Kwanini Posta wamejaa wazee na ukiritimba mwingi?

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
4,581
4,631
Hivi kwanini Posta wamejaa wazee tupu?
Halafu ni kwanini wana ukiritimba wa parcel za watu?
Utasikia njoo kesho
Nenda Posta fulani mzigo wako haupo humu
ukifika huku wanakwambia umefika lakini bado hatujazitoa kwenye gari

Posta huu ukiritimba mpaka lini?

Hivi hili shirika ni kwanini Serikali inaliacha linakufa " kifo cha mende?

Hivi wizara husika na Serikali hivi Posta wamewapaka dawa gani hamlifatilii hili shirika?

Huku arusha ndo wana mizinguo balaa
Mzigo mpaka uupate hola! Ushapoteza nauli na muda wako wa kutosha

I hate this stupidy behaviour
 
Watumishi wa umma ndo walivo..ufanyaji huo wa kazi ni tangu ujana,nilienda posta mjini,dar,nilitaka kumiliki sanduku,nimeingia hakuna wa kunikaribisha wala kunielekeza..
 
Kuna mmoja alinijibu hapa Arusha nikamfundisha kuwa dawa ya moto ni moto. Hadi leo nikifika tu nahudumiwa fasta.
 
Kuna kipindi hua natamani wazee wote wastaafu kutoka serikalini waachiwe vijana wanaoweza kwenda na kasi ya dunia. Wazee wengi wako slow sana, na waka ka mentality flani ka utumishi wa umma wa miaka ya 80
 
hizi changamoto zilete uanzishwaji wa shirika lingine la binafsi kutatua hizi kero....
 
Kuna kipindi hua natamani wazee wote wastaafu kutoka serikalini waachiwe vijana wanaoweza kwenda na kasi ya dunia. Wazee wengi wako slow sana, na waka ka mentality flani ka utumishi wa umma wa miaka ya 80

Shida ni mentality. Watumishi wa umma wamejiona watwana. Sidhani kama tatizo ni umri pekee.
 
Nimesikia wanabadilisha mameneja nchi nzima..ni kweli kwa anayejua zaidi? Hawa jamaa sijui hufanya nini huko ofisini.
 
Acheni tu majirani watucheke ILA ukweli watanzania CUSTOMER CARE hakuna, yaani ni fafa kubwa...nenda airport ya kilimanjaro utashangaa...mbaya zaidi uwe umetokea nchi za wenzetu huko...mgeni anafika airport vijana wako busy wanapiga story hawana muda, mazingira yenyewe sio safi
 
Ni kweli hawa jamaa hawajali kabisa wateja. Wauze hisa fulani (20%) kwa shirika kubwa kama DHL, Amazon, Parcel force, Fedex, ili kuongeza ufanisi, customer service, kubalidisha utamaduni ndani la shirika hili.

Wawape hawa nafasi za uongozi waweze kulinyoosha vizuri, wapitie kila kitu upya.
 
Kuna kipindi hua natamani wazee wote wastaafu kutoka serikalini waachiwe vijana wanaoweza kwenda na kasi ya dunia. Wazee wengi wako slow sana, na waka ka mentality flani ka utumishi wa umma wa miaka ya 80
Tatizoooo ni mfumo mzima Wa uongozi na system nzima ya utendaji. Hata wakija vijana system isipo badilika Usitegemee kuna mabadiliko yoyote
 
Back
Top Bottom