Kwanini Mungu yupo?

Kwanini Mungu yupo?

Mcqueenen

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2019
Posts
7,262
Reaction score
12,618
NB: Huu mjadala sio wa kubishana kama mungu yupo au hayupo.
Hapa ninataka kuwauliza Kwa upole wale tunaoamini tayari kuwa Mungu yupo...Je, kwanini yupo?

Yaani siulizi mungu ametokea wapi/ametokanaje...
Hapa naulizia Kuna ulazima Gani wa yeye kuwepo? na kwanini yupo?

Mfano mtu akiuliza kwanini viti vya kukalia vipo, huwezi kujibu kwasababu mbao zikikatwa na kuchongwa vizuri zinatengeneza kiti, hapa utakuwa umejibu viti vinatokanaje....jibu zuri ni kwasababu vinatufanya binadamu tukae na kupumzika, hivyo tumevitengeneza...Inamaana bila kuwepo binadamu wenye shida ya kukaa basi viti visingekuwepo...

Kwahyo napouliza kwanini Mungu yupo? Siulizii chimbuko lake ametokana na Nini, ila naulizia ni sababu Gani iliyompelekea/iliyomlazimu yeye awepo.

Kuna wanaosema Mungu yupo ili auumbe ulimwengu, kwahyo function kubwa ya Mungu ni kuumba na kuendesha ulimwengu.

Hilo jibu kwangu halitoshelezi kwakuwa, Ningeuliza kwanini Huu ulimwengu upo?, Kwani Kuna ulazima ulimwengu uumbwe?

Kama Kuna ulazima wa ulimwengu kuwepo, basi Inamaana ulimwengu una thamani kuliko Mungu, kama binadamu tulivyo na thamani kuliko viti. Maana sisi ndo tumeleta viti, basi Ulimwengu umemleta Mungu.(yaani kama ni lazima ulimwengu uwepo, basi ulimwengu ndio umemlazimu Mungu awepo kama ambavyo Nyumba zinawalazimu mafundi ujenzi kuwepo,Simu zinawalazimu wauza simu kuwepo,Magari yanawalazimu madereva kuwepo, wahalifu wanalazimu polisi kuwepo nk.)

Lakini common sense inakataa.
Ingewezekana TU kusiwe na chochote, Hamna Dunia,hamna,Nyota,Hamna sayari, na Hakuna Mungu.

Sasa kwakuwa hivi vitu vipo, Je ni kwanini vipo?

Na kama ingewezekana kusiwepo kitu,Je ni Nini kililazimisha Mungu awepo?

Na kama mungu alikuwepo kabla ya Ulimwengu, na hakulazimishwa kuumba ulimwengu (angeamua angeacha na kubaki mwenyewe) Je yeye kwanini yupo? Nini kilipekea yeye kuwepo?

Kwanini Mungu yupo?
 
Unatafuta nini!?..namaanisha ukijua kwa nini yupo unapata nini?..unahitaji nini katika hilo?
Nitajua kwanini sisi tupo duniani.
Ni swali la muhimu sana...ambalo hata wewe unatakiwa ujiulize.

masheikh, wachungaji, misahafu visituchimbe biti tuogope kuuliza maswali ya muhimu hapa duniani, sisi kama binadamu.
 
Mapepo hayo. Matunda ya Kundalini hayoo. Ma dimon yame watawala.
Wafia dini hapo ndipo mnapofeli.
Mtu kauliza maswali yake,
Badala ya kutoa majibu unaanza kusema eti ana mapepo.
Huoni kuwa wewe ndiye mwenye mapepo?

Yaani watu kama nyie ndiyo mnafanya watu wazidi kuamini Mungu hayupo.

Mtu akiuliza swali, toa majibu.
 
Nitajua kwanini sisi tupo duniani.
Ni swali la muhimu sana...ambalo hata wewe unatakiwa ujiulize... masheikh,wachungaji,misahafu visituchimbe biti tuogope kuuliza maswali ya muhimu hapa duniani,,,sisi kama binadamu.
Qur'an haijakuchimba biti,sijui biblia...binadam ana ukomo wa ung'amuzi.

Kama ambavyo nyumbu kwa umoja wao dhidi ya Simba wasingeliwa ndivyo binadam na uelewa/upembuzi wa Mambo ulivyo kwake,ana ukomo..na Kama unataka kujua kwa nini upo hapa,Qur'an inasema tumeumbwa ili tuabudu
 
Qur'an haijakuchimba biti,sijui biblia...binadam ana ukomo wa ung'amuzi...Kama ambavyo nyumbu kwa umoja wao dhidi ya Simba wasingeliwa ndivyo binadam na uelewa/upembuzi wa Mambo ulivyo kwake,ana ukomo..na Kama unataka kujua kwa nini upo hapa,Qur'an inasema tumeumbwa ili tuabudu
Kwahyo Jibu lako ni kuwa binadamu hatuwezi kung'amua swali langu??
Kwanini hatuwezi? Je Quran imesema hatuwezi kung'amua swali langu?

Kama tumeumbwa kuabudu...kwanini tunaabudu? Mungu anapata faida Gani na ibada zetu?
 
Kwa muktadha wa uislam 'ibada ni kufuata utaratibu uliowekwa'..Kuna ibada za hiyari Kama swala,kufunga(hiyari ya lazima) na Kuna ibada za lazima,kula,kulala,kuhema/pumua...ndiyo maana Qur'an inasema mtatuabudu mtake msitake,anapata faida gani.

Hilo anajua yeye,Qur'an inasema hii dhimma ya usimamili wa walimwengu(ukhalifa) ambayo binaadam aliikubali,wakipewa viumbe wote wakakataa lakini binaadam akaikubali
 
Kwa muktadha wa uislam 'ibada ni kufuata utaratibu uliowekwa'..Kuna ibada za hiyari Kama swala,kufunga(hiyari ya lazima) na Kuna ibada za lazima,kula,kulala,kuhema/pumua...ndiyo maana Qur'an inasema mtatuabudu mtake msitake,anapata faida gani..Hilo anajua yeye,Qur'an inasema hii dhimma ya usimamili wa walimwengu(ukhalifa) ambayo binaadam aliikubali,wakipewa viumbe wote wakakataa lakini binaadam akaikubali
Ok, Niliuliza kwanini tumeumbwa ukasema ili tuabudu, nikauliza ibada ni Nini/Ina faida gani...Hapa umenijibu dhima/aina za ibada...nimeona umeweka dhima 3.
1.kuswali,kufunga,kuhiji nk.
2.Kula,kulala,kupumua nk.
3.Usimamizi wa Dunia.

Hapa ni sawa na mtu aulize kazi ya gari ni Nini wewe useme ni kuwaka,kuzungusha matairi,kuwasha taa,kupiga honi kunywa mafuta na kuwasha feni.

Unaposema binadamu tumeumbwa ili tupumue/tule ni sawa na kusema gari limeundwa ili linywe mafuta.

Mimi nishajua tayari kuwa gari linakunywa mafuta na kupiga honi na kuzungusha matairi (Binadamu anasali, anafunga,anakula,analala,anapumua,anasimamia Dunia)..Ninachotaka kujua ni kwanini gari linafanya yote hayo??,kwanini limetengenezwa??

Swali Nililouliza ni hivi: Je, binadamu tunazaliwa, tunapumua kuishi, tunasali,tunasimamia Dunia,tunakula na kulala na tunakufa....ili iweje?

Mungu alituumba tufanye yote hayo ili yeye apate faida Gani??

Na hiyo faida tukiijua inaweza(labda) kutupa mwanga wa kwanini huyo Mungu yupo.
 
Tatizo unataka majibu yako na siyo Mambo yalivyo..inaelekea hujanielewa..faida nimesema anajua yeye,ni Kama wewe na mwanao,utataka akuheshimu,unapata faida gani akikuheshimu!?..unaweza kutuonesha faida ya mwanao kukuheshimu!?
 
Kuheshimiwa Kuna faida nyingi sana...Tena sio Kwa mwanangu TU, natamani niheshimiwe na kila mtu. Kuheshimiwa Kuna faida nyingi ila faida kuu, ni kuwa ukiheshimiwa huwezi kufanyiwa mambo mabaya kama
Kutukanwa,Kuibiwa,Kupigwa,kudharauliwa,Kutengwa,nk. Nk.
Kumbuka sisi binadamu ni social primates ..yani tunaishi Kwa kutegemeana sana.

Turudi Kwa Mungu, yeye anatutegemea sisi? Jibu ni nadhani utasema ni Hapana.
Na kama ukisema ndiyo, Bado swali litabaki kuwa "Je sisi binadamu na Mungu tunaotegemeana, tupo Ulimwenguni Kwa Nini?"

Sasa sidhani utajibu hiyo ndio.

Tuendelee...Kama hapana Mungu hatutegemei...Sasa sisi ametuumba wa Nini??

Mimi binadamu sitegemei Simu ili niishi, lakini nimeunda simu inayowaka,inayotumia chaji,inayotachi(kama binadamu anavyokula na kusali) ili niitumie Kwa faida zangu binafsi kama Kuwasiliana,Kutunza kumbukumbu nk.
Kama simu Haina hizo faida siwezi kuinunua/kuiunda.

Sasa Mungu aliyetuumba sisi wanadamu na hatutegemei, Je ni kwanini alituumba? Tuna faida Gani kwake?

Na most importantly, Je hiyo faida tunayompatia Ina uhusiano wowote na Sababu ya yeye mwenyewe kuwepo???
 
Mