Kwanini Profesa Lumumba alikuwa akimsifia Hayati Rais Magufuli?

Naona unatafuta ugomvi na Samia. Ndani ya miezi miezi mitano ashaenda Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda. Na hapo kuna Korona!
Madam yupo katika "rehearsal" ktk nchi za maziwa makuu kabla ya kuanza ziara za kwenda nchi za mbali za ughaibuni huko kwa mabeberu kutembeza bakuli la misaada.
 
Na Thadei Ole Mushi.

Tumekuwa tukiona Mara kwa Mara Prof Lumumba wa Kenya akimsifia Sana Rais Magufuli. Watu wengi hujiuliza kanunuliwa? Au ana interest gani na Rais Magufuli au na Tanzania? Leo nitawapitisha katika eneo Moja tu la kwa Nini huwa wanaona Mh Magufuli ni Rais Bora wa kipindi hiki wakilinganisha na wa kwao Uhuru Kenyata. Twende sawa.....

David Ndii mwanauchumi wa Kenya aliwahi kusema Kuna haja ya kutafiti kama Ziara za Rais Kenyata nje ya Nchi Zina Manufaa. Duru za Kibajeti nchini Kenya zinaonyesha kuwa Rais Kenyata ametumia matrilioni ya Shilingi katika safari zake nje ya Nchi.

Kwa miaka sita tu Rais Kenyata kufikia 2019 alikuwa ameshakwea pipa Mara 92 kuhudhuria shughuli mbalimbali nje ya nchi shughuli nyingi zikiwa Ni kuaapishwa na kutafuta Mikopo kwenye mataifa ya Kibepari.

Mwaka 2015 pekee Rais Kenyata alisafiri safari 21 katika mwaka mmoja. Kwa miaka mitano ya Kwanza Kenyata alisafiri zaidi ya Mara 43 nje ya Nchi huku mtangulizi wake Mwai Kibaki kwa miaka 10 alisafiri Mara 33 tu. Wachambuzi wa Mambo nchini Kenya wanakosoa vikali Sana Kitendo Cha Rais Kenyata kusafiri Mara kwa Mara na kuligharimu Taifa Hilo mabilioni ya Shilingi.

Hali ipoje kwa Tanzania?

Kwa miaka Mitano Rais Magufuli alitoka nje ya mipaka ya nchi yetu Mara 8.

Safari ya kwanza aliifanya Tarehe 6-8 Mwezi wa nne mwaka 2016 ambapo nchi ya kwanza kuitembelea ilikuwa Rwanda. Siku ya kwanza Rais Magufuli alikutana na Mwenyeji wake Rais Kagame mpakani Rusumo ambapo walizindua one stop border na kufungua Daraja la Rusumo. Siku ya Pili Rais Magufuli alihudhuria maadhimisho ya miaka 22 ya mauaji ya Kimbari Rwanda.

Safari ya Pili alikwenda Uganda ambapo alisafiri Tarehe 12 Mwezi wa tano 2016. Wakati Rais akipanga kwenda Uganda Mezani kulikuwa na mwaliko wa kuhudhuria mkutano wa Ant-Corruption uliokuwa ufanyike London Ila alikataa mwaliko huo akaelekea zake Uganda kwa Jirani yetu Museven. Lengo la Safari hii ilikuwa Ni mazungumzo ya Bomba la mafuta toka Uganda kuja Tanzania. Wakati Kenyata anarudi akakuta tayari Rais Magufuli na Museven washasinishiana mkataba.

Safari ya Tatu Rais Magufuli alitembelea Kenya kwa Jirani Mwingine hii ilikuwa safari ya Mwisho kwa mwaka 2016 ambapo alisafiri Tarehe 31-1 Mwezi wa kumi. Ziara ya siku Mbili. Safari hii ilikuwa na lengo la kuimarisha biashara ya Kenya na Tanzania.

Safari ya nne ilifanyika 2017 ambapo Rais Magufuli alielekea Ethiopia Tarehe 29-2 Mwezi wa pili. Mh Rais alihudhuria mkutano wa 28 wa nchi za Africa. Hii ilikuwa safari yake ya kwanza njee ya Africa Mashariki toka awe Rais.

Mwaka huo huo 2017 Tarehe 9-11 Mwezi November Rais Magufuli alifanya Ziara ya tano ambapo alisafiri kwenda Tena Uganda. Uganda ndio nchi pekee ambayo ilipata bahati ya kutembelewa na Rais Magufuli Mara mbili. Hakuna nchi nyingine kwa kipindi Cha miaka mitano umepata bahati hiyo. Rais Magufuli alikutana na Mwenyeji wake Mtukula ambapo walizindua one stop border na baadaye alielekea Ruzingwa kuweka jiwe la Msingi la bomba la mafuta. Mwaka 2017 alifanya Ziara mbili tu na hii ilikuwa Ni ya Mwisho kwa mwaka huo.

Mwaka 2018 Rais Magufuli hakutoka kabisa nchini.

Mwaka 2019 Rais Magufuli alifanya Ziara ya sita ambapo alihudhuria kuapishwa kwa Cyril Ramaphosa Africa Kusini Tarehe 25-26 Mwezi wa tano. Kwenye Ziara hii waliongozana na Rais Kikwete kwenye ndege Moja.

Ziara ya Saba aliifanya Namibia wakati akirudi toka Afrika Kusini ambapo alipitia Namibia. Hii ilikuwa Tarehe 27-29.

Ziara ya Mwisho kabisa aliifanya kipindi hicho hicho akirudi nyumbani tokea Afrika Kusini ambapo alipitia Zimbabwe Tarehe 29-30
Mwezi wa tano. Hii ni Ziara yake ya nane.

Safari za Rais hugharimu nini?

Kwa kutumia reference ya awamu iliyopita. Rais alipokuwa akisafiri kila safari moja ya nje alikwenda na watu 50. Hawa walikuwa wanausalama, waandishi wa habari, na watendaji mbalimbali wa serikali kutegemeana na Safari.

Kila Mtu kwenye safari moja alilipwa kiasi cha chini dola 400 kwa Siku. Huyu ni ofisa wa ngazi za chini kabisa.

Gharama za Kila safari ilikuwa inategemea ni sehemu gani Rais anakwenda. Mfano nchi za Ulaya na America posho kwa siku hulipwa kwa Daraja A ambazo ni Dola 420 kwa Siku kwa mtu mmoja.

Nchi za Asia na Africa hulipwa daraja B ambapo hulipwa dola 380 kwa siku.

Kwa hiyo kama safari itachukua siku tano utazidisha dola hizo Mara tano.... Iwe ni kwa daraja A Au B.

Gharama hizi hazijumuishi kitu kinachoitwa pocket Money,Nauli, Fedha za Suti kwa kila Safari nk. Yaani kila safari ni lazima vitu hivyo viwepo.

Mfano Leo wakienda Kenya lazma upate Suti kesho wakienda Uganda unapata nyingine. Vivyo hivyo kwa mahitaji mengine.

Hili ni eneo ambalo tulikubaliana kwenye Ilani yetu ya chama Kuwa tutalidhibiti ili fedha hizi tuzitumie kuondoa umaskini wa watanzania.

Ole Mushi
0712702602

View attachment 1878877
Huyo profesa "njaa kali" alikuwa anajilengesha teuzi kwa Magufuli.
Alijua Magufuli alikuwa ni mlevi wa sifa kiasi kwamba angeweza hata kumpa uteuzi wa balozi wa heshima mahali. He was such desperate!!
 
Soma mageuzi ya china ndo utaelewa.
Walifungua milango na kutokuwa kisiwa wakaruhusu sekta binafsi na joint venture kwa miradi mikubwa, ikiwemo pia kwenda kuiba maarifa na technology ulaya wakazalisha kwa bidii wakakuza export leo wamezipita nchi nyingi tu za magharibi kiuchumi.
China wameanza kuendelea lini na wamefungua mipaka lini?Hadi sasa China serikali na chama chao ndio boss,utafanya chama kinavotaka au wanakupoteza.Siasa za kimagharibi tunapotezeana muda hiv
 
Deni la taifa,kivuko,kituo cha mafuta mwanza,meli ya samaki,Chato international, kununua wapinzani,ikulu mpya, kuhamia dodoma, kurudia chaguzi nk unadhani kodi kiasi gani iliyopotea hapa? hii pesa kama imepelekwa kwenye kilimo na kuwapa elimu na ujuzi wa kuzalisha vijana nchini export ingekua tusingehaika na dabo tozo,au kutegemea kupandisha kodi.
Magufuli hakuwa Mungu kuna makosa alifanya lkn ukiangalia kwa ujumla amefanya mambo makubwa sana ktk kipindi kifupi generally he was focused hao wanaokulipeni mmseme vibaya nao walipata chance badala ya kudeliver wakaenda kubembea marekani.
 
Panafrocanisit kumtetea diktator aliyejenga uwanja wa ndege kijijni kwake??? Ni upumbavu tu
Ule ni uwekezaji kwa ajili ya utalii ambao alipanga kufungua kwenye mbuga zilizo eneo hilo la chato kifo kimevuruga sana mipango na kutoa mwanya kwa waharibifu kama wewe kumsema vibaya shujaa wa nchi hii.
 
Na Thadei Ole Mushi.

Tumekuwa tukiona Mara kwa Mara Prof Lumumba wa Kenya akimsifia Sana Rais Magufuli. Watu wengi hujiuliza kanunuliwa? Au ana interest gani na Rais Magufuli au na Tanzania? Leo nitawapitisha katika eneo Moja tu la kwa Nini huwa wanaona Mh Magufuli ni Rais Bora wa kipindi hiki wakilinganisha na wa kwao Uhuru Kenyata. Twende sawa.....

David Ndii mwanauchumi wa Kenya aliwahi kusema Kuna haja ya kutafiti kama Ziara za Rais Kenyata nje ya Nchi Zina Manufaa. Duru za Kibajeti nchini Kenya zinaonyesha kuwa Rais Kenyata ametumia matrilioni ya Shilingi katika safari zake nje ya Nchi.

Kwa miaka sita tu Rais Kenyata kufikia 2019 alikuwa ameshakwea pipa Mara 92 kuhudhuria shughuli mbalimbali nje ya nchi shughuli nyingi zikiwa Ni kuaapishwa na kutafuta Mikopo kwenye mataifa ya Kibepari.

Mwaka 2015 pekee Rais Kenyata alisafiri safari 21 katika mwaka mmoja. Kwa miaka mitano ya Kwanza Kenyata alisafiri zaidi ya Mara 43 nje ya Nchi huku mtangulizi wake Mwai Kibaki kwa miaka 10 alisafiri Mara 33 tu. Wachambuzi wa Mambo nchini Kenya wanakosoa vikali Sana Kitendo Cha Rais Kenyata kusafiri Mara kwa Mara na kuligharimu Taifa Hilo mabilioni ya Shilingi.

Hali ipoje kwa Tanzania?

Kwa miaka Mitano Rais Magufuli alitoka nje ya mipaka ya nchi yetu Mara 8.

Safari ya kwanza aliifanya Tarehe 6-8 Mwezi wa nne mwaka 2016 ambapo nchi ya kwanza kuitembelea ilikuwa Rwanda. Siku ya kwanza Rais Magufuli alikutana na Mwenyeji wake Rais Kagame mpakani Rusumo ambapo walizindua one stop border na kufungua Daraja la Rusumo. Siku ya Pili Rais Magufuli alihudhuria maadhimisho ya miaka 22 ya mauaji ya Kimbari Rwanda.

Safari ya Pili alikwenda Uganda ambapo alisafiri Tarehe 12 Mwezi wa tano 2016. Wakati Rais akipanga kwenda Uganda Mezani kulikuwa na mwaliko wa kuhudhuria mkutano wa Ant-Corruption uliokuwa ufanyike London Ila alikataa mwaliko huo akaelekea zake Uganda kwa Jirani yetu Museven. Lengo la Safari hii ilikuwa Ni mazungumzo ya Bomba la mafuta toka Uganda kuja Tanzania. Wakati Kenyata anarudi akakuta tayari Rais Magufuli na Museven washasinishiana mkataba.

