Kwanini si muumini wa Serikali Tatu...

Idadi ya wanaaotaka Tanganyika haina maana, kilicho muhimu ni hoja za wanaotaka Tanganyika kama zina mashiko ukilinganisha na serikali 1 au serikali 2.

Serikali moja ingewezekana kama znz ingatoa kiasi ilichotoa Tanganyika.
Miaka ya 80 znz ukarudisha ilichotoa kutengeneza Tanzania, Tanganyika ikabaki yenyewe ikitegemea kuwa muda utatoa jibu.

Serikali mbili haiwezekani. Wenye kutaka serikali 2 hawana hoja wala takwimu. Wanachokitumia ni kujibu za wale wa serikali tatu. Kuna ushahidi usio na shaka kuwa CCM imeshaunda tume zaidi ya tano na zote hazikuja na jibu la serikali mbili. Sijui hii CCM ya leo inatoa wapi majibu kwasababu wenye CCM walishasema mbili haiwezekani.

Chaguo lililobaki ni serikali 3 ili kila mmoja asimame kwa miguu yake. Kama itawezekana na heri iwe, ikishindikana basi jahazi lipasuliwe.

Serikali tatu inaonekana kama kichaka kwa znz kutaka kile inachokitaka na si kile kinachopaswa kutengeneza muungano . Znz imekuwa na mkono mkubwa kwasababu ndio mtoto pekee anayeongea na baba yake,akitaka pipi na toy anapewa. Mtoto Tanganyika yupo tumboni hana kauli hata kama pipi ziendazo znz ni damu ya mama yake.Sasa arudishwe ili mzazi awangalie kutokana na sifa zao.

Lakini kwanini tupoteze muda kujadili kitu tunachoona sasa hakina uwezekano?
Kwanini tusipasue jahazi kama Sub continent India, Yugoslavia, Snegambia, Ethiopia na eritrea, Misri na Syria ili kila mmoja asimame na nationalism yake?

Kwanini tuwe na muungano wa chuki ambayo sasa ni sawa na ya 'jirani' yetu? Kwanini tusiachane tukiwa na mapenzi na upendo?

Kwanini tusiwe na kura ya maoni kama Puerto Rico, Sudan kusini, Timor, Quebec na Canada ili tufahamu watu wanataka nini bila kuhisi elfu ishirini au milioni moja wanataka nini?
Lini tuliulizwa kama bado tunahitaji muungano?
Endapo hatuhitaji kwanini ukungumizwe vinywani mwetu?
 
mringi ahsante.

kuungana kuwa kitu kimoja imebaki kuwa ndoto. Unapokubali 'ndoa' kila mshiriki anatakiwa atoe au apoteze sehemuili kuwe na maridhiano. Tulikuwa na serikali ya Yanganyika and Zanzibar, tukaenda katika Tanzania bara na visiwani. Znz wakajiondoa katika Tanzania na kuwa znz huku wakiwa na hisa za jina Tanzania.
Leo Watanganyika ndio muungano,wznz hawapo ila tu pale penye masilahi.
Na kuthibitisha hilo ni mara ngapi wamevunja katiba ya muungano?

Tanganyika imebaki yenyewe na sasa inataka irudi rasmi ili nayo ijisimamie kwa mambo yake na si ya wote. Tata ameeleza vizuri sana kuhusu hili. Haiwezekani mznz asimamie shughuli za Tanzania asiyoiamini kuwa ipo.
Akatoa mfano, waziri wa afya anasimamia Tanzania ipi maana znz haipo katika Tanzania isipokuwa jina tu.

Option ya kwanza ilikuwa kuvunja muungano na waliokuwa na uwezo huo ni wznz kwasababu wao wana vyombo vinavyoweza kutekeleza hilo. Mtanganyika ambaye ni Mtanzania hawezi kujivunja (autolysis), lakini kwa kukosa dhamira ya kweli ya kuvunja muungano tuliwaambia wasilete wajumbe wa tume ili iwepo kura ya maoni kwanza.
Wao wakaleta na sasa wanasimamia muungano wa mkataba ambao ni kuhusu jambo moja tu yaani ulinzi na usalama.

Kama ni hivyo basi kuna njia mbili
Tanganyika irudi ili ijadiliane na mwenzake kuhusu hilo ikiwa na hadhi ya kulinda masilahi yake kikamilifu na ijiulize kama kuna haja ya kuwa na muungano wa ulinzi na usalama tu au tunaweza kuwa na MoU ya jambo hilo.
Lau kana haliwezekani basi tuvunje muungano jambo litakaloleta suluhu ya kudumu.

Majadiliano ya Tanganyika na znz yawe kwatika kura ya maoni ambayo ndiyo itatoa uelekeo kama ipo haja ya serikali 3 au tuvunje muungano. Suluhu ya kudumu itapatikana kwa kusikiliza wananchi na si viongozi.

Kura ya maoni inaweza kutupa jibu zuri sana.
 
Haswaaa!
Tuliwaambia mapema akina Warioba wanapaswa kuongozwa na weledi na si wanasiasa.
Hakukuwa na sababu za wao kukubali hadidu za rejea kwasababu tu wamepewa au maslahi.

Nafasi moja imebaki, kwanza kuirudisha Tanganyika haraka sana, na pili kuuliza wananchi kwa njia ya kura ya maoni. Ili kuwauliza wananchi lazima kuwepo na pande mbili sawa ambazo ni SMZ na Serikali ya Tanganyika.
Hilo litajenga legitimacy kama uliyosema.

Baadhi yetu tunasema Tanganyika irudi kwanza.
Hata kwa kufikiria tu vipi leo serikali ya muungao itungiwe katiba wakati Tanganyika haikushiriki katika utungaji wa katiba hiyo?

Mambo yote yaliyopo katika rasimu yana sehemu mbili, kwanza uhalisia kwa vile imefikria mawazo ya SMZ na pili ni hisia kwavile kuna hisia tu za uwepo wa Tanganyika.

Hii maana yake ni kuwa wznz wana uwakilishi, Watanganyika wanawakilishwa na nani?
Nani amekubali kwa niaba ya Watanganyika kuwa jambo abcd lifanywe kwa utaratibu 1,2,3 kama rasimu ibnavyosema?

Baada ya kura ya maoni ambayo Tanganyika itashiriki kama mshirika wa muungano, ndipo mambo muhimu yajadiliwe.Tunaunda nini kwa sababu zipi. Ni dhahiri hadi wakati huo tutakuwa na serikali 2, maswali yatakayofuata endapo itaamuliwa hiyo ya tatu inagharamiwa vipi kwanza kabla ya kuanza kufikiria kugawana nafasi kama wznz na SMZ inavyodai sasa. Narudia wznz na SMZ (Upo ushahidi kuhusu hili usio na mashaka)

Kam hatutaweza kushauriana basi tuvunje jahazi kila mmoja achukue 'time yake'.
Kinyume cha hivyo ni kutowatendea haki Watanganyika ambao hadi sasa hakuna anayesimamia masilahi yao.

Fikiria wznz wanataka muungano wa ulinzi na usalama tu!
Je nani anajua kuwa Mtanganyika ana mahitaji hayo na atakubaliana na hilo tena tukijua gharama zake kubwa. Sasa leo ukitengeneza rasimu bila uwepo wa Tanganyika umeitendea vipi haki?
Kwanini kiwepo kitu kitakachiwabebesha mzigo bila wao kuulizwa.
 

"ndugu yangu sijui ulijifunzia toka wapi hata ukaja na conclusion hiyo. Inawezekana kwa upande wa tanganyika, lakini kwa huku zanzibar tunajielewa fika nini tunakitaka na tuna sababu zetu za msingi tu.

ni tume kwa busara, hekima na uelewa wao ndio wakaja na draft ya serikali tatu. ukweli kwa zanzibar kutokana na meoni yetu tuliyotoa kwa wingi hatujakosa kabisa. tutajisoma hapa sote washirika, je ni kweli tunataka kuwa na muungano wa haki kwa pande zote mbili ama la?"
 
Tiba ni moja tuwe serikari moja tu inatosha Mfano kule USA kuna Nchi 52 lakini serikari ni moja tu na haina kero za Muungano wala Wizara za muungano Cha Msingi ni ZNZ atawale Gavana au Waziri Mkuu na Tz bara atawale Gavana kisha Rais awe Mmoja tu na makamu wake wahamie Dodoma hapo kero na gharama kubwa ya kuendesha muungano ghari Duniani itakwisha .kwani Lengo la Nyerere ilikuwa kuanzisha muungano unaokuwa na kujibadilisha kwendana na wakati yaani kutoka Muungano Analogia wa 1964 na Kuwa Muungano Digtal Kama miungano ya kule UK kwa mama Marikia . Serikari tatu ni njia rahisi ya kuvunja Muungano Ndio Maana wale wasiotaka muungano wanataka serikari tatu ili yaje Kama ya kule URUSI chini Yeltsin au hapo sudan tu kuna vioja lukuki .serikari moja Ndio jawabu la kila jema juu ya muungano Ghari kama huu wetu kinyume na hapo ni Zenji wajiandae Kuwa Raia wa Nchi jirani na watalipia Viza na vibali vya kuishi bara huku Umeme na chakula toka Bara vikilipiwa kwa Dola na Uchumi wa Bara kukua kwa kasi ya ajabu kwani pesa toka hazina haina mgao kwenda Zenji itabakia Bara huku viongozi wakichapa kazi bila stress za kero za muungano .kwa kweli ili Haya yasitokee tunahitaji serikari moja tu
 
Last edited by a moderator:

Serekali moja ipi?mkuu wazanzbr kuufuta uzanzbr eti tu kisa muungano hatupo tayari kwa hilo tena sahau,huku zanzbr ni mamlaka kamili tu,kama mlishindwa kuifuta zbr kwa miaka 50 msitarajie kuifuta kwa kipindi hiki,zanzbr kwanza.
 
Tatizo kubwa tunalolifanya hapa ni kuwasemea Watanzania. Viongozi wetu wame-assume kuwa watanzania wanapenda muungano.


Warioba pia amekuja na assumption hiyo hiyo na kunyambulisha mambo yatakayo kuwa ya muungano na yasiyokuwa ya muungano kwa assumption kuwa watanzania ndio muungano huo wanaoutaka.


Suala la muungano ni suala pana na ndilo limebeba mantiki nzima ya Rasimu ya Katiba.


Ndilo suala kubwa linalo determine muonekano wa Nchi yetu. Ukisoma mawazo ya Nyerere pamoja na kwamba changamoto tunazokabiliana nazo sasa ni tofauti na wakati ule ila Nyerere alikuwa anatutahadharisha tusivunje muungano kwa majibu mepesi mepesi.

Hata sasa bado suala la msingi hatujalijadili. Tusivunje Muungano badaye tukajilaumu. Muundo wowote wa Muungano ufikiwe kwa kuwashirikisha wananchi wa pande zote mbili uwiano ukizingatiwa (percentage of population in each country).


Suala ambalo huwa najiuliza ni Je watanzania wanahitaji muungano? Kwa hali ya sasa Wazanzibar wanalalamika pia waTanzania bara wanalalamika. hata wakati mwingine na viongozi wa pande zote mbili wanalalamika. Kwa hali hii kama unahitajika basi inatakiwa wananchi waelimishwe vya kutosha.

Je umuhimu wa muungano ni nini?
Je ni kwa ajili ya Ulinzi na Usalama, kwa ajiri na mambo ya Kiuchumi, Je ni kwa sababu tumeisha oleana (Kijamii) nk!

Hili suala likipata jibu linaweza kutusaidia hata kujua kama tunahitaji kuwa na serikali moja, mbili au tatu (kulingana na uzito wa umuhimu wake). Na pia litasaidia kujua ni vitu gani viwe vya muungano na vipi visiwe vya muungano.


Kwa kifupi tunahitaji kura ya maoni juu ya muungano kabla ya kuandika katiba mpya . Huwezi kuamuka tu unaungana na jirani yako bila kujua kwa nini munaungana.


Bila kujibu suala hili Muungano wa kulazimisha nchi mbili hautafika mbali. Utakufa tu! Viongozi wasilazimishe katika suala hili.
 
Serekali moja ipi?mkuu wazanzbr kuufuta uzanzbr eti tu kisa muungano hatupo tayari kwa hilo tena sahau,huku zanzbr ni mamlaka kamili tu,kama mlishindwa kuifuta zbr kwa miaka 50 msitarajie kuifuta kwa kipindi hiki,zanzbr kwanza.
Una uhakika na unachosema kuhusu kuifuta?
 
MMKJ. Ni au tunakuwa na serikali moja na majimbo au tuuuvunje muungano..period .. Tofauti na hapo tunatafua kuuvunja muungano kwa njia ndefuuuuu!!!!!!!!!
 

Yan pamoja na maelezo marefu hapo juu HAYA NDO MaWazo yako?nnamashaka na kiwango chako cha ufaulu darasani...ni watu kama nyie tu msiotofautishwa na mbuzi wakat gitaa likipigwa.
 
Serekali moja ipi?mkuu wazanzbr kuufuta uzanzbr eti tu kisa muungano hatupo tayari kwa hilo tena sahau,huku zanzbr ni mamlaka kamili tu,kama mlishindwa kuifuta zbr kwa miaka 50 msitarajie kuifuta kwa kipindi hiki,zanzbr kwanza.
Yap ni kuifuta,zanzbr kutoka empire mpaka sasa mkoa,inatosha kwa sasa tuachiwe tupumue,zanzibr kwanza.
Unauhakika unajua unachoongelea? Huu uzi ni mkubwa nakusihi uache kuuchafua, utendee haki yake.
 
Mzee Mwanakijiji, Kobello, na wengine wote mnaopendelea serikali moja:Kwanza niseme kwamba kwa kweli tupo wengi sana tunaopendelea Tanzania ifuate mfumo wa serikali moja lakini nadhani tofauti yetu na yenu zipo katika maeneo makuu mawili: ·

Kwanza, kwa upande wetu, tunaangalia zaidi 'practice' kuliko 'theory', na katika hili, tunaona wale wote wenye kupendelea mfumo wa serikali moja katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni ‘wishful thinkers'.
·

Tofauti ya pili baina yetu na nyie ni kwamba, mnapendelea Zanzibar to ‘sacrifice' na kukubali serikali moja, bila ya kujalisha kwamba kwa kufanya hivyo kutaongeza kero zaidi muungano zilizopo sasa.


Ukweli utaendelea kubakia kwamba – kama kung'ang'ania mfumo wa serikali mbili ndio imekuwa ndio chanzo cha kumuacha mgonjwa (muungano) kwenye ‘coma' kwa miaka 50, basi mfumo wa serikali moja utakuwa ni msumari wa mwisho katika jeneza la mgonjwa huyu ambae yupo mahututi kwa miaka hamsini. Tumekuwa tukijadili kwa takwimu na kila namna kwamba njia pekee ya kumwokoa mgonjwa huyu ni kwa kufuata mfumo wa shirikisho la serikali tatu kama ilivyodhamiriwa chini ya mkataba wa muungano (1964) – serikali ya kwanza ikiwa ile itakayo simamia masuala ya Zanzibar ambayo yapo nje ya muungano; serikali ya pili ikiwa ni ile itakayosimamia masuala ya Tanganyika ambayo yapo nje ya muungano, na serikali ya tatu ikiwa ni ile itayayosimamia masuala yaliyokubaliwa na pande zote mbili kwamba yawe ndio ya kushirikiana/muungano, ambapo tume ya warioba imependekeza yawe maeneo saba tu.


Tutazungushana sana kwa hoja lakini ukweli utaendelea kubakia kwamba, iwapo nia yetu ni kuendeleza muungano, hasa kwa kurekebisha kasoro zilizolelewa na CCM kwa miaka karibia 50, tumebakiwa na OPTION moja tu ambayo ni:
· Kuhakikisha kwamba there is considerable devolution of power to state governments (Tanganyika & Zanzibar) and in which the people of both sides will be able to exercise considerable and significant autonomy and power. Tumewasilisha hoja zetu nyingi sana juu ya faida za mfumo wa aina hii vis a vis unitary government lakini for some reasons, upande wa pili wa hoja bado upo nyuma.

Mkuu Mzee Mwanakijiji, Kobello na wote wenye mapenzi na mfumo wa serikali moja, ni muhimu mkumbuke kwamba iwapo wazo la serikali moja lilionekana sio la busara siku ya muungano Aprili 26, 1964, katika kipindi ambacho kulikuwa na uwanja na fursa nyingi for experimentation kutokana na dunia kugawanyika katika makundi mawili makubwa kufuatia ‘Cold War', this idea (serikali moja) is even less of an option nyakati hizi/miaka hamsini baadae. Tuachane na nadharia, badala yake tuangalie practicality za mifumo tunayoijengea hoja:
· Hakuna upande wa muungano (sio Tanganyika wa Zanzibar) ambao upo tayari to dissolve their separate identities and autonomy. Tukianza na Zanzibar, under any unitary system tunayoipigia debe, however constructed, Zanzibar itapoteza its autonomy kwa kiasi kikubwa sana. Na hii hoja ndio ilipelekea mwalimu akatae wazo la Karume la mfumo wa Serikali moja, 1964. Tukija upande wa mshirika wa pili wa muungano (Tanganyika), ambae ni bigger partner, under any unitary system tunayoipigia debe, however constructed, mshirika huyu (Tanganyika) ataishia pia kuwa ni dominant partner. Na kama tunavyoelewa, manung'uniko ya upande wa Zanzibar wakati wote yamekuwa kwamba – mfumo uliopo (unitary system), has taken their autonomy away ‘constitutionally', na kutishia Zanzibar kuelekea kuwa kama ni ‘manispaa' ndani ya muungano. Sasa kwanini tupendeleze hali hii wakati in our sober minds tunaelewa fika kwamba, kabla ya muungano, kama ilivyokuwa kwa Tanganyika, Zanzibar pia ilikuwa ni dola huru? Isitoshe, tofauti na Tanganyika ambayo ilijipatia uhuru wake kwa majadiliano huku washiriki wakiwa wamevaa suti wakinywa kahawa na biskuti kule Lancaster hall, uhuru wa wazanzibari ulipatikana mitaani kupitia umwagaji mkubwa wa damu. Tusifanye mzaha na cultural and historical national identities.

Kobello, katika nyakati hizi za democratic devolution of power and resurgence of various expressions of identifies, sio tu kwamba mergers of nations/countries is hardly desirable, pia ni vigumu sana kujadilika na kufikia muafaka towards that end. Various forms of unity between and among countries barani afrika zinawezekana bila ya kulazimika to resort to mergers and the dissolution of cultural and historical national identities. Mzee Mwanakijiji, nadhani unakumbuka kwamba ni Nyerere mwenyewe in the 1960s ndiye aliyepingana na Vision ya Kwame Nkrumah kuhusiana na serikali moja ya Afrika. In the short run, Mwalimu alionekana kutokuwa na vision yenye manufaa kwa afrika zaidi ya Nkrumah, lakini kupitia practice (tofauti na theory ya Nkrumah), in the ling run, Vision ya Mwalimu Nyerere ikawa ndio yenye mashiko.
Vinginevyo sio kweli kwamba Mwalimu alipendelea mfumo wa serikali moja. Vile vile, hakupendelea mfumo wa matangamano ya majimbo bali mfumo wa shirikisho. Kwa mfano, kupitia OAU, Mwalimu Nyerere alithibitisha haya kwa maneno yake mwenyewe huku akiwa na hamasa kubwa juu ya mfumo wa shirikisho barani Afrika kwamba - mfumo wa serikali moja au mfumo wa tangamano la majimbo usingefaa katika mazingira ya Kiafrika; Mwalimu Nyerere alitoa waraka mrefu ambao pia ulipatiwa fursa ya kuchapishwa kwenye African Forum, ambapo alisema yafuatayo [Source: Julius K. Nyerere: The nature and requirements of African Unity" Katika African Forum Vol 1, Na. 1 (1965), ukusara 46. Kwa makala yote, soma kurasa 38 – 52]:

Dhana hii ya Mwalimu juu ya mkataba wa muungano wa shirikisho pia inathibitishwa na makala moja ya gazeti la Observer la Uingereza toleo ya Aprili 20, 1964 ambapo Nyerere alinukuliwa akisema:
Iwapo umma wa Zanzibar bila ya ushawishi kutoka nje, na kwa sababu zao wenyewe, wataona kuwa muungano una hasara kwa uhai wao, sitowapiga mabomu kuwalazimisha. Muungano utakuwa hauna tena sababu ya kuendelea iwapo washiriki wake wataamua kuukana
.


Suala la pili ambalo ningependa kulijadili linahusiana na hoja yako nyingine ambayo kwa kiasi Fulani ni kama ina ‘question' integrity ya tume ya warioba kuhusiana na hoja ya Serikali TATU". Nadhani kuna umuhimu wa kuitendea haki tume ya jaji warioba, hasa kwa kutumia muda wetu kidogo kutafiti ni wapi wametoka na hoja husika. Mzee Mwanakijiji, kuhusiana na pendekezo la mfumo wa shirikisho la serikali tatu, Tume ya Jaji Warioba haijabuni kitu chochote kipya zaidi tu ya kurejea katika makubaliano ya awali baina ya waasisi wa muungano - Mwalimu Nyerere na Mzee Karume. Tume ya warioba imetambua kwamba miaka hamsini ya muungano imezaa kero na manun'guniko kuliko faida na mafanikio.
· Sasa inakuwaje leo tuanze kumshutumu Jaji Warioba na tume yake wakati wanachofanya ni kurekebisha makosa yaliyojitokeza kufuatia uchakachuaji wa mkataba wa muungano (1964) kwa karibia miaka 50?

Issa Shivji (PhD, University of Cambridge, UK), ni miongoni mwa constitutional lawyers wanaoheshimika sana barani afrika. Katika moja ya kazi zake (see let the people speak: Tanzania down the road to neo-liberalism) anasema kwamba (uk 90):

"The Acts of the union were the first union constitution"
·

Je hauoni kwamba hii ndio mantiko iliyotumiwa na tume ya warioba? Mkataba wa muungano (1964) uliotiwa sahihi na Mwalimu Nyerere na Mzee Karume, unaanza kwa kusema yafuatayo:

MKATABA WA MUUNGANO Baina ya JAMHURI YA TANGANYIKA
Na JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR
·

Je: hapa hatuoni kwamba kabla ya tarehe ya muungano (Aprili 26, 1964), Tanganyika na Zanzibar zilikuwa ni dola mbili huru zenye mamlaka kamili ndani ya mipaka yake? Sasa kwanini iwe ni makosa kwa tume ya Warioba kuzingatia ukweli huu kama njia ya kurekebisha mapungufu ya muungano wetu? Mkataba wa muungano unaendelea kusema yafuatayo:


Kufuatia maneno haya, je hauoni kwamba hoja yako ifuatayo inajichanganya?
…tunapinga kwa sababu ya mantiki nzima ya kuwa na serikali tatu na nchi mbili! lakini wenzetu wanataka tuwe na nchi mbili na serikali tatu!


Mzee mwanakijiji, tusichanganye baina ya dhana ya ‘nchi' na dhana ya ‘serikali' tunapojadili mfumo wa utawala ndani ya muungano wa nchini mbili. Serikali tatu ndani ya nchi mbili maana yake ni rahisi sana kuelewa:
· Nchi mbili zinapoungana, nchi hizi zinakuja na serikali zake ambazo idadi yake huwa sio chini ya serikali mbili. Kinachofuatia ni makubaliano juu ya masuala yepi yawe ni ya kuungana na kuyaendesha chini ya serikali ya pamoja, na masuala yepi yaendelee kusimamiwa na serikali shiriki, kila serikali kivyake. Kweli Mzee Mwanakijiji huoni mantiki hapa? Tunachojadili hapa ni muungano wa viongozi wa serikali mbili (1964) ambapo masuala ya kushirikiana yalikubaliwa yawe kumi na moja tu. Nje ya masuala haya, ina maana kulikuwa na haja na pia ulazima wa kuwepo kwa serikali nyingine mbili za kusimamia masuala yaliyo nje ya muungano (masuala ya Tanganyika na masuala ya Zanzibar). Sasa msimamizi wa masuala haya huwa sio NCHI bali SERIKALI. Nadhani unajichanganya unapotumia dhana ya "nchi" badala ya dhana ya ‘serikali' katika kujadili mfumo bora wa utawala, kwani ni serikali ndio huwajibika kwa wananchi, sio nchi;

Tukirudi kwenye Mkataba wa Muungano ambao ndio precedence ya hoja ya Tume ya Warioba, Mkataba huo unaendelea kusema hivi:

NA KWA KUWA Serikali za jamhuri ya muungano wa Tanzania na Jamhuri ya watu wa Zanzibar zinapendelea ya kwamba jamhuri hizi mbili ziungane kuwa jamhuri moja huru kwa masharti yafuatayo:

Mzee Mwanakijiji, nadhani unaelewa kwamba sababu kubwa ya kuyumba kwa muungano nini kutokana na ukiukwaji wa makubaliano yote hayo hapo juu, kwani muda mchache baada ya mkataba kutiwa sahihi (1964), kilichofuatia ikawa ni uchakachuaji wa mkataba husika, kwa kuanzia na Katiba ya muda ya JMT (1965), na baadae katiba ya kudumu ya JMT (1977). Kwa mfano ukiangalia Katiba ya sasa ya JMT (1977), utaona yafuatayo:

Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano. 2.-(1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo.
· [FONT=&quot [B]Mzee Mwanakijiji[/B] hauoni tatizo hapa? Kiini cha mgogoro kinaendelea kuwa ni Katiba ya JMT (1977), tofauti na wanasiasa wanavyopenda tuamini kwamba mgogoro ni matokeo ya chuki ya watanganyika kwa wanzazibari au chuki ya wazanzibari kwa watanganyikai. Chuki zilizopo ni matokeo ya mapungufu yaliyojitokeza kwa miaka karibia 50. Ni kwa mantiki hii, rasimu ya katiba ikaja na pendekezo la mfumo wa shirikisho la serikali tatu. [/FONT] Kama nilivyojadili awali, Rasimu ya katiba haijaja na kitu kipya, badala yake imerejea mkataba wa (1964) ambapo Rasimu inasema hivi:

Tuzidi kujikumbusha maneno ya issa shivji kwamba:
"The Acts of the union were the first union constitution"


Nikiingia kwenye hoja yako nyingine, kuna sehemu unamnukuu Mwalimu Nyerere kama ifuatavyo:

Mkuu Mzee Mwanakijiji, nadhani unaelewa kwamba suala la muungano halikuwa ni suala la vyama vya siasa. Kama utakubaliana nami katika hili, basi hoja nzima ya Mwalimu inakosa mashiko from the outset, na kuishabikia ni muendelezo wa uchakachuaji wa mkataba wa muungano (1964). Suala la Muungano halikuwa ni suala la Vyama Vya Siasa, na hakuna hata sehemu moja ndani ya mkataba wa muungano (1964) ambayo inataja maneno ‘chama/vyama vya siasa' au majina ya ‘TANU' au/na ‘ASP'. TANU ilianza kujipenyeza katika suala la muungano muda mchache baada ya mktaaba wa muungano kusainiwa, na kukolea zaidi kupitia katiba ya Muda (1965) wa miaka 13 - kinyume na mkataba wa muungano kwani kwa mujibu wa mkataba, mchakato wa katiba ya kudumu ya JMT ulitakiwa uanze ndani ya kipindi cha miezi kumi na mbili i.e. kabla ya Aprili 26, 1965. Kilichofuatia 1965 ni Katiba ya muda iliyokuwa inasubiria mahari kwa ajili ya ndoa ya TANU na ASP yatimie. Pia kuna sehemu unasema kwamba:
Na maneno haya ya Nyerere yasikike kwenye masikio yaliyoziba ya watawala wetu walioshindwa!


Ambapo unamnukuu mwalimu kama ifuatavyo:


Mzee Mwanakijiji, naomba niulize tena:

  • Je, ni wapi katika mkataba wa muungano (1964) panaposema kwamba Muungano ni suala la Vyama vya siasa?
  • Pia je, kwanini unapenda kujadili kugawa madaraka kwa serikali tatu as if it is synyomous to dividing the country into pieces?

Kuna sehemu unajadili kwamba:
Serikali tatu haitotatua matatizo ya Muungano itayaongeza tu.
· Sisi tumejadili kwa kina juu ya kero zilizopo na kwanini serikali tatu itazitatua kero husika; Kwanini nyinyi hamji na hoja kujadili matatizo yaliyopo kwa miaka karibia 50 sasa, yatatatuliwa vipi na mfumo wa serikali moja? Vinginevyo kuna mjadala nilianzisha siku kadhaa zilizopita ambapo nilijadili kwa kina kwanini shirikisho la serikali tatu litaleta ufanisi zaidi kisiasa, kiuchumi na kijamii kuliko unitary system mnayoipendelea. Unazidi kusema kwamba:
Tunaopinga serikali tatu hatupingi kwa sababu ya gharama tu, hili ni jambo dogo zaidi…
Nafarijika kuona unakubali kwamba suala la gharama ni jambo dogo zaidi. Naomba nisisitize kwamba lets focus on efficiency ya mfumo - politically, socially and economically kuliko kuweka focus kwenye gharama kwani as long as kuna efficiency, costs will always be justified. Mataifa makubwa kama marekani na mengineyo yanafanya mambo mengi sana ndani na nje ya mataifa yao kwa gharama kubwa lakini mwisho wa siku, as long as kuna ufanisi kisiasa, kiuchumi na kijamii, walipa kodi always wanakuwa tayari kubeba gharama husika. Nina uhakika kwamba hata kwa Tanganyika na Zanzibar, this argument prevails.

Cc Nguruvi3, Jasusi, joka kuu, Pasco, MTAZAMO
 
wale wote waliofaidi na wanaofaidiki muundo wa serkali 2 hawatapinga kamwe serkali 2. mi nawashangaa eti serkali tatu muungano utavunjika mara ni gharama najiuliza kwanini serkali 2 hazijafanya? hamuoni sasa kuwa na serkali 2 ni sawa na kutokuwa na kiranja na hivo kifo kiko wazi? sewrkali tatu itaimarisha muungano na kuleta nidhamu kwa serkali ya muungano ambaye ndiye MSIMAMIZI MKUU AWA SERKALI 2 ZILIZOPO. KWANI KWA SASA SERKALI 1 IKO JUU YA NYINGINE AU? NI HILI NDO LINALOLETA SHIDA KUWA ZANZIBAR WANASIMAMIWA NA TANGANYIKA KAMA HAJAJUA KWAHIVYO SULUHU NI KUWA NA SERKALI TATU MOJA IKIWA JUU ZILE 2 ZIKIWA CHINI YAKE. HAMUELEWI NINI CCM. SASA MJADALA WA KATIBU ULIKUWA WA NINI? ACHENI UKIGEUGEU MLIFIKIRI RAHISI NYO
 
Last edited by a moderator:
wale wote waliofaidi na wanaofaidiki muundo wa serkali 2 hawatapinga kamwe serkali 2. mi nawashangaa eti serkali tatu muungano utavunjika mara ni gharama najiuliza kwanini serkali 2 hazijafanya? hamuoni sasa kuwa na serkali 2 ni sawa na kutokuwa na kiranja na hivo kifo kiko wazi? sewrkali tatu itaimarisha muungano na kuleta nidhamu kwa serkali ya muungano ambaye ndiye MSIMAMIZI MKUU AWA SERKALI 2 ZILIZOPO. KWANI KWA SASA SERKALI 1 IKO JUU YA NYINGINE AU? NI HILI NDO LINALOLETA SHIDA KUWA ZANZIBAR WANASIMAMIWA NA TANGANYIKA KAMA HAJAJUA KWAHIVYO SULUHU NI KUWA NA SERKALI TATU MOJA IKIWA JUU ZILE 2 ZIKIWA CHINI YAKE. HAMUELEWI NINI CCM. SASA MJADALA WA KATIBU ULIKUWA WA NINI? ACHENI UKIGEUGEU MLIFIKIRI RAHISI?
 
Last edited by a moderator:

Kwa kuanza tu, labda sijaelewa unapomaanisha kuwa wengi wetu tungependa muundo wa muungano wa serikali moja. Wengi wetu kina nani?

kama unazungumzia watanganyika, basi ina maana kuwa watanganyika wengi wangependa zanzibar iwe annexed. Kwanini wasipende Rwanda au Burundi ziwe annexed pia? Kuna manufaa gani au undugu gani kati ya mhangaza wa Kagera na Mkojani wa Pemba? Huo ukaribu sidhani kama ni mkubwa kulinganisha na watutsi wa Rwanda, au kati ya Waha na wahutu wa Burundi.

Nimetoa mifano hiyo nikitaka kukusisitizia kuwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar umetokana kwa kiasi kikubwa na matakwa ya Serikali ya Mapinduzi Ya Zanzibar na siyo serikali ya Tanganyika. Kwa hiyo unaposema wengi wetu tungependa serikali moja, unaashiria kuwa watanganyika wengi wangependa serikali moja, na kwa kuwa wazanzibari hawapendi kuupoteza "utaifa" wao hili jambo ni almost impractical, but it's the only sensible way.

Nia yetu si kulinda muungano, bali kuilinda katiba yetu ambayo inafuata misingi ya haki na Demokrasia. Kwa hiyo tutapiga longolongo miaka nenda, miaka rudi lakini ukweli ni kuwa muungano uliopo ambao wanaotaka serikali tatu wanajaribu kuuokoa, siyo tu kwamba haujafuata misingi ya haki, bali misingi ya demokrasia pia.

Foundation ya muungano huu ambao tunapigania kuutunza tayari ni weak na kinachotakiwa sasa hivi ni kurudi kwenye drawing board na kupata ridhaa ya wananchi wa pande zote mbili.

La sivyo, serikali ya muungano haitakuwa na nguvu yeyote katika suala lolote litalohusu serikali yeyote. Serikali kuu haitakuwa na mamlaka ya kugawa majimbo, haitakuwa na madaraka ya kudhibiti mfumo wa kiuchumi na kimaisha wa serikali yeyote ile, kwa mfano Zanzibar ikiamua kuwa na serikali ya kifalme inayofuata "Sharia", serikali kuu haiwezi kufanya lolote, na watanganyika sidhani kama wapo tayari kuupa ulinzi na usalama serikali ya kifalme ambayo imewekwa kidemokrasia.

Tanganyika ikitaka kujenga bomba la gesi kwenda malawi au Zambia, jambo hili litatakiwa lithibitishwe na likubaliwe na serikali kuu kwanza kwa sababu litakuwa ni jambo litaloathiri Jamhuri ya muungano na siyo Tanganyika peke yake ... Je, watanganyika watakuwa tayari kupangiwa na wazanzibari vyanzo vya mapato yao? Kwa sababu kimazingira, bomba la gesi likivuka mpaka, ni issue ya Jamhuri ya Muungano. Je, Zanzibar wakijenga bomba la gesi kwenda Mombasa, na wabunge wa Muungano kutoka Tanganyika waka-Veto ... patakalika?

Homogeneity nature ya wazanzibari, hili pia ni suala linalotakiwa kuangaliwa kwa undani zaidi. State kama hizi zinahitaji strong central government ili kulinda haki za minorities. Zanzibar haipo mixed kama Bara na kuungana na state ambayo composition yake socially haifanani na nyingine huwa kunaleta chaos kama central government inakuwa haina nguvu.

Kwa kifupi, central governments kwenye unions zilizofanikiwa inabidi itumie Carrot and Stick approach. Most of the times Carrot huwa ni assurance of power holding while the stick ni revenue cut au central policy execution by the sub national government. Sasa kwa central government iliyopendekezwa na Warioba, naomba uniambie what's the carrot and whats the stick and how big and long are the carrot and stick respectively?
 
hivi jamani kuna haja gani ya kugombana au kuchukiana wakati kila mtu anahaki ya kutoa maoni yake?then hizi habari za nyerere kasema,,nyerere kasema itakua mpaka lini?mambo yamebadilika sana,,na lazima tuende na mda,,mbona hatutumii kauli zake katika kutokomeza rushwa?au madawa ya kulevya?
mchakato wa uundwaji katiba mpya ndio unaendelea tusubiri tupige kura za maoni then tutajua
 
Mchambuzi; nimekusoma vizuri sana na kurudia mara kadhaa kukusoma tena na kukuelewa kabisa. Bahati mbaya naamini kuwa hoja yako imejengwa bila kuzingatia tatizo kubwa sana la Muungano katika mfumo wa sasa na hata ukiwa katika serikali tatu - Zanzibar haitaki kuacha kuwa nchi. Tulipoungana - na umeeleza vizuri - tuliunganisha nchi mbili kuunda nchi moja. Ni kwa sababu hiyo Katiba ya Muungano inasema hivi katika Ibara ya Kwanza kabisa:

Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano

Rasimu ya Katiba ya sasa haiitangazi nchi itakayozaliwa kuwa ni nchi moja; as a matter of fact inasema kitu cha ajabu sana; inasema:

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Shirikisho lenye
mamlaka kamili ambayo imetokana na Muungano wa nchi mbili za
Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambazo kabla
ya Hati za Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 zilikuwa nchi
huru.

Magenius wetu wameshindwa kutangaza hilo shirikisho ni nchi; na nitakuambia kwanini. Kwa sababu mbeleni wanataka kuirudisha Tanganyika!

Kwanini hili ni muhimu? Well, Zanzibar haitaki kuacha kuwa nchi na tayari inadai mamlaka zaidi na zaidi ya kama nchi huru inayojitegemea. Tena wapo Wazanzibari wengi ambao wanaamini kabisa kuwa katika Muungano wa 1964 Zanzibar haikufa kama nchi isipokuwa Tanganyika tu. Sasa watu wengi wanaona kuwa ilikuwa ni kosa kwa Tanganyika kupotea na Zanzibar kubaki lakini hawaoni kuwa lilikuwa kosa kubwa kwa Zanzibar na yenyewe kutokufa! Ni kwa sababu hiyo watu wameamini kuwa kwa vile Zanzibar ipo "basi" Tanganyika nayo iwepo.

Sasa kinachorudishwa katika "serikali tatu" ni nchi ya pili! Hairudishwi serikali! Inarudishwa nchi inaitwa Tanganyika halafu hiyo nchi itakuwa na serikali yake "kama" ilivyo Zanzibar! HIvyo, kutakuwa na nchi mbili zinaunda shirikisho! NI kwa sababu hiyo shirikisho siyo nchi moja tena bali ni nchi mbili zenye serikali tatu! Serikali ya Nchi ya Zanzibar (ambayo bado ipo) na serikali ya nchi ya Tanganyika (ambayo itarudishwa) na serikali ya ushirikiano (Shirikisho) ambayo kwa kweli itakuwa na madaraka lakini haitokuwa na eneo au nchi - haijalishi Katiba inasema nini.

Nimesema haitakuwa na eneo au nchi kwa sababu kama Zanzibar katika Katiba yake inasema hivi (Ibara ya Kwanza):

Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la
Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka
na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

Sasa, sote tunakumbuka mjadala wa "Zanzibar ni nchi au si nchi"? Kikwete alikoroga zaidi kwa hotuba yake Bungeni alipogusia hili aliposema mojawapo ya vitu vya ajabu kabisa kusemwa na Rais wa Tanzania; kuwa "Zanzibar ni nchi ndani ya Jamhuri ya Muungano". Ukikubali hoja hiyo ya Kikwete - na kwa kweli inatokana na ukweli wa hali ilivyo - ni lazima ukubali kuwa kurudishwa kwa Tanganyika kutafanya kuwe na nchi ya Tanganyika "ndani ya Muungano" na hivyo Muungano utakuwa na nchi mbili. Zikifanya mambo yote ya ndani kama nchi kamili lakini kwenye mambo yale saba yanayopendekezwa na kina Warioba basi ndiyo yatakuwa chini ya Jamhuri ya Muungano!

Sasa ndugu yangu Mchambuzi; serikali tatu inatokana na ukweli kuwa tunataka kurudisha nchi ya Tanganyika. Sasa sina tatizo na kurudishwa kwa Tanganyika lakini ukiirudisha Tanganyika kama nchi NI LAZIMA uwaulize wananchi waka kama Wanataka Muungano na Zanzibar! Huwezi kurudisha nchi ya Tanganyika halafu uwasukumize kwenye Muungano na nchi nyingine ... Zanzibar.

Sasa ili tuzungumzie 'serikali tatu' ni lazima tuamuze kama Zanzibar itaendelea kuwa nchi baada ya shirikisho au la; kama watakuwa tayari kufuta hiyo ibara waliyoibadilisha 2010 ili wasema kuwa wao ni "sehemu" ya Jamhuri ya Muungano. Unafikiri Wazanzibari watakubali? Au Watanganyika tukubali kusema sisi ni "sehemu" ya Jamhuri ya Muungano bila kujitaja kuwa na "sisi" ni nchi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…