Kwanini si muumini wa Serikali Tatu...

Kwanini si muumini wa Serikali Tatu...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,095
Reaction score
43,305
Aprili 30, 1992 aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais John Samwel Malecela alitoa hotuba ndefu Bungeni ambapo alipinga hoja ya serikali tatu. Kwanza alipinga kwa sababu tume ya Nyalali ilipata asilimia 49 tu ya watu 36299 waliotoa maoni walitaka serikali tatu. Kwamba watu karibu 17,000 ndio walitaka serikali tatu na kwa hilo tu tume ikapendekeza serikali tatu. Hata sasa suala la serikali tatu hatujaambiwa ni watu wangapi wanataka hilo kwenye tume ya Warioba hadi Tume iliingize kwenye rasimu ya Katiba. Na idadi hiyo inaendana vipi na wale wengine waliotaka mifumo mingine ya serikali.

Malecela alisema kwa uthabiti hivi:
Sisi hatuoni kuwa kuna hoja ya kisheria na ya kisiasa ya kubadili mfumo wa sasa wa Serikali mbili na kuanzisha mfumo wa Serikali tatu. Tunaamini kuwa mfumo wa Serikali tatu, utadhoofisha Muungano wetu kisiasa na kiuchumi.

Nyerere akielezea hili kwenye kitabu chake cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania (UWHT) anasema hivi:

Waziri Mkuu aliisahau hotuba hii; na wabunge waheshimiwa walisahau shangwe zao na
makofi yao. Wakapitisha Bungeni, "kwa kauli moja", Azimio la kutaka Serikali ya Tanzania ilete
muswada wa kubadili Katiba ya Nchi yetu ili kuwa na Serikali ya Tanganyika "ndani ya Muungano",
kwa madai ya kwamba hayo ndiyo " matakwa ya wananchi wa Tanzania.
Lakini ukweli wa suala hili unabaki pale pale: Wananchi wa Tanzania hawadai Serikali ya Tanganyika;
na mimi nasema, ukifufua Tanganyika, utaua Tanzania. Fahari wawili hawakai zizi moja: "Yeltsin"
wa Tanganyika' ataua Muungano. Lakini pia sababu zile zile za ukabiIa na udini na tamaa za
uongozi zitakazoua Tanzania hatimaye zitaiua Tanganyika nayo.

Nyerere aliona - na mimi nakubaliana naye - suala la kudai Tanganyika wakati ule kama ilivyo leo ni suala la tamaa ya uongozi na matokeo yatakuwa ni yale yale.

Nyerere aliona kuwa watu wa Tanzania wanachotaka ni kuwadhibiti viongozi wao. Yeye aliona kwa usahihi kabisa kuwa kuleta Tanganyika haitatatua tatizo la viongozi wahalifu kwani sasa utakuwa na viongozi wabovu kwenye Muungano na wengine kwenye Tanganyika na Zanzibar. Alisema suala basi ni kuweka utaratibu wa kuwawajibisha viongozi sawasawa.

Nyerere akaelezea vizuri kwanini wakati wa Muungano hatukwenda kwenye serikali moja au kwenda serikali tatu. Alisema hivi:

Tanganyika na Zanzibar zilipoamua kuungana na kuwa Nchi Moja, tungeweza kufuata mmojawapo wa
mifumo hiyo ya kawaida. Lakini tulishindwa kufanya hivyo kwa sababu ya udogo wa Zanzibar na
ukubwa wa Tanganyika. Zanzibar ilikuwa na watu laki tatu (300,000) na Tanganyika watu milioni kumi
na mbili (12,000,000). Muungano wa Serikali Moja ungefanya ionekane kama Tanganyika imeimeza
Zanzibar. Tulikuwa tunapigania Uhuru na Umoja wa Afrika; hatukutaka tutuhumiwe hata kwa makosa,
kwamba tunaanzisha ubeberu mpya!

Kwa hiyo mimi nilipinga mfumo wa Serikali Moja. Shirikisho la Serikali Tatu lingekuwa ni gharama
kubwa mno kwa Tanganyika. Zanzibar ingeendesha Serikali yake na kuchangia gharama za kuendesha
Serikali ya Shirikisho; na Tanganyika ingefanya vivyo hivyo. Lakini ni dhahiri kwamba mchango wa
Tanganyika ndio hasa ungeendesha SerikaIi ya Shirikisho. Kwa hiyo Tanganyika ingeendesha Serikali
yake ya watu 12, 000, 000 na pia ndiyo ingetoa sehemu kubwa ya kuendesha Serikali ya Shirikisho la
watu 12,300,000.

Ni Watu wanaofikiri kwa ndimi zao wanaodhani kuwa gharama ya Serikali yoyote kati ya hizo
ingekuwa ndogo. Gharama ya Serikali ya Tanganyika isingekuwa ndogo, (waulizeni Wazanzibari), na
wala ya Serikali ya Shirikisho isingekuwa ndogo. Hata bila ya gharama za mambo yasiyo ya
Shirikisho. Na gharama zote hizo kwa kweli zingebebwa na Tanganyika.

Ni vizuri kuangalia hizo namba leo hii; Zanzibar ina watu kama milioni 1.3 na Bara kuna zaidi ya watu milioni 45. Hivyo serikali tatu kwa mantiki ya Nyerere bado Tanganyika itabeba mzigo mkubwa zaidi - kuwa na serikail ya kuhudumia watu milioni 45 na pia kuchangia mchango mkubwa kwa serikali ya watu milioni 46.3.

Nyerere alikutana na viongozi wa chama na wabunge wa CCM na kuwashawishi kuipinga hoja ya serikali tatu na serikali nayo. Lakini alipoondoka kwenye Asia akiwa kwenye ziara ya Nchi za Kusini (alikuwa Mwenyekiti) huku nyuma serikali na viongozi wakashindwa kupinga kwa hoja maridhawa kabisa serikali tatu (kama tunavyoona sasa). Nyerere aliandika kwa ukali na uwazi hili tena kwa mshangao. Alisema:

Nilipouliza kwa nini hawakupinga hoja ya Serikali tatu kama tulivyokuwa tumekubaliana majibu ya viongozi wetu wakuu yalikuwa ni ya ajabu kabisa. Ati wabunge wenye hoja baada ya kuonana na mimi Msasani walikwenda Bungeni wakiwa wakali kama mbogo! Tena walikuwa wakiwatukana wenzao (yaani wabunge wa Zanzibar) kwa kuwataja majina.

Hizi ni sababu za ajabu sana za kuwafanya viongozi watu wazima watelekeze msimamo mzima wa Chama chao na makubaliano ya watu makini kuutetea msimamo huo na waamue kuikumbatia hoja ya mbogo wakali! Huu ni uongozi wa ajabu kabisa!

Nyerere alifikia hitimisho ambalo hata leo tunaliona. Watu wanataka serikali ya Tanganyika kwa sababu wamechoka na Wazanzibari. Nyerere anasema hivi:

Ndivyo viongozi wetu waheshimiwa wanavyojaribu kufanya hata katika suala hili la Muungano.
Wanataka kuvunja Tanzania maana "wamechoka na Wazanzibari"; lakini hawataki kusema hivyo wazi wazi. Wanachosema ni kwamba wanataka Serikali ya Tanganyika "ndani ya Muungano", ingawa wanafahamu, maana si watu wapumbavu, kwamba ukifufua Tanganyika utaua Tanzania.

Muundo wa Muungano unabadilika na si lazima uwe serikali tatu
Mimi siamini katika serikali tatu kwa kiasi kikubwa kwa sababu zile zile za Nyerere. Lakini pia ninaamini kuwa wananchi ndio wana haki ya kuamua mfumo wa Muungano na hata uwepo wa Muungano wenyewe. Sasa hivi watu wanajadili serikali tatu kwa sababu wamekatazwa kujadili kuuvunja Muungano! Watu wamekubali kuwa ni lazima tuungane hivyo tutafute namna ya MUungano. Mimi naamini wananchi ndio wanapaswa kuamua kwanza kama Muungano uwepo na wakishaamua hivyo uwe wa namna gani.

Nyerere anasema hivi:
Muundo wa Muungano, pamoja na kwamba hatutaki uwe ukitibuliwatibuliwa mara kwa mara, ni suala
la sera, si amri ya Mungu. Vyama vya siasa mbalimbali vinaweza vikawa na maoni mbalinbali kuhusu
muundo unaofaa kwa Katiba ya nchi yetu. Muundo utakaokubaliwa na wananchi walio wengi ndio
utakaokuwa sehemu ya Katiba ya nchi yetu. Muundo wa Serikali mbili unakubaliwa na wananchi,
lakini unatokana na sera ya TANU na ASP, na kwa sasa CCM. Chama Cha Mapinduzi kikipenda
kinaweza kubadili sera hiyo ya muundo wa Serikali mbili bila kuuliza wananchi kwanza. Kinaweza
kufunya hivyo kwa kuhisi kuwa hivyo ndivyo wananchi wengi watakavyo; lakini pia kinaweza kufanya
hivyo kwa sababu kinaamini kuwa inafaa kufanya hivyo, hata kama wananchi wengi hawakudai au
hawapendi mabadiliko.

Na Hapa chini ndio msimamo wangu vile vile: Kwanini tunalazimishwa kujadili serikali tatu. Kwanini tumesalimu amri na kufikiria serikali tatu? Kwanini CCM wameamua tujadili serikali tatu na sisi tunajadili serikali tatu. Hivi kweli watu wanafikiria hili wazo la serikali tatu limetokana na wananchi kwenye maoni ya tume ya Warioba au ni carryover ya mjadala wa 1992?

Nyerere anasema:
Nasema, niliamini kuwa ni kosa kwa Halmashauri Kuu ya Taifa kukubali chama kiulize wananchi
kama inafaa tuwe na Serikali Tatu. Kwanza, kwa sababu hiyo niliyoeleza; na pili, hata kama CCM
ingependa kubadili sera yake, kwa nini turukie Serikali Tatu? Kwa nini tusitake maoni ya wananchi
kuhusu Serikali Moja! Au hata kuhusu SerikaIi za Majimbo? Tumejadili katika vikao gani
tukakubaliana kuwa miundo mingine yote haifai ila muundo unaofaa ni ule wa Serikali Tatu? Au hata
Bunge lenyewe, limejadili miundo mbali mbali ya Muungano katika kikao gani hata wabunge
waheshimiwa pamoja na waheshimiwa mawaziri wetu wakafikia uamuzi baada ya mjadala kwamba
muundo peke yake unaofaa ni huu wanaopendekeza, wa kuwa na Serikali Tatu?

Na maneno haya ya Nyerere yasikike kwenye masikio yaliyoziba ya watawala wetu walioshindwa!

Hizi zote ni mbinu za viongozi wetu waheshimiwa kutaka kukiingiza Chama katika njia moja tu
nyembamba, na kutuburura kama vipofu tuitumbukize nchi yetu shimoni. Ni jitihada za kukifanya
chama na sisi wengine wote tukubali msimamo wao wa kutaka kuigawa nchi yetu.

Serikali tatu haitotatua matatizo ya Muungano itayaongeza tu. Tunaopinga serikali tatu hatupingi kwa sababu ya gharama tu - hili ni jambo dogo zaidi lakini tunapinga kwa sababu ya mantiki nzima ya kuwa na serikali tatu na nchi mbili! lakini wenzetu wanataka tuwe na nchi mbili na serikali tatu!

