Iduku
Member
- Aug 24, 2020
- 35
- 108
Habari wana jamvi! Leo nimewiwa kueleza machache kuhusu fursa za kufanya kazi nje ya nchi,mtazamo wangu binafsi na baadhi ya vijana waliopo hapa Tanzania na hata wale walio nje ya nchi wakifanya kazi huko au biashara. Hapa nitaeleza kile nilichokiona na kukutana nacho kwenye mchakato wa kutafuta ajira na fursa hizi za nje. Kwa vile Jamii forum ni jukwaa huru la watu kutoa mawazo,kuibua hoja,kukosoa na kujenga hoja basi ni sehemu sahihi kuleta mijadala.
Hata hivyo kuna wana jamvi humu sijui ni kwa kukosa elimu ya matumizi ya mitandao au kutokustaarabika au ushamba? Huwa hawana hoja mara zote hutukana au kutumia lugha za kuudhi,kila penye mijadala nyeti inayogusa maisha ya watu huleta kebehi na huchukua nafasi kutaka kutapeli watu: Hili ni tatizo kwa jamii yetu inatupasa tubadilike si busara sasa Jamii ya Kitanzania kukosa ustaarabu na kutokuaminika kwenye vitu nyeti.
Twende kwenye mada: Mwaka sasa nimekuwa nikipitia mada mbali mbali zinazoelezea fursa za kazi nje ya nchi hasa kwa nchi za Mashariki ya kati,Ulaya na Marekani; mada hizi zilinivutia na kunishawishi kujua zaidi na kutaka kupata fursa hizo maana nami ni miongoni mwa vijana wa Kitanzania tunaopambana kujikwamua kimaisha na imekuwa ndoto yangu kuwa penye nafasi nikafika nchi za nje nitachakarika sana kulingana na fursa zilizopo huko ili baadaye nirudi hapa kwetu Tanzania kuwekeza hata kama nitaajiri vijana watano shambani au kwenye gereji kwangu hiyo itakuwa ni furaha kuwa nimesaidia jamii yangu.
Kwanini vijana tunatamani kwenda huko (kuhalalisha nia),nitaeleza sababu chache ninazoona ni za msingi.
1. Mfumo wa elimu tulioipata toka shule za upili mpaka vyuo vikuu haujatujenga kuja kujikwamua kwa wakati. Sitaeleza kwa undani maana walio wengi wanaelewa homa ya graduates wengi hapa Tanzania; hivyo kukaa kusubiri ajira na kuzunguka kwenye ofisi za umma/watu na makampuni miaka nenda rudi ni upotezaji wa muda na nikutoelewa kuwa kijana ni rasilimali mhimu sana akiwa kwenye umri wa kufanya kazi; hivyo hii ni sababu tosha kwa kijana kushawishika kutafuta ajira nje ya nchi.
2. Uwepo wa fursa na rasilimali zinazohitaji mitaji yakueleweka kuzitumia. Si sahihi kuwa vijana wanaoenda nje ya nchi ni wavivu au wameacha fursa hapa nchini. Zipo fursa nyingi lakini zinahitaji rasilimali pesa kuzichangamkia. Vijana hawakopesheki kwenye mabenk au taasisi za fedha maana hawana dhamana nje ya vyeti vyao achana na waliotoka kwenye royal families, hapa naongelea kijana wa Kitanzania toka familia za chini.Fursa pekee wanayoiona ni kujiunga na makundi ya kisiasa kupata unafuu humo na wengine wamejikatia tamaa hawajui kesho itakuwaje maana hata mikopo ya vikundi ina milengo ya kisiasa. Je wote tuendeshe boda boda? Hivyo bado kuna sababu ya kutafuta suluhu hata beyond boarders.
3. Ipo mifano ya Watanzania waliotoka nje ya nchi na wamerudi wakiwa wamepiga hatua kubwa kiuchumi wamefungua biashara,wanamiradi mashambani na kwingineko. Hii haiondoi ukweli pia kuwa wapo vijana walipata bahati ya kutoka kwenda huko wamekumbwa na masaibu yali/nayowagharimu maisha yao;hii ni kutokana na sababu kuu mbili kukosa uaminifu binafsi wa kimaadili na tamaa ya pesa nyingi za haraka..hii sababu ya pili haiondoi ukweli kuwa vijana wa Kitanzania wana ari ya kufanya kazi halali,wanajituma wakipata nafasi na wanajielewa.
