Mwl. JK Nyerere alikuwa na akili nyingi sana.. Alibaini kuwa kutokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia hakukuwepo na haja tena ya kuhamia Dodoma bali kuwajengea uwezo wananchi ili waweze kupambana na umaskini, maradhi na ujinga!
Kwa akili ya kawaida tu... Ukihamia Dodoma ni lazima uendelee kuilinda zaidi Dar (gharama maradufu).
Jiulize, unahamia Dodoma ghafla ghafla bila kuwekeza kuboresha miundombinu yake ya barabara, maji safi, maji taka, n.k.... Je, umefanya tafiti ukajua itachukua muda gani kufikia mkwamo kama ule uliopo Dar??
Unaweka nguvu nyingi kuhamia Dodoma unaokoa nini? Au unaleta utofauti gani? Au bado unatafuta katikati ya nchi ndo uweke makao makuu??
Hiki ni kipindi ambacho badala ya kuzilundika idara, taasisi na wizara za serikali sehemu moja (centralization) ilitakiwa zitawanywe kwenye kila jiji hapa nchini kwa uwezo, nguvu na juhudi zile zile... Mfano Wizara ya Ardhi ijengwe Dodoma, Madini Mwanza, Utalii Arusha, Usafirishaji, Bandari Dar, Gesi Mtwara, n.k... Yaani kila jiji na kila Kanda ipate uwekezaji wa maana wa makao makuu ya ofisi, idara na taasisi za serikali...
Hatua hii ingechochea maendeleo ya miundombinu na mzunguko wa fedha kwenye shughuli mbalimbali za uchumi mikoani...!! Ikumbukwe kuwa kwenye nchi kama hii serikali ndo mwajiri kiongozi na mwenye job security nzuri... Badala ya kusambaza rasilimali watu na rasilimali fedha mikoani... Tunazitoa Dar na kwenda kuzilundika tena Dodoma...
Huu utawala wa sasa umeshindwa kabisa hayo mapambano. Badala yake wamekuja na vita wanavyoviweza vya maendeleo ya vitu... Yes, mtajenga sana vitu lakini ni vyema mkafahamu kuwa grafu ya ujinga, umaskini na maradhi inazidi kupanda juu!!