Kwanini Serikali imesamehe Shilingi Trilioni 424?


Basi kama hata tupate Robo ya 190 $ billion
 
Lissu aliita hiyo report Professorial rubbish. Alikuwa Sawa. Kama migodi mitatu ingekuwa inatoa faida hivyo basi nchi kama Botswana au Namibia Wangekuwa wanaishi peponi kwa madini waliyonayo.

..wamepewa mlungula ndiyo maana wakaachana na madai wakaanza mazungumzo na kukubali kishika uchumba.
 
Mrahaba wa 4%!!! Ambao hata wenyewe hautekelezwi Kwa asilimia 100%: waulize halmashauri zilizo na migodi watakuambia hata hiyo 4% utekelezaji wake ni wa mbinde!!
 
Haya ndiyo majibu kwa mleta hoja?Utetezi gani huu wa kujustify kupoteza 420+Trillions? Hakika hatupo salama kama nchi,nani kawasamehe hawa wezi?In exchange with what?
 
ACACIA wameandika barua kwa DPP ya kukiri na kuomba msamaha na wamekubaliwa kulipa kulingana na urefu wa kamba!
DPP?Ndiyo mwakilishi wa maslahi mapana ya Watanzania?Huyu ndiye aliwapa kazi ya kuchunguza uozo katika sekta ya madini kina Professor Mruma,Ossoro & Company?
 
Kama hichi ndicho tulichopata inamaana kilichodaiwa na kamati hakikuwa na uhalisia wowote na ni proffesorial rubbish.
 
Unataka kutuaminisha kuwa serikali ya awamu ya tano na hao wahenga wanafanana akili?Tunaenda kinyumenyume kama nchi?
Kama ni uwendawazimu ulianzia kwa mababu zako waliopokea gololi na kutoa almasi!
 
Mkuu kuna hesabu ngumu sana kuzijua hususan linapokuja kufananishwa kwa vipimo babaishi kama hayo matipa na ma landrover...
Unajiuliza hiyo tipper ni canter, txd50, scania 124 au dumper? Je na hiyo landrover ni short au long base? 110 au freelander? Si neno itutoshe kujua ni matipa na landrova moja!!!
Heri kenda chukua kuliko....
 
Unataka kutuaminisha kuwa serikali ya awamu ya tano na hao wahenga wanafanana akili?Tunaenda kinyumenyume kama nchi?
Kama hao Babu zangu walikuwa wapumbavu,kwa nini mnafanya maamuzi ya Kitaifa kwa mtindo wao.Hata hivyo wale walikuwa hawana Doctorate, Professerial Intelligence kama waliosamehe Trillions zetu tulizoibiwa.Pia walipeana vipande vya Almasi na siyo fedha ya Wananchi wa Tanzania kiasi kinachozidi bajeti ya serikali kwa miaka zaidi ya 10.
Hujajibu swali,ni kina Kabudi na nani wenye uwezo wa kusamehe wezi?Nani kawatuma?Watajeni tuhangaike nao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…