Nini kifanyike? Huku tukiendelea kuwahimiza vijana wajiajiri ilihali sisi tumeajiriwa, viongozi na wanasiasa lazima waelewe kuwa tatizo la ajira ni suala mtambuka na halipo Tanzania tu,waelewe wao ndo watunga sera ambazo kwa kiasi kikubwa zimeshindwa kumsaidia kijana wa Kitanzania kujiajiri huku maelfu ya vijana wakihitimu vyuo na kubaki kulanda landa mijini: Ni wakati sasa Serikali iwe na sera za wazi kuhusu fursa za kazi nje ya nchi, mathalani huduma za uwakala wa kazi za nje kwa Tanzania bado zinafanyika kwa uficho; Taasisi ya Serikali kama TAeSa inapaswa iweke wazi Takwimu za mawakala walioidhinishwa Tanzania kufanya shughuli za kuunganisha watanzania na kazi za nje.
Serikali itoe elimu kuhusu dhana potofu ya kuwa watanzania wakienda nje kufanya kazi wanateswa,iendelee kuimarisha balozi zetu huko nje na watanzania wanaojikuta kwenye masaibu waelezwe taratibu za kufuata kabla hawajaenda nje,na waepuka kuvunja sheria za kazi au nchi hizo na waajiri wao na inapotokea wametendewa kinyume wajue pakuripoti.
Unyanyasaji haupo nje kwa kwa vile watu wapo kule ugenini,hata hapa nchini unyanyasaji upo mwingi na wakati mwingine ni mkubwa kuliko huo ambao jamii inaamini watu wanatendewa huko nje. Mfano kukosa kazi ni unyanyasaji tosha ambao athari yake kila mtu anaiona.
Nchi ya Kenya, Nigeria na nyingine barani Afrika wamepiga hatua sana kwenye hili,wale waliopo nje mara nyingi wanashuhudia kukuta wakenya wengi wakifanya kazi huko mashariki ya kati, ulaya na Marekani. Hata hapa kwetu inawezekana tukapunguza kiasi changamoto za ajira kwa kuwa na sera za wazi na usimamizi mzuri wa watu kwenda mataifa mengine kufanya kazi.
Naelewa zipo changamoto nyingine kama ugumu wa kupata hati ya kusafiria,hili linawezekana kuangaliwa upya hasa kama huduma za uwakala na kazi za nje zitakuwa nyingi na za uwazi.
Hii ni kuwatia moyo vijana wenzangu kuwa tunapotafuta ajira hapa nchini tujue pia kuwa hata huko nje kuna fursa na zinaweza kututoa toka tulipo kuliko kutafuta kazi miaka zaidi ya mitatu hapa hapa huku hujui utaipata lini,hujui utaishi wapi na vipi.Hii ni hatari na imeendelea kuongeza vijana wenye msongo wa mawazo na wengine wanafanya matukio ya ajabu sana maana wamekata tamaa.
Wito wangu kwa watanzania waliopo nje ni kuwa unganisha vijana wenzenu tulipo nyumbani huku na tupo tayari kuvuka boda kutafuta maisha; Ninyi ndiyo mabalozi wetu huko,akifika huko Mtanzania mwenzio hatachukua ridhiki yako ila atawajibika kivyake kujikwamua.
Hii tabia ya kutoaminiana na kutelekezana kwa watanzania inaanzia hapa hapa nyumbani,baadhi ya diaspora wanasema watanzania siyo wakuwaamini maana akifika huko anabadilika! Hii haiwezi kuwa jumla kiasi hiko na si wote, hivi kama wa- Nigeria tunaowajua ni matapeli sana lakini wao wanaitana huko nje,hata ndg zetu wakenya je sisi ndo mioyo yetu ni midogo tusiweze? Kwanini tuwaachie kina Ernest Makulilo peke yao, wakati watanzania wapo karibia mabara yote ya Dunia?
Ni wakati sasa wa kushare fursa za ajira nje ya nchi kwa watanzania wote,aliye tayari afuate taratibu na akipata akafanye kazi kwa uaminifu ili awe balozi kwa wengine. Nawatakia kazi nje na kila la heri wapambanaji wenzangu;