Kwanini Russia hataki kuwekeza kwenye Aircraft Carrier kama USA?

Hiyo kitu ikitakiwa kuzamishwa,itatumiwa water missile(Teoperdo) za kisasa. Haitakua ni shambulizi la Air to surface/water bali ni la water to water missile attacks, na hapo ndipo shida ya kuzilinda inapoanzia. Lakini hiyo ni possible kwa nchi kubwa kama Russia,China lakini pia hata Iran(huwez kuibeza Iran pia)
Zinaitwa TORPEDO/TORPEDOES.

Kuhusu hizo Torpedoes tayari nimekwisha ku-Address ama kulitolea ufafanuzi.

Moja ya jukumu kubwa la Battle Group ni kuhakikisha hayo yote uliyoyasema yanashughulikiwa.

Kuna vitu kama Electronic Warfare bila kusahau Anti-Submarine Warfare ambapo tayari uwekezaji mkubwa umefanyika hapo na kuhakikisha kuwa masuala mbalimbali ikiwemo kukabiliana na mashambulizi kama hayo hususani kupitia Submarines yanadhibitiwa.
 
Kufanya mashambulizi sio hoja. Hoja kuu ni kwamba Ikizamishwa ni hassra kuu. Na wamarejani wanasa kwenye vita yoyote kubwa adui Target yake ya kwanza ni Carrier.

Kufanya mashambulizi hilo haliba ubishi ila tambua kwa vita kubwa na chi zenye silaha za kuweza kuzamisha basi ni hatari.

Na tambua Nyambizi pia zina uwezo wa kuzamisha hizo Carrier.
Unazungumzia "vita kubwa" kwa muktadha gani?

Hiyo "vita kubwa" unaipimaje maana katika Modern Warfare vita kubwa ni Full-Scale Nuclear War na matokeo yake ni Mutual Assured Destruction.

Nimeelezea jinsi gani Carrier inavyoweza kuhimili mashambulizi na si kuhimili tu bali pia kuweza kukabiliana nayo kikamilifu kwa kutumia mifumo yake binafsi achilia mbali Carrier Group ambayo huipatia uwezo zaidi wa kutekeleza majukumu yake na mahali popote ilipo mifumo yote hii hufanya kazi kuhakikisha kuna usalama wa kutosha.
 
ICBM Sio Ishu
$ 4 billions watatengeneza,ila sio kwa quality na size ya Geradl R Ford...Hata inayobeba ndege 15 bado ni carrier..Halafu wazipaki kwenye maji gani,kila mahali barafu?..Mchina na anafyatua ma Carrier kila mwaka,je unafikiri nae hajaona faida yake?.Technolojia ya ICBM kila nchi sasa hivi wameshai master sio issue tena,wala kuwa na Nuclear sio issue tena sababu haunazo peke yako,..Lakini Navy Dominance sio kila nchi inaweza,inahitaji hela na budget kubwa,ndo maana hata mchina anapambana ili ku dominate pacific fleet...
Haupo siriaz MKUU
 
Acha kuongopa ndugu M16 zinauzwa mpaka madukani uko Marekani na silaha sio Kama pipi unauziwa ovyo tu hata izo unazosema zinauzwa mpakani ni kwa sababu ya vita mwisho wa siku zinangukia kwenye mikono ya watu Ila sio kwamba wanatoa moja kwa moja kiwandani.

Hata leo hii ukitaka silaha ya marekani unaenda Syria au Iraq au Afghanistan uwezi kukosa zipo Kama uchafu kwa sababu ya Vita wala hamna silaha adimu zaidi ya nuclear tu

Sent from my itel S33 using JamiiForums mobile app
Nilisikia kuwa Tz walinunua nyambizi kutoka North Korea by black market kuna kaukweli hapo ?
 
1574420668176.png

Hii ni Russian aircraft carrier, imejaa scandal sababu ya ukata. Kwanza ilikuwa inaitwa BAKU wakati wa USSR, Baada ya hapo ikabadirishwa jina na kuitwa Admiral Gorshkov.

Baadaye wakaiuza kama mtumba kwa India wakaibatiza jina la Vikramaditya maana yake "STRONGER THAN THE SUN"

Ikiwa safarini kuelekea india kutokea Russia mfumo wake wa kuzalisha umeme "boiler" ukapasukapasuka, Russia wakadai tatizo ni Matofari fake yaliyotumika kutengenezea hiyo boiler kutoka China
 
Bahari ilizo izunguka Russia na hari ya hewa yake ni disadvantage(hasara) kwa Urusi. Urusi kasikazini imepakana na bahari ya Arctic(barafu tupu), Mashariki(Kamchatika) Urusi ina eneo dogo la bahari lenye barafu muda mwingi, uku ikipakana na Alaska ya Marekani. Magharibi kasikazini(Baltic Sea) baridi pia ni Kali,pia kazungukwa na maadui Sweden, Finland na kazalika, uku akiwa na Pwani ndogo ya Santa Petersburgh. Kusini Magharibi( Black Sea/Sochi), hapo kidogo kuna Joto lakini pwani ni ndogo sana, amebanwa na Ukraine, Georgia Na Turkey. Kwahiyo kijiografia ya bahari ,Urusi akiwa na Carriers, zitatekwa mapema kwenye vita, sababu Urusi hana Makoloni ya mbali kuzilinda meli zake katika Missions. Marekani(USA), ana fedha, ana bahari zenye joto kusini(Savvana Texas, New Orleans, Miami, Kalolinas, e.t.c), ana bahari kubwa ya Mashariki ya Atlantic ambapo hakuna nchi au bara lingine mbele yake, anaenjoy Carriers suplimacy, USA ana bahari Magharibi (Pacific), anaenjoy suplimacy sababu hakuna nchi nyinhine mbele yake. USA ana Alaska, visiwa vya American Samoa, Guam, Hawaii, Solomoni islands, Puerto Rico na vingine vingi mbali na ardhi yake kumuwezesha kupaki Carriers zake kabla na baada ya Missions. USA ana faida kwa kila jambo kuliko nchi yeyote duniani.

Jamani fanyeni tafiti kwanza kabla ya kakalilishwa na propaganda za magharibi RAW!!

Hivi huna habari kwamba Urusi ndio inaongoza Duniani kwa kumiliki ICE BREAKERS NYINGI zenyewe uwezo wa kuvunja barafu hata ikiwa na ukubwa gani, haya mambo ya kudai eti Urusi haiwezi kupitisha meli zake za kivita na mizigo huko kasikazini kutokana na uwepo wa barafu all the year round. madai hayo ni ndoto za mchana.

Haya tuje kwenye masuala ya air craft carriers, binafsi nazichukulia kama ni floating coffins, sishangazwi na Bunge la Merikani kuhoji usalama manowali zenyewe pamoja na carrier group nzima, kitu cha kwanza ni rahisi kuzi target kutokana na spidi zike kuwa ndogo, pili saizi za meli zenyewe ni kubwa mno any formidable anti ship missile possessed by Russian, Chinese and Russian/Indian (BramhMo) won't miss them.

Narudia kusema kwamba hivi sasa tishio kubwa la air craft carriers na group zake ni Russian stealth high speed submarine drones laden with 400 Megatonne thermonuclear payload each, drones vile vile zina uwezo wa kupiga mbizi mpaka kwenye kina chenye urefu wa kufikia mita elfu moja Chini ya Bahari, hivyo, si rahisi kuzi-detect, sasa drone ikilipuliwa chini ya Bahari hakuna American aircraft carrier na group lake linaweza ku-survive mlipuko na Tsunami utakao sababishwa na Russian stealth submarines drones explosion - silaha hii ndiyo inamtia wasi wasi sana Uncle SAM na kibaya zaidi hana kinga dhidi ya tishio la Submarine drones.
 
😀 😀 😀 M16 zipo US kama uchafu,daah sasa kule si nyumbani mkuu??..Sawa na wewe kushangaa korosho kujaa mtaani mtwara..Mimi nazungumzia nje ya marekani,Hata huko Afghanistani nina uhakika kuipata M16 sio rahisi kama kuipata AK 47.
 
Wakati USSR inasambalatika, kulitokea na mgawanyo wa Mali, ivyo aircraft carrier iliyokuwepo wakati wa USSR iligawiwa kwa UKRAINE, na kwakuwa uendeshaji wa iyo kitu ni gharama, UKRAINE wakaiuza kwa India, ivyo Basi kutengeneza izo Carrier ni gharama na uendeshaji wake ni ghali pia....
 
Hahaaaa Mkuu kuna silaha za kuzamisha Carrier na zinabebwa na either Nyambizi au Ndege au meli. Kwa kifupi jua labisa China na Russia wana makombola ya kuweza kuazamisha carrier
Carriers azitembei tu kihole holela zipo well equipped to protect against any attacks, ndio maana hakuna anaezisogelea.

Ukiona ndege za Russia zinapaa karibu na carrier kwa mbwembwe jua wahusika washaona hizo ndege hazina silaha tangia zipo mbali.

Usijeshangaa kukuta carrier ina uwezo wa kurusha makombora 60 kwa pamoja ndani ya dakika chache sana na kila moja likafuata ndege au kombora linalo elekea kwakwe na zika reload kwa dakika chache sana kufanya assault hizo. Na inasindikizwa na submarine inapoenda kwenye mission meli yoyote ya hatari inazamishwa kabla aijafika; uliza Argentina kilichowakuta.

That’s a floating military base wanaozitengeneza wanafikiria yote.
 
Vita kubwa ni Vita inayo weza kihusisha Powerful countries, mfano China, Russia na Usa, hawa sio tu Silaha za atamizi bali pia wana kila aina ya silaha za hatari kabisa ambazo kamwe hazowezi fanya vita kuwa rahisi.

Na ndo nikasema hizo Carrier sio kwa vita kati ya USA na RUSSIA.
Unazungumzia "vita kubwa" kwa muktadha gani?

Hiyo "vita kubwa" unaipimaje maana katika Modern Warfare vita kubwa ni Full-Scale Nuclear War na matokeo yake ni Mutual Assured Destruction.

Nimeelezea jinsi gani Carrier inavyoweza kuhimili mashambulizi na si kuhimili tu bali pia kuweza kukabiliana nayo kikamilifu kwa kutumia mifumo yake binafsi achilia mbali Carrier Group ambayo huipatia uwezo zaidi wa kutekeleza majukumu yake na mahali popote ilipo mifumo yote hii hufanya kazi kuhakikisha kuna usalama wa kutosha.
 
Back
Top Bottom