Kwanini Profesa Lumumba alikuwa akimsifia Hayati Rais Magufuli?

Oct 13, 2018
35
259
Na Thadei Ole Mushi.

Tumekuwa tukiona Mara kwa Mara Prof Lumumba wa Kenya akimsifia Sana Rais Magufuli. Watu wengi hujiuliza kanunuliwa? Au ana interest gani na Rais Magufuli au na Tanzania? Leo nitawapitisha katika eneo Moja tu la kwa Nini huwa wanaona Mh Magufuli ni Rais Bora wa kipindi hiki wakilinganisha na wa kwao Uhuru Kenyata. Twende sawa.....

David Ndii mwanauchumi wa Kenya aliwahi kusema Kuna haja ya kutafiti kama Ziara za Rais Kenyata nje ya Nchi Zina Manufaa. Duru za Kibajeti nchini Kenya zinaonyesha kuwa Rais Kenyata ametumia matrilioni ya Shilingi katika safari zake nje ya Nchi.

Kwa miaka sita tu Rais Kenyata kufikia 2019 alikuwa ameshakwea pipa Mara 92 kuhudhuria shughuli mbalimbali nje ya nchi shughuli nyingi zikiwa Ni kuaapishwa na kutafuta Mikopo kwenye mataifa ya Kibepari.

Mwaka 2015 pekee Rais Kenyata alisafiri safari 21 katika mwaka mmoja. Kwa miaka mitano ya Kwanza Kenyata alisafiri zaidi ya Mara 43 nje ya Nchi huku mtangulizi wake Mwai Kibaki kwa miaka 10 alisafiri Mara 33 tu. Wachambuzi wa Mambo nchini Kenya wanakosoa vikali Sana Kitendo Cha Rais Kenyata kusafiri Mara kwa Mara na kuligharimu Taifa Hilo mabilioni ya Shilingi.

Hali ipoje kwa Tanzania?

Kwa miaka Mitano Rais Magufuli alitoka nje ya mipaka ya nchi yetu Mara 8.

Safari ya kwanza aliifanya Tarehe 6-8 Mwezi wa nne mwaka 2016 ambapo nchi ya kwanza kuitembelea ilikuwa Rwanda. Siku ya kwanza Rais Magufuli alikutana na Mwenyeji wake Rais Kagame mpakani Rusumo ambapo walizindua one stop border na kufungua Daraja la Rusumo. Siku ya Pili Rais Magufuli alihudhuria maadhimisho ya miaka 22 ya mauaji ya Kimbari Rwanda.

Safari ya Pili alikwenda Uganda ambapo alisafiri Tarehe 12 Mwezi wa tano 2016. Wakati Rais akipanga kwenda Uganda Mezani kulikuwa na mwaliko wa kuhudhuria mkutano wa Ant-Corruption uliokuwa ufanyike London Ila alikataa mwaliko huo akaelekea zake Uganda kwa Jirani yetu Museven. Lengo la Safari hii ilikuwa Ni mazungumzo ya Bomba la mafuta toka Uganda kuja Tanzania. Wakati Kenyata anarudi akakuta tayari Rais Magufuli na Museven washasinishiana mkataba.

Safari ya Tatu Rais Magufuli alitembelea Kenya kwa Jirani Mwingine hii ilikuwa safari ya Mwisho kwa mwaka 2016 ambapo alisafiri Tarehe 31-1 Mwezi wa kumi. Ziara ya siku Mbili. Safari hii ilikuwa na lengo la kuimarisha biashara ya Kenya na Tanzania.

Safari ya nne ilifanyika 2017 ambapo Rais Magufuli alielekea Ethiopia Tarehe 29-2 Mwezi wa pili. Mh Rais alihudhuria mkutano wa 28 wa nchi za Africa. Hii ilikuwa safari yake ya kwanza njee ya Africa Mashariki toka awe Rais.

Mwaka huo huo 2017 Tarehe 9-11 Mwezi November Rais Magufuli alifanya Ziara ya tano ambapo alisafiri kwenda Tena Uganda. Uganda ndio nchi pekee ambayo ilipata bahati ya kutembelewa na Rais Magufuli Mara mbili. Hakuna nchi nyingine kwa kipindi Cha miaka mitano umepata bahati hiyo. Rais Magufuli alikutana na Mwenyeji wake Mtukula ambapo walizindua one stop border na baadaye alielekea Ruzingwa kuweka jiwe la Msingi la bomba la mafuta. Mwaka 2017 alifanya Ziara mbili tu na hii ilikuwa Ni ya Mwisho kwa mwaka huo.

Mwaka 2018 Rais Magufuli hakutoka kabisa nchini.

Mwaka 2019 Rais Magufuli alifanya Ziara ya sita ambapo alihudhuria kuapishwa kwa Cyril Ramaphosa Africa Kusini Tarehe 25-26 Mwezi wa tano. Kwenye Ziara hii waliongozana na Rais Kikwete kwenye ndege Moja.

Ziara ya Saba aliifanya Namibia wakati akirudi toka Afrika Kusini ambapo alipitia Namibia. Hii ilikuwa Tarehe 27-29.

Ziara ya Mwisho kabisa aliifanya kipindi hicho hicho akirudi nyumbani tokea Afrika Kusini ambapo alipitia Zimbabwe Tarehe 29-30
Mwezi wa tano. Hii ni Ziara yake ya nane.

Safari za Rais hugharimu nini?

Kwa kutumia reference ya awamu iliyopita. Rais alipokuwa akisafiri kila safari moja ya nje alikwenda na watu 50. Hawa walikuwa wanausalama, waandishi wa habari, na watendaji mbalimbali wa serikali kutegemeana na Safari.

Kila Mtu kwenye safari moja alilipwa kiasi cha chini dola 400 kwa Siku. Huyu ni ofisa wa ngazi za chini kabisa.

Gharama za Kila safari ilikuwa inategemea ni sehemu gani Rais anakwenda. Mfano nchi za Ulaya na America posho kwa siku hulipwa kwa Daraja A ambazo ni Dola 420 kwa Siku kwa mtu mmoja.

Nchi za Asia na Africa hulipwa daraja B ambapo hulipwa dola 380 kwa siku.

Kwa hiyo kama safari itachukua siku tano utazidisha dola hizo Mara tano.... Iwe ni kwa daraja A Au B.

Gharama hizi hazijumuishi kitu kinachoitwa pocket Money,Nauli, Fedha za Suti kwa kila Safari nk. Yaani kila safari ni lazima vitu hivyo viwepo.

Mfano Leo wakienda Kenya lazma upate Suti kesho wakienda Uganda unapata nyingine. Vivyo hivyo kwa mahitaji mengine.

Hili ni eneo ambalo tulikubaliana kwenye Ilani yetu ya chama Kuwa tutalidhibiti ili fedha hizi tuzitumie kuondoa umaskini wa watanzania.

Ole Mushi
0712702602

FB_IMG_1628005213257.jpg
 
Thadei Ole Mushi ,

..inabidi ujumlishe na safari ambazo VP na PM walimuwakilisha Raisi nje ili kuweza kujua idadi kamili na ya uhakika ya safari za Magufuli.

..inajulikana kwamba Magufuli alikuwa hasafiri kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua, hivyo alikuwa akiwakilishwa na wasaidizi wake ambao ni VP na PM.

..VP au PM anaposafiri kwa niaba ya Raisi, basi itifaki, ukubwa wa msafara, na gharama, hushabihiana na msafara wa Raisi mwenyewe.
 
Wote walisoma zamani waliunganishwa na falsafa ya kipindi kile.

Miaka ya 70 80 kulikuwa na vitabu vingi Sana vya ujamaa vingi vilitoka urusi vilikuwa vinawapandikiza chuki wanafunzi kuwachukia wazungu yaani kama ya magharibi na kuwapandikiza uongo mwingi Sana eti matatizo ya waafrika chanzo ni wazungu kupitia ukoloni, ubeberu na ukoloni mambo leo.

Ni syllabus zilizolenga kuwaandaa wanafunzi wawe na mawazo ya mashariki.
 
Tukirudi kwenye awamu ya nne, Rais Kikwete bila Shaka alikua na safari nyingi kuliko awamu ya tano na hii ya sita.. lakini Rais Kikwete aliweza kuendesha nchi na kuajiri kila mwaka na kuongeza mishahara kila mwaka
Unafahamu aliacha deni kiasi gani hazina? Na wizi kiasi gani ulifanyika ?
 
Wanafana falsafa wote walisoma syllabus za zamani kipindi cha vita baridi mawazo yao yameegemea kambi ya Urusi.Na sio mawazo huru ( marealistic)
 
Mrithi wake kama ni kuacha deni na hasara ana phd plus tuzo juu ya kutia nchi hasara.
Magufuli was better 1000 than kikwete. Na Magufuli tuliletewa na kikwete kurekebisha mule alimo haribu. Umesahau? Alituletea jembe.
 
Wote walisoma zamani waliunganishwa na falsafa ya kipindi kile.

Miaka ya 70 80 kulikuwa na vitabu vingi Sana vya ujamaa vingi vilitoka urusi vilikuwa vinawapandikiza chuki wanafunzi kuwachukia wazungu yaani kama ya magharibi na kuwapandikiza uongo mwingi Sana eti matatizo ya waafrika chanzo ni wazungu kupitia ukoloni, ubeberu na ukoloni mambo leo.

Ni syllabus zilizolenga kuwaandaa wanafunzi wawe na mawazo ya mashariki.
Leo hii watamdanganya Nani?Wakawadanganye bibi zao huko mashambani.
 
Patrick Lumumba ni pan africanist.

Hili ndiyo jibu fupi la hili swali.
 
Lumumba ni pan Africanist Uchwara alikua anamfagilia Dikteta mwendazake kwakua alikua analipwa ili kumfagilia tu aonekane mwema , kuna clip zipo kabisa alizosainishwa fedha na dalali Msigwa kwa kazi maalum ya propaganda ya kumsifia Dikteta, njaa ni kitu kibaya sana hasa kwa wasomi wa kiafrika
 
Magufuli was better 1000 than kikwete. Na Magufuli tuliletewa na kikwete kurekebisha mule alimo haribu. Umesahau? Alituletea jembe.
Watu uwa wanasahau hii. JK simkubali lakini natambua alijua mapungufu yake yatasahihishwa na JPM japo kuna muda aliona dogo anakuwa too much :)
 
Akiwa Rais wa JMT, pia hayati JPM alifanya pia ziara nchini Malawi.
 
Naona unatafuta ugomvi na Samia. Ndani ya miezi miezi mitano ashaenda Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda. Na hapo kuna Korona!
 
Unaweza usisafiri nje lakini zikatumika pasipo tija mfano msururu wa misafara ya kujipigia kampeni, kununua wapinzani, kurudia chaguzi feki, kujenga miradi isiyo na tija, kuwalipa waimba kwaya watunge Nyimbo za sifa,nk.Kumbe ukisafiri nje tija zinaonekana mfano kuibrand nchi,kuvutia Wawekezaji,nk.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom