Kwanini Russia hataki kuwekeza kwenye Aircraft Carrier kama USA?

Mmatumbi ambaye hujui hata kutengeneza bunduki unamuongelea Mrusi, Wabongo kujifanya wajuaji wa mambo ya nchi zingine tubatisha
Mkuu kwan ukifanya ukosoaji constructive tu utapungukiwa na nini?kama hujaona la kukufunza hapo kwann ww usitoe funzo kwa hoja mbadala?!au unafikiri hapa ni MMU?
 
Ak-47 ya Warusi inauzwa $ 150 wakati M16 ya wamarekani inauzwa $ 700.je! tukija kwenye ubora wa kazi ipi Bora Kama sio Ak-47.

Gharama ni mbwembwe tu kulingana na utengenezaji wako. Sio kwa sababu marekani anatengeneza kwa gharama ukajua kutakuwa na ubora mkubwa.patriot ya marekani ni Bei kubwa Sana kwa mfumo 1 Ila ukija kwenye uwanja wa Vita ni chujio

Sent from my itel S33 using JamiiForums mobile app
Hiki ndio kitu watu hawaelewi! Hata katika bajeti za mataifa mbalimbali, USA anaonekana kuwa na bajeti kubwa kwa sababu hizihizi.
 
Kutengeneza carrier ya kisasa mfano kama Gerald R.Ford (Nimitz Class),Ni $13 Billions.Ni pesa nyingi kwa budget ya Jeshi la Urusi kwa mwaka.Hio moja itakula almost 25% ya budget ya ulinzi ya Urusi.Sasa hapo ni kuchagua,watengeneze hiyo moja for that money au wanunue Units kama 20 za S500 surface to air missiles kutoka Almaz Antey..

Hizo bajet unazilinganishaje na nchi nyungine hiyo Nimitz ikiundiwa nchi kama urusi inakula 4B US dollar . Marekani kumlip tu kibarua wa kawaida ni dolala kama 20 wakati nchi nyingine hata dola hata 8 mpaka 9 wanapiga kazi
 
Masikini, ila ndiyo taifa linaloinyima usingizi hiyo US yako,,
Huu mjadala kama ungekua umekuja na jibu hili toka awali ulikua hauna haja ya kuendelea mkuu ulikua wapi sku zote hizo aseee


US Hali Halali Kwa RUSSIA
 
Kwenye kamati iliyoundwa na Bunge la Congress kuiangalia budget ya trump kwenye ulinzi, jamaa walikuja na jibu moja tu.
Kwenye vita kati ya US-China au US-Russia zote USA atapigwa vibaya, hakuna eneo anapoweza furukuta!!..
Achana na story za kwenye kahawa ndugu
 
Vita kati ya Marekani na Urusi au Marekani na Uchina ni vita kati ya nchi zenye nguvu kijeshi lakini haimaanishi na wala sio Guarantee kwamba ni vita kubwa.

Vita kubwa ni matokeo ya vita kutokana na aina ya vita inayopiganwa, silaha zinazotumika, idadi ya majeshi na mataifa inayojumuisha.

Ni rahisi sana kuzungumza kuizamisha Carrier kuliko kutenda na hilo limekwisha kufanyika kitaalamu na si 'kisisasa' ili kupata majibu ya uwezo wa hizi Carrier kimapambano.

Katika Conventional Warfare yoyote ile kati ya hizo 'nchi kubwa' itahusisha vitengo vya kijeshi zaidi ya kimoja. Hapa nazungumzia, kutakuwa na uhusika wa Air-Force n.k. kuweza kuiendesha hii vita.

Wakati wowote ambao Carrier inakuwepo katika majukumu yake, lazima kunakuwa na vitengo vingine vya kuiendesha Operesheni ya kijeshi ama vita.

Airforce inakuwa na jukumu la kuziwinda Missile Launch Facilities pamoja na Missile Batteries zilizopo katika Range ili kuzidhibiti kwa mtindo wa Electronic Warfare ama kuzishambulia kwa makombora pale inapobidi.

Navy inaiendesha Carrier Group inayohusisha pia Submarines za kisasa zitakazokuwa na kazi maalumu ya kukabiliana na hatari zote za majini hususani zile zitakazokuwa zikiiwinda Carrier.

Wakati adui anaiwinda ama anauwinda msafara wa Carrier Group atalazimika kuzipenya hizi Layers zote za kiulinzi na hili si jambo la kuleta ushabiki na maneno ya kisisasa. Ni jambo lenye madhara makubwa kwa jeshi lolote la adui litakalojaribu kufanya hivyo.

Ni kiasi gani cha Firepower atakacho Risk adui ili kutekeleza Mission kama hii ya kuizamisha tu Carrier huku pia akijaribu kuikabili Retaliation yake hata kama ni nchi yenye nguvu kijeshi kama China ama Urusi?

Uendeshaji na masuala ya kiulinzi ya Carrier Battle Groups ni suala la 'Uwezo' tu na hilo linafanyika kwa wenye uwezo huo. Mengine ni maneno tu ya kisiasa.
wakat waule msuguano wa us na Iran, Iran waliweza kuzisogelea hiz ceria na kuchukua picha ya kila kinachoendelea na namna wanavoweza kuzishambulia bila wao us kuona nahali yakua wanarada na mitambo yahali yajuu,,,

Nimesema hivi ili ujue nijinc Gan nchi zilizoendelea kitecnologia ya silaha ningum marekan kupigana nao, Mara nyingi San inakua namatisho nakuzowekea vikwazo lakin sio kuzishambulia Sina Maan kua zitaishinda marekan hapana ila hasara zitakazoitia nikubwa kuliko nandomaana wakishatasimin hasara yake wanaacha,
 
Watu wengi sana wamekuwa wanajiuliza hilo swali na kuona kwamba kitendo cha kuto kiwa na hizo aircraft carrier ni kosa kubwa mno kwa Urusi.

Billi Clinton, Rais wa Zamani wa USA aliwahi kusema kwamba Endapo kutatokea Vita kubwa cha kwanza USA watakacho jiuliza ni je ziko wapi aircraft carrier?

Ziko salama huko ziliko?

Maana yake ni kwamba aircraft carrier za USA si salama kabisa kwa Major War na nni hatari tupu na ukisoma hata Wachambuzi wa kivita wanasema kwa vita kubwa kabisa inabisi USA afiche aircraft carrier zake.

Kwa nini?
1. aircraft carrier moja inaweza kuwa na askari na wafanyakazi wapatoa 15,000/ hii ni hatari mno kwa shambulio moja tu inakuwa ni hasara ya karine kwa Usa.

2. Kwa sasa nchi kama China na Russia tiyari wana Makombola ya kuweza kuzamisha Meli hizi za USA hii ndo huwa kila mala inaibua mijadala hata kwenye Bunge la Marekani.

3. Hasara kubwa itakayo patikana endapo Meli hii itazama. Kumbuka ni Meli ghari sana sasa inazamishwa na Ndege kama 30 au 7p hivi plus wanajeshe kama 15,000.

Uki google kuna Mijadala sana kwenye Bunge na hata Congress ya Marekani kuhusu aircraft carrier kama bado zinahitajika au la.

Urusi kuona hivyo ndo maana yeye nawekeza kwenye Meli za kawaida na Nyambizi pamoja na Makombola mengine.

Aircraft carrier ni kwa Vita na nchi ndogondogo hizi ambazo hazina techinolojia ya kutosha kuweza kuzamisha hizo meli.

Ila huwezi peleka aircraft carrier kwenye Full war na Nchi kama China au Urusi.

Kwenye Fullu War hizo aircraft carrier zita fichwa kabisa make kwanza ndo zitakuwa Target namba 1 make mpigo mmoja impact ni kubwa sana.

HIVYO Urusi haoni haja ya kuwa na aircraft carrier kwa sababu hajiandai kupigana na nchi ndogo bali kubwa na nchi kubwa hizo aircraft carrier hawezi zipeleka mbele kamwe.

Urusi ana jiandaa na Silaha za masafa marefu anaipiga New York akiwa Moscow.

😁😁😁 Mimi natabasamu tu kwa sababu kuna mataifa ambayo hayawezi kupigana direct war hata siku moja kwa sababu yana nguvu ambazo almost ni sawa.

Marekani Urusi na china hawawezi kupigana vita vya moja kwa moja kwa sababu kwanza hakutakuwa na mshindi.

Na USA, Russia na China iwapo watapigana direct war basi jua kuwa hakuna kitakachobaki duniani maana hapa silaha za nuclear hazitaepukika kutumika na nafikiri unajua jinsi Nuclear weapons zinavyofanya destruction, that's why nakwambia wakipigana hawa hakuna kitakachobaki duniani, duniani nzima itageuka kuwa jangwa na mtasahau kuwa binadamu aliwahi kuishi duniani 🤔🤔🤔
 
Eyi uwanja wa ndege!!! Mkuu I naelewa unachokizungumzia kweli?
Carrier inapoenda kwenye mission kunakuwa na carrier group. Katika hii group kuna ckrvettes(sub hunter), destroyer(ulinzi wa anga, SAM systems), subs na supply ships. So carrier inabaki na kazi ya kubeba ndege kuzisogeza karibu na war theatre. So huenda jamaa anasema ukweli, its just a mobile airport.
 
Kujenga silo + kutengeneza kichwa cha nuklia na kombora lake unajua ina cost bei gani ndugu
Sijui mkuu, tujuze tuongeze maarifa.

Mkuu kuhudumia hizo carrier si mchezo alafu kumbuka silaha nyingi za nyuklia za Urusi ya Sasa zilitengenezwa toka enzi za USSR kipindi uchumi upo imara.
 
Kuna sababu nyingi kwanini Russia haina Aircraft carrier nyingi kama USA, Sababu zake zina mizizi milefu ambayo ilikuwapo kabla hata ya Russia ya sasa yani zilikuwapo tangu kipindi cha USSR, Soviet Union ilikuwa na uchu wa kutaka kuwa na jeshi kubwa la majini lakini kuna vikwazo vingi vilivyo zuia jitihada hizo na vikwazo hivyoviyvo ndio vilivyolithiwa na Russia ya sasa.
Russia mpaka sasa ina Aircraft carrier moja tu inayofanyakazi ambayo ni Admiral Kuznetsov, hii ilianza kutumika mwaka 1990, na zilitakiwa ziwe mbili lakini moja haikufanikiwa kumalizika na ilitelekezwa baada ya kuvunjika Umoja wa Kisoviete, ilikuwa chuma chakavu mpaka China ilipo inunua kutoka Ukraine mwaka 1998, hii ndio imekuja kuwa Liaoning, Na hata hiyo moja iliyo baki bado haina uwezo wowote wa kivita bali ni mkangafu tu, moja ya operation yake inayo kumbukwa ni ile ya Syria ya mwaka 2016 ambapo kelele za vyombo vya habari vya Russia viliipamba wakati wa operation hiyo na hakukuwa na matokeo yeyote katika uwanja wa vita zaidi ya kupoteza ndege mbili kwenye operation hiyo na tangu tarehe 15 Oktoba 2016 wakati ikiwa inatoka Kola bay, mwanzoni kabisa wa operation hiyo Kuznetsov ilionesha kutokuwa na imani na utengemavu wake ambapo ilibidi iongozane na na meli zingine saba (7) za kijeshi ikiwemo Pyotr Velikiy hii ni battlecruiser inayotumia nuclear kama chanzo kikuu cha nishati, pia iliongozana na Udaloy-class destroyers mbili swala ambalo ni la kawaida kwa Aircraft carrier kuongozana na kundi kama hili lakini uwepo wa Tugboat ulionesha hakuna ukawaida bali kuna chombo kibovu kinachotiliwa shaka kwa maana kazi kubwa ya Tugboat ni sawa na za gari za Breakdown yani kuvuta meli mbovu. Tangu iliporudi kutoka kwenye kampeni ya Syria mpaka sasa Admiral Kuznetsov ipo tu inafanyiwa ukarabati na si combat ready hii inaonesha wazi kuwa Russia haiwezi kumudu gharama za kukarabati kikamilifu vyombo vikubwa kama Aircraft carrier maana kuna nyingine ambazo zilitelekezwa bila ya ukarabati hadi kufikia hatua ya kuwa decommissioned.
Zipo sababu nyingi za Russia kushindwa kufikia malengo ya kuwa na jeshi kubwa la majini lenye Aircraft carrier nyingi, kwa mimi binafsi nahisi ni kama zifuatazo;

Kwanza kabisa Russia haina nguvu za kiviwanda, hakuna assembly line za kuaccommodate miradi mikubwa kama ya kuunda aircraft carrier na kama ina mpango wa kumiliki kwa wingi nyambizi hizi inapaswa kuagiza kwa nchi kama china au counterpart wake USA, ukilinganisha na uweza wa marekani kwenye nguvu za kiviwanda au China ya sasa, na hii hoja inadhihilishwa wazi kipindi cha WW2 USA ilikuwa inauza siraha na mahitaji ya vita kwa nchi zote za Allied forces mpaka Russia yenyewe na Marekani iliisaidia sana Russia kwenye vita hii, Henry Tzard aliona ni bora kukabidhi kwa USA vumbuzi zote za kivita na sayansi za Uingereza ili tu iweze kutumia Assembly line za USA. Kama ulikuwa haujui, jumla ya Ammunitions ambazo USA ilizarisha katika kipindi cha 1943 mpaka 1945 zinaweza kutokemeza population ya sasa ya dunia mara 11 net.

Pili mazingira ya kijiografia, Russia haijazungukwa na maji mengi kama ilivyo USA, na hata sehemu zenye maji bado hazipo kwenye tension ya kufanyikia vita yani sio sehemu za kimikakati ya kivita hususani eneo la bahari ya Arctic ambalo sehemu kubwa ni polar kiasi kwamba hata Aircraft carriers zinaweza kupata changamoto nyingi na kiuchumi ns ufanisi si salama kuoperate hizi meli kwenye barafu ngumu na nene kama za Arctic, Arctic Ocean huwa ni sehemu Russia inaogopa sana kushambuliwa lakini kimkakati si sehemu tishio kama inavyodhani. Admiral Kuznetsov ni moja ya vessels zinazounda Arctic Fleet maarufu kama Red Banner Northern Fleet ambayo kwa sasa inajulikana kama White Sea Flotilla, Ukiacha Finnish blokade kwenye kikosi cha Petsamo kipindi cha Winter War ya 1939 na 1940, engagement nyingi za kamandi hii huwa zinatokea Atlantic ocean hii inamaana kimikakati eneo kubwa la maji yanayo pakana na Russia si tishio kiasi cha kuhitaji kuwa na Aircraft carrier nyingi, kitu ambacho ni tofauti kwa USA ambae anapaswa kujirinda katika bahari ya Pacific sehemu ambayo haina historia nzuri kwenye vita, hii ni sehemu ya kimkakati sana kwa USA kwenye kurinda masilahi yake kwenye nchi za Asia lakini pia kurinda pwani ya magharibi (west coast) United States Indo-Pacific Command (USINDOPACOM) zamani United States Pacific Command (USPACOM) ina jukumu la kurinda zaidi ya maili milioni mia moja (100) za mlaba hii ni sawa na asilimia 52 ya eneo lote la uso wa Dunia.

Tatu, Russia anaoneka kuvutiwa sana kwenye kuwa na nguvu za ardhini yaani land powers, hii ni kutokana na mahusiano na nchi anazopakana nazo, na historia ya vita za nyuma, ukiacha Russo Japanese war 1904-1905, Vita nyingine zote za Russia kama WW1 and WW2 uwanja wa vita ulikuwa ni main land ya Russia, Kwa sasa Russia inahisi maeneo hatari ni mipaka inayo pakana na nchi za kibeberu sanasana Ulaya ya magharibi ambapo nchi nyingi inapakana nazo kwa ardhi.

Nne Russia, imewekeza sana kwenye ballistic missile na nyingi ni intercontinental long-range missles mfano mzuri ni makombora aina ya РС-28 Сармат yanayo julikana na NATO kama SS-X-29 au SS-X-30 haya ya operational range ya zaidi ya kilomita 18,000 na yana kasi ya zaidi ya mara ishirini (20) ya sauti yani Mach 20.7 sawa nazaidi ya kilomita 7 kwa sekunde, makombora ya hivi yanadhihirisha wazi kuwa hakuna haja ya kuwa na platform kama Aircraft carrier ili kumsogelea adui kwa maana yana uwezo wakufika mahala popote hapa duniani.

Hata hivyo Russia bado ina nia ya kuendereza mpango wake kupanua vikosi vya majini hii ni pomoja na kuwepo kwa mpango ulio vunjika wa kununua Aircraft carrier mbili kutoka Ufaransa ambapo Ufaransa iliasitisha mazungumzo hayo baada ya Russia kuvamia visiwa vya Crimea, Pia Russia ina mpango wa kumiliki Aircraft carrier sita (6) ifikapo 2025 japokuwa si mpango wa kuaminika kwani Russia imejawa na siasa na propaganda za kikomunisti ambazo huwa si rafiki kwenye uvumbuzi wa mambo ya kivita kwa kuwa watu binafsi hawapo huru kufanya tafiti za kivita kwa lengo la kuja kuizia serikali, jambo ambalo ni tofauti kwa Marekani ambao wao wanasoko huria na kila mtu anaweza kuiuzia serikali ubunifu au uvumbuzi wowote wenye lengo la kuboresha nguvu za kijeshi za nchi.​
 
Watu wengi sana wamekuwa wanajiuliza hilo swali na kuona kwamba kitendo cha kuto kiwa na hizo aircraft carrier ni kosa kubwa mno kwa Urusi.

Billi Clinton, Rais wa Zamani wa USA aliwahi kusema kwamba Endapo kutatokea Vita kubwa cha kwanza USA watakacho jiuliza ni je ziko wapi aircraft carrier?

Ziko salama huko ziliko?

Maana yake ni kwamba aircraft carrier za USA si salama kabisa kwa Major War na nni hatari tupu na ukisoma hata Wachambuzi wa kivita wanasema kwa vita kubwa kabisa inabisi USA afiche aircraft carrier zake.

Kwa nini?
1. aircraft carrier moja inaweza kuwa na askari na wafanyakazi wapatoa 15,000/ hii ni hatari mno kwa shambulio moja tu inakuwa ni hasara ya karine kwa Usa.

2. Kwa sasa nchi kama China na Russia tiyari wana Makombola ya kuweza kuzamisha Meli hizi za USA hii ndo huwa kila mala inaibua mijadala hata kwenye Bunge la Marekani.

3. Hasara kubwa itakayo patikana endapo Meli hii itazama. Kumbuka ni Meli ghari sana sasa inazamishwa na Ndege kama 30 au 7p hivi plus wanajeshe kama 15,000.

Uki google kuna Mijadala sana kwenye Bunge na hata Congress ya Marekani kuhusu aircraft carrier kama bado zinahitajika au la.

Urusi kuona hivyo ndo maana yeye nawekeza kwenye Meli za kawaida na Nyambizi pamoja na Makombola mengine.

Aircraft carrier ni kwa Vita na nchi ndogondogo hizi ambazo hazina techinolojia ya kutosha kuweza kuzamisha hizo meli.

Ila huwezi peleka aircraft carrier kwenye Full war na Nchi kama China au Urusi.

Kwenye Fullu War hizo aircraft carrier zita fichwa kabisa make kwanza ndo zitakuwa Target namba 1 make mpigo mmoja impact ni kubwa sana.

HIVYO Urusi haoni haja ya kuwa na aircraft carrier kwa sababu hajiandai kupigana na nchi ndogo bali kubwa na nchi kubwa hizo aircraft carrier hawezi zipeleka mbele kamwe.

Urusi ana jiandaa na Silaha za masafa marefu anaipiga New York akiwa Moscow.
Kuna mambo upo sahihi, lakini kuna mambo haupo sahihi, Aircraft ndio tumani la mwisho kwa USA, na wala si sehemu hatari, Wamerekani watauliza kuwa zikowapi sio kwa kuogopa kama zitakuwa zimezama, bali wataogopa kupoteza tumaini lao la mwisho. Nikupe kisa cha zamani kidogo, Aubuhi ya tarehe 7 mwezi wa 12 mwaka1941 wakati Japani inashambulia Pear horbor, yalitokea makosa mawili yaliyo igharimu Japani kupoteza uwezekano wa kushinda vita kabisa.

Kwanza kabisa licha hasara kubwa iliyo fanywa na vifo vya askari ambao hawakujianda kivita, Japani hakuweza kuipata hata Aircraft carrier moja. Battleships, cruisers, destroyers na boat zongine nyingi zilipatwa lakini Aircraft carrier hazikuguswa unajua sabubu ni nini, Aircraft carrier ni sawa na vikosi zinapo tia nanga ni biashara na zinapo sail ni biashara, kama Mitsuo Fuchida angeweza kurudisha muda nyuma ilikuwa ni kwaajiri ya kuzitafuta wapi zilipo kambi hizi za majini.

Pili wakati, mapaka USA imejipanga kuzuia mashumbulizi ya Pear harbor, Japani haikufanikiwa kabisa kugusa matenki ya mafuta kwaajiri ya meli za kivita, kitu ambacho kama Isoroku Yamamoto alimlaumu Mtsuo Fuchida ni huu upumbavu wa kuacha tenki zile za mafuta,
Maana licha ya maafa yaliyo wakumba wamarekani lakini walivyogundua kuwa Kambi hizi za majini na tenki za mafuta hazijiathiriwa na shambulio hilo, walishagiria sana kwani waliona uelekeo wa kushinda vita upo upandewao.

Hapo ni enzi hizo, kwa sasahivi mifumo na fleet zinazo kuwa pamoja kusindikaza hizi Manuawali ni disaster mzee. kwanini si rahisi kushambulia Aircraft carriers?

Kipindi cha vita baridi, aircraft carrier zilikuwa zipo hatarini zaidi, kwa maana ukilinganisha size yake na maendeleo ya makombora ya masafa marefu yenye ufanisi wa shabaha wa hali ya juu, ilikuwa sirahisi kwa mtu kuikosa Aircraft carrier kwa ukubwa wake, lakini leo hii Fleet kubwa ya Aircraft carrier za US ni Nimitz class ambazo zimeboreshwa na zote ni nuclear powered, Nimitz class zinaweza kwenda kwa kasi ya maili 35 kwa saa hii inamaana ndani ya dakika 30 inaweza kuwa sehemu yeyote ndani ya maili 700 za mlaba na baada ya dakika 120 inaweza kuwa popote ndani ya maili 9000 za mlaba, hii inamaana mpaka ICBM inafikia target ya awali, yenyewe itakuwa imeshaondoka muda mrefu sana, na hii hoja inaungwa mkono na moja ya masharti ya kudeploy Aircraft carrier ni kuwa haitakiwi kusima inapotoka safe harbor na huwa zipo kwenye mwendo muda wote.

Nimitz class, zinatumia nuclear, maana yake zinaweza kwenda umbali wowote bila ya kuhitaji kujaza mafuata kwa kipindi cha zaidi hata ya miaka ishirini (20), maana yake inauwezo mkubwa wakumanuva baharini na kucheza michezo yeyote kuraghai na meli za adui bila hofu ya kusuburia tanker kwaajiri ya kujaza mafuta, umbali ambao Nimitz class zinaweza kwenda ni mbali kuliko vyombo vingi vya majini vya sasa vinapoweza kufika na zinauwezo wa kupambana na hali zote chafu za bahari.

Ndenge zinazokuwa kwenye Aircraft carrier zinaweza kuzuia shambulio lolote lenye lengo la kutaka kuangamiza meli hizi, Nimitz class kama USS George H.W. Bush huwa ina squadron ya airwing inayohusisha ndege aina ya McDonnell Douglas F/A-18 Hornet hii ni multirole fighter jet ambayo inaweza kuruka kwa haraka na kuact kama Fighter, Air superiority, interceptor na Attack Aircraft, pia huwa zinakuwapo ndege aina ya Lockheed Martin F-35 Lightning II hii ndege pia si ya mchezo mchezo, maana na yenyewe ni Multirole fighter jet na pia F35B ambazo ni kwaajiri ya kutumika na jeshi la maji zinaweza kuruaka kwa haraka ikwa pamoja na vertical take-off and landing, F35 inamifumo ya kielektroniki ikiwemo mfumo maarufu wa C3 yani command communicate and control, pia kuna mifumo kama Sensor fusion, spread aperture na network centric warfare inazipa uwezo ndege hizi kujua na kusadia kumpa taarifa pilot aweze kufanya maamuzi ya kumaliza kazi aliyotumwa kwa haraka na umakini wa hali ya juuu, hizi ndege zina high precision guided missles ambazo zinaweza kuintercept kombora lolote lilokusudiwa kwenda kuipiga Aircraft carrier.

Sensors zilizo fungwa kwenye Aircraft carrier pia zimeunganishwa na vifaa vingine vya jeshi. Jeshi la Maji la Marekani limetumia miongo kadhaa kujua jinsi ya kuunganisha vifaa vyake vyote vya vita vilivyotawanyika kwenye mtandao mmoja. hivyo Aircraft carrier hazitegemei tu sensor zake kujua kama ipo hatarini au la, Aircraft carrier huwa inapokea na kuchakata habari endelevu kutoka kwa meli za kivita na nyambizi za chini ya bahari, kutoka kwenye drones na ndege za upelelezi na hata kutoka kwenye satelaiti za upelelezi. Sio tu kwamba Aircraft carrier zinakuwa na situational awareness popote itakapokuwa yaani (uelewa wa kina juu ya hatari zinazoweza kutokea), pia zinaweza kutumia silaha za meli na vifaa vingine vya kivita vilivyopo mbali ili kuzuia vitisho ambavyo vinaweza kuikabili.

Pia hata siku moja hautaiona Aircraft carrier inaenda nyenyewe kwenye operation yeyote ile, ukiona imetumwa sehemu ujue ni kundi la vifaa hatari huwa vinaisindikiza, popote itakapokwenda huwa inakuwa na meli nyingine nyingi za kivita, hapa utakuta Anti submarines, battle ships, destroyers, interceptors ambazo zina makombora ya kulinda anga na maji bila kusahau nuclear powered attack and ballistic submarines na zote huwa zinaenda kwa mfumo ambao umelenga kuikinga Aircarft carrier, huu mfumo huwa na matabaka matatu ambayo yote yana ufanisi wa zaidi ya asilimia 80. Mzee kiufupi you can't touch the Matriach because the Matriach is the Liverpool and the Liverpool will never walks alone, fuatilia mara ya mwisho armada ya USA mwaka 2017 kwenye penisula ya Korea jinsi USS Carl Vinson ilivyoongozana na vyombo vingine, trust me ni nusty idea kujaribu ujinga wowote ule.

Licha tu ya kulindwa na vyombo vingine Aircraft carrier zina mifumo yake ya kujilinda, huwa zinakuwa na makombora ya Surface to Air, sensor, na mifumo ya kukomandi na kubadiri target za makombora ya adui, kuna mifumo ya automatic ya bunduki zenye calliber kubwa, kiasi kwamba ufanisi wake ni wa hali ya juu kuliko hata wa binadamu, kuna mifumo ya kuzuia makombora ya majini na Torpedos, sensor zenye uwezo wa kukagua flow ya bahari na kujua chini kuna nini.

Kiufupi Russia haina uwezo na bajeti kwa sasa kumiliki hizi meli ndio maana imeoptout lakini kwa USA, Aircraft carriers ni moja ya last line of deffense katika taifa lao na hawata acha kumili sasa wala kesho na zitaendele kuundwa kila zitakapo hitajika. Kwa kumbukumbu zilizo kuwepo ni mara moja tu ambapo US Aircraft carrier USS Ronald Reagan imewahi kuzamishwa na sio kuzama kiukweli ukweli bali ni kwenye simulation za michezo ya kivita mwaka 2005, Nyamibizi iliyo fanikiwa kuizamisha inatekinolojia ya hali ya juu na ipo kimya kiasi kwamba hakuna sonar sensor inayoweza kuisikia, Nyambizi mpya za Swideni zinazo tumia hybrid injini ya dizeli na umeme na hazina uwezo wa kukaa chini ya maji kwa muda unaozidi wiki mbili hivyo si rahisi kuweza kupambana kwenye high water bila ya kuhitaji tanker ili ijaze mafuta.
"If you bring wars in their homes they will lose their homes"
 
Back
Top Bottom