Kwanini Rais wa Kisiwa cha Puerto Rico analindwa sana wakati hiki Kisiwa kinasifika kwa amani duniani?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,689
109,117
Tokea Rais wa hiki Kisiwa cha Puerto Rico aingia madarakani sasa nadhani anamaliza mwaka wake wa pili kama siyo wa tatu Sisi Wakazi wa huku tumekuwa tukishuhudia mara kwa mara jinsi Ulinzi wake ulivyokuwa mkali hadi unatisha kiasi kwamba kuna muda Rais wetu huyu anaweza akawa tu anataka kuongea na Sisi wana Kisiwa wake lakini kwa ule Ulinzi wake tu huwa tunakimbia kwa uwoga.

Na kinachotushangaza sana Sisi wana Puerto Rico ni kwamba hiki Kisiwa chetu tokea huko nyuma kinasifika kote Ulimwenguni kuwa kinaongoza kwa amani na utulivu sasa tunashangaa huyu Rais wetu huu Ulinzi wake mkali huu unatokana na nini labda? au ameshaambiwa kuna hatari inatuijia wana Puerto Rico?

Natamani sana huyu Rais wa Puerto Rico japo yuko mbali Kijiografia angepata hata muda tu wa kuona aina ya Ulinzi aliokuwa nao Rais wa Kwanza wa Tanzania na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Burito Nyerere labda angejifunza Kitu kwani hakuwa na Ulinzi mkubwa na mkali japokuwa ' Mabeberu ' walikuwa wakimvizia ila alilindwa mno na ' Dua ' njema za Wananchi wake aliowaongoza na waliokuwa wakimpenda huku hadi leo wengi wao wakiwa wanamlilia.

Jamani wana JamiiForums karibuni sana huku Kisiwani Puerto Rico japo kusema ukweli nimepakumbuka mno nyumbani nchini Tanzania na sijui ni lini nitarudi kwani siku hizi huku kuna Sheria Kali za upataji wa Pasipoti na Viza kwa Kusafiri.

Nawasilisha.
 
Sababu wanazijua wenyew walinzi wake sio kila kitu ukijue mzee
 
Puerto Rico ya Tanzania

Naomba jiheshimu basi tafadhali na kuna mada ambazo GENTAMYCINE huwa nafanya sana ' Ukomedi ' wangu mliouzoea lakini siyo hii sawa? Mimi nipo huku Kisiwani Puerto Rico na ndiko makazi yangu yalipo siku nyingi hivyo nimemaanisha kweli huku huku niliko na ya huko Kwenu Tanzania labda uliko Wewe sasa Mimi siyajui labda unihadithie tu Wewe.
 
Nimekuelewa mkuu
 
Back
Top Bottom