Kwanini Shirika la Viwango Tanzania (TBS) hawapewi kibali cha kuajiri tangu 2019 leo 2023

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,333
8,252
Ni jambo ambalo nimekuwa nikijiuliza siku nyingi. Leo naomba niliseme ili nyote mpate kulisikia.

Kati ya mashirika ambayo hayajaajiri tangu mwaka 2019 ni pamoja na TBS. Mara ya mwisho waliajiri mwaka 2018.

Nina uhakika kati ya mashirika yenye uhitaji mkubwa wa wafanyakazi ni pamoja na TBS pengine linaweza kuwa linamfuatia TRA kwa uhitaji. Sasa tunashangaa ndio shirika ambalo siku hizi halitangazi ajira tena.

Nini sababu.

Kabla sijaendelea ndugu msomaji embu rejea nafasi za kazi za mwisho kutangazwa TBS mwaka 2018.

Itapendeza sana ajira za hili shirika zikirudishwa. Ni shirika ambalo hutoa ajira nyingi sana.
 
Serikali kuwatafuta kwa mitutu watoto ili waende shule alafu wakimaliza masomo biashara inaishia hapo na wahitimu kurudi mtaani kuanza kuzurura huku serikali hiyo hiyo ikikataa kuwapa ama kuweka mazingira ya wao kupata ajira ni sawa na kuwahujumu wazazi na familia za hawa wahitimu.

Kwa mzazi kuliko hili jambo kutokea anaona ni bora abaki na mwanae nyumbani kwake hiyo miaka 4-9 amfunde na kumfundisha mwanae maarifa huenda akasaidia familia baadae ama hata kuoa/kuolewa akawa na familia yake ya kawaida. Wazazi wanaumia sana na haya mambo ya eti watoto lazima wasome, ili litokee nini wakati hata wale waliohitimu juzi wamegeuka wazururaji na wadangaji

Kutoa ajira ni jukumu la serikali na wazazi na wanafunzi wanayo haki ya kuandamana kudai ajira maana serikali ndo baba na mama. Wananchi wanalipa kodi, mali za Taifa ziko mikononi mwa serikali kwa niaba ya wananchi, bado serikali inaajiri watu wasiozidi 20000 kwa mwaka wakati wahitaji ni zaidi ya 300000 kwa mwaka.

Ajira za binafsi ama makampuni binafsi hayawajibiki kwa mwananchi kama serikali yao hivyo kuwaambia wajiajiri ama waajiriwe na makampuni ni njia ya serikali kuukimbia ukweli, pesa nyingi zinaishia khchezewa na watu kula bata maofisini kwa kununua magari ya mamilioni badala ya kuongeza ajira serikalini.

Huu nao ni unyonyaji kwa wananchi wa Taifa hili
 
Unajuaje labda wanaajiri kimyakimya.... Hivi si kuna ile wakiomba watumishi kama kuna watu kwenye database ya utumishi wanapel3kwa bila hata kutangaza hizo nafasi?
 
Serikali kuwatafuta kwa mitutu watoto ili waende shule alafu wakimaliza masomo biashara inaishia hapo na wahitimu kurudi mtaani kuanza kuzurura huku serikali hiyo hiyo ikikataa kuwapa ama kuweka mazingira ya wao kupata ajira ni sawa na kuwahujumu wazazi na familia za hawa wahitimu.

Kwa mzazi kuliko hili jambo kutokea anaona ni bora abaki na mwanae nyumbani kwake hiyo miaka 4-9 amfunde na kumfundisha mwanae maarifa huenda akasaidia familia baadae ama hata kuoa/kuolewa akawa na familia yake ya kawaida. Wazazi wanaumia sana na haya mambo ya eti watoto lazima wasome, ili litokee nini wakati hata wale waliohitimu juzi wamegeuka wazururaji na wadangaji

Kutoa ajira ni jukumu la serikali na wazazi na wanafunzi wanayo haki ya kuandamana kudai ajira maana serikali ndo baba na mama. Wananchi wanalipa kodi, mali za Taifa ziko mikononi mwa serikali kwa niaba ya wananchi, bado serikali inaajiri watu wasiozidi 20000 kwa mwaka wakati wahitaji ni zaidi ya 300000 kwa mwaka.

Ajira za binafsi ama makampuni binafsi hayawajibiki kwa mwananchi kama serikali yao hivyo kuwaambia wajiajiri ama waajiriwe na makampuni ni njia ya serikali kuukimbia ukweli, pesa nyingi zinaishia khchezewa na watu kula bata maofisini kwa kununua magari ya mamilioni badala ya kuongeza ajira serikalini.

Huu nao ni unyonyaji kwa wananchi wa Taifa hili
Wanaishia kufanya ufisadi ,kuharibu na kuhujumu mali za uma kwa wizi na kulipana mishahara ya kufuru na anasa za kipumbavu kwa kodi za wananchi wakati taasisi za serikali nyingi ni ovyo na zina uhaba wa vitendea kazi na wafanyakazi , wanajifanya wanabana matumizi , kumbe upuuz wa kujinufaisha matumbo yao .
 
Kwani TBS bado upo si nilisikia kwa sasa majukumu wemepewa mamlaka fulani fulani
 
Ni jambo ambalo nimekuwa nikijiuliza siku nyingi. Leo naomba niliseme ili nyote mpate kulisikia.

Kati ya mashirika ambayo hayajaajiri tangu mwaka 2019 ni pamoja na TBS. Mara ya mwisho waliajiri mwaka 2018.

Nina uhakika kati ya mashirika yenye uhitaji mkubwa wa wafanyakazi ni pamoja na TBS pengine linaweza kuwa linamfuatia TRA kwa uhitaji. Sasa tunashangaa ndio shirika ambalo siku hizi halitangazi ajira tena.

Nini sababu.

Kabla sijaendelea ndugu msomaji embu rejea nafasi za kazi za mwisho kutangazwa TBS mwaka 2018.

Itapendeza sana ajira za hili shirika zikirudishwa. Ni shirika ambalo hutoa ajira nyingi sana.
Hata TANESCO, NECTA, SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA, TANAPA, NGORONGORO ni muda mrefu sana wamekaa kimya
 
Back
Top Bottom