Kwanini Serikali ilituficha kuugua kwa Dkt. Magufuli?

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,227
113,580
Kama sikosei, mpaka sasa Rais Samia keshaongea na waandishi wa habari kama mara mbili hivi.

Ni zaidi ya mwezi sasa tokea alipoongea na wahariri wa vyombo vya habari/ waandishi wa habari toka ikulu ya Dar es Salaam.

Wiki moja au mbili zilizopita, akafanya mahojiano na Salim Kikeke wa BBC.

Katika nyakati zote hizo mbili, sikusikia kabisa akiulizwa ni kwa nini serikali yake ilituficha kuhusu kuugua kwa Rais Magufuli.

Wananchi hatukupata taarifa zozote zile zilizo rasmi hadi tukaishia kutegemea habari umbea na zisizo rasmi kupitia mitandao ya kijamii.

Kimya kilipozidi kutanda, tukaanza kudokezwa dokezwa kuwa hali si nzuri, mara sijui yupo anachapa kazi, mara sijui anafanywa nini…

Haikupendeza hata kidogo. Na hata vyombo vya habari vya kimataifa viliripoti kuhusu tetesi za kutoonekana kwa Magufuli.

Kwangu hili halikubaliki kabisa!

Wananchi kama waajiri wa hawa viongozi wetu, tuna haki ya kujua kuhusu afya za viongozi wetu.

Hapa simaanishi kila kitu kuhusu afya. Namaanisha tu ile kwa ujumla wake.

Kama mtu anaumwa, kalazwa, tuna haki ya kujua.

Mambo ya kuficha/ kufichwa halafu mnakuja tu kuambiwa mtu kaaga dunia, hayafai.
Hivyo, ningependa sana kujua kwa nini wananchi hatukupewa taarifa.

Na itokeapo fursa ingine ya Rais Samia au hata waziri mkuu Majaliwa kuongea na waandishi wa habari, ningependa kuona na kusikia wakiulizwa ni kwa nini hawakutufahamisha kilichokuwa kinaendelea.

Pascal Mayalla take note and spread the word.
 
Ndugu waache wafu walale, hata kama ukiambiwa leo hii sababu za kufichwa ugonjwa wa Mwendazake bado haitasaidia chochote kile.

Ukiambiwa sababu ndiyo Mwendazake atafufuka?

Rais Samia anamambo mengi sana ya msingi ya kuyashughulikia sasa hivi na siyo hizo petty issues za ugonjwa wa Marehemu.

Nchi iko kwenye wakati mgumu hii, tozo kila kona, inflation rate iko juu, covid-19 na makandokando ya chanjo yake, kesi za ugaidi, katiba mpya na jinamizi lake, wana CCM kila mmoja amekuwa kambare kila mtu anaongea na kupayuka hovyo hovyo halafu wewe unatuletea hadithi za marehemu?

Mwacheni huyu Madam ashughulike na hayo ya muhimu kwanza kabla hii nchi haijamshinda.
 
Can we let bygones be so?
No!

We have to hold our leaders [who work for us] to account.

They have a solemn responsibility to be forthright with us.

If we let bygones be bygones, we will be giving them the license to willy-nilly take us for a ride whenever they feel like it and they can invoke that bullshit to eschew their responsibilities knowing that no one cares to know.

I’m not here for it. You shouldn’t either!
 
No!

We have to hold our leaders [who work for us] to account.

They have a solemn responsibility to be forthright with us.

If we let bygones be bygones, we will be giving them the license to willy-nilly take us for a ride whenever they feel like it and they can invoke that bullshit to eschew their responsibilities knowing that no one cares to know.

I’m not here for it.
Sawa,
If it is so.,
Tusimbane Samia atleast she admitted the Man is sick prior his death..

Ilaa Katelephone alichosema dahhh.
 
Back
Top Bottom