa civilised kabla ya mtu mweupe kwani huyu mtu mweupe anatokana na mtu mweusi ......jua jambo moja tu kila unapo kuwa na RANGI NYEUSI sn ndio unakuwa na health skin hii ni fact sio Jokes na unapo kuwa mweupe sn ndio ngozi inapokuwa haina afya kwa maana huna kabisa SKIN PIGMENT.

Mtu mweusi anapigwa vita kila corner ili kumdidimiza tu kifikra na kiuchumi sababu wanaogopa kuja kulipiza kisasi kwa mambo yaliyofanyika nyuma .

Hata shule HISTORY mnayo fundishwa ni uwongo mtupu na mambo mengi yapo ya uwongo hata unakumbuka GEOGRAPHY tulikuwa tunaambiwa AFRICA ni BARA la TATU KWA UKUBWA BAADA YA AMERICA ulikuwa uwongo mtupu.



Sent from my SM-G975F using JamiiForums mobile app
 
Christopher Columbus alipofika West Indies na Amerika aliwapata watu weusi wakiwa mateka wa vita kwenye Indian village, alipouliza ni vipi akajibiwa kuwa Hawa walikamatwa katika Kijiji kingine Cha watu weusi. Pia aliweza kupata mishale ya dhahabu Kwa jina GANA sawa na alizoziona kule ulaya na west Afrika Kwa jina Hilo Hilo. Ili kuhakikisha usahihi wa mishale hiyo, alirudi nazo ulaya na kufanya chemical analysis confirming their similarities.
Haiti na Dominican republic, Honduras na Mexico zilikuwa na watu weusi according to Colombus own Journals.
Mahindi na pamba zilikuzwa Afrika kabla mzungu kuja nazo which are native to America's.
Lugha zinakaribiana ie Darras in South America na Jarras in West Africa pia ndizi Yana majina sawa nk. Tafuta Dr.Ivan Sertima na Cheikh anta Diop Kwa maelezo zaidi.
Watu wa kwanza kufika America ni Vikings na Waafrica, Nilivyojuwa hilo ndio niliamini hii historia imepinduliwa juu chini
 
Ukishaamini asili yako ni laana basi unakuwa umelaaanika na mawazo yako mwenyewe.
 
naomba uanze kwa kusoma historia ya mwanadamu wa sasa homo sapiens utaelewa sis tumetokawapi mpaka kufika hapa. Hakuna mwanadamu hapo ulimwengu ambaye asili yake sio afrika.

Mutation na evolution haitokei kwa vizazi vinne au vitano kwa viumbe kama binadamu wazungu walitoka afrika miaka 12000 iliyopita , so mazingira yalipekea kutokea mutation ya gene inayocontrol melanin ikawa inapungua nguvu na chance ya kusurvive kwa watu waliokuwa weupe ikawa kubwa kwasababu sehemu walizokuwa wazungu hakuna jua so weupe waliweza kutengeneza vitamin D nyingi zaidi ya watu weusi waliokuwa huku ulaya . Ndio maana mpaka leo watoto wote ulaya wanapewa dawa ya vitamin D na waafrika wa ulaya wanashauriwa watumie vitamin D sana maana ngozi yao inapunguza uwezo wa kufonza nguvu za kujua kutengeneza vitamin d

kusema iamini sayansi na uokoe namaanisha kuwa sayansi ndio itakuokoa usipate magonjwa uondokane na ujinga na kukuepusha na utapeli mwingi wa huu ulimwengu

Napenda kuwaalika Kiranga Scars kuongezea information pale ambapo hapajatosha.

Mkuu habari yko mimi naungana na wewe na hoja yako hii ni ya ukweli kabisa hiki ndicho kilichokuwepo.

Umemjibu vizuri kabisa VLADIMIR putina kuhusu hoja aliyotoa na mimi hapo kwa kuongezea ni kwamba nakubaliana na wewe ya kwamba evolution haitokei vizazi vinne au vitano na ni kweli asili ya mwanadamu ni Africa.

Uingereza kuligunduliwa fuvu la Cheddar man ambaye ni binadamu wa kale zaidi kuishi uingereza na alikuwa mweusi tiii na mpaka leo fuvu lake lipo makumbusho lakini cha kushangaza wanasayansi waliamua kuwapima DNA watu waliokuwa karibu na eneo fuvu lilipogunduliwa na wakagundua DNA zao zinafanana kabisa na za Cheddar man na cha kushangaza walikuwa wazungu pure hapo ndipo walipokubaliana kwamba ni mazingira ndiyo yaliwafanya wawe wazungu
 
Mimi wa kwanza!
Ngoja nijaliwa kwa uelewa wangu.
Mbongo {African}siyo mweusi tu bali yeyote anaweza kuwa muafika.
Kuhusu rangi nyeusi isikupe shida ni Nature yenyewe ikumbukwe hili bara linapata jua kamili hivyo kuwa weusi nikwasababu ya ngozi iweze kuhimili miale mibaya ya jua {mawazo yangu}
Halafu bara letu ni zuri kuliko huko unakokusifia sisi hatuna mavimbunga sijui yakutisha, masunami,matetemeko,mavolcano hata kama yapo lakini siyo kama wao.
Pia kuhusu kutawaliwa na weupe ni sawa hii inaitwa kutesa kwa zamu hata sisi tulishawahi kuwatawala ila sema ilifichwa na hao hao kuogopa aibu,
Kuna mtu alikuwa anaitwa Malkia wa Sheba,kuna hawa jamaa Mafarau wa misri,inasemekana walikuwa weusi kabisa na hii ijulikana kupitia ugunduzi wa ile miili kufukuliwa kwenye makabuli huko Cairo na kukuta jamaa ni weusi tii.
Ngoja waje wataalam wakupe mkuu.
Mtoa mada kaja na facts kwa kutoa mifano iliyo hai wewe umekuja na nadharia tupu sasa huoni kwamba mtoa mada yupo sahihi?
 
Wahindi wengi ni weusi, Australia kabla mzungu ilikuwa watu weusi, Papua new guinea weusi, Hawaii kabla mzungu weusi, Amerika ilikuwa weusi kabla colombus kufika, Spain & Portugal(Iberia) ilikuwa watu weusi wakati moors walitawala Uhispania, South Amerika vile vile haswa Equador, Honduras, Colombia na Caribbean.
Wakaenda wapi? Kwahiyo baada ya ujio wa mzungu katika maeneo hayo weusi wakatokomea ama unamaanisha nini?
 
Rangi ya mwafrika inatokana na mazingira ukandaa tunaoishi ni wajua kali so melalinin inablock uv ili isiharibu seli za ngozi ili tusipate kansa,
kuwa nyuma kimaendeleo hii naiweka katika sehemu mbili kwanza vurumai la ukoloni/utumwa(dini za kigeni) la pili ni sisi waafrika kutotaka kuendelea na misingi yetu ya maisha kuvurugwa mfano hatu mfumo wa kupata viongozi sahihi viongozi wetu ni kama sio washamba wa wazungu/non-african basi wanawatumikia wazungu/non-african.

nimalize kwa kusema , iamini sayansi uokoke
Kuna sehemu yenye jua kali kuzidi bara Asia specifically Uarabuni? Lakini mbona ni weupe na jua haliwaathiri.
 
mimi sijaamini kwamba ni mbaya ila weupe (wazungu) ndo wanaiona ni mbaya ndo maana wanatubagua na kutuita nyani, na wakaenda mbali zaidi na kusema sisi na uzao wa shetani.
Hata vibonzo vya shetani utakuta vinachorwa katika sura ya kutisha tena nyeusiiii.
 
Andalusia 700AD - 1400 AD Granada and Cordoba in Spain. Ndio maana wahispania na Portuguese wako tofauti sana kimaumbile ukilinganisha na wenzao kutoka Britain na Scandinavia.
Utofauti wao unatokana na nini? Ukiniambia maumbo utakuwa upo wrong maana kama mantiki yako ni kwamba Waafrika waliwatawala hao wazungu basi maeneo hayo pangekuwa na machotara wengi ila sehemu ambayo ni wazungu watupu zaidi ya 95% basi ni Spain.
 
Hoja yako ya kwanza kuhusu Weusi Ni hoja ya kijinga kabisa kabisa...

Yani mbugani Swala ajiulize kwanini kwanini sisi tunaliwa sana na Simba?

Yani badala ya kujivunia kuwa uko Unique unaanza kusema Weusi ni laana? Ndugu unakosea sana, tena sana.

Umepewa bara kubwa hili lina kila kitu, nasema kila kitu, post yako ilitakiwa ianze kwenye aya uliyoanza kuzungumzia uduni waaendeleo ya Afrika hapo ungekuwa unaongea vitu vya msingi...
Kuwa unique pekee sio sifa njema kama uko nyuma kwa kila kitu. Unaweza kuwa unique halafu u unique ukawa wenye sifa mbaya.
 
Jiulize kwanza,
1.binadamu yupi ana hasira za kijinga kuliko wengine?

2. Binadamu yupi ana wivu wa kijinga kuliko wengine?

3. Binadamu yupi ni mwizi, mbinafsi na muongo kuliko wengine?

4. Binadamu yupi ni mjuaji na mpenda masifa kuliko wengine?

5. Binadamu yupi hajiamini badala yake anaamini binadamu wengine.

NB. Kwa kifupi ili tupate ukweli na kujiamini zaidi mataifa ya Africa lazima yaungane ili wajue nguvu zetu. Walitugawa ili iwe rahisi kututawala na kupunguza uwezo wetu.
 
Jiulize kwanza,
1.binadamu yupi ana hasira za kijinga kuliko wengine?

2. Binadamu yupi ana wivu wa kijinga kuliko wengine?

3. Binadamu yupi ni mwizi, mbinafsi na muongo kuliko wengine?

4. Binadamu yupi ni mjuaji na mpenda masifa kuliko wengine?

5. Binadamu yupi hajiamini badala yake anaamini binadamu wengine.

NB. Kwa kifupi ili tupate ukweli na kujiamini zaidi mataifa ya Africa lazima yaungane ili wajue nguvu zetu. Walitugawa ili iwe rahisi kututawala na kupunguza uwezo wetu.
Lini waafrika walikuwa wamoja hadi useme wamewagawa ?
 
Wahindi wengi ni weusi, Australia kabla mzungu ilikuwa watu weusi, Papua new guinea weusi, Hawaii kabla mzungu weusi, Amerika ilikuwa weusi kabla colombus kufika, Spain & Portugal(Iberia) ilikuwa watu weusi wakati moors walitawala Uhispania, South Amerika vile vile haswa Equador, Honduras, Colombia na Caribbean.
Ona hapa ramani ya rangi za ngozi miaka kadhaa iliyopita.
1640611936223.png

Utaona hata Afrika si "weusi" wote, maana kabla ya Wabantu kufika Afrika Kusini wakazi asilia si weusi. Vivyo hivyo Uhindi Kusini wako weusi sana. Pamoja na Australia. Watu "weupe" wanaweza kuishi pekee penye Jua kidogo. Siri yake ni kinga cha melanini katika ngozi (kinga dhidi ya mionzo hatari), na pia haja ya kupata Jua la kutosha ili mwili uweze kujenga vitamini (na hapa weusi-weusi wana hasara penye Jua kidogo).

Wataalamu huamini kwamba rangi nyesui kiasi ilipotea kwenye kaskazini kama miaka 6000 - 10,000 iliyopita, ilhali "weusi" uliongezeka kwenye ukanda wa tropiki penye Jua kali.
 
we jamaa inaonekana unajua vizuri mambo ya human evolution na natural selection, ebu tuchambulie basi haya mabadiliko ya rangi yalitokeaje kulingana na muda wao pia, bila kusahau why rangi nyeusi iko nyuma kwa kila kitu kuanzia civilization, technologies na kuishi kitumwa wakati tumeukalia utajiri
Nadharia ya mageuzi(Evolution) inaweza kuwa mada rahisi au ngumu kuielewa. Leo nitajaribu kuifanya iwe nyepese, nitatoa mifano mirahisi sana. Kabla sijakujibu swali lako kuhusu rangi ya mwafrika, nitaanza kuelezea maana ya nadharia ya mageuzi(Evolution/evolution theory), uteuzi wa asilia(natural selection) baadae ntakuja asili ya mwanadamu na mwafrika na kujibu maswali yako ya ustaarabu(civilization) japo itakuwa subjective zaidi.

Nini maana ya Nadharia ya mageuzi(Evolution)? kwa lugha raisi ni maendeleo ya maisha hapa duniani, evolution ndio inayoongoza uwepo wa maisha hapa ulimwenguni zaidi ya miaka 3.5 billion iliyopita. Maisha yalianza kama bacteria na hao bacteria wakagundua sex(kujamiiana) wakaanza kufanya mabadiliko mpaka dunia kukatokea binadamu , samaki, bacteria ,mijusi ,vyura na nk. Kuelewe zaidi kuhusu evolution tutachukulia mfano wa wanyama ila ntatumia mfano wa ndege na baadae mbwa(nikizungumzia artifical selection).

Kwa wanyama evulution inaanzia pale kwenye mbegu za kiume(sperm cell) and yai la kike(egg) cell hizo huwa zinapata mutation kwasababu ya kimazingira au kwa bahati mbaya tuu (kumbuka hii ni bahati tu hamna cell inaamua ipate mutation) . Baada ya hii mutation kinachofuata ni kuunganisha hizi seli mbili na kutengeneza mtoto. Watoto wote wanaozaliwa japo wana fanana na wazazi wao ila kila mmoja ni wakipekee, pia viumbe wanapenda kuzaa watoto wengi kwasababu ya kuongeza nafasi ya jamii yao kuishi, maana watoto wengi wa viumbe hufa wakiwa watoto. Nikitolea mfano hili jambo la upekee wa watoto ni pale watoto wa wazaa mmoja wanakuwa wengine warefu, wengine wafupi, wengine wananguvu wengine wanyonge na hizi tabia zao zinachangia katika natural selection.

Sasa tuje kwenye natural selection hapa ndio utaelewa nini maana ya evolution vizuri. Tuanze na mfano aliotumia darwins.
Katika kisiwa flani x kuna ndege walipeperushwa na kibunga kutoka bara la amerika wakatua kwenye hiko kisiwa x. Hiko kisiwa kilikua na vyakula ya kutosha na hakukuwa na maadui ambao walikuwa wanawau . Ndege wakazaliana sana (kumbuka kuwa kiumbe chochote hapa duniani kinakazi tatu amabazo ni kujistiri asife, kutafuta chakula akishashiba anatafuta kiumbe mwenzake na kuzaa nae) kama unakumbuka hapo juu kuwa mzazi mmoja anazaa watoto wenye tabia na muonekano tofauti japa wanafanana na wazazi wao na wao wenyewe kwa asilimia fulani. Kwahiyo jamii ikaongezeka na chakula kiaanza kupungua , hapo ndio vurugu linapoanza . Kwahiyo katika utofauti wao, kuna ndege walipata midomo ya kupasua mbegu , wengine kula wadudu na wengine kula vitu vingine ila kuna wengine hawakuzaliwa na sifa za kama hao ndege wengine kwa hiyo wao kupata chakula ikawashida wakafa njaa na DNA zao hazikupitishwa kwa vizazi vingine. Tukirudi kwa walioweza kuishi wakawa wanajitenga kutokana na sehemu zao za kula, kwahiyo wapasua mbegu wakawa wanakaa kivyao na wala wadudu wakawa wanakaa kivyao(kizungu wanaita Niche).

Hii ikapelekea ndege kwenye niche moja kuzaliana na kurithisa tabia na muonekana wa kupasua mbegu na vilevile wale wala wadudu walifanya hivyo hivyo. Ikumbuke kila kizazi kinazidi kutofautiana na kizazi kilichopita kwahiyo kutokana na ushindani wale viumbe waliokuwa wanaweza kupambana ndio walioweza kuishia na kuzaliana (hii inaitwa population pressure which bring survival of the fit enough) ikapita miaka zaidi ya mamilion japo walikuja ndege wa iaina moja kwenye kisiwa baadae wakawa tofauti kabisa kufika hatua wakawa aina ya ndege tofauti(specie) kiasi kwamba hawawezi tena kuzaa (wapasua mbegu walikua hawawezi tena kuzaa na walala wadudu).
Darwin's_finches_by_Gould.jpg

hapo juu ndio ndege niliowazungumzia.

Kwa mfano huo wa juu nadhania umeanza kuelewa maana ya evolution. Ikumbukwe evolution haipangi kuwa hii kitokee huwa anatokea kwa bahati ila natural selection ndio inamalizia kazi ya kuchukua wale ambao wameweza kuhimili mazingira. Kwa kuongezea tuu evolution pia haiweizi tokea kwa kitu ambacho hakipo mfano pundamilia hana mabawa kama ndege hii itampasa pundamilia arudi hatua nyingi nyuma za kievolution afikie ile hatua ambapo zebra na ndege walishare mzee wao mmoja(so evolution has no reverse).

Mfano wengine ni kati ya mwanaume na mwanamke wanaume hawahitaji maziwa ila yapo hii inatokana na gharama ya kutengeneza gene inayoondoa maziwa kwa mwanaume kuwa kubwa sana na vilevile jinsi ya ovary zinabadilika kuwa pumbu na kinembe kuwa uume (Nimetumia mfano wa mwanaume kutokea kwa mwanamke , kwasababu binadamu wa kwanza kinadharia na kiushahidi alikua mwanamke).
Kwahiyo cha kuchukua kutoka hapo juu kabla hatujaendelea mbele ni evolution hutokea kwa bahati(bila mpangilio) ila inapangwa vizuri na natural selection, pia evolution hairudi nyuma(kama yanga nyuma mwiko😂🤣😂) .

Mpaka sasa nahisi utakuwa umeshanielewa mambo ya kuhusu evolution na natural selection sasa tunaweza kuikabili nadharia ya asili ya mwanadamua. Kabla hatujaenda mbali nataka kukusihi ufute ile picha uliyosoma sekindari na shule ya msingi kama sisi tumetokana na sokwe na evolution of a man/evolution ni kama mstari mmoja
wrong_evolution.png

Hii picha ya juu imetumika kuchanganya watu wengi ulimwenguni japo ilitumika kurahisia maelezo . Kwahiyo chukulia asili ya binadamu na mabadiliko yake kama picha hapo chini.
man_tree.jpg

Binadamu anatoka na genus Homo na specie Sapiens, japo sisi ndio specie iliyobaki kwenye genus homo na sisi ni wamisho kufika hapa duniani. Sitoelezea sana jinsi ya sisi imekuwaje tumeweza simama na kuwa na akili hii ianhitaji uzi wake maalumu.
Tuje sasa kwenye mada yenyewe kwanini mwafrika ni mweusi na wengine ni weupe na kwanini nchi zinazoitwa zina joto hazina watu weusi.

Naomba nikukumbushe tuu kuhusu mutation niliyoelezea hapo kuwa kila kiumbe kanapitia mutation na hizo mutation kama zikitokea kwenye mbegu za uzazi basi sitarithishwa kwa vizazi vijavyo. Binadamu wa kwanza alikuwa mweusi na mpaka sasa mwafrika ni mweusi inatokana na gene moja inayoitwa melanin(gene ni kipande kwenye DNA ambayo ndio inataarifu kiwanda cha kutengeneza protini(ribosome)) hii melanine ndio inatupa dark pigmentation lakini inatumika kuzuia seli za binadamu za ngozi zisiuliwe na UV kutoka kwenye jua , maana miale ya UV huwa zina haribu cell DNA ambayo inaleta leta cancer ndio maana albino huwa wanapata cancer za ngozi kwasababu hawana/haifunguki hii gene ya melanin. Ila pia miale ya jua inatusaidia kutengeneza vitamini D(kwa ajili ya mifupa na meno) kwasababu sisi binadamu hatuna uwezo wakutengeneza vitamini yeyote( sina uhahika labda kuna chache tunaweza tengeneza).

kwahiyo baada ya kungundua umuhimu wa melanin na umuhimu wa vitamini D tuanze sasa safari ya binadamu kubadilika rangi, Kama inavyojulikana binadamu wa kale alikua mtu wa kutangatanga kwahiyo kundi la bindadamu liliondoka huku tanzania(Afrika mashariki) miaka kati ya (10000 - 10000) hiko kipindi bado dunia ilikua na baridi hao watu walipofika bara la ulaya tena hapo caucasus walifanya makazi wengine walisambaa kwenda asia wengine waliingia amerika ya kusini. Ila tutajadili ya hawa wa ulaya kufanya uzi uwe mfupi.

Kama nilivyokwisha kueleza mambo ya evolution na natural selection, tuanze angalia sababu ya kwanza ni uchache wa miale ya jua kwahiyo binadamu wa enzi hizo wakaanza pata tabu kutengeneza vitamini D3 kwaajili ya meno na mifupa nadhani mnajua mtu akiwa na mifupa milaini hawezi kimbia kwahiyo kutafuta chakula kwakwe inakuwa shida (nakukumbusha kiumbe chochote kina kazi tatu kwa mtirirko kuishi kula na kuzaa) kwahiyo watu wenye mifupa milaini walikufa mapema bila kuzaa na vizazi vyao vilipata vurugu lile lile na kwenye meno kama unameno mabovu kupata magonjwa na kushambuliwa na bacteria,virus na vidudu vingine ni rahisi kwahiyo nao walikufa mapema na ikumbukwe kibogoyo hali nyama (enzi hizo binadamu alikua hajagundua kilimo so chakula ni nyama au matunda).

Ikumbukwe evolution haisimami kwahiyo katika wale waliofika ulaya wakazaa watoto ambao ni weupe wao ikawa rahisi kutumia miale hafifu ya jua la ulaya kutengeza mifupa yenye nguvu kwahiyo waliweza kupata chakula na wao wakazaa watoto walirithisha hizo mitutation za melanin D so baada ya vizazi vingi watu weusi walipotea na wakabaki wazungu hapo tunaona natural selection watu wote unaowaona ni weupe asili yao jua ni hapo Caucasus.

Nikijibu swali la kwanini waarabu hawawi weusi tena , ninakujibu kwa nadharia mbili ya kwanza nilishasema kuwa evolution huwa hairudi nyuma kwasababu ya gharama na yapili inaitwa collective learning hii imesaidia binadamu asibadilike bali aishi na kuyaongoza mazingira yake. Mwarabu mweupe (Ikumbukwe uarabu ni tamaduni na sio race) yupo hapo jangwani si zaidi ya miaka 6000 hii haiwezi mpelekea abadilike haraka na hivyo pia kipindi mwarabu mweupe anaanza tawala hapo mashariki ya kati kilimo kilishagunduliwa na nguo pia zilishagundulia kwahiyo jua halikuweza kumchoma kama vile wazee wake walivyotoka afrika wanatembea uchi. uwezo huu wa jamii kujifunza maarifa kutoka kwa vizazi vilivyopita ndio inaitwa collective learning hii ndio imasaidia binadamu kuweza kupambana na natural selection kwa kiasi kikubwa.

Tuje kwenye civilization hilo ni somo lingine kubwa nimeona nisilijibu kwasasa ila ntabainisha vitu vya kusoma ili uweye elewa . tatufa za sababu kwanini mageuzi ya kiviwanda yalitokea UK na sio china( wakati china ilikua inachimba makaa ya mawe na chuma zamani kukilo uingereza)
NB: Mimi sio mtaalamu wa maswali ya evolution, nimejifunza yote haya kwa kuwa ni udadisi wangu kwahiyo kama kuna taarifa hapo nimeandika sio sahii naruhusu kurekebishwa na kama kuna kitu kinahitaji ufananuzi zaidi naruhusu pia kujaziwa. Elimu ni bahari sayansi haina mwisho hamna kitu sahii milele kwenye sayansi bali sayansi ipo kufichua uongo wa nadharia za huu ulimwengu.
Mimi ni mfuasi wa evolution na natural selection , nameandika hii ili msomaji wangu usipate maswali kuhusu niliyoongea kama nayaamini au nafundisha nisichoamini pia siamini katika mambo ya dini,mizimu,uchawi ,mungu na mashetani yake.
chamwisho kabisa mimi sio mwandishi mzuri nimejitahidi kuandika kwa kiswahili hizi mada ngumu naoma tuvumiliane kwa makosa ya kisafuri na kisanifu.
 
Back
Top Bottom