Safari ya Tatu Rais Magufuli alitembelea Kenya kwa Jirani Mwingine hii ilikuwa safari ya Mwisho kwa mwaka 2016 ambapo alisafiri Tarehe 31-1 Mwezi wa kumi. Ziara ya siku Mbili. Safari hii ilikuwa na lengo la kuimarisha biashara ya Kenya na Tanzania.

Safari ya nne ilifanyika 2017 ambapo Rais Magufuli alielekea Ethiopia Tarehe 29-2 Mwezi wa pili. Mh Rais alihudhuria mkutano wa 28 wa nchi za Africa. Hii ilikuwa safari yake ya kwanza njee ya Africa Mashariki toka awe Rais.

Mwaka huo huo 2017 Tarehe 9-11 Mwezi November Rais Magufuli alifanya Ziara ya tano ambapo alisafiri kwenda Tena Uganda. Uganda ndio nchi pekee ambayo ilipata bahati ya kutembelewa na Rais Magufuli Mara mbili. Hakuna nchi nyingine kwa kipindi Cha miaka mitano umepata bahati hiyo. Rais Magufuli alikutana na Mwenyeji wake Mtukula ambapo walizindua one stop border na baadaye alielekea Ruzingwa kuweka jiwe la Msingi la bomba la mafuta. Mwaka 2017 alifanya Ziara mbili tu na hii ilikuwa Ni ya Mwisho kwa mwaka huo.

Mwaka 2018 Rais Magufuli hakutoka kabisa nchini.

Mwaka 2019 Rais Magufuli alifanya Ziara ya sita ambapo alihudhuria kuapishwa kwa Cyril Ramaphosa Africa Kusini Tarehe 25-26 Mwezi wa tano. Kwenye Ziara hii waliongozana na Rais Kikwete kwenye ndege Moja.

Ziara ya Saba aliifanya Namibia wakati akirudi toka Afrika Kusini ambapo alipitia Namibia. Hii ilikuwa Tarehe 27-29.

Ziara ya Mwisho kabisa aliifanya kipindi hicho hicho akirudi nyumbani tokea Afrika Kusini ambapo alipitia Zimbabwe Tarehe 29-30
Mwezi wa tano. Hii ni Ziara yake ya nane.

Safari za Rais hugharimu nini?

Kwa kutumia reference ya awamu iliyopita. Rais alipokuwa akisafiri kila safari moja ya nje alikwenda na watu 50. Hawa walikuwa wanausalama, waandishi wa habari, na watendaji mbalimbali wa serikali kutegemeana na Safari.

Kila Mtu kwenye safari moja alilipwa kiasi cha chini dola 400 kwa Siku. Huyu ni ofisa wa ngazi za chini kabisa.

Gharama za Kila safari ilikuwa inategemea ni sehemu gani Rais anakwenda. Mfano nchi za Ulaya na America posho kwa siku hulipwa kwa Daraja A ambazo ni Dola 420 kwa Siku kwa mtu mmoja.

Nchi za Asia na Africa hulipwa daraja B ambapo hulipwa dola 380 kwa siku.

Kwa hiyo kama safari itachukua siku tano utazidisha dola hizo Mara tano.... Iwe ni kwa daraja A Au B.

Gharama hizi hazijumuishi kitu kinachoitwa pocket Money,Nauli, Fedha za Suti kwa kila Safari nk. Yaani kila safari ni lazima vitu hivyo viwepo.

Mfano Leo wakienda Kenya lazma upate Suti kesho wakienda Uganda unapata nyingine. Vivyo hivyo kwa mahitaji mengine.

Hili ni eneo ambalo tulikubaliana kwenye Ilani yetu ya chama Kuwa tutalidhibiti ili fedha hizi tuzitumie kuondoa umaskini wa watanzania.

Ole Mushi
0712702602

View attachment 1878877
Punguzeni Mishahara ya Wabunge
ONDOENI Viti Maalumu havina Tija
Acheni kununua MAGARI ya Gharama kubwa kwa Watendaji NCHI MASIKINI ina MATUMIZI MAKUBWA kuliko hata Nchi Tajiri

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Magufuli was better 1000 than kikwete. Na Magufuli tuliletewa na kikwete kurekebisha mule alimo haribu. Umesahau? Alituletea jembe.
Kwa research ipi.Dodoma imebuma,Chato airport inaota nyasi.mawaziri wapo dar, watendaji wikiend wapo dar jtatu dodoma kaa kimara road ushuhudie hizo v8 zinavyotafuna kodi zetu.
Nataka niombe Chato airport nikafugie popo, maana ni useless, ndege ya mwisho kutua pale ni iliyopeleka maiti Hakuna tena itakayotua pale.
 
Magufuli hakuwa Mungu kuna makosa alifanya lkn ukiangalia kwa ujumla amefanya mambo makubwa sana ktk kipindi kifupi generally he was focused hao wanaokulipeni mmseme vibaya nao walipata chance badala ya kudeliver wakaenda kubembea marekani.
Tofautisha propaganda na results,we unazungumzia kufanya propaganda,jambo dogo tu moja tbc wanalirudia mara elf 10 itashindikana kuonekana kafanya makubwa.
 
Tukirudi kwenye awamu ya nne, Rais Kikwete bila Shaka alikua na safari nyingi kuliko awamu ya tano na hii ya sita.. lakini Rais Kikwete aliweza kuendesha nchi na kuajiri kila mwaka na kuongeza mishahara kila mwaka
Kuajiri na kuongeza mishahara pekee sio maendeleo. Maendeleo ni pamoja, na Afya bora, makazi, miuondo mbinu ya simu, umeme, barabara, Ulinzi, kilimo, kudhibiti kupanda kwa gharama za maisha, kuendeleza elimu, zote msingi sekondari na vyuo. N.k
 
Lumumba ni pan Africanist Uchwara alikua anamfagilia Dikteta mwendazake kwakua alikua analipwa ili kumfagilia tu aonekane mwema , kuna clip zipo kabisa alizosainishwa fedha na dalali Msigwa kwa kazi maalum ya propaganda ya kumsifia Dikteta, njaa ni kitu kibaya sana hasa kwa wasomi wa kiafrika
Katiba mpya ndio maendeleo, na hata hii ya sasa ikibadilishwa tunatafuta tena katiba mpya nyinhine ili afya, makazi, kilimo, miuondo mbinu ya simu, barabara, maji safi na salama, Kuboresha elimu N.K vitapatikana.
 
Unaweza usisafiri nje lakini zikatumika pasipo tija mfano msururu wa misafara ya kujipigia kampeni, kununua wapinzani, kurudia chaguzi feki, kujenga miradi isiyo na tija, kuwalipa waimba kwaya watunge Nyimbo za sifa,nk.Kumbe ukisafiri nje tija zinaonekana mfano kuibrand nchi,kuvutia Wawekezaji,nk.
Uxuri wa Jamhuri ya JF kila mmoja huandika na kila mmoja anajua kila kitu.

Magufuli akitumia lita mmoja ya mafuta tuu anakuwa amelipa Tozo za bandarini, ushuru, kodi na kuzalisha faida kwa na Shirika yote yaliyo husika kujitoa, kusafirisha kuihifadhi na kuuza hiyo lita moja.

Vile vile anakuwa dreva wa gari kuhudumiwa, maji ya rejeta , vilainishi, na wana usalama kilipwa, mbali ya kwenye mikusanyiko watu wanaendeleza shuguli za kibiashara na kiuchumi.

Kwa hiyo kwa lita hiyo mmoja iloyotumika ndani ya gari moja ambalo alilitumia Magufuli nchini lilitoa michango ya ajira na kundeleza shuguli za kiuchumi kwa watu zaidi ya 200 kwa kila kituo alichosimama.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom