Mzee unanitisha Sasa ...Kuna mtu unaemjua alieuliwa?.Sikia sasa; .Ukisema neno ''mungu''!! hatujui una maanisha mungu gani!! bado weye mwenyewe hujui unacho uliza!! kwa sababu Miungu wapo weeengi tangia zama,
Hata Biblia Takatifu imewataja baadhi ya miungu wengii tu kuwa walikuwepo na wapo.. km mungu Baal, Osilis nk!...na hao miungu iliwasaidia sana walio iamini! Mfano mungu wa Misri huyu alishindana na Musa sana tu!!
mungu wa wafilist waliye muamini mpaka akawasaidia kumtia hatiana mbaya wao samsoni, huyu alimshinda Mnadhili wa Mungu tangu tumboni Bwana Samson, kupitia Delila mpaka akatobolewa Macho.
hivo samsoni akasota kweli kweli! nadhani unajua! Washami pia walikuwa na mungu wao aliye washindisha vita...wahaya wana mungu wao wa mazao mpaka leo anaitwa ''Umukama we charo''
Wakurya wana ''Nyanokwe'' anae wapa, Mazao, mvua, nguvu vitani, ndo maana wakurya wanapenda jeshi! na hawashindwi mstari wa mbele!...
Wabondei, wasambaa, wazaramo nk! wana mungu wao maarufu kama ''kiti'' huyu wanamjengea vinyumba vidogo! vidogoo! vya nyasi
size ni usawa wa ugoko! wanapalilia pale na huyo mungu wao anawalinda kweli kweli! Wachaga ndo usissikie wao kila December lazima wanaenda kuonana na kumchinjia Mungu wao Wanyama km ng'ombe mbuzi,
Hapo wanapata damu ya utakaso maarufu wanaita kisusio! lengo ni ili wafanikiwe ktk Maisha yao na Biashara zao! na kweli wako mbali ktk hii Biashara!
Wazungu wao wana muabudu mungu wao, Mzungu vilevile! huyu wanamuomba ili awape nguvu watawale Dunia ktk nyanja zooote!! na kweli kawapa miguvu tele!! hakuna wa kupinga ktk hili!
na wao wanaenda kuhiji Vatican kila mda unapo waruhusu kufanya ivo!...hapo nimekupa kwa kiasi tu, na kuna mungu mwingine yeye huyo hafananishwi na kitu chochote huyo yuko kivyake vyake tu!!
na huyo haoni tabu watu wake kuua wasio muamini, na kumsema hovyo! hovyo!! hata weye leo hii ukimsema hovyo! watakusaka mpaka wakuue popote ulipo hapa Duniani! na Listi ya wanao windwa ni kubwaa!
kusema kweli huyo simtaji nisije uawa Bureee!! wanakula kichwa........ sasa weye ndugu yangu sema wewe unamsema mungu gani huyooooo! kati ya hao wooote hapo juu? make list ni kuuubwa sana?
ila ujichunge mno kuhusu hao miungu make kuna maeneo ukigusa tu unaliwa kichwa hapo hapo mbele ya computer yako!! hayaa yangu ni hayo!
Ok, Sasa hizi ibaada zipo kwaajili Gani? Na Kwa manufaa ya nani?Uko safi, naanza kupenda namna unavyofikiria.
Chukulia hii Hypothetical Experiment; Aassuming tungekuwa tunaweza kufanya expereiment kwa kutumia binadamu aliye hai:
KWAMBA umchukue mtoto mdogo aliyezaliwa leo, mpeleke akaishi peke yake porini na kwamba hakuna kitu kinachoweza kumdhuru huko na wala hakuna hitaji analoweza kukosa. Akue akiwa huko peke yake na akili yake iendelee kuwa kawaida pasipo kuwa kasoro yoyote, huku akiwa hana kabisa interaction na binadamu mwingine yeyote, na possibly asijue kabisa kuwa wapo binadamu wengine zaidi yake yeye.
Baada ya kuwa amkekuwa mtu mzima huku akiwa anaendelea kuishi katika mazingira hayo, unadhani nje ya kufanya kazi za kawaida kujipatia mahitaji yake ya kawaida kama vile chakula na maji, nini kingine cha ziada ambacho ni lazima tu atakifanya atake asitake, ukizingatia kuwa huwa anaona:
1. Jua linachomoza mashariki na kuzama magharibi kila siku;
2. wakati mwingine mvua ikinyesha na mawingu yakiwa yanatembea angani kila siku
3. kila kitu kilichoko juu angani na vyote vilivyoko juu ya ya ardhi, n.k.
Mtu yeyote MWENYE AKILI TIMAMU, akishayaona mambo haya yote, kitakachofuata baada ya hapo ni IBADA. Sasa, whether atafanya Ibada ya kumwabudu Mungu wa kweli ama la; hilo sasa litakuwa ni swala jingine. Naturally mtu yupo kwa ajili ya Ibada; kitu core kwa kiumbe yeyote anayeitwa binadamu ni Ibada
Hata hivyo, Ibada nazo pia zipo nyingi. Zipo za kwenye majumba ya Ibada na zipo za nje ya majumba ya Ibada. Kwa mfano, kufanya kazi zako sawasawa na na sheria za nchi ikiwa ni pamoja na kuwatendea haki watu wanaofika ofisini kwako wakihitaji msaada wako; hiyo nayo pia ni Ibada nyingine
Hizi ndiyo mojawapo ya Ibada ambazo kwazo Mungu alikuumba ili umwabudu
Unaposema muda unamaanisha Nini? Majira au?ndio haswa binadamu katika mfumo wa maumbile ya mwili ndio amejiwekea mda kwa sababu ana mwanzo na mwisho kimwili , mda ni dhana yakufikirika tu mjomba , kulingana na mabadiliko ya nchi , ndo maana mda ni tofauti kulingana na eneo moja na jingne , yani ni kupanga tu kwamba tukiona jua la utosi ni sa sita , tukiona mvua zinanyesha ni mwezi wa tatu masika na hyo dhana tunaijenga kichwan kwa mda mrefu , ndo maana umehisi inauhalisia kbsa , na ndio maana una limit nguvu kuu kwenye mda.
Mungu ndio mtoa pumzi na chanzo cha upendo kwetu sisi wanadamu.
Ulimwengu si sababu ya Mungu kuwepo kwani yeye ndiye aliyeuumba.
Angeendelea kuwepo hata asingeumba ulimwengu na sisi wanadamu.
Kiukweli imani zetu za kidini hazituweki wazi sana juu ya sababu hasa ya Mungu kuumba ulimwengu.
Kwanini asingeacha tu??
Kuumba ulimwengu kunamfaidisha nini hasa??
Kutokuumba ulimwengu kunahasara gani kwake??
Je, hakujua anguko la mwanadamu kabla ya uumbaji wake??
Zaidi, baadhi ya dini zinatuambia kwamba kulingana na ukuu wa Mungu, baadhi ya maswali hayawezi kujibika kwa akili zetu na tutapata nafasi ya kuuliza maswali yanayo tutatiza tufikapo mbinguni.
NB: Huwezi kuelezea uwepo wa Mungu nje ya imani za kidini (ni swala la imani tu).
Point yangu ni kwamba, kupitia ufafanuzi wako kuwa Mungu ni energy unakuwa umekubali kuwa Mungu sio muumba wa kila kitu.ni kweli sifi kinachofanyika ni hyo energy kuchange kwenye state nyingne tu , swala la uumbaji naomba tutazame kwenye mfumo wa energy kuwa tu kwenye state nyngne. chukulia mfano wa watoto wawili walio tumboni kwa mama yao , huko ndn wajadili swala la kwamba hakuna mama , ndivyo sisi tunaona hakuna Mungu , siku ukipata mafanikio ya kutoka kwenye gereza la mwili utajua kumbe kuna mengne zaidi ya ulivyokua unafikiri kwemye mwili wenye mipaka yake.
Basi hapo tatizo liko kwako, huna uwezo wa kumuelewesha mtu akaelewa au swali ni gumu huna majibu na hutaki kukubali kuwa hujuiEti mtu unataka kujua √(3) inafanywaje hali hujui 1+1 inafanywaje !!! 🤣--- elimu zingine zahitaji kupitia hatua baada ya hatua.
Basi hapo tatizo liko kwako, huna uwezo wa kumuelewesha mtu akaelewa au swali ni gumu huna majibu na hutaki kukubali kuwa hujui
Mungu ni creation ya mwanadamu kichwani kwake naamini ilitokana na kushindwa kujibu maswali magumu yaliyomkabiri au kutaka control ya binadamu wenzake, hakuna proof yeyote ya uwepo wa mungu, ingawaje kwa akili yetu ndogo naamini kuna kitu kimetuzidi uwezo ndio maana hatuelewi mambo mengi,infact hatujui hata tumetoka wapi tunaelekea wapi, enjoy tuu safari ya maisha labda kuna siku tutakuja kujua ukweli wa kila kitu kuanzi9a atoms mpaka galaxies na universe kwa ujumla
Hujui chochote pia acha kujidanganyaKama wewe hujui usidhani na wengine ni kama wewe.
Hapana Mungu amekuwepo hata kabla ya huu ulimwengu kuwepo, uthibisho huu ulimwengu sio binadamu ndio walianza kuumbwa bali ni majini kwanza kabla ya wanadamuKwahyo viumbe wote wa kwenye Huu ulimwengu ndio wamemfanya Mungu awepo?
Hawa viumbe wasingekuwepo na Mungu asingekuwepo?
Mungu ni undefined object,achunguziki kisayansi zaidi ya kiroho.Shetan pamoja na nguvu zake zote still hawezi fikia ukuu wa MunguKivyovyote TU, au vyote kama unaweza please
unachozungumza bado ni illusion tu wakati ni sasa future ni matazamio tu ambayo bado hayajatokea , muda unapata mantic kunapokua na mwanzo na mwsho , unaposema nitachemsha yai umeitengeneza future kichwan inaweza isitokee , ila unapochemsha yai ndo kitendo kinakua sio illusion , siku ni zile zile matukio ni yale yale nanapata mantic yanapotokea now ila ukiyazania bado inakua ni illusionUnaposema muda unamaanisha Nini? Majira au?
Maana muda upo TU ila majira ndio Wanadamu tumeyatengeneza.
Ni sawa na umbali; Hivi vipimo vya kilometer, centimeters,maili,heka,mita, Tumevitengeneza TU sisi binadamu, ilikuwa inawezekana kabisa centimeter 1 tungeifanya Ikawa sawa na kilomita 10 au centimeter tungeiita Magufulita na maili tukaita samiamita...ni sisi na Sheria zetu TU.
Lakini haimaanishi huo umbali wa centimeter 1, kilomita 2,maili 3 haupo.....Hata tukisema tupime Kwa kamba umbali wa Maili 1 halafu tuuite kilomita 8, Bado ule umbali tulioupima haubadiliki urefu wake, hata kama Leo tuuite ni kilometer 10 na kesho tuite centimeter 3...umbali wenyewe utabaki palepale haubadiliki.
Kwahyo kwasababu hizi kilometer, metre,maili, centimeters zimetengenezwa na binadamu, isiwe kigezo Cha kusema hakuna Space, Hakuna nafasi, Hakuna Umbali...kwamba kwakuwa kilometer ilitengenezwa na binadamu basi unaweza kukanyaga Tambo Moja TU ukaupita huo umbali kwasababu hiyo nafasi haipo ni illusions TU.
Muda upo, ingawa vipimo vya sekunde,siku,masaa,mwaka,miezi vimetengenezwa na binadamu...Tungeweza kusema mwaka una miezi 10 TU yenye siku 40 kila mwezi...na kusingekuwa na shida yoyote, lakini muda unaopimwa Kwa hivyo vipimo upo....lazima matukio yaendelee...Muda ukisimama inamaanisha matukio yamesimama...
Kama hakuna muda Inamaana hakuna mabadiliko, yani mfano unapokuwa unapika Yai halitakiwi kuiva....Maana likiiva limebadilika, na likibadilika limeshaonesha kuwa kuna muda uliopita lilikuwa halijapikwa,maana kuku hatagi mayai yaliyopikwa.
Baada ya muda kupita ndio tukio la kupikwa likafanyika na Yai likaiva....Hiyo ni athari ya muda.
kma Mungu ni super energy na energy ndo imefanya maumbile yote yanayooneka na yasio uonekana yawepo katika frequence mbalimbal , nawezaje kusema hiyo energy haija umba kila kitu?Point yangu ni kwamba, kupitia ufafanuzi wako kuwa Mungu ni energy unakuwa umekubali kuwa Mungu sio muumba wa kila kitu.
Hilo ni jambo ambalo nataka nikuone unakubali kabla ya kuenda mbele zaidi
Haya mambo ya dini yanachangamoto nyingi.Mimi swali la je, hakujua anguko la binadamu? naweza kumsamehe hata akisema atatuambia tukifika mbinguni...
ila swali la kwanini tunamuabudu na kumsifu?...kama asipotuambia sababu za kwanini tunafanya hivyo tukiwa Bado duniani.
Inamaana anatupa command ya kufanya vitu Tena Kwa vitisho kuwa tusipovifanya anatupeleka motoni....Halafu sababu ya kufanya hivo vitu hatuambii.
.inakuwa kama anafanya udikteta Fulani usiomfaidisha yeyote...sio yeye Mungu sio sisi binadamu
Wewe mwenyewe huwa unafanya Ibada. Kwa nini huwa unafanya?Ok, Sasa hizi ibaada zipo kwaajili Gani? Na Kwa manufaa ya nani?
Babu nadhani bado uko shule! mie sikutishi ila natamka ukweli! ......wengi wamekufa mfano Suleiman Rushdie, anatafutwa auliwe, na zawadi NONO! itatolewa mpaka sasa IKO HIVO! ukiwa na ubavu kamsake!Mzee unanitisha Sasa ...Kuna mtu unaemjua alieuliwa?.
Ila Mimi Ningeuliza Kwa Yule Mungu aliwaumba watu wote wa dini zote, wazungu Kwa wahindi Kwa waafrica.
Sasa kama sio viumbe ndio wamemfanya Mungu awepo, Je sababu ni nini?Hapana Mungu amekuwepo hata kabla ya huu ulimwengu kuwepo, uthibisho huu ulimwengu sio binadamu ndio walianza kuumbwa bali ni majini kwanza kabla ya wanadamu, binadamu ameumbwa kwa mfano wa Mungu baada ya majini kugoma kumuabudu Mungu.Kabla ya majini kuwepo duniani,vipo viumbe vingine vingi pia katika sayari zingine nje ya Dunia.
Mfano UFO, malaika,nk.
Na still pana mamilioni ya sayari zingine ambazo hazijagundulika kwa macho ya sayansi ya mwanadamu.