Kwanini Mwalimu Nyerere aliwafukuza Waisrael akawaacha Wapalestina?

Nyerere aliitikia wito wa umoja wa nchi za Afrika, OAU wakati huo, kuvunja uhusiano wa kibalozi na Israel kufuatia vita vya Yom Kippur kati ya Israel na Waarabu mwaka 1973. Yom Kippur ni sikukuu ya Kiyahudi. Misri na Syria ziliamua kushambulia Israel kwa pamoja, Misri upande huu na Syria upande ule, siku hiyo ya sikukuu ya Kiyahudi wakijua ulinzi utakuwa pungufu. Kweli ndani ya siku tatu walifanikiwa kutwaa maeneo kadhaa ya Sinai (kwa Misri) na Golan Heights (kwa Syria) ambayo yalikuwa yametekwa na Israel katika 'Vita vya Siku Sita' vya Mwaka 1967. Israel ikajipanga na kurudisha mapigano na kuyatwaa upya ndani ya wiki mbili maeneo yote yaliyokuwa yamekombolewa na wakaenda mbali zaidi na kutwaa maeneo mengine mapya.
Kutokana na kuongezeka kwa maeneo ya nchi za Kiarabu yaliyokuwa yanakaliwa na Israel, na kuonyesha mshikamano na Waarabu kwa ubabe huo wa Israel, OAU iliamua kuvunja uhusiano na Israel. Nchi mbili pekee za Afrika ndizo hazikuenda na uamuzi huo; nazo ni Malawi na Afrika Kusini, bado ikiwa ya kibaguzi siku hizo.
Juzi Jumamosi Wapalestina wameshambulia Israel wakijua siku hiyo ni ya mapumziko kwa Israel. Sijui nini kitafuata.
Watafutika kabisa hakuna namna
 
Are you sure tumechelewa kuendelea? Au unavaa miwani ya mbao tu? Kwa taarifa yako Tanzania ni moja na nchi 10 zenye uchumi mkubwa Afrika zikiwa ni pamoja na Nigeria, Egypt, Morocco, S/Africa, Ethiopia, Ghana, Kenya, Angola na Algeria
Uchumi mkubwa wwnyewe ndio huu wa kutungiwa sheria ni kosa kudadisi takwimu zinazotolewa na serikali
 
Nyerere alisitisha uhusiano na Israel katika kutekeleza sera zake za kupinga ukandamizaji na uonevu wa binadamu wa aina yoyote ambao ungetokea mahali popote bila kujali rangi na itikadi.

Kwa mtazamo na msimamo wake huo ndiyo uliomfanya aiunge mkono Palestina kwa hali na mali kwa gharama ya kuvunja uhusiano na Israel,nchi ambayo kiuchumi ilikuwa na mwelekeo wa kuwa mshirika makini na muhimu kwa Tanzania.

Kama ambavyo alivyoifanya Tanzania kutumia rasilimali zake kusaidia kwa hali na mali nchi za Zimbabwe, Namibia ,Msumbiji,Angola na Afrika ya kusini katika harakati zao za kudai uhuru na haki,..ndivyo Nyerere alivyoiunga mkono Palestina.

Lakini kwa mshangao wake Nyerere, ilikuwa ni Palestina hiyo hiyo iliyomuunga mkono Idd Amin wakati wa vita ya Kagera mwaka 1978.
Ikumbukwe Palestina na Libya ni nchi zilizoiunga mkono Uganda kwa kutoa silaha na wapiganaji ardhini.
Tanzania iliungwa mkono na Algeria kwa nguvu zote kwa kupewa shehena ya silaha nyingi hadi vita ilipoisha.

Kwa kupitia funzo hilo,nafikiri Tanzania ni vizuri kuendelea na sera yetu ya kutofungamana na upande wowote.
Hii sera maana yake ni ..siyo lazima rafiki yako awe rafiki yangu,au adui yako lazima awe adui yangu pia,..ugomvi wenu siyo lazima unihusu...,na ugomvi wangu na mtu siyo lazima wengine wahusike
ZIONIST CRIMES
75 years of ethnic cleansing
15 years of blockade
Confiscation of Palestinian lands
Pogroms on Palestinian towns
Desecration of Palestinian sacred sites
Daily raids into Palestinian homes
Constant humiliation of a entire people
Nothing about today is "unprovoked."
 
