Kwanini Serikali haijengi Techinical College Kanda ya Ziwa badala yake wanarundika vyuo vyote Dodoma?

Kwanini serikali ilundike mavyuo kanda moja na kusahau pengine? Sisi sote ni watanzania.
 
Punguza jaziba kama vyuo vya tech vipo moshi na arusha, na umbali wa moshi na arusha ni kilometre ngap? Na kwanini kanda nzima ya ziwa hakuna chuo cha tech au university ata kimoja au sisi sio sehemu ya hii nchi? au wanaangalia vigezo gani ili kujenga hivi vyuo? mtuambie na sisi tupate kukidhi hivyo vigezo ili watoto wetu nao wapate kusoma kwenye vyuo vya karibu na nyumbani
 
Ata miundombinu ya barabara nayo ni shida, hakuna maji na ziwa lipo karibu hii serikali hii!!!!!??
 
Achana na hii serikali ya mafala wasiojua potential ipo wapi ndo maana hili linchi litaaki hivi hivi miaka 1000, waendelee kujenga dar na pwani kwa watu wa huko ndo wanastahili kusoma na miundombinu bora.
Yaani serkali ya CCM itakuja kukumbuka shaka kumekucha mmetuchezea sana kanda ya ziwa tunashukuru Magufuli kutukumbuka! Yaani hata chuo kikuuu kimoja hamna?
 
Panapo na chuo kuna fursa nyingi za biashara sio tu elimu
Basi ungejenga hoja vizuri, ulitumia kichaka cha usomi, nikakuuliza huo usomi waliupatia wapi, si ni huko vyuo viliko? Au unaogopa kulipa nauli? Hujui ukilipa nauli Ally's Star, Isamilo, Zuber na wengine hunafaika?
 
Huko Mwanza mjengewe vyuo vya uvuvi, kama ni vyuo vya ufundi basi iwe ufundi baiskeli...
 
Hata vyuo vya afya tu wamegoma kuongeza hapa bongo vipo vi3 tu
 
Ushsuri mzuri.
Well said
 
Nimependa hoja nzuri
 
Wewe acha uzwazwa
Dar peke yake inachangia 89%
 
Dodoma ndio makao makuu ya nchi, wacheni wivu. Watanzania wote watasoma popote pale. Wacheni makao makuu papendeze.
 
Dodoma ndio makao makuu ya nchi, wacheni wivu. Watanzania wote watasoma popote pale. Wacheni makao makuu papendeze.
Ngoja tusubiri chuo kikubwa cha TEHAMA alichosema mama! Labda kanda ya ziwa itakumbukwa!
 
Ata miundombinu ya barabara nayo ni shida, hakuna maji na ziwa lipo karibu hii serikali hii!!!!!??
kitombile atlast umekuja kufunguka ukweli kaka😂😂 mi nilikuambia hii nchi yetu bado sana hii miji bado sana misri wanategemea mto nile tu unaotoka hapa kwetu lakini mwanza hapo maji meusi 🚶🚶
 
kitombile atlast umekuja kufunguka ukweli kaka😂😂 mi nilikuambia hii nchi yetu bado sana hii miji bado sana misri wanategemea mto nile tu unaotoka hapa kwetu lakini mwanza hapo maji meusi 🚶🚶
Kanda ya ziwa tuseme ukweli ni sehemu ambayo inajiendesha yenyewe bila msaada wowote wa serikali kabisa mfano Kuna ziwa maji shida,ukienda mijini barabara ndo shida kabisa mfano mwanza jiji kubwa vibarabara sasa ni kichekesho,kigoma na kagera ndo usiseme huko.Serikali imejitahidi kujenga kadaraja kabusisi/kigong kelele nchi nzima udhani kanajengwa Congo.Huduma za hospitali tunawashukuru sana kanisa katoliki la sivyo tungekufa kibudu,elimu sasa nako tushukuru kanisa katoliki la sivyo ni kifo cha mende.Ila sasa kila siku migodi mikubwa inafunguliwa na watu wanachoambulia ni kufa kwa kansa kwa sababu ya machemical ya migodi na mbuga kubwa za wanyama zipo kama serengeti.Serikali iwe makini sana la sivyo inchi yetu kuna siku itakuwa vipande vipande.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…