Kwanini Pengo asiende mwenyewe kuhiji Butiama? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Pengo asiende mwenyewe kuhiji Butiama?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by BAK, Feb 22, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,687
  Likes Received: 82,538
  Trophy Points: 280
  Pengo amtaka Mkapa kwenda kuhiji Butiama
  Basil Msongo
  Daily News; Saturday,February 21, 2009 @19:00

  Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo, amemtuma Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, kwenda kuhiji alipozikwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, na kufikisha shukurani zake kwa kazi aliyoifanya kujenga mazingira yaliyoliwezesha Kanisa kupata mafanikio.

  Kadinali Pengo pia alimshukuru Mkapa, marais waliomtangulia na mrithi wake, Rais Jakaya Kikwete, kwa kuendeleza mazingira hayo yaliyoliwezesha Kanisa kufanikiwa katika shughuli zake za kiroho na kijamii. “Nenda kamwambie nakushukuru,” alisema Kadinali Pengo katika viwanja vya Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph Dar es Salaam jana kwenye ibada ya kuadhimisha miaka 25 tangu alipopata daraja la uaskofu Januari 6, 1984.

  Baba wa Taifa alifariki dunia Oktoba 14, 1999 katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas, London, Uingereza na alizikwa katika kijiji cha Butiama mkoani Mara. Kadinali Pengo (55) alianza kazi hiyo ya kichungaji katika jimbo la Nachingwea mkoani Lindi na baadaye akapanda daraja kuwa Askofu wa kwanza jimbo la Tunduru, Masasi Februari 12, 1987. Kuanzia Julai 22, 1992 amekuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

  Kadinali Pengo pia ameshatimiza miaka 11 tangu alipopata Ukadinali, Januari 18, 1998 ambapo Baba Mtakatifu Yohane Paulo wa II alimpa daraja hilo na kumsimika Februari 21 mwaka huo huo, katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Rome, Italia.

  Licha ya majukumu ya kuongoza waumini zaidi ya milioni moja katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Kadinali Pengo pia ni Rais wa Baraza la Maaskofu wa Katoliki Afrika na Madagascar na mlezi na mdhamini wa Mabaraza ya Maaskofu Mashariki ya Afrika. Kiongozi huyo alisema Kanisa limepata mafanikio kwa kuwa nchi imekuwa ikitoa mazingira ya kuweza kufikia mafanikio hayo.

  Alitoa mwito kwa viongozi na wananchi wasikubali kuipoteza tunu ya amani iliyopo nchini. “Amani tuliyonayo katika Taifa letu si kitu cha kuchezea,” alisema katika ibada hiyo iliyohudhuriwa na Mkapa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, maaskofu wa majimbo, majimbo makuu, mapadre, watumishi wa kanisa wa kada mbalimbali, na waumini wengine.

  “Tusiruhusu ukabila, udini na utaifa kuharibu amani ya Taifa letu,” alisema kiongozi huyo na kusisitiza kuwa hilo ni ombi la dhati kutoka kwake na ni muhimu likazingatiwa.Naye Askofu Mkuu Msaidizi wa Jimbo hilo, Methodius Kilaini, alimweleza kiongozi wake huyo kuwa anapendwa na waumini na wanathamini kazi anazozifanya katika jimbo.

  “Wanathamini moyo wako kwa wanyonge na kwa wenye shida,” alisema Askofu Kilaini na kuongeza kuwa, zawadi kuu aliyoichagua Kadinali Pengo kwa ajili ya Jubilei yake ya Fedha (miaka 25), ni gari kwa ajili ya wananchi wa Mafia mkoani Pwani.

  Wakati wa mahubiri katika ibada hiyo, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha, Josephat Lebulu, alimtaka Kadinali Pengo aendelee kukemea maovu bila kuogopa na asiache kufanya kazi za kichungaji na akichoka, atambue kuwa bado ana kazi za kufanya na atapata mafanikio. “Usichoke, kazi yetu haina kuchoka bali tunaishia kuwa mishumaa,” alisema kiongozi huyo wa Kanisa na kuwataka waumini wamuombee Kadinali Pengo amudu majukumu aliyonayo kuchunga kanisa kiroho na kimwili.

  Aliwataka waumini kuacha kuwashutumu viongozi wa kiroho kwa kuwa wao ni wanadamu, hivyo wana udhaifu sawa na wanadamu wengine lakini kwa kuwa wanatekeleza matakwa ya Mungu, hata kama wanadamu wakiwakataa, kazi za kichungaji zitaendelea.

  Februari 17 mwaka huu, Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Benedict wa XVI aliandika ujumbe wa kumpongeza Kadinali Pengo kwa kutimiza miaka 25 ya uaskofu. Alimsifu kwa unyenyekevu, ukarimu, utii na upendo alionao kwa kanisa na juhudi zake za kuhimiza umoja na amani.
   
 2. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2009
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Ukubwa wa fungu la zaka inayolipwa na Mkapa unatosha kumpofusha Pengo!
   
 3. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Gag,
  Unaweza kufafanua zaidi? Unataka kusema Pengo kamwagia sifa asizostahili Ben (mazingira ya amani blah blah), au kampendelea kumtuma kwa "St" Julius of Butiama?
   
 4. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2009
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Injinia,
  Nakumbuka Pengo alivyokuwa critical kwa serikali ya Mwinyi, nami nilikubaliana naye kwa kiasi kikubwa kwani kuna mambo ambayo nafikiri yalikuwa yakifanyika kinyume na ilivyotakiwa yafanyike na nikamuona kama shujaa.
  Inaniuma sana shujaa wangu anapogeuka na kuaangalia tu mafanikio ya kanisa lake. Hivi ni amani ipi anayoihubiri katika taifa ambalo majambazi kabla ya kukamatwa yanaandaliwa makao keko yanayolingana na hadhi zao kwa gharama za mlipa kodi anayelazimika kulala kitanda kimoja na mgonjwa mwenzake wodini kwa kuwa vitanda havitoshi? Ni amani ipi anayoihubiri wakati kila siku ndugu zetu albino wanauwawa na waziri anayehusika na usalama wao akisema hilo si tatizo kubwa? Anahubiri amani gani kwenye nchi ambayo mwizi wa baiskeli anawambwa msalabani wakati wezi wa mabilioni wanapewa protection wanayohitaji na serikali?
  Injinia, mimi ni mkatoliki, na najivunia Mwalimu Nyerere kuwemo kwenye mchakato wa kuona kama anaweza kuwa mtakatifu. Lakini Pengo kujaribu kumhusisha mwalimu na hawa mafisadi kachemsha kwelikweli, iwe kwa msukumo wa udini au sababu nyingine.
   
 5. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #5
  Feb 22, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  duty has no sweet hearts
   
 6. K

  KGM Senior Member

  #6
  Feb 22, 2009
  Joined: May 21, 2007
  Messages: 188
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  Kama kuna jipu ambalo linahitaji kutumbuliwa ni hawa viongozi wa Dini.
  Yaani ni mafisadi wa kutupwa, Yaani wanakwaza waumini wao.

  Dini Tanzania zinatumika sana kuficha maovu. Nimeumia sana roho kusikia kiongozi wa Dini anafanya mambo kama haya.
   
 7. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  Pengo wafu hawana nguvu,unapomwambia Mkapa akatoe shukrani kwenye kaburi la Nyerere nashindwa kukuelewa kama kiongozi wa dini unamshauri mtu akamshukuru mfu(maiti)marehemu !.Nyerere ni mwanadamu kama walivyo binadamu wengine hatupaswi kumwabudi au kumshukuru au kwenda kusali katika kaburi lake kwasababu Mwenyezi mungu ametukataza kufanya hivyo.Najua kadinali Pengo huoni ufisadi aliotufanyia Mkapa wa kuuza rasilimali zetu,kujiuzia mgodi wa Kiwira,kununua radar,kubinafsisha bandariyetu kwa mafisadi,kununua ndege ya rais kwa bei kubwa ilihali watanzaia bado ni masikini wa kutupwa,kuratibu wizi wa fedha BOT na nk.Viongozi wa dini wa aina ya Pengo ni wa kuogopwa kama ukoma,madhara aliyotuachia Mkapa mpaka leo watanzania bado tunaumia.Pengo inaelekea huna kazi za kufanya au huna kitu cha kuongea.itakuwa jambo zuri na la hekima kukaa kimya.Watanzania wa leo si mabwege.Tunajua kuna mkakati maalumu wa kumsafisha Mkapa mbele ya jamii ya kimataifa na watanzania lakini kadri mnavyotumia mbinu zenu dhaifu ndivyo mnavyoharibu.Ukweli hauitaji nguvu kubwa ya kuutetea bali uongo na uovu unahitaji nguvu kubwa sana kama ya Kadinali Pengo.
   
 8. M

  Mkandara Verified User

  #8
  Feb 22, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Sasa hapa ndipo napokataa dini kuingilia maswala ya Utawala..statement kama hizi zitawafanya waumini wa dini na madhehebu mengine kujiuliza maswali mengi...
  Huyu Kardinali Pengo inabidi afahamu anaishi na watu gani ktk mazingira gani!..
   
 9. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #9
  Feb 22, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,969
  Likes Received: 222
  Trophy Points: 160
  Mkandara viongozi wa dini wa zamani viongozi wa sasa wanaganga njaa kama siye huku.Ndio mana kauli zao mara nyingi zina utata inategemea wakati huo anaongea na nani.
   
 10. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #10
  Feb 22, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Endelea kuosha kinywa hadi kitakate..Inaonekana hukuswaki asubuhi.
   
 11. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #11
  Feb 22, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Haya maneno yanatokana na post hiihii (post # 1) au tunasoma post tofauti? Maana naona kama vile ndo umeamka muzee, unaongelea vitu visivyohusiana kabisa...!
   
 12. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #12
  Feb 22, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Sioni hoja hapa.

  Yaani wewe ulitaka kwenye hii jubilei yake, aje na lundo la malalamiko kama wafanyavyo watu wa dini ya upande wa pili?

  Au unataka kutafsiri kuwa anamaanisha kuwa serikali na dini zinazishirikiana ili dini ya Pengo ishamiri? Sidhani kama unahitaji darubini kuona kuwa hili haliwezekani.
   
 13. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #13
  Feb 22, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Sio lazima kuchangia kila thread muzee. Kuosha kinywa hakuna dili wala nini, labda kama hujasukutua kinywa asubuhi.. :D
   
 14. M

  Mkandara Verified User

  #14
  Feb 22, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  MtindiowaUbongo,
  Mkuu acha unazi hauna maana sisi watu wote wazima hapa..soma vizuri maelezo ya huyu kiongozi wa dini utaelewa nachozungumza.. Ni Ujinga mtupu... samahani lakini, - kwani kila unaposhukuru kuwezeshwa wewe ina maana kuna wengine hawakuwezeshwa..
  Kwa nini wewe unashindwa kuamini upande wa madai ya kutowezeshwa ila unaamini na kukubali upande wa kuwezeshwa kama sii mvua ilikunyeshea!
   
 15. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #15
  Feb 22, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Father Sivalon, mmarekani aliyekuwa anafundisha UDSM alishasema mengi kuhusina na hili ambayo tamati yake ikawa ya mwembechai...Sasa naona Pengo kimakosa anakumbushia maumivu ya wengine kwa kutambua mafanikio yake.

  Hata hivyo yawezekana alikuwa akimpa somo MKAPA ajirudi. Just imagine MKAPA na madhambi yake dhidi ya watanzania anaenda kutembelea kaburi la Nyeyere?

  omarilyas
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Feb 22, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,687
  Likes Received: 82,538
  Trophy Points: 280
  Bahati mbaya wafu hawasemi, kama wangekuwa wanasema Mwalimu angekataa kata kata Mkapa kutembelea kaburi lake lakini familia ya Mwalimu inaweza kabisa kufanya hivyo kwa niaba yake. Kama kumbukumbu yangu ni nzuri Mkapa alipokelewa katika familia ya Mwalimu kama mmoja wa wanafamilia mara baada ya maovu yake kuanza kuanikwa hadharani nakumbuka mmoja wa wanafamilia alitamka hadharani kwamba Mkapa inabidi aende Butiama akajitete kuhusu tuhuma nzito za kifisadi dhidi yake vinginevyo wangemuondoa kama mmoja wa wanafamilia ya Mwalimu. Sijui kama Mkapa aliwahi kuitikia huo wito na kwenda kujitetea kule Butiama.
   
 17. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #17
  Feb 22, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Nasikia na hawa wanarogana sana kupata vyeo huko sinagogini mwao......
  aaarg na nyie na huyo mwalimu wenu.....kwani yeye mbona alikuwa mdhambi tu zaidi ya Mkapa......
   
 18. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #18
  Feb 22, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Mimi sioni haja ya Rais na Marais wastaafu watatu (Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa) kuwepo pale. Kwani ni national issue? Au kwa lipi jema alilofanya Polycarp Kadinali Pengo? Upuuzii mtupu. Watu wa dini waendelee na mambo yao ya kiroho na wanasiasa waendelee na siasa ...
   
 19. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #19
  Feb 22, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,431
  Trophy Points: 280

  ......gagnija ..inawezekana wewe sio mkatoliki ..lakini kwa kifupi kanisa katoliki huwa halitegemei wala kukubali kumtegemea muumini mmoja kwa mapato....hata kama unayo pesa ya kujenga na kulisha kanisa lote peke yako hawatakubali zaka yako peke yako...kwani kanisa ni la watu wote,mkapa anajuwa utaratibu huo...hata kama anatoa sadaka atakuwa kama waumini wengine wenye uwezo tu....

  nikirudi kwenye mada ...nemebahatika kupata huduma za makadinali RUGAMBWA na PENGO....wote walikuwa na mshango mkubwa kila mmoja kwa wakati wake.

  Wakati wa utawa wa cardinal pengo ...ndio wakati serikali iliruhusu kanisa kuendelea na huduma za shule na hospitali,amefanikiwa kiasi kikubwa kujenga mashule mengi .....sasa hivi hapa dar karibu kila parokia inayo shule.....na kila kitongoji kuna kanisa...amefanya juhudi kubwa sana kuunganisha nguvu za waamini,...

  amefanikiwa kwa upande wa upashanaji habari kwa kuanzisha magazeti na kuimarisha redio [au uanzisha]....na kuanzisha televisheni .

  mahospitali yamefunguliwa kwenye parokia nyingi.....

  kwa kushirikiana na maaskofu wengine ...baada ya kuruhusiwa na serikali ndani ya miaka 15 ....wameweza kuimarisha hospitali ya rufaa ya BUGANDO,....pia wameweza kuimarisha hospitali zao zilizoenea kila wilaya nchini[ambazo nyingi ndio zinatumiwa na serikali kutoa huduma ya hospitali za wilaya kwenye maeneo ambayo bado serikali haina hospitali zenye hadhi hiyo.....

  katika kipindi hicho wameweza kujenga vyuo vikuu ,iringa,mwanza,moshi,etc...vyote vikijulikana kama st.augustine... pia wameweza kujenga chuo kikuu cha teknelojia dar es salaam [st.joseph college of engineering and technology]...tunawashukuru maaskofu,mapadre,watawa,waumini na wote wenye mapenzi mema kwa mafanikio hayo makubwa...ambayo mengi yametokana na juhudi za ndani na michango ya waumini...hasa katika enzi hizi ambazo misaada kutoka ulaya kuendesha makanisa imeshakoma.....na misaada mingi kutoka rome inaelekea sehemu zenye maafa ya vita,...etc[ie congo,east europe,darfur etc]
   
 20. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #20
  Feb 22, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,431
  Trophy Points: 280
  ......walipewa mwaliko na wakahudhuria ..hawakulazimishwa .........wangeweza pia kuacha kwenda..sasa wewe shangaa kwa nini wamehudhuria wote...!

  ni vigumu kwa mtu mwenye akili kupuuza role ya kanisa katika huduma za jamii....hasa pale unapokuta karibu asilimia 40% ya huduma za jamii zinatolewa na kanisa........watanzania wengi wapo vijijini....na huko ndiko wanakotoa huduma,...hawana haja ya kufungua kwa wingi huduma hasa za afya mijini ambako mnapata private hospitals ,,,,..vijijini watu wengi wana shida na wanapewa huduma nzuri kwa kuchangia kidogo au bila malipo..........sasa kama mtu anataka kuwaona hawa kina pengo hawana maana basi na yeye apeleke huduma huko ...afikiri ni rahisi!!!!

  afteral wale unaoshangaa kwa nini wamehudhuria pale ...watoto wao ndio wanaosoma....st.marian,kifungilo,st.joseph....etc.
   
Loading...