Sasa unajisaidiaje bila connection?
Connection inaleta transfer of technologies, una wataalam au magenius wa kubuni teknolojia yako mwenyewe? Kwa kizazi cha wabongo kinachowaza ngono muda wote?
Kuilaumu historia sio njia ya kujinasua katika umaskini tulio nao sasa.

Umaskini tunaukaribisha watu wa kizazi cha leo kisicho na curiosity ya kutenda kitu kwaajili ya maendeleo kwa taifa, na tunategemea serikali ndiyo itende kitu ili kuleta maendeleo ndani ya nchi na kubadilisha hali ya maisha ya kila mmoja.

Hakuna mtu anajiskia fahari katika kutenda kitu kwa ajili ya taifa, wote tunataka taifa litufanyie kitu bila sisi kulifanyia kitu,

Nyerere amefariki 1999 still mpaka sasa mnamlaumu yeye kama sababu ya kukwama,
Kwahiyo tutaishi kwenye umaskini hadi afufuke ili aje atuongoze tena katika njia nyingine ya maendeleo??
 
Misingi ikiharibika, na jengo lishajengwa, inahitaji sacrifice kubwa kuanza upya.
 
ZIONIST CRIMES
75 years of ethnic cleansing
15 years of blockade
Confiscation of Palestinian lands
Pogroms on Palestinian towns
Desecration of Palestinian sacred sites
Daily raids into Palestinian homes
Constant humiliation of a entire people
Nothing about today is "unprovoked."
Nyerere kuisaidia palestine na kuiacha Israel ukitizama kimantiki ilikuwa inasababishwa na vita baridi iliyoidominet dunia kwa wakati huo.

Kiuhalisia Israel ni nchi iliyokuwa ikipewa support fro the capitalist countries kama uingereza na washirika wake ukiwa ni msaada wa hali na mali na uamuzi huu ulifanyika ndani ya UN mwaka 1948 kunatokea Balfour declaration, kwa wakati huo ili waisrael walikuwa katika wakati mgumu kutokana na Adolph Aloyce Hitler kuwafanyia massacred and persecution.

Waingereza walihakikisha wajews wanapata sehem ndani ya palestine ili waishi hapo na ndy nchi hiyo inapata kutangazwa rasmi katika mkutano wa UN mwaka 1948,

Nchi hii inakuwa mshirika wa nchi za magharibi zinazofuata capitalism ideology kama vile uingereza na marekani.

Wapalestine wanakuwa na support from the other side inayoamini katika socialism ideology, Tanzania nayo baada ya uhuru wake mwaka 1961 ikawa ni nchi inayofuata socialism ideology.
Kanuni ya kuwa chini ya hizi ideologies ni kuisupport nchi mshirika wako na kuikandamiza nchi iliyokuwa upande wa pili.

Tanzania imekuwa benefited kwenye socialism katika mambo mbali mbali ya kimaendeleo kutoka kwa nchi washirika wake kama vile China na Russia.

Pesa za ujenzi wa miundombinu mbali mbali ndani ya nchi pia Tanzania imepokea misaada mbali mbali, silaha, elimu pamoja na scholarships za kwenda kusoma nchi za nje kama Cuba, Russia na China.
 
Soma niliposhajibu..., Principles Tumefaidika nini ? Unadhani kipindi kile Tanzania ilikuwa na Sifa kiasi gani kwenye upiginia Uhuru wa nchi nyingine za Kiafrika ? Waulize kina Museveni kuna kipindi alisema hii ni kama Hijja au Sehemu ambayo watu wa Imani wanakwenda kutoa Tribute (kizazi hiki mgekuwa na akili) mgeweza kuki-market watu wakawa wanakuja kutembea na kushukuru Msaada wa Babu zao waliopata kutoka Tanzania.... (that is Priceless) Lakini ukiwa unapima every Success na Dollar Signs huwezi kunielewa...
Hupimi success in Dollar wakati hiyo success imetumia Dollars au hizo harakati Tanzania tulizifanya bure bila gharama.

Basi sawa unamtetea Nyerere kwenye suala la Palestina. Vipi suala la Biafra kujitenga nalo Nyerere aliunga mkono nalo unamteteaje. Suala la Morocco kujitenga nalo aliwaunga mkono separatists.
Wakati huo amefanya muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo hataki utengano.

Nchi hata vyoo hamna ila vipaumbele vikawa kiherehere kila kona ya dunia. Sasa nini ilikuwa maana ya kuwa mwanachama wa NAM. Hizo sera za Nyerere zilikuwa zake binafsi, hazikuwa na mtazamo wowote kitaifa na mashiko hamna. Leo hii hata kiongozi awe nani pale Iran hawezi kuitambua Israel, sababu ni sera ya kitaifa sio sera ya mtu binafsi.

Nyerere alikuwa na kiherehere chenye kuhatarisha usalama wetu, uchumi na utengamano. Ndio kilisababisha ampe hifadhi Milton Obote baada ya kupinduliwa na Amin pale Uganda. Uliona wapi kwingine nchi maskini, kiongozi wa nchi anapewa political asylum nchi jirani kabisa na anakuja na wapiganaji wake wanapewa mafunzo na uwezeshaji.

Hao wenyewe Israel hawanunui ugomvi usiowahusu na wasio na maslahi nao. Israel haija silaha Ukraine wala kuisaidi Urusi, wakati huo Ukraine imetoa statement ya kuinga mkono Israel dhidi ya Hamas. Sababu Ukraine inapata support kutoka kwa walewale wanaoipa support Israel.

Diplomasia za nchi haziendi kishamba hivyo kama misaada ya waumini wa kanisa. Utaishia kuwa tambala la deki, huna mshirika kazi kujitia ujuaji kwa kila mgogoro duniani. China wana uchumi mkubwa ila unaona wamekula mute kwani wajinga? Wana migogoro yao wanayolazimika kuingia, sio kila kitu unajifanya unachukua upande.
 
Unaonekana unamchukia Nyerere sana unatamani we ndiyo ungepata nafasi ya kuwa yeye.

Lawama zako zipo kihisia sana.
 
Wewe gharama kwako ni dollar amount ? Gharama ya majirani zako kuwa katika ukoloni kwa watu walioamini kwenye PAN AFRICANISM how much is that in dollars ? Unaweza kununua kwa kiasi gani ?

Kwahio kwa mawazo yako aliwaunga mkono kwanini ?

What do you mean hakuna vyoo ? Au ndio yaleyale ya kuona choo cha ku-flash na maji ndio maendeleo wakati mtu / watu walikuwa na vyoo vya pit ambavyo kulingana na mazingira yao ni sustainable au wewe leo unajiona mjanja haja zako zote zinapoenda ziwani alafu unazinywa kwenye maji.....; Sera ya Kitaifa ni nini na inapangwa wapi..., mimi nimekwambia Tanzania hatufangamani na upande wowote ila kama kuna injustices ni ubinadamu hata kama msaada hautapelekwa ni jukumu kwa mtu / binadamu kuukemea
Nyerere alikuwa na kiherehere chenye kuhatarisha usalama wetu, uchumi na utengamano. Ndio kilisababisha ampe hifadhi Milton Obote baada ya kupinduliwa na Amin pale Uganda. Uliona wapi kwingine nchi maskini, kiongozi wa nchi anapewa political asylum nchi jirani kabisa na anakuja na wapiganaji wake wanapewa mafunzo na uwezeshaji.
Kwahio unadhani bila Obote kuja Tanzania Amin asingetaka kuichukua Kagera ? Wewe ndio wale unafuga nyoka jirani au unaona nyoka jirani na unamuacha aendelee kula kuku na bata wa jirani wakati akimaliza huko huenda akaja kwako..., kwahio kwako wewe Jirani yako kiongozi angeomba aje ajibanze kwako ungemfukuza kwamba usilete vita...,
Hao wenyewe Israel hawanunui ugomvi usiowahusu na wasio na maslahi nao. Israel haija silaha Ukraine wala kuisaidi Urusi, wakati huo Ukraine imetoa statement ya kuinga mkono Israel dhidi ya Hamas. Sababu Ukraine inapata support kutoka kwa walewale wanaoipa support Israel.
Ninaongelea injustices kwa yoyote anayofanya sio nani amefanya, sio lazima upeleke bunduki na risasi kwa watu wauwane ila unaweza ukakemea (sidhani kama Tanzania iliwasaidia kwa silaha za vita watu wakapigane) hayo yanafanywa na some western countries na sio kwa upendo bali wapo kwenye Biashara....
Diplomasia za nchi haziendi kishamba hivyo kama misaada ya waumini wa kanisa. Utaishia kuwa tambala la deki, huna mshirika kazi kujitia ujuaji kwa kila mgogoro duniani. China wana uchumi mkubwa ila unaona wamekula mute kwani wajinga? Wana migogoro yao wanayolazimika kuingia, sio kila kitu unajifanya unachukua upande.
Hio ndio inatiwa kutokuwa na misimamo wala unaposimamia..., Ndio maana nimekwambia Nyerere was consistent kwa kila anachokisimamia na alikiweka wazi hakuogopa nani atamfikiria vipi au kupoteza ushirika..., Mshirika wako akiwa principles zako na msimamo wako na sio nani amefanya nini utaheshimika and that is the stuff which leaders are made of........
 
Nyerere alisitisha uhusiano na Israel katika kutekeleza sera zake za kupinga ukandamizaji na uonevu wa binadamu wa aina yoyote ambao ungetokea mahali popote bila kujali rangi na itikadi.

Kwa mtazamo na msimamo wake huo ndiyo uliomfanya aiunge mkono Palestina kwa hali na mali kwa gharama ya kuvunja uhusiano na Israel,nchi ambayo kiuchumi ilikuwa na mwelekeo wa kuwa mshirika makini na muhimu kwa Tanzania.

Kama ambavyo alivyoifanya Tanzania kutumia rasilimali zake kusaidia kwa hali na mali nchi za Zimbabwe, Namibia ,Msumbiji,Angola na Afrika ya kusini katika harakati zao za kudai uhuru na haki,..ndivyo Nyerere alivyoiunga mkono Palestina.

Lakini kwa mshangao wake Nyerere, ilikuwa ni Palestina hiyo hiyo iliyomuunga mkono Idd Amin wakati wa vita ya Kagera mwaka 1978.
Ikumbukwe Palestina na Libya ni nchi zilizoiunga mkono Uganda kwa kutoa silaha na wapiganaji ardhini.
Tanzania iliungwa mkono na Algeria kwa nguvu zote kwa kupewa shehena ya silaha nyingi hadi vita ilipoisha.

Kwa kupitia funzo hilo,nafikiri Tanzania ni vizuri kuendelea na sera yetu ya kutofungamana na upande wowote.
Hii sera maana yake ni ..siyo lazima rafiki yako awe rafiki yangu,au adui yako lazima awe adui yangu pia,..ugomvi wenu siyo lazima unihusu...,na ugomvi wangu na mtu siyo lazima wengine wahusike
Nomaaaa
 
Uchumi mkubwa wwnyewe ndio huu wa kutungiwa sheria ni kosa kudadisi takwimu zinazotolewa na serikali
Ni World Bank ndiyo wanatoa Takwimu hizo siyo Tamzania. Kama unajuwa kusoma, Soma hapa:-

African giants: The 10 largest economies on the continent

Screenshot_20231009_191900_Google.jpg
 
Wewe gharama kwako ni dollar amount ? Gharama ya majirani zako kuwa katika ukoloni kwa watu walioamini kwenye PAN AFRICANISM how much is that in dollars ? Unaweza kununua kwa kiasi gani ?
Kuingilia masuala ya kisiasa ya Uganda ilikuwa ni kuikomboa dhidi ya ukoloni? Biafra vs Nigeria ni ukoloni? Morocco na separatists ni ukoloni?

Sasa kama ule wote ni ukoloni, kwanini Kagera salient kubaki Tanzania baada ya vita isiwe ukoloni?
Kwanini Zanzibar kuwa part ya Tanzania isiwe ukoloni?
Kwahio kwa mawazo yako aliwaunga mkono kwanini ?
Kwa kiherehere chake na misimamo yake binafsi ambavyo havina tija kwa taifa.
What do you mean hakuna vyoo ? Au ndio yaleyale ya kuona choo cha ku-flash na maji ndio maendeleo wakati mtu / watu walikuwa na vyoo vya pit ambavyo kulingana na mazingira yao ni sustainable au wewe leo unajiona mjanja haja zako zote zinapoenda ziwani alafu unazinywa kwenye maji.....;
Mambo ya vyoo naona yamekuuma sana. Ni kielelezo tu wa umaskini wetu
20230301_204027~2.jpg

Sera ya Kitaifa ni nini na inapangwa wapi..., mimi nimekwambia Tanzania hatufangamani na upande wowote ila kama kuna injustices ni ubinadamu hata kama msaada hautapelekwa ni jukumu kwa mtu / binadamu kuukemea
Unakemea kwa gharama zipi na ili iweje, kwanini kila jambo lisikupite. Opportunity cost gani unaingia.
Tungekuwa serious na mambo yetu mbona tungefika mbali.

Hao Palestina tuliwatetea kwenye cause yao na ajabu wakawa upande wa adui yetu, walimtetea Mwislamu mwenzao aliyewasaidia kuiteka ndege ya Israel. Wao walikuwa allies wa Uganda, sisi tulikuwa viherehere wa Palestina.
Kwahio unadhani bila Obote kuja Tanzania Amin asingetaka kuichukua Kagera ?
Kwanini nidhanie? Leo hii Kagame akipinduliwa akahamia Tanzania na majeshi yake kisha akapewa mafunzo na JWTZ na silaha unadhani serikali ya whatsoever pale Rwanda itakuwa sawa na Tanzania?

Tulifaidika nini na Obote kuweka kambi Tanzania, kuanzisha mashambulizi ya kumpindua Amin, kuanzisha insurgency dhidi ya Uganda. Museveni kuishi Tanzania hadi kupata mtoto, kupewa mafunzo Tanga na kupewa silaha za kufanya uvamizi kwa Amin?

Kenya walipungukiwa nini walipokaa neutral kwenye vita ya Tanzania na Uganda?
Wewe ndio wale unafuga nyoka jirani au unaona nyoka jirani na unamuacha aendelee kula kuku na bata wa jirani wakati akimaliza huko huenda akaja kwako..., kwahio kwako wewe Jirani yako kiongozi angeomba aje ajibanze kwako ungemfukuza kwamba usilete vita...,
Nchi sio chumba chako au nyumba yako ya matofali, haiendeshwi kiagape kama unavyotaka. Kila maamuzi yana risk hivyo huwezi ingia risk kisa sifa za kijinga na wakati benefit hakuna.
Hata Amin hakwenda Congo au Kenya au Rwanda majirani alivyopinduliwa, alienda Libya na hawakukaa naye akaenda Saudi Arabia.

Unadhani Kambona angekimbilia Kenya badala ya Uingereza Nyerere angekuwa na mahusiano mazuri na Kenyatta?
Ninaongelea injustices kwa yoyote anayofanya sio nani amefanya, sio lazima upeleke bunduki na risasi kwa watu wauwane ila unaweza ukakemea (sidhani kama Tanzania iliwasaidia kwa silaha za vita watu wakapigane) hayo yanafanywa na some western countries na sio kwa upendo bali wapo kwenye Biashara....

Hio ndio inatiwa kutokuwa na misimamo wala unaposimamia..., Ndio maana nimekwambia Nyerere was consistent kwa kila anachokisimamia na alikiweka wazi hakuogopa nani atamfikiria vipi au kupoteza ushirika..., Mshirika wako akiwa principles zako na msimamo wako na sio nani amefanya nini utaheshimika and that is the stuff which leaders are made of........
Kama Nyerere alikuwa na misimamo ya nchi za Nigeria na Morocco kujitenga. Kwanini hakuwa na msimamo uleule kutaka Zanzibar ijitenge?

Nyerere alikuwa anaongoza taifa hivyo alitakiwa awe na misimamo yenye tija kwa taifa. Sio misimamo inayotia hasara na mwishowe hamna faida tunapata.
Hii ni nchi, mambo ya misimamo binafsi kama unataka baki nayo uongozee familia yako. Huwezi ongoza Tanzania taifa kwa ujumla alafu kisa wewe ni Mwislamu basi uiunge nchi kwenye OIC. Au kisa Mkristo basi upinge wawekezaji Waarabu wenye tija, au kisa Mwislamu ukubali wawekezaji Waarabu wasio na faida. Kila kitu kinafanywa kwa kutanguliza maslahi ya taifa, sio sifa au mawazo personally ya mtu.

Nchi serious inatengeneza washirika, hairopoki kila kitu mwishowe inakuwa kiherehere. Ukiwa na mshirika ni bega kwa bega, ukiwa kiherehere huyo unayejipendekeza kwake ana washirika wake. In times of need atachagua mshirika sio kiherehere. Palestina ilimchagua Amin over Nyerere sababu hiyo. Libya pale Ghadaffi alimchagua Amin wakati alikuwa anamheshimu Nyerere sababu ni alliance. Ikulu haingozwi na akili za kuongoza sebuleni.
 
Miongoni mwa makosa ya mwalimu ndiyo hayo!, Tanzania ingekuwa mbali mno, uzuri wakihamia wamehamia, hawageuki nyuma, hawana akili mbilimbili kama wahindi.
Huu ndiy uivu wa kufikiri! Zaire, Cng Brz, Uganda....zte zilikuwa na uhusian wa karibu na Israel, wameendelea kutushinda? Maendeleo ni maamuzi yak hakuna mtu atakayekuletea maendele, hata katika maisha yak biinafsi. Acha ukupe!
 
Unaonekana unamchukia Nyerere sana unatamani we ndiyo ungepata nafasi ya kuwa yeye.

Lawama zako zipo kihisia sana.
Kumkosoa mtu ndio kumchukia? Mbona unatumia akili za mashabiki wa soka Tanzania.
Nyerere mwenyewe alitaja makosa yake kwenye Tujisahihishe, ina maana alikuwa anajichukia?

Nyerere ni Rais bora zaidi kati ya waliotokea Tanzania, kwangu mimi. Kuwa Rais wangu bora hakunifanyi nisiseme makosa yake
 
Kuingilia masuala ya kisiasa ya Uganda ilikuwa ni kuikomboa dhidi ya ukoloni? Biafra vs Nigeria ni ukoloni? Morocco na separatists ni ukoloni?

Sasa kama ule wote ni ukoloni, kwanini Kagera salient kubaki Tanzania baada ya vita isiwe ukoloni?
Kwanini Zanzibar kuwa part ya Tanzania isiwe ukoloni?
Kwamba Tanzania tunasifika kuwa mstari wa mbele wa kugombania Uhuru wa nchi za Kiafrika kwa kupigana / kuhusika na Uganda (ambao walituvamia) Unazungumzia kwanini Nyerere alihusika na Issue za Morocco ? Ngoja niache kwenda Deep Sana nikupe tu article ujisomeee Kumbuka hapa point kubwa ni kukwambia Kukomboa your fellow man ni more of a success kuliko any dollar amount....

In 1979, Mwalimu Nyerere was among the then Organisation of African Unity’s (OAU) “wise” leaders who met in Monrovia to seek an an end to the war. However, the then King of Morocco boycotted. Nevertheless, they “unanimously called for Morocco to call a cease-fire and withdraw from the disputed area.”