Mimi napinga serikali tatu - naamini kama kweli watu wanataka tuimarishe Muungano basi ni kuunda nchi moja, serikali moja mifumo mbalimbali au utengano! Kwani nani kasema ni lazima tuungane? Hatutakuwa nchi ya kwanza duniani kuvunjika na watu kuendelea kuishi pamoja na ujirani mwema.
 
mkjj hizo siasa za kumfanya kama nyerere mungu wetu achana nazo hazitusaidii,

kwanza nyerere alikua akidanganya na kutisha watu, si kweli kabisa kama serikali tatu ati tanganyika itakua na gharama ya kushugulikia watu wake na wa muungano plus watu wake. upuuzi tu serikali tatu maana yake mbili zitashughulikia maslahi ya nchi zao na muungano itasimamia yale mambo waliokubali kuyasalimisha kwa wote.


muundo huu tulionao, wa serikali ya TANganyika kujifanya ruhani na big brothers umeleta manunguniko mengi, umejenga chuki na hasama kubwa baina ya wazanzibari na watanganyika. na nnaamini kwa kua tu zanzibar ni ndogo lakini kama zanzibar ingekua kama kenya pangekua peshanuka. unazani kenya wangekubali kudhalilishwa rais wao na kufukuzwa kazi na rais wa nchi nyengine?


niwe muwazi hutowakuta wazanzibari walio wengi wenye kuunga mkono uamuzi wa nyerere kwa kutumia chama kumfukuza kazi rais jumbe. na nenda kafatilie zanzibar utagundua wazanzibari wanampenda sana na sana jumbe kuliko nyerere na wanaamini wazi kua nyerere alipinda hati za muungano kwa maslahi yake binafsi.

muungano wa serikali mbili uko bayana kua ni kuisokota zanzibar na kuichukulia ni subdivision ya tanganyika. muungano wa serikali tatu utatoa fursa sawa kwa nchi mbili zilizounda muungano. nnasikitika kusema ww mkjj si mpenda haki, na wala hupendi haki itendeke. unapenda kuona zanzibar inaangamia au kua sehemu ya tanganyika.

tuje kwenye muundo ulio sawa, tuwe na serikali ndogo ya muungano na iwe inachangiwa kwa usawa, wazanzibari hawajakataa kuchangia muungano, na vikao vimefanyika na wazanzibar wamekubali tuuunde mfuko wa pamoja wa matumizi na mapato ya muungano, mbona watanganyika mmekataa kwa nn ? sababu ni ile ile kuisokota zanzibar.

kua na serikali tatu na nchi mbili ni suluhisho zuri sana, maana lile la ubig brother litakufa, pili kila nchi itakua na nguvu ya kusimamia rasilimali zake na kupanga sera zake zauchumi kwa uhuru.
 
Mimi napinga serikali tatu - naamini kama kweli watu wanataka tuimarishe Muungano basi ni kuunda nchi moja, serikali moja mifumo mbalimbali au utengano! Kwani nani kasema ni lazima tuungane? Hatutakuwa nchi ya kwanza duniani kuvunjika na watu kuendelea kuishi pamoja na ujirani mwema.
Hitimisho lako linajitosheleza na lipo waziwazi ila Wazanzibari katu hawatakubali nchi yao kugeuzwa mkoa,wilaya au jimbo chini ya serikali moja (hii ni sababu tosha kuuvunja muungano) hivyo ni bora tuuvunje tu turudi kuishi kama zamani (kabla ya muungano),
 
Mimi siamini katika serikali tatu kwa kiasi kikubwa kwa sababu zile zile za Nyerere. Lakini pia ninaamini kuwa wananchi ndio wana haki ya kuamua mfumo wa Muungano na hata uwepo wa Muungano wenyewe. Sasa hivi watu wanajadili serikali tatu kwa sababu wamekatazwa kujadili kuuvunja Muungano! Watu wamekubali kuwa ni lazima tuungane hivyo tutafute namna ya MUungano. Mimi naamini wananchi ndio wanapaswa kuamua kwanza kama Muungano uwepo na wakishaamua hivyo uwe wa namna gani.


Na maneno haya ya Nyerere yasikike kwenye masikio yaliyoziba ya watawala wetu walioshindwa!

Serikali tatu haitotatua matatizo ya Muungano itayaongeza tu. Tunaopinga serikali tatu hatupingi kwa sababu ya gharama tu - hili ni jambo dogo zaidi lakini tunapinga kwa sababu ya mantiki nzima ya kuwa na serikali tatu na nchi mbili! lakini wenzetu wanataka tuwe na nchi mbili na serikali tatu!
Mi nadhani huu mjadala wa Muungano uahirishwe kwa miaka 20, na watu wa elimishwe, historia ya kweli iandikwe na ifundishwe mashulei Kizazi kijacho kiamue muungano uweje
 
Mtu wa Pwani;7140801]mkjj hizo siasa za kumfanya kama nyerere mungu wetu achana nazo hazitusaidii,kwanza nyerere alikua akidanganya na kutisha watu, si kweli kabisa kama serikali tatu ati tanganyika itakua na gharama ya kushugulikia watu wake na wa muungano plus watu wake. upuuzi tu serikali tatu maana yake mbili zitashughulikia maslahi ya nchi zao na muungano itasimamia yale mambo waliokubali kuyasalimisha kwa wote
Naomba nikujibu kwa hoja yako. Wazanzibar mumekuwa mnatoa majibu mepesi kwa maswali magumu. Hoja ya Nyerere ipo hapo iwe ni ya kipuuzi au ya kijanja. Unachotakiwa ni kuonyesha wapi kuna matatizo au wapi hakuna tatizo.

Unaposema Nyerere ni mpuuzi nakuomba wewe utufafanulie yatakapokubaliwa mambo 7 kwa mfano na kuwa na serikali ya shirikisho yatagharamiwa kwa utaratibu gani? Nikupe mfano tu, gharama za serikali ya muungano zikiwa sawa na trilioni moja hebu mzanzibar tueleze tunagawana vipi gharama hizo?
muundo huu tulionao, wa serikali ya TANganyika kujifanya ruhani na big brothers umeleta manunguniko mengi, umejenga chuki na hasama kubwa baina ya wazanzibari na watanganyika. na nnaamini kwa kua tu zanzibar ni ndogo lakini kama zanzibar ingekua kama kenya pangekua peshanuka. unazani kenya wangekubali kudhalilishwa rais wao na kufukuzwa kazi na rais wa nchi nyengine?
Hapa tayarii umeshakubali kuwa Tanganyika ni big brother kama ambavyo mungu amepanga
niwe muwazi hutowakuta wazanzibari walio wengi wenye kuunga mkono uamuzi wa nyerere kwa kutumia chama kumfukuza kazi rais jumbe. na nenda kafatilie zanzibar utagundua wazanzibari wanampenda sana na sana jumbe kuliko nyerere na wanaamini wazi kua nyerere alipinda hati za muungano kwa maslahi yake binafsi.
Hakuna tatizo kuamini, kama ingekuwa kutafakari na kufikiri tatizo lingekuwepo. Wazanzibar wana haki ya kuamini kabisa kuwa Jumbe alikuwa mwisrael na hakuna mwenye haki ya kuwazuia kuamini hivyo hata kama ukweli ni kuwa Jumbe ni mwafrika
muungano wa serikali mbili uko bayana kua ni kuisokota zanzibar na kuichukulia ni subdivision ya tanganyika. muungano wa serikali tatu utatoa fursa sawa kwa nchi mbili zilizounda muungano. nnasikitika kusema ww mkjj si mpenda haki, na wala hupendi haki itendeke. unapenda kuona zanzibar inaangamia au kua sehemu ya tanganyika
MMM hapaswi kukufurahisha ili kutoa haki nadhani!!! Unaposema itatoa fursa sawa hebu tufahamishe fursa hizo sawa ni zipi?
tuje kwenye muundo ulio sawa, tuwe na serikali ndogo ya muungano na iwe inachangiwa kwa usawa, wazanzibari hawajakataa kuchangia muungano, na vikao vimefanyika na wazanzibar wamekubali tuuunde mfuko wa pamoja wa matumizi na mapato ya muungano, mbona watanganyika mmekataa kwa nn ? sababu ni ile ile kuisokota zanzibar.
Mtanganyika yupi amekataa maana hakuna kitu kama hicho. Sasa kama mnaongea na wake zenu vyumbani sisi tutajuaje kuwa mumeamua kuanzisha mfuko wa pamoja?
Pili, wewe umesoma hadi darasa la ngapi maana unaposema kuchangia sawa ninapata picha kuwa hukuwahi kuhudhuria somo la hesabu. Hivi unajua kitu kinaitwa mchango kinatokana na nini? Sasa hivi narudisha kiwango nyuma, nasema hivi kama gharam za muungano ni trillion moja tukichangia sawa znz inabaki na nini
kua na serikali tatu na nchi mbili ni suluhisho zuri sana, maana lile la ubig brother litakufa, pili kila nchi itakua na nguvu ya kusimamia rasilimali zake na kupanga sera zake zauchumi kwa uhuru
Kama u big brother utakufa basi hakuna hata sababu ya kusubiri muungano uvunjwe. Ukweli utabaki kuwa wewe huwezi kuwa baba mbele ya babako yako hata kama unataka iwe hivyo. Ni kanuni za asili ambazo mjinga atajitahidi kuzibadili kwa mawazo.Ni kama wznz kutamani siku moja jua litoke magharibi kwasababu znz wanahitaji hivyo.

Hoja yangu kubwa hapa si kujibu hoja ya mada ni kuonyesha udhaifu mlio nao wzn katika suala hili. Wewe huna tofauti na mwanasheria wa nchi yako aliyesema tatizo kuuubwa sana la muungano ni wznz kusafiri kuja Dar hata kama tunajua nusu yao wanaishi bara bila kuwa viongozi.Tunawaomba sana sana mjenge hoja za maana kwasababu tumechoka kusikia hoja za kitoto jamani
*************************************************************************************************************************************************


Mwanakijiji, siku zote nimesesimama katika haya
1. Kura ya maoni ili tujue kama wananchi bado wanahitaji muungano.
Moja ya mambo yaliyovunja nguvu za G55 ni pale ilipotaka kujigeuza kuwa Tanzania bila kuwauliza Watanzania. Kwasasa fursa hiyo ipo. Kura ya maoni ili tujue hatima ya kila mmoja.

2. Kuvunja muungano kama kura ya maoni haipo.
Wazanzibar ambao wana serikali watusaidie nasi tutawasaidia kujenga hoja.

3. Yote yakishindikana na hakuna njia basi ni serikali 3. Katika serikali 3 mwenye kisu ndiye anayekula nyama. Ukiwepo usawa basi usiishie njiani uende katika gharama bila kuangalia u big brother.
Atakayeshindwa basi akubali kuwa dogo na hapo asubiri big brother atasema nini.
 
MM

Sababu zlitakazoua huu Muungano, unazifahamu vizuri, mojawapo ni kukosa kabisa utetezi wa maana na wenye hoja, kutoka kwa watawala na walioko madarakani.
 


3. Yote yakishindikana na hakuna njia basi ni serikali 3. Katika serikali 3 mwenye kisu ndiye anayekula nyama. Ukiwepo usawa basi usiishie njiani uende katika gharama bila kuangalia u big brother.
Atakayeshindwa basi akubali kuwa dogo na hapo asubiri big brother atasema nini.


Nguruvi, mimi naamini hili la serikali tatu ni njia ndefu ya kuvunja muungano. Kwneye suala la serikali tatu kuna vitu viwili: Kwanza, tunaaminishwa kuwa Watanganyika wengi wanataka serikali ya Tanganyika. Hili halikuwa kweli 1992 na halijawa kweli sasa. Bado Watanganyika hawajaulizwa kama wanataka serikali ya Tanganyika na hasa kama wanaitaka ndani ya Muungano. Wazanzibar nao hawajaulizwa kama wanataka kubakia ndani ya Muungano au wawe nje ya Muungano. Hivyo, kuwaleta kwenye serikali tatu tutakuwa tumetatua tatizo ambalo halipo; yaani tatizo la idadi ya serikali.

Tatizo lilipo sasa hivi ni suala la nchi mbili kuunda nchi moja siyo suala la idadi ya serikali. Hapa ndipo wanasiasa wetu na wanasayansi ya siasa waliposhindwa kabisa kutusaidia.

Tanzania na Zanzibar ni nchi moja ina serikali mbili au
Tanzania na Zanzibar ni nchi mbili zenye serikali mbili
Zanzibar ni "nchi ndani ya nchi" kama alivyosema Kikwete au ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano?
n.k

Sasa kwa muda mrefu (miaka 20 to be precise) tumekwepa swali la msingi kabisa la kuamua hatima ya taifa/mataifa yetu. Je Muungano unahitajika na kwanini? Je, tukivunja Muungano ni vitu gani haviwezi kufanyika tena? Je, Tanganyika na Zanzibar zinaweza kuwepo bila ya Muungano? Sasa kama majibu yote yanaashiria kuwa Tanganyika na Zanzibar zinaweza kuwa mataifa mawili kwa njia za amani kabisa na kila moja ikiwa huru kabisa kama ilivyo kwa nchi nyingine za eneo letu kwanini tusiamue kufuata njia hiyo na badala yake kulazimisha matatizo?

Lakini kubwa ambalo naliona ni kuwa wapo watu wanafikiria kuwa kurudisha Tanganyika kutaondoa malalamiko ya Wazanzibari! Kana kwamba Tanganyika ikirudi basi Zanzibar itajiona iko na mwenzie sawa kwenye Muungano! Sasa in theory linaweza kuwa kweli lakini hapo ndio Watanganyika watajikuta wana matatizo zaidi! Hivi kutakuwa na usawa kweli kati ya Tanganyika na Zanzibar? Kweli Watanganyika watajiona wako sawa na Wazanzibari kiasi cha kukubali Zanzibar iwe na nguvu ya veto kwa mambo ya Muungano ambayo yatawanufaisha Watanganyika wengi zaidi? Tayari tumeshasikia dalili za kudai parity katika teuzi na utumishi wa umma; hivi kweli katika "Muungano" huo Watanganyika watakubali wagawane nafasi nusu kwa nusu na Wazanzibari kwa vile zimeingia "nchi mbili'?

Njia pekee ya kuimarisha Muungano ni kwenda serikali moja kubwa na mifumo mingine ya utawala (kama Canada na Quebec, UK na Scotland (ambayo kuna dalili inataka kuwa taifa huru baada ya zaidi ya karne kadhaa ya Muungano), au China na Hong Kong au Macau? Serikali tatu ni kuahirisha tatizo tu ambalo kimsingi tunataka kuwapa watoto wetu kazi ya kulishughulikia. Suala ni Muungano uwepo au usiwepo. Tukishaamua hili haya ya serikali na utawala yanakuja wenyewe lakini sasa mtu mmoja (Kikwete) alishaamua Muungano uwepo na hivyo wengine wote tucheze ngoma aliyopiga yeye.
 
nguruvi3 unanifurahisha sana unaposema kua gharama za muungano zikiwa trilioni tatu zanzibar wataweza kuchangia nusu kweli ? kwanza kwa vp zifike huko? lkn tatu kutokana na mchanganuo mapato ya kuendesha serikali ya muungano yameainishwa na kuelezwa kila mara na hata jaji warioba, kua hilo si ttz mapato yatapatikana na kila nchi itaweza kuchagia kwa usawa.

ww unauangalia huu muungano tulionao ambao zanzibar iendeshe yake mwenyewe kisha ichangie muungano ambao sehemu kubwa ni tanganyika. hapo ndipo ttz lilipo

ntakupa mfano wa EAC ni jumuia yenye nchi tano rwanda na burundi ni nchi ndogo na hata uchumi wake ukilinganisha na kenya na tanzania naamini ni mdogo, lkn jee wameshindwa kuchangia? naamini unajua kua tunapoamua mambo yepi ya kuungana tutaweza kuyaendesha. ila huwezi kunambi mm nna milioni moja na ww milioni arubaini kisha useme tuchanganye kila kitu halafu unambie tugawe gharama sawa sawa, iko wazi mm wa milioni utanizulumu ntakua nnalisha watu wako.

tukija kwenye Tatu kama rasimu inavyoelekeza na inahitaji marekebisho kidg tutachagua maeneo muhimu ambayo tutaweza kushirikiana na kuyachangia gharama zake. na nnaamini itatoa fursa kwa watanganyika kuinjoy resource zao kama ilivyo kwa wazanzibari.

pia itajenga nguvu ya kuhisi serikali ya muungano ni yetu sote, sio kama leo watanganyika ndio muungano. kisha kiujanja wanajidai wao wamepoteza. kilimo si muungano michezo si muungano biashara si muungano kwa hayo machache ila tanganyika kwa mwemvuli wa muungano wanashiriki na kujiwakilisha na kunuaika na kila kitu kwa koti la muungano bila hata kuishauri zanzibar, bali zanzibar wakitaka dogo lile kuhusu lolote lile kwa lisilo la muungano mpaka waombe ruhusa kwa big brother. Mfano TFF wao ndio wanaoiwakilisha Tanzania wakati hawana ridhaa ya wazanzibar kwenye michezo.

suali la mfuko wa pamoja wa fedha limeongelewa wazi ila serikali ya tanganyika haijawa tayari kuliongea na kulitekeleza. amini usiamini malalamiko mengi na chuki hizi tulizonanzo baina ya ndugu wa damu ni huu muundo wa muuungano.

mkjj tunamuelewa ghilba zake mm na yy tupo hapa tokea 2006 na nnamjua na anijua vyema hoja zangu tukija kwenye suali zima la muungano. sisi tupo tayari kwa muungano wa haki na heshima na usawa ila kwa huu wa kikoloni kwa kweli hatuukubali. tulipindua 1964 ili kujiamulia mambo yetu wenyewe. tulikubali kuungana si kua tulishindwa kuendesha nchi yetu bali kuamini umoja ni nguvu na kuengeza heshima ya kujiamulia na kupata uzoefu kupitia kwa wenzetu
 
Binafsi ninaamini katika serikali tatu, na watu leo hawaelewe tu, kisayansi kero kuu ya Muungano ni kutokuwepo kwa Tanganyika,

Nitarudi baadae kwakirefu, maneno ya Mwalimu yenyewe tu yanakosoleka kwa uhalisia uliopo sasa!
 
Mwanakijiji
Nasema in worst case scenario serikali 3 ni bora. Sasa hivi wanaongelea parity kwasababu wapo wenyewe. Nimeliongelea sana kuwa kuna element za nationalism katika Zanzibar kwasababu hakuna Tanganyika.

Baada ya kusoma rasimu wamegundua kuwa nationalism wanaojivunia ina tatizo mbele ya safari yao Tanganyika ikirudi. Ndio maana wamekubali, narudia kwa msisitizo Kamati ya maridhiano ambayo basically ni ya akina Seif wasiotaka kusikia neno Tanzania sasa hivi wamekubali kusema kiwepo kitu kinaitwa Tanzania-Zanzibar. Hizi ni dalili za kukubali kuwa uwepo wa Tanganyika utaondoa kujibanza mgongoni wanakohitaji in fact na kuondoa nationalism yao

Suala la kuvunja muungano si la Tanganyika, ni wao hawataki kwasababu wana kila opportunity ya kufanya hivyo. Ni Ung'ang'anizi wao vinginevyo wangeshafanya siku nyingi sana.
Mbona mafuta na gesi waliondoa siku moja. Tatizo hata kama Tanganyika hawataki wao wanataka.

Ili kuweza kuachana nao suala la kura ya maoni ni muhimu sana.

Kuhusu parity za kugawana vyeo na nafasi, hilo dawa yake ni moja tu.
Kwanza tunaweka gharama za muungano atakayeshindwa kuchangia basi atasubiri anayechangia anasema nini, kama hawataki tunavunja jahazi.
Huoni hapo ni pazuri pa kutokea? Na hilo litawezekana kama kuna kiongozi wa Tanganyika na si kama ilivyo sasa.

Kiongozi wa Tanganyika atasimama na kusema yeye hawezi kuchangia muungano halafu kukawa na upuuzi wa kugawana vyeo. Nina uhakika hakuna kiongozi wa Tanganyika atakayekuwa na bunge la Watangnyika na wananchi wa Tanganyika atakayekubali kuendelea kubeba mzigo wakati ana taifa lake lenye matatizo lukuki.

Ndio maana tunasema
1. Kura ya maoni
2. Ikishindikana vunja muungano
3. Ikishindikana Tanganyika irudi itetee watanganyika na rasilimali zao ikiwa ni pamoja na gharama za muungano.

Kama hakuna uwajibikaji sawa basi znz ikae kimya isubiri Tanganyika wanasema nini, kama hawataki wanaondoka.Hakuna mtu wa kuwabeba tena na wala Watanganyika hawaihitaji znz kwa lolote

Tanganyika bila znz huru au ndani ya shirikisho inawezekana na ni faraja sana kwa Mtanganyika.

 
mkjj mbona unakimbia hoja, unataka kunambia vp kuhusu EAC, Tanganyika mna watu wengi kuliko rwanda au burundi mbona hamjadai muwe na wabunge wengi badala ya Tisa sawa na waburundi na rwanda?

jee watendaji wa Tanzania ni wengi kuliko burundi kwenye EAC ? mbona kwenye EAC organs za EAC zimegawanywa vyema na kila kwenye nchi washirika pasipo kujali ukubwa au udogo iweje iwe sewe kwa wazanzibari kudai utumishi sawa kwenye muungano ? wazanzibari hawadai kwenye Tanganyika, wanadai usawa kwenye muungano na ndio maana tukataka tuangalie maeneo machache ambayo tunahitaji kushirikiana na huko tuwe sawa ktk uendeshaji na maamuzi.

na kuwepo tanganyika ndio muhimu sisi tumeungana na tanganyika na ikitokea kuna ttz kwenye uendeshaji wa serikali ya muungano wa kuamua ni washirika nao ni wazanzibari na watanganyika.

huu muungano ni wa ss kama hatuutaki tutauvunja hata kwenye mbili au moja. lkn kama alivyosema mwanasheria kama muundo utaovunja muungano violently ni huu wa mbili.

mkjj jipe muda kutafakari na kutolazimisha hoja, kama kweli tunataka kusonga mbele ni tatu nyengine zozote ni uzushi
 
Mtu wa Pwani...kwani kuna muungano kati ya nchi za Africa ya Mashariki?
 
Muungano ni Msalaba tu kwa Watanganyika.
Kabla ya kuungana mbona maisha yalikuwepo tu.
Ina maana tunahofia nn kujitawala bila muungano?
Majimbo ndo kila kitu au tuuvunje muungano.
 
mkjj lengo la EAC mwisho nikufikia shirikisho la kisiasa kwa hio ndio upo muungano. na ss tunaandika katiba mpya ya shrikisho la tanganyika na zanzibar.

halafu jibu hoja mbona EAC kuna usawa kwa nn ss tushindwe?
 
Binafsi ninaamini katika serikali tatu, na watu leo hawaelewe tu, kisayansi kero kuu ya Muungano ni kutokuwepo kwa Tanganyika,

Nitarudi baadae kwakirefu, maneno ya Mwalimu yenyewe tu yanakosoleka kwa uhalisia uliopo sasa!

MM,
Tusidanganyane, tumebakiwa na option mbili tu, Kuwa na serikali moja au tatu. Serikali mbili haiwezekani tena. Hata ccm leo wakilazimisha itachukua miaka michache tutarudi kwenye tope la matatizo ya kero za muungano.

Na kwa kuwa Wazanzibari hawataki kuua utaifa wao kama sisi watanganyika tulivyoua tanganyika yetu, basi kama Yereck wa Nyerere anavyosema serikali tatu haikwepiki. Naishukuru Chadema kuliona hili mapema na kuiweka ktk sera yake.

Tatu, ktk dunia ya Leo kama ni kweli kwamba serikali tatu itavunja muungano na kama muungano utavunjika kweli miaka kadhaa ijayo, kwani kuna tatizo gani? watz hawatakuwa wakwanza kuvunja muugano wao, duniani kote mifano iko mingi ya miungano iliyovunjika, and by the way ndivyo tulivyokuwa kabla ya 1964.

Nne, Muungano uliopo hauwatendei haki watanganyika. Ni muugano wa chako ni chako, ila changu ni chetu sote. Yaani mimi siwezi kuwa waziri Zanzibar, ila mzanzibari anaweza kuwa waziri Tanganyika kupitia Serikali ya MUUNGANO. Leo hii mzanzibar ni waziri wa Afya wakati afya haiko ktk muungano. Zanzibar kuna waziri wa afya. Waziri wa afya wa Muungano kiuhalisia ni waziri wa afya wa Tanganyika. kwa hiyo waziri wa afya kutoka zanzibar anaongoza wizara ya Serikal ya Tanganyika iliyofutwa kiaina huko nyuma. SASA kwa nini iwe hivyo?

Tano, Ni jambo la bahati nzuri sana kwamba, wanaoongoza kuupinga muungani ni wazanzibar, na naomba tuwape haki yao. Wazanzibar wamediriki kusema wao hawataki kuwa koloni la Tanganyika. sisi tuna hofu nini?

Mwanasheria mkuu wa zbar kasema kero kubwa ya muungano ni kutokuwepo kwa serikali ya Tanganyika. We should not fear the unknown, we should face the challenges of 3 governments, na kama muungano utavunjika, tutakuwa kama tulivyokuwa kabla ya mwaka 1964, si vita.
 
mwanakijiji sasa nadhani unapotaka kutupeleka siko kabisaa

[h=3]Mwanasheria mkuu Zanzibar: Kutokuwepo serikali ya Tanganyika ndio kero kuu ya Muungano![/h]
Awashangaa wanaotaka Zanzibar iendelee kuwa manispaa
Asema kutokuwepo Serikali ya Tanganyika ndio kero Kuu ya Muungano
Awasuta wanaotaka Serikali Mbili



Na Salim Salim

Mwanaseria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi wa Zanzibar leo amesema lengo la kuandikwa kwa Katiba Mpya si kuyafanyia Marekebisho katiba iliyokuwepo sasa bali ni kandika Katiba Mpya katiba ambayo itakuwa Muarubaini kwa kero za Muungano na Muungano wenyewe.


Mwanaseheria Mkuu liyasema hayo leo asubuhi alipokwa akifunguwa Baraza la Katiba la Vyuo Vikuu liliondaliwa na

ZAHILFE Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Zanzibar liliofanyika katika Ukumbi wa Salama Hal Bwawani.

Alilisifu Baraza hilo na kusema kuwa ni Baraza la Vijana wasome na kuwasifu Vijana kwa ile sifa yao kubwa ya kuleta mapinduzi katika jamii yeyote.

Alimtaja kijana Sir King ndie waliosababisha Zanzibar iiteme Tanganyika mwaka 1895 Ogast na Tanganyika kuangukia katika mikono wa Wajerumani.


Na kumtaja Gerald Pota alietumwa na Waingereza kuja kuunda Serikali na kumpangia Mfalme mshahara ambako alikuwa akilipwa paund 250 kwa mwaka.


Msingi wa Muungano wa Tanzania ni kuungana kwa Nchi mbili huru Tanganyika na Zanzibar lengo la kuungana kwa nchi mbili hizi ni kufanya mambo yao pamoja na kupata faida zaidi na sio Nchi moja kuitawala Nchi nyengine alisema, hukua akiendela kusema:


Zanzibar si mkowa wala wilaya, Zanzibar ni Nchi, katika Muungano tulikubaliana baadhi ya mambo kufanya pamoja na sio Zanzibar kuwa Jimbo la Tnganyika.


Alisema duniani kuna miungano mingi mizuri akiutolea mfano Muungano wa Uswis ambao una Serikali 24 na ule wa Muungano wa Maerkali wenye Serikali 52 na kusema kuwa ni uongo kuwa Serikali Tatu zitavunja Muungano na kusema

Serikali Mbili ndizo zitakazovunja Muungano, na hata Muungano wa Serikali Tatu ukivunjika si kioja.

Serikali Tatu hazitovunja Muungano Serikali Mbili ndizo zitakazo vunja Muungano.

Alisema Uruhani wa Serikali ya Tanganyika ndio kero kubwa ya Muungano na Serikali tatu itairudisha Serikali ya Tanganyika ambako kero kubwa itakuwa ishatatuliwa.


Aliitaja Sheria ya Kuanzishwa na Bank Kuu ya Tanzania kuwa aliisaini Karume mwenyewe lakini Karume alipoona mapungufu ya Seria hiyo ndio maana akaanzisha PBZ.


Aidha alisema kama Zanzibar inataka kuishtaki TFF itashinda na TFF haitokuwemo FIFA kwani TFF haiwakilishi Tanzania kama ilivyokuwa ZFA ilivyokuwa haiwakilishi Tanzania.

Hivi hatuoni haya kubakia hivi hivi kuwa Manispaa wakati Zanzibar ilikuwa Empire alihoji Mwanasheria Mkuu na kuendelea kusema hivi tutamuamini vipi mtu ambae leo anasema Zanzibar si Nchi atakapokuwa Rais wa Tanzania ambao

Zanzibar haitokuwa na Mamlaka atasema Zanzibar ni jimbo la Tanganyika na kumalizia kusema wengi wa Watanganyika wanachuki na Zanzibar.


Aliwataka wanafunzi hao kuzungumzia mambo ya Muungano na kutaka kuwe na usawa "Bila ya kuwa na usawa katika Mungano huu huo si Muungano bali ni ukoloni" alisema, na kutaka kuwe na mfumo wa usawa katika Baraza la Mawaziri na Bunge na kuwe na makubaliano ya thuluthi mbili kila upande katika kupitisha sheria na kuengezwa au kupunguzwa mambo ya Muungano.


Alisema katika Muungano wa Serikali Tatu ni lazima Rasilimali zitumike kwa Usawa na sio kama hivi sasa Tanganyika inavyotumia Rasilimali za Muungano wao peke yao katika kusoma na kuinyima Zanzibar.


Tume ya Pamoja ya Fedha haijaanza kazi mpaka leo, na katika Muungano kuna mapato ya Muungano na Matumizi ya Muungano na Mapato ya Muungano siku zote huwa mengi ambako Tnganyika hawataki tugawane.

Alisema si kweli kama Muungano wa Serikali tatu una harama bali Muungano wa Serikali Mbili ndio wenye gharama na

Zanzibar ndio inaharamika zaidi, aliwataka viongozi wawe wakweli na waache kuwapotosha wananchi.

Aliwaonya Wazanzibar kuwacha kulumbana na badala yake kukaa pamoja kuidai nchi yao.
Alisema Serikali ya Umoja wa Kitaifa iliundwa ili kuondowa tofauti kwa Wazanibar na kusema kuwa kuundwa kwa

Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni kuala gumu kuliko mabadiliko ya Muungano.

Alisema Wanaotaka Seriakali Mbili hoja zao hazina msingi na hakuna haja ya kubakia kwenye Serikali mbili na wengi wanaotaka Serikali Mbili wanalinda maslahi yao ya kidunia.

Hoja yangu nawataka wanaotaka Serikali Mbili na Wanaotaka Mkataba wakae pamoja wajadiliano Mfumo wa Muungano wa Serikali Tatu mfumo ambao utakuwa na Mslahi na Zanzibar.


Awali Mwenyekiti wa ZAHILFE alikanusha taasisi yake kuandaa kungamano la tarehe 6 mwezi wa 7 lililofanyika Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kingeni na badala yake kongamano hilo liliandaliwa na Mkowa wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vywa CCM na kusema Taasisi yake haina mafungamano na chama chochote cha siasa.


Kongamano hilo lilianza na Wimbo wa Taifa wa Zanzibar na lilihudhuriwa na baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.
Marais 10 wa Serikali za Wanafunzi waliochangia katika Kongamano hilo walitaka Zanzibar yenye Mamlaka Kamili na Usawa Katika Muungano.

Chanzo Mzalendo.net
 
mkjj lengo la EAC mwisho nikufikia shirikisho la kisiasa kwa hio ndio upo muungano. na ss tunaandika katiba mpya ya shrikisho la tanganyika na zanzibar.

halafu jibu hoja mbona EAC kuna usawa kwa nn ss tushindwe?
Naona unashindwa kutetea hoja zako na kuanza kung'ang'ania kitu ambacho ni tofauti na kinachoongelewa hapa.

EAC SIYO SHIRIKISHO!

Sifa za shirikisho la kisisa
1. Ngazi mbili za serikali zinazoongoza watu na ardhi moja. Na,

2.Kila ngazi ya serikali ina suala angalau moja ambalo ina uhuru kamili wa kujiamulia, na

3.Kuna uhakika kikatiba na uhakika huo ni guaranteed kuwa uhuru huo unaweza kutekelezwa kwenye eneo la ardhi/mipaka ya ngazi moja ya serikali.


Muhimu zaidi ya yote hayo, ngazi. Ngazi inamaanisha eneo moja yaani serikali moja ni ya juu zaidi ya serikali nyingine. Lazima kuwe na katiba ambayo ni ya juu ya katiba nyingine.

KATIBA YA EAC, KAMA IPO AU ITAKUWEPO .... HAINA NGUVU JUU YA SUALA LOLOTE KWA SERIKALI YEYOTE. Kwa kifupi haina maana na hatuna haja ya kuisikia hapa.
 
Ukiacha hili la viongozi kuwa na uroho wa kutaka kuongoza sioni mantiki ya Serikali tatu,kwa sababu kama ni kero zinazoshindikana kutatuliwa tukiwa kwenye mfumo wa serikali mbili ni ngumu kwa kiwango kikubwa zaidi tukiwa na Serikali tatu...
Kuna wimbi dogo la watu wenye nguvu wanaoshabikia serikali tatu na wakati huo huo kuna wimbi kubwa la watu wenye uwezo wa wastani wasiojua kwanini wanataka serikali ya Tanganyika, wanaodai serikali tatu ambao hata hivyo wakiulizwa sababu hawana!
Nionavyo hii mbegu tunayopanda leo(kama itafanikiwa) sio miaka mingi tungali hai tutapita tena kwa wananchi(japo wakati utakua hauruhusu) kuwataka mawazo ya kurudisha mfumo uliokuwepo(wa serikali mbili).
 
Mkuu wangu Nguruvi3 nimependa sana uliposema hapo juu kuwa, ndani ya serikali 3, mwenye kisu kikali ndiye atakayekula nyama! Tafsiri ya wazi hapa ni kuwa ni lazima tufanyiane undava undava tu, na huo ndio ukweli na hakuna namna ya kuukwepa ndani ya serikali 3. Sioni nafasi ya Tanzania endelevu chini ya serikali 3. Sioni namna yoyote ya Usisi na Uwao kutufikisha kokote zaidi kwenye shimo la giza!
Kwa Mazingira na Nyakati(FIKRA) kama zetu, basi hakuna namna ya kuupuuza UMOJA na tukabaki salama! Bado naheshimu mawazo ya nchi moja, serikali moja, taifa moja. Siku zote mtu nguvu ya mtu mweusi ni Umoja!
Kila tunachoota leo chema chini ya serikali 3 au 2, hakiwezi kufikiwa kama hatutakuwa wamoja, na hakuna namna yoyote ya kujihakikishia Umoja chini ya Serikali 3 au 2.
Hii ni Afrika, tusijifananishe na wengine. Kuna namna zetu sahihi na mahususi kwetu za kuendesha mambo yetu!
Mungu wetu anaita sasa!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom