Ng'wamapalala
JF-Expert Member
- Jun 9, 2011
- 6,811
- 6,506
Hajabadilisha "kauli mbiu" yake LET ZANZIBAR GO! amekuja kivingine tu.My perceptions ni kuwa Mwanakijiji ni mmoja kati ya watu ambao wanapenda muungano uvunjike ndio maana kaja na hoja ya serikali moja.
Huyu Mtu wa Pwani hana hoja ni wa kumwacha.Naona unashindwa kutetea hoja zako na kuanza kung'ang'ania kitu ambacho ni tofauti na kinachoongelewa hapa.
EAC SIYO SHIRIKISHO!
Sifa za shirikisho la kisisa
1. Ngazi mbili za serikali zinazoongoza watu na ardhi moja. Na,
2.Kila ngazi ya serikali ina suala angalau moja ambalo ina uhuru kamili wa kujiamulia, na
3.Kuna uhakika kikatiba na uhakika huo ni guaranteed kuwa uhuru huo unaweza kutekelezwa kwenye eneo la ardhi/mipaka ya ngazi moja ya serikali.
Muhimu zaidi ya yote hayo, ngazi. Ngazi inamaanisha eneo moja yaani serikali moja ni ya juu zaidi ya serikali nyingine. Lazima kuwe na katiba ambayo ni ya juu ya katiba nyingine.
KATIBA YA EAC, KAMA IPO AU ITAKUWEPO .... HAINA NGUVU JUU YA SUALA LOLOTE KWA SERIKALI YEYOTE. Kwa kifupi haina maana na hatuna haja ya kuisikia hapa.
Tena ikifika wakati wa suala la muungano hata wasomi wanakuwa na akili za ajabu sanaHizi sintofahamu zote zinakuja kwa sababu tulichagua njia isiyo sahihi katika safari yetu ya kuutafuta utaifa na mshikamano ambazo ndiyo nguzo za Muungano.
Kwa sasa tuko katikati ya safari tunashindwa kuamua kama tuendelee na safari au turudi mwanzo.
Ni vigumu sana kurekebisha jambo la kisiasa ambalo mwanzo wake ulifanyika kimakosa. Hiki ndiyo tunachokiona kwa sasa.
Kama Tume ya Jaji Warioba isingekuwa imefungwa na hadidu za rejea kuhusiana na Muungano, basi ninatumaini tungekuwa kwa sasa tunafahamu nini wananchi wanataka kuhusu hili 'dudu' muungano kwa ustawi wa 'mataifa' yao. Kitu cha kushangaza kwa sasa tunasema tunataka serikali tatu wakati hata hiyo serikali ya pili haijulikani muundo wake na hata wananchi wake sijui wanaishi wapi.
Kura ya maoni ndiyo mzizi wa fitina na kuwepo kwanza kwa nchi ya pili ndiyo mwanzo wa usawa katika kutafuta political legitimacy kwenye negotiation table.
Serikali tatu kwenye political environment hii iliyopo ni hukumu ya kuvunja muungano lakini katika gharama kubwa ambayo ingekuwa offset na kura ya maoni.
Ukimsoma Baba wa Taifa ukamwelewa vizuri utashangaa jinsi tunavyofikiri sasa!! Mwalimu alikuwa anajadili muungano bila kujifunga na serikali mbili tu lakini unaona anashangaa wanaong'ang'ania serikali tatu bila kujadili alternative zingine tena bila majadiliano rasmi kuhusu aina zingine zote za muungano kabla hatujasimama na kutaka serikali tatu tu ambayo inakwenda kuvunja muungano taratibu.
Natamani kuona maoni ya wanasiasa wa sasa hasa kwa kupangua hizi hoja za Mwl Nyerere zilizowekwa hapa (maana wote wanataka serikali tatu).
CC Zitto , John Mnyika , Wilbroad Slaa , Nape Nnauye , Tundu Lisu bila kumsahau Mchambuzi
Mwanakijiji kwanza nataka nikuulize maswali yangu ukiyajibu utakuwa umenishawishi nikubaliane na hoja yako.
1. Kwa nini mpaka sasa kuna serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati Katiba ya Tanzania inasema Tanzania ni nchi moja
2. Kwa nini wanasema Zanzibar ni nchi katika katiba yao ya Zanzibar
3. Kwa nini wana wimbo wa taifa, wa bendera, wana Majeshi yao na Rais wao ni Amrijeshi wa majeshi hayo.
4. Kwa nini Wao Zanzibar na sisi Tanzania Bara au Tanzania na wala siyo tanganyika
5. Kwa nini chao ni chao na chetu ni chao pia, mfano madini ya muungano mafuta na gasi ya Zanzibar?
6. Kwa nini mpaka sasa hatuna mawaziri katika wizara zao ila wao wana wiziri kwenye wizara zetu mfano wizara ya Afya
7. Kwa nini waitwe Wazanzibar na sisi tusiitwe Watanganyika wakati neno Zanzibar na Tanganyika vilistaili kurokuwepo bali Tanzania
8. Kwa nini mpaka sasa tuwabebe kwa kuchangia pato wakati tukijua wao uchumi wao ni mdogo wakitegemea karafuu zao ambalo sasa kiuchumi haina kitu wakiwa wameua uchumi wa utalii kwa uendawazimu wao wa utamaduni
Maswali magumu unatoa majibu mepesi,kwani muasisi wa sera mbovu c ndio huyo nyerere?usione taabu kusema nyerere ndie alietengeneza hili bomu.
Ukweli ndiyo huo. Ila kuchokana si dhambi .. ni hulka ya binadamu. Na watu wanapochokana ukiwalazimisha kukaa pamboja wanataishia pabaya zaidi. Ndiyo maana kuna taratibu kama talaka, n.k. zinazosaidia watu waachane kwa amani. Hii ndiyo mantiki zilizofuatwa na nchi kama Ethiopia/Eritrea; Czech/Slovakia; Russia & nchi zilizokuwa za kisovieti, etc. Nchi zilizojaribu kung'ang'aniza muungano kama Serbia & FYR (za Croatia, Bosnia, Montenegro, n.k.) au Sudan/Sudan Kusini ziliishia kupigana vitani. Tusilazimishe muungano kama tumechokana. Tuige mfano mzuri wa Scotland ambao wamewachoka sana England; na wameamua wananchi waamue wenyewe kwenye ballot box mwaka 2015.Nyerere alifikia hitimisho ambalo hata leo tunaliona. Watu wanataka serikali ya Tanganyika kwa sababu wamechoka na Wazanzibari.
Hitimisho lako linajitosheleza na lipo waziwazi ila Wazanzibari katu hawatakubali nchi yao kugeuzwa mkoa,wilaya au jimbo chini ya serikali moja (hii ni sababu tosha kuuvunja muungano) hivyo ni bora tuuvunje tu turudi kuishi kama zamani (kabla ya muungano),
Ah wapi Nyerere aliwaachia kitu kizuri bahati mbaya yeye peke yake alikiamini uzuri wake...
Mi nadhani huu mjadala wa Muungano uahirishwe kwa miaka 20, na watu wa elimishwe, historia ya kweli iandikwe na ifundishwe mashulei Kizazi kijacho kiamue muungano uweje