Kwanini Serikali isiweke utaratibu wa soko la ndani kununua korosho?

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,586
4,271
Wandugu,

Nimekuwa nasikia kuwa soko la Korosho huko Duniani sio nzuri hali iliyopelekea wakulima wetu kubaki na korosho zao.

Mtazamo wangu: Kwa kuwa mikoa ambayo haizalishi Korosho ambayo ndio mingi bei yake ipo juu sana (kuanzia shs 20,000 kwa kilo iliyo banguliwa); hii bei ni ya juu sana kwa sababu wa uhaba wa korosho sokoni.

Kwa nini Serikali isiweke utaratibu wa soko la ndani kununua hiyo korosho kutoka kwa wakulima kwa bei Elekezi?

Nafikiri kwa kufanya hivyo wakulima watapata bei nzuri tena kwa wakati. Nakumbuka CHINA wamekuwa wakifanya hivyo kwa kutegemea soko la ndani kwanza hivyo na hapa kwetu tukijipanga vizuri itawezekana kwa mazao tunayo yahitaji/tumia.

Kwa sasa Mtanzania kununua Korosho kwa wakulima ni sawa na kutorosha Nyaraka za Serikali

KARIBU WAZIRI MPYA WA KILIMO WASAIDIE WAKULIMA WA KOROSHO!
 
Korosho ilikuwa bidhaa kubwa sana ya anasa kwenye ndege na maeneo ya kitalii hoteli na mabaa,

Lockdown watu wapo ndani wanakunywa chai na biscuit.

Soko la ndani kilo iliyobanguliwa ikiuzwa bei sawa na karanga 3,000 kilo, watu tunaweza kuanza utamaduni wa kuila..ila korosho ya 20,000 kilo kila mtanzania atakula robo kilo na siyo kilo 2.

Everyday is Saturday............................. :cool:
 
Back
Top Bottom