bigilankana
Senior Member
- Dec 15, 2009
- 144
- 4
Mh Great Thinker, tuombe Mungu tusifike huko, ni hatari!
Hata hiyo GUN keshaishika huyu au keshaona mateso ya watu kwenye vita. Tunaropoka tu.
Mh Great Thinker, tuombe Mungu tusifike huko, ni hatari!
Hivi mnataka hawa wazee waendelee kufanya kazi mpaka lini wakati vijana wanaomaliza vyuo hawana ajira? Sasa hivi kuna madarasa mengine yanatoa vijana zaidi ya 10 wenye upper second lakini wanabakizwa 3 tu kwa sababu ya hawa wazee wanaoendelea na mikataba. Nafikiri ni wakati wa kutoa ajira kwa vijana sasa kwani tukiendekeza hii mikataba mpaka Prof. afikishe miaka sabini itafika wakati kutakuwa hakuna replacement yao kwani watakuwa wazee watupu. Bravo JK Bravo Prpf. Mkandara and Prof. Maboko. Kazeni uzi huohuo lakini muajiri vijana kwa wingi angalau 50 kila mwaka. DIRA IWE AJIRA KWA VIJANA.
He is being punished for biting the hand that feeds him. Do you know that our leaders in third world countries behave like rouge village chiefs?
Hatma ya mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Mwesiga Baregu, kuendelea na mkataba wa ajira katika Chuo hicho, bado ni kitendawili kutokana na mkanganyiko uliojitokeza kati ya Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma) na chuo hicho.
Profesa Baregu, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), aliomba kuendelea na kazi ya kufundisha chuoni hapo baada ya kustaafu mwaka jana, lakini ilielezwa na wanataaluma kuwa Utumishi ilikataa ombi lake kwa sababu za kisiasa.
Hivi karibuni, Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala ya chuo hicho, Dk. Benson Bana, alisema Menejimenti ya Utumishi wa Umma ilikataa maombi ya Profesa Baregu kuendelea kufundisha katika chuo hicho.
Alisema maombi ya Profesa huyo mwandamizi kutaka kuendelea na ajira yake yalishapelekwa na UDSM serikalini lakini yalikataliwa.
Katika hali ya kushangaza, jana Menejimenti ya Utumishi wa Umma ilisema imepekua orodha ya majina ya wahadhiri wa chuo hicho walioomba kuongezewa muda wa ajira baada ya mikataba yao kumalizika, lakini jina la Profesa Baregu halimo.
Rehema Mbulalima wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano katika Menejimenti ya Utumishi wa Umma, alisema wamepekua orodha hiyo tangu Juni mwaka jana, lakini hawakuona ombi la Profesa Baregu.
Waulizeni hao UDSM walileta maombi hayo lini maana kati ya walioomba kuanzia Juni mwaka jana jina la Profesa Baregu halipo, alisema baada ya kuwasiliana na wakubwa wake wa kazi.
Nipashe iliwasiliana na Dk. Bana na alithibitisha kuwa ombi la Profesa Baregu lilishafikishwa Utumishi.
Kumbukumbu zinaonyesha kuwa jina lake lilipelekwa Utumishi na hiyo ndiyo statement (taarifa) ya chuo lakini kwa details (maelezo) zaidi mpigie DVC (Naibu Makamu Mkuu wa Chuo) Utawala na DVC (Naibu Makamu Mkuu) Taaluma, watakupa maelezo ya kina juu ya kinachoendelea, ukiwakosa hata VC (Makamu Mkuu wa Chuo) mwenyewe. Muulize atakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kueleza suala hilo kuliko mimi, alisema Dk. Bana.
Aliongeza kuwa atafanya sherehe kubwa siku atakaposikia Profesa Baregu ameongezewa mkataba, maana ni mwanataaluma muhimu wanayemtegemea kwa kiasi kikubwa katika siasa za kimataifa. Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala, alipoulizwa iwapo ombi la Profesa Baregu lilipelekwa Utumishi na majibu waliyopata ni yapi, alisema atatoa jibu la nini kinachoendelea baada ya wiki mbili.
Nipe wiki mbili nitakueleza mchakato mzima unavyoendelea na nakuhakikishia ni bonge la stori, ila kama una haraka na kutoa hiyo habari we andika unachokijua, ila mimi nitasema yangu baada ya wiki mbili, alisema huku akicheka kwa nguvu kitendo kinachoashiria kuwa kuna jambo linalojificha katika suala hilo.
Dk. Bana aliliambia Nipashe kuwa bado anamhitaji Profesa Baregu katika Idara yake kwa asilimia 150 na hata chuo kikuu kizima kinatamani arejee kazini.
Profesa Baregu ana talenti sana, na kitaaluma hakuna Profesa kama huyu hapa Tanzania na Afrika Mashariki na naweza kusema hata Afrika nzima katika siasa za kimataifa, hakuna kama huyu maana amebobea si kawaida na anategemewa na nchi nyingi, alisema.
Hivi karibuni, baadhi ya wanachama wa Chama cha Wanataaluma wa UDSM (Udasa), walishinikiza kurejeshwa kwa Profesa Baregu chuoni hapo na kutishia kuwa watafanya maandamano ikiwa hataongezewa mkataba.
Mhadhiri wa Taasisi ya Taaluma za Maendeleo (IDS), chuoni hapo, Profesa Gaudence Mpangala, alisema suala hilo lina mkono wa kisiasa.
Alisema wahadhiri wanahitajika sana katika chuo hicho na akatoa mfano kuwa hata yeye alishastaafu, lakini bado anaendelea kufundisha.
Mhadhiri katika Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala chuoni hapo, Dk. Exavery Lwaitama alisema, kutoridhia mkataba kwa mhadhiri ambaye amekuwa akitoa maoni tofauti na serikali inavyotaka ni hatari.
Profesa Baregu kama mchambuzi wa masuala ya siasa na utawala, amekuwa akikosoa utendaji wa serikali tangu awamu ya pili hadi ya sasa.
Wengine walienda wapi?mpiganaji pekee aliyebaki UDSM
unajua mimi ningekua Baregu ningejihisi furaha sana , maana jamii inanipigania ningali hai, kwetu waswahili tunatabia yakusifu na kuwathamini watu wakifa, kinyume kwa huyu mwanazuoni aliebobea, ni ishara ya kukubalika na kuheshimika. heshima kwako Baregu.
wamemezwa na mafisadi papa...wengine walienda wapi?