Behaviourist
JF-Expert Member
- Apr 8, 2016
- 39,902
- 95,409
Mimi sipingi kulipa kodi kwa kuwa Taifa haliwezi kuwa hai bila kodi.Mimi napinga style inayotumika kukusanya kodi hii.Hii kodi ya majengo haina shida yoyote wala huko nyuma haijawahi kuwa na shida yoyote kwa wananchi ila sasa hivi ina shida kwa sababu mtindo unaotumika katika kuikusanya haumake sense.Ni mtindo ambao upo kama kibonzo cha kuchekesha..
Kujitoa kwa ajili ya nchi kwa njia ya kodi hakujawahi kuwa jambo jepesi kwa wafanyakazi na wafanyabiashara ila wanyonge hawawezi kuelewa kwa wepesi.
Mfano wewe, unapigana kuhakikisha mpangaji hakusanyi tsh 33 kwa siku ya serikali kutoka kwa mwenye nyumba ila hujawahi kuwa na tatizo na mfanyabiashara kuikusanyia serikali VAT ya 18% ya mauzo yake ya kila siku na akisahau kuituma kwa wakati alipe adhabu ya 225,000/= per month plus interest.
Huyu anatumia muda wake, nguvu zake, resources zake kuhakikisha anaikusanya hiyo kodi na inafika kwa serikali bila malipo na akichelewa anaadhibiwa.
Pamoja na madhara ya hizi tozo, wanyonge ni wakati sasa wa kujua tafsiri ya neno kodi ili ukisikia mfanyakazi analalamika au mfanyabiashara analia basi uelewe kilio hicho maana yake ni nini.
Kwa sasa wewe pigana maana umezoea kuwa kuna watu ndio wanatakiwa wateseke na kodi za hii nchi wengine wanufaike na hospitali, barabara sababu wanaitwa wanyonge.
WENGINE WAELEWA TULIPE KODI MPAKA MBADALA UTAKAPOPATIKANA.