Kwanini nikiomba ajira kwa Mohammed Enterprises Tanzania Limited - MeTL huwa siitwi?

Mwamba1961

JF-Expert Member
Dec 10, 2016
490
250
Habari zetu,

Mimi nimekuwa nikiomba kazi zinazotangazwa na Mohammed Enterprises Tanzania Limited - MeTL ila nimekuwa sipati majibu ya kuitwa, ila nikituma sehemu nyingine naitwa.

Unahisi nakosea wapi?
 
Sim Card

JF-Expert Member
Dec 30, 2019
890
1,000
1. Huenda applications huziandiki vizuri.
2. Sifa huna kwa kazi husika.
3. Una elimu kubwa sana.
4.Hufuati taratibu za kuomba kazi husika mfano unaficha taarifa zako.
5. Huna uzoefu wa kazi.
6. Kimombo hukijui au una mapungufu eneo hilo.
7. Mshahara unaotaka ni mkubwa.
8. Umbali wa unakoishi na kazi ilipo.
9.Huenda kazi inayotangazwa imesitishwa au inasubiri.
10. Kampuni haina tena uwezo wa kuajiri zaidi nk nk nk
 
Mibas

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
3,980
2,000
Pole, kama unahisi una sifa lakini unabaniwa kwa uonevu sema nikuunganishe na Human resources Director wa MeTL au local recruitment manager wa hio kampuni huenda watakusaidia. Vinginevyo fika ofisini kwao pale Morogoro rd. Uwaulize kulikoni?
 
Alvin Slain

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
6,381
2,000
Huo muda unaozungukia majibu ya maombi ya kazi, Ungejiajiri mwenyewe baada tu ya miezi michache ungegundua kwamba kujiwekeza mwenyewe ndio siri ya mafanikio yako.
 
kinje ketile

JF-Expert Member
Dec 12, 2015
1,427
2,000
Bro..kwanza we hapa Tz unashabikia klabu gani....? Tuanzie hapo........hahahah...ni jokes..!
 
Mwamba1961

JF-Expert Member
Dec 10, 2016
490
250
Pole, kama unahisi una sifa lakini unabaniwa kwa uonevu sema nikuunganishe na Human resources Director wa MeTL au local recruitment manager wa hio kampuni huenda watakusaidia. Vinginevyo fika ofisini kwao pale Morogoro rd. Uwaulize kulikoni?

Niunganishe na Hr wao, Mimi ni Mechanical engineering Technician
 
mbu wa dengue

JF-Expert Member
Jun 2, 2014
6,402
2,000
Habari zetu,

Mimi nimekuwa nikiomba kazi zinazotangazwa na Mohammed Enterprises Tanzania Limited - MeTL ila nimekuwa sipati majibu ya kuitwa, ila nikituma sehemu nyingine naitwa.

Unahisi nakosea wapi ??
Kiukweli hata mimi nimeomba kazi mara nyingi sana kwa MO nikawa siitwi kabisa. Tena nikawa naomba za aina zote yaani za rank ya chini na rank ya juu lakini holaa.

Sasa badae kufuatilia nikasikia kwamba pale ni sehemu kuna figisu sana na watu wanapeana kazi kindugu,yaani yale matangazo ni kuwazuga watu tu.

Na kingine tena nikasikia kwamba pale mazingira ya kazi sio mazuri yaani unyonyaji wa kulipwa mishahara midogo na majungu sana ndio maana watu wanaacha kazi mara kwa mara,ndio maana utashangaa kila baada ya miezi 3 wanatangaza tena kutafuta watu.

Sidhani kama inahusiana na mambo ya udini kama wengine walivyosema maana ingekuwa ni udini mimi wangeniita na kunipa kazi maana mimi ni muislam.
 
Mwamba1961

JF-Expert Member
Dec 10, 2016
490
250
Kiukweli hata mimi nimeomba kazi mara nyingi sana kwa MO nikawa siitwi kabisa. Tena nikawa naomba za aina zote yaani za rank ya chini na rank ya juu lakini holaa.

Sasa badae kufuatilia nikasikia kwamba pale ni sehemu kuna figisu sana na watu wanapeana kazi kindugu,yaani yale matangazo ni kuwazuga watu tu...

Duh kumbe ...
 
Bakariforever

JF-Expert Member
Aug 30, 2017
460
500
Bro..kwanza we hapa Tz unashabikia klabu gani....? Tuanzie hapo hahahah...ni jokes..!

Harafu ungejua wanaoongoza kutumia bidhaa za Mo ni mashabiki wa YANGA hata huyo Mo angekuwa anachagua kama ajira kipaumbele mashabiki wa Yanga wa kimataifa kwanza ndo waje hao wanyama pori wengine
 
Mwamba1961

JF-Expert Member
Dec 10, 2016
490
250
1. Huenda applications huziandiki vizuri.
2. Sifa huna kwa kazi husika.
3. Una elimu kubwa sana.
4.Hufuati taratibu za kuomba kazi husika mfano unaficha taarifa zako.
5. Huna uzoefu wa kazi.
6. Kimombo hukijui au una mapungufu eneo hilo.
7. Mshahara unaotaka ni mkubwa.
8. Umbali wa unakoishi na kazi ilipo.
9.Huenda kazi inayotangazwa imesitishwa au inasubiri.
10. Kampuni haina tena uwezo wa kuajiri zaidi nk nk nk
hahaha
 
Sivan

JF-Expert Member
Jul 17, 2020
928
1,000
Musipoitwa munalalamika mukiitwa na kupewa kazi munalalamika munanyonywa basi ulalamishi mpaka kifo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom