African Football League Draw: Simba kuanza na Al Ahly

Scars

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
44,384
105,225
Leo majira ya saa 12:30 kwa saa za hapo Afrika mashariki na kati CAF watatoa draw ya makundi kwa timu zinazoshiriki michuano ya AFL.

Ikumbukwe kuwa Simba ndio mwakilishi pekee wa michuano hii kwa hapa Tanzania.
IMG_8390.jpeg
Simba imepangwa kukutana na mabingwa wa Afrika, Al Ahly ya Misri katika michuano mipya ya CAFAfricanFootballLeague itakayoanza mwezi Oktoba mwaka huu.

Simba itaanzia nyumbani katika mchezo rasmi wa ufunguzi, na mechi zitakuwa ni kwa mfumo wa mtoano zikianzia robo fainali.

Matokeo ya droo kwa mechi zote yako hivi:-

Simba vs Al Ahly.
TP Mazembe vs Esperance,
Enyimba vs Wydad AC,
Petro Atletico vs Mamelodi Sundowns

================

Ratiba ya michuano hiyo imepangwa leo Septemba 2, 2023 ambapo Simba inatarajiwa kuanza kwa kuikaribishwa Al Ahly ya Misri, mchezo wa kwanza ukitarajiwa kuchezwa Oktoba 20, 2023 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Michuano hiyo inasimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) pia inatambulika kwa jina la African Football League inashirikisha timu 8, inaanzia hatua ya Robo Fainali ikiwa katika mfumo wa mtoano.

Mechi nyingine za Robo Fainali; TP Mazembe vs Espérance Sportive de Tunis, Enyimba FC vs Wydad Athletic Club, Atlético Petróleos de Luanda vs Mamelodi Sundowns.
 
- Lengo Ni Kuhakikisha Kuw Vilabu vinaweza kujitegemea na Kutengeneza Faida Kupitia Haya Mashindano na Kufanya Vizuri kwenye Mashindano ya Vilabu Duniani
 
Back
Top Bottom