A confidential briefing in the US thus captured our clear stance:

“FROM THE TANZANIAN STANDPOINT, THE PURPOSE OF THE MONROVIA MEETING IS TO SEEK AGREEMENT OF ALL PARTIES TO THE IMPLEMENTATION OF THE OAU MONROVIA SUMMIT RESOLUTION REGARDING THE WESTERN SAHARA. AS EXPLAINED TO US, THE RESOLUTION CALLS FOR THE HOLDING OF A REFERENDUM IN THE TERRITORY OF WESTERN SAHARA IN WHICH RESIDENTS WOULD BE ASKED WHETHER THEY WISHED THE PRESENT STATUS QUO TO CONTINUE OR DESIRED SELF-DETERMINATION. HAVING FORMALLY RECOGNIZED THE [SAHARA ARAB DEMOCRATIC REPUBLIC] SADR AS THE LEGAL GOVERNMENT OF WESTERN SAHARA IN NOVEMBER 1978, TANZANIA INTERPRETS A VOTE FOR SELF-DETERMINATION TO MEAN INDEPENDENCE AND THE INSTALLATION OF A POLISARIO BACKED GOVERNMENT IN THE TERRITORY”

The briefing also observed that Tanzania viewed Morocco as the chief impediment to the resolution. It also noted that Mwalimu Nyerere was committed to persuade the King. Yet it concluded:

“WE BELIEVE NYERERE IS ATTENDING THE MONROVIA MEETING BECAUSE OF HIS STRONG VIEWS ON THE WESTERN SAHARA ISSUE. HE REGARDS MOROCCAN POLICY IN THE WESTERN SAHARA AS MISGUIDED, DESTRUCTIVE OF AFRICAN UNITY AND NEO-COLONIAL IN ITS ATTEMPT TO SUBJUGATE THE SAHARAN PEOPLE BY FORCE OF ARMS. NYERERE, CONVERSELY, SUPPORTS POLISARIO AS LEGITIMATE FORCE FIGHTING FOR SELF-DETERMINATION AND INDEPENDENCE OF THE TERRITORY…. FROM OUR VANTAGE POINT, WE BELIEVE NYERERE WILL EXERCISE VIGOROUSLY HIS CONSIDERABLE SKILLS OF PERSUASION UPON KING HASSAN TO BEGIN NEGOTIATION PROCESS AND PERMIT THE WESTERN SAHARA POPULATION TO EXERCISE ITS RIGHT OF SELF-DETERMINATION”.
Kwa kiherehere chake na misimamo yake binafsi ambavyo havina tija kwa taifa.
Kwamba kwa Heshima na Kuwa kwake among viongozi wa Afrika kulikuwa hakuna tija ? Kwako tija ni nini ? Kuna tija zaidi ya kumsaidia your fellow man unapoona injustices...
Mambo ya vyoo naona yamekuuma sana. Ni kielelezo tu wa umaskini wetuView attachment 2777037
Unaongelea vyoo vya shule yaani karne hii au kipindi kile kujenga choo kwako unaongelea Rais, Unawajua DANIDA na nchi za NORDIC zilivyosaidia kujenga na kukarabati mashule ?, Mimi nakwambia kama tu kuchimba shimo cha choo (ambacho kwa shule yenye watu wengi ni more sustainable inawashinda leo issue sio kukosa au kupata fedha bali ni matatizo between the ears) By the way Nyerere amekufa lini hadi leo hii huusishe mishaps zako na yeye....
Unakemea kwa gharama zipi na ili iweje, kwanini kila jambo lisikupite. Opportunity cost gani unaingia.
Tungekuwa serious na mambo yetu mbona tungefika mbali.
Tungefika mbali sana wapi..., Na tangia amekufa ni wapi timefika..., kwanini jambo likupite kama wewe unaona African Liberation ndio everything ukianza kuchagua hili likupite ili ufanye lile au nani anakupa nini hakuna tofauti na prostitute anayejiuza kwa highest bidder
Hao Palestina tuliwatetea kwenye cause yao na ajabu wakawa upande wa adui yetu, walimtetea Mwislamu mwenzao aliyewasaidia kuiteka ndege ya Israel. Wao walikuwa allies wa Uganda, sisi tulikuwa viherehere wa Palestina.
Aisee kwamba Unatetea mtu atakayekutetea kesho na sio kile kinachofanyika ? Yaani mtizamo wako na wangu tutakesha..., Unatetea injustices na sio nani amefanya, mbona hili jambo lipo wazi kabisa....
Kwanini nidhanie? Leo hii Kagame akipinduliwa akahamia Tanzania na majeshi yake kisha akapewa mafunzo na JWTZ na silaha unadhani serikali ya whatsoever pale Rwanda itakuwa sawa na Tanzania?
Unajua akipunduliwa akiwa Rais aliyechaguliwa na wananchi technically huyo ni Rais na sisi majirani tunaweza kumuhifadhi (ukizingatia stability and the devil you know and all that)....
Tulifaidika nini na Obote kuweka kambi Tanzania, kuanzisha mashambulizi ya kumpindua Amin, kuanzisha insurgency dhidi ya Uganda. Museveni kuishi Tanzania hadi kupata mtoto, kupewa mafunzo Tanga na kupewa silaha za kufanya uvamizi kwa Amin?
Unajua Obote alikuwa Rais akapinduliwa na sio vinginevyo ?, Kabla ya Museveni hajachukua Uganda unajua stability ya Uganda ilikuwaje ?
Kenya walipungukiwa nini walipokaa neutral kwenye vita ya Tanzania na Uganda?
Ulitaka Kenya aingilie vita vya Uganda na Tanzania ili iweje ? Na angeingilia huoni kwamba isingekuwa vita ya nchi mbili bali all of East Africa and before you know it Vita vya Afrika.., Uingiliaji wa nchi kwenye vita ni kukemea na vita viishe na sio kuchochea viingilie, na sisi uingiliaje wetu ulikuwa ni mashinikizo wa kumaliza sio kuendeleza
Nchi sio chumba chako au nyumba yako ya matofali, haiendeshwi kiagape kama unavyotaka. Kila maamuzi yana risk hivyo huwezi ingia risk kisa sifa za kijinga na wakati benefit hakuna.
Kwamba kuikomboa Africa na huenda in the end Afrika kusimama as an empire against marginalization of western countries hakuna benefits...
Hata Amin hakwenda Congo au Kenya au Rwanda majirani alivyopinduliwa, alienda Libya na hawakukaa naye akaenda Saudi Arabia.
Unadhani kwanini ?, Unadhani hio sio sababu ya uchizi wake....
Unadhani Kambona angekimbilia Kenya badala ya Uingereza Nyerere angekuwa na mahusiano mazuri na Kenyatta?
Huu mfano mbona umekaa kushoto..., Yaani mpinduaji ndio akaribishwe ? Unadhani Nyerere angepinduliwa Kenya wasingemkaribisha ?
Kama Nyerere alikuwa na misimamo ya nchi za Nigeria na Morocco kujitenga. Kwanini hakuwa na msimamo uleule kutaka Zanzibar ijitenge?
What happened in Zanzibar was it the same kama hizo nchi ?
Nyerere alikuwa anaongoza taifa hivyo alitakiwa awe na misimamo yenye tija kwa taifa. Sio misimamo inayotia hasara na mwishowe hamna faida tunapata.
Hii ni nchi, mambo ya misimamo binafsi kama unataka baki nayo uongozee familia yako. Huwezi ongoza Tanzania taifa kwa ujumla alafu kisa wewe ni Mwislamu basi uiunge nchi kwenye OIC. Au kisa Mkristo basi upinge wawekezaji Waarabu wenye tija, au kisa Mwislamu ukubali wawekezaji Waarabu wasio na faida. Kila kitu kinafanywa kwa kutanguliza maslahi ya taifa, sio sifa au mawazo personally ya mtu.
Haya umeyatoa wapi ?
Nchi serious inatengeneza washirika, hairopoki kila kitu mwishowe inakuwa kiherehere. Ukiwa na mshirika ni bega kwa bega, ukiwa kiherehere huyo unayejipendekeza kwake ana washirika wake. In times of need atachagua mshirika sio kiherehere. Palestina ilimchagua Amin over Nyerere sababu hiyo. Libya pale Ghadaffi alimchagua Amin wakati alikuwa anamheshimu Nyerere sababu ni alliance. Ikulu haingozwi na akili za kuongoza sebuleni.
Nchi serious ina misimamo yake wala haiwi swayed na kina nani wamesema, haichaguliwi rafiki wala adui wala haipangiwi cha kufanya....., hapo watu wakijua hayo wala hawatakuletea za kuleta...,

Nikimnukuu 2Pac - 'I'd rather die like a man, than live like a coward'
 
Back
Top Bottom