Kwanini Pilato hakutenda haki alifuata makelele ya watu?

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
15,983
11,400
Pilato alivyopelekewa shauri la Yesu na kulipitia kwa umakini hakuona hatia juu ya Yesu. Lakini makelele yakamshinikiza amhukumu akakubaliana na umati ulivyotaka japo hakuona hatia juu yake.

Je angeamua kusimamia haki ingekuwake? Angepinduliwa au badae wananchi wangemwelewa na kukubaliana nae? Au watu wangejichukulia hatua mkononi?

Na hali ya sasa yapo mambo ya hovyo na yasiyo na tija na ya uongo watu wanashinikiza kana kwamba ndiyo haki na kushinikiza yatekelezwe. Je tukubaliane tu kupisha makelele kama ya wayahudi au tusimamie kweli?
 
Ukweli au uongo wa jambo haujifichi
Ni kweli kiongozi lazima uwe na msimamo wako lakini kuna wakati lazima usikilize hisia za watu waliokuweka hapo juu,mimi sitaki kuamini kwamba kelele ambazo wananchi wanampgia huyu kiongozi zote ni za uongo,zingine zina ukweli ndani yake
 
Lakini makelele yakamshinikiza amhukumu akakubaliana na umati ulivyotaka japo hakuona hatia juu yake.
Huenda na yeye alisikiliza makelele ya kwenye Mitandao, huyu mwenzie kasema kuwa hatayasikiliza japo anayasoma kucha kuchwa.
 
Pilato alikuwa sio dikteta.. alikuwa a Mungu ndani yake roho ya huruma kulinganisha na komwe wenu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom