Nchimbi na Makonda, natambua mngependa marafiki zenu wawe ma DC na Wakurugenzi. Lindeni sana kumwelekeza Mkuu wa TAMISEMI (Mhe. Rais) adharani

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
Kutumbuana kunarudisha nyuma maendeleo ya nchi yetu. Makonda kaenda pangani kakutana na mkurugenzi aliyewahi kukorofishana naye kisha amemwelekeza waziri atumbue uteuzi wake huku akijua kabisa wakurugenzi wanateuliwa na Mhe. Rais.

Sitashangaa Makonda kuwa na kiburi chukumwelekeza Mhe. Rais atumbue na kuteua bila kuweka wazi sababu za kufanya hivyo. Tukumbuke huu utaratibu unatumia gharama kubwa sana ambazo hazina tija.

Viongozi wenye kufahamu mifumo ya utendaji wa serikali wanapofanya ziara kama anayofanya nchimbi na Makonda huwa wanaandika ripoti ya kazi. Kupitia hiyo ripoti ndipo ueleza hali waliyokutana nayo kisha kupendekeza wapi panapwaya na nini kifanyike.

Kupitia ripoti hiyo wasaidizi wa Mhe. Rais akiwepo Karibu Mkuu Kiongozi upitia ripoti husika na kufanya uchambuzi ikiwemo kuverify yale yaliyoelezwa kisha kushauri MAMLAKA ya uteuzi nini wafanye..

Mfumo huu unasaidia sana separation of power lakini pia unaondoa hiki kinachotokea sasa cha mtu kumchukia mtendaji kisha anaagzliza aondolewe. Tukiendelea na huu utaratibu wakitibu mwenezi kumwelekeza Mhe rais atumbue tena akiwa kwenye jukwaa tunashusha hadhi ya mamlaka yake.

Lakini pia kwa upande mwingine aliyependekeza kwenye jukwaa aondolewe asipoondolewa utaona umedharaulika. Natumaini hii misingi walipaswa kuisimamia akina Kinana kwa sababu wapo muda mrefu kwenye mfumo wa chama na serikali. Muundo wa sasa wa TAMISEMI upo kwa Mhe. Rais hivyo unapofanya kosa ukatoa maelekezo unamwelekeza Mhe.Rais na siyo Waziri.

Vijana tupunguze miemuko na cheap popularity tufanye kazi kisayansi. Tujifunze kutoa nafasi kwa wakubwa zetu waweze kuheshimika kuliko sisi kujiona ndio kila kitu.

Fanyeni ziara zenu, kamilisheni kazi, andikeni ripoti na mtoe mapendekezo kisha mpeni Mhe.Rais muda wa kutafakari na kutoa maamuzi ya haki. Kama mtaendelea kudhani TAMISEMI ni Mchengelwa mtakuwa mmepotoka. Mamlaka ya uteuzi kwa TAMISEMI ni Mhe. Rais.

Mkitaka kutuelewa sisi wazee wenu mtatuelewa ila mkishupaza shingo mtaishia kufanya siasa majukwaani zisizo na matunda. Kila mtu ana mtu wake, hii ni zamu yenu itumieni kwa busara na hekima.
 
Kama nawee ni mzeee wa kuongea mfano, basi hili Taifa Lina wazee wajinga.

Huu ujinga Huu ndio umetuchelewesha , acheni kushauri uozo Kwa kuhisi ndio Hekima.

Mtu anafanya ujinga , ujinga wa wazi kabisa, basi angefanya ujinga Mmoja, pengine unaweza dhan anasingiziwa, wee Kila Mahali Raia wanakunyooshea vidole tu, Kila Mahali ni malalamiko juu yako

Alafu bado uhitaji Tume, Mara kuandika vile Mara vilee, yaan Makonda atakapomaliza Ziara ya mikoa 20, Kila Mahali alipopita aandike Ripoti , Sijui nani aisome, Kisha aone hapa inafaa kumfikishia Rais ??.

Ndo sasa maamuzi yafanyike??.

Hivi nani ameturoga?.
 
Kutumbuana kunarudisha nyuma maendeleo ya nchi yetu. Makonda kaenda pangani kakutana na mkurugenzi aliyewahi kukorofishana naye kisha amemwelekeza waziri atumbue uteuzi wake huku akijua kabisa wakurugenzi wanateuliwa na Mhe. Rais...
Bwashee kumbe ni wewe Mkurugenzi wa Pangani? Mbona ukiwa live ni mweupe hivyo kichwani?
 
Kutumbuana kunarudisha nyuma maendeleo ya nchi yetu. Makonda kaenda pangani kakutana na mkurugenzi aliyewahi kukorofishana naye kisha amemwelekeza waziri atumbue uteuzi wake huku akijua kabisa wakurugenzi wanateuliwa na Mhe. Rais...
Separation of power is merely a, wastage of time. Obviously, we need action in order to reach our goal.
 
Hoja yako ingekuwa na nguvu na kueleweka vyema sana kwa wote wasomaji ikiwa ungeonyesha kuwa ni wapi mkurugenzi husika alikosana na kupishana na mheshimiwa Makonda. Pia ungeeleza ni vipi na kwa ushahidi upi maelezo yako na kitendo cha Mheshimiwa makonda kuwa kinasukumwa na chuki binafsi.pia ungeeleza na kujikita katika kueleza kuwa yake aliyotuhumiwa na kulalamikiwa na wananchi kuwa siyo ya kweli na kwamba ni vipi wanamsingizia.

Lakini umetoa tuhuma isiyo na ukweli wala uthibitisho kuwa hatua zinazochukuliwa na chama zidi ya watendaji na viongozi wanaofanya kazi kwa mazoea zina lengo la kupachika watu wao. Na vipi watapachika watu wao wakati hata wewe mwenyewe unasema anayeteua ni Rais .

Mwisho ningependa kukwambia kuwa ni lazima tukomeshe na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.tuache watanzania kuleta umungu mtu katika ofisi za umma . Tuwe wanyenyekevu tuwapo kwenye ofisi za umma. Huo ni ushauri wangu kwenu ninyi mlio maofisini.

Sisi wananchi tunataka huduma bora kutoka kwenu ,tunataka tufikapo katika ofisi za umma tupokelewe vizuri ,kusikilizwa na kupewa huduma stahiki na kwa wakati. Na siyo kuzungushwa mwaka mzima .
 
Back
Top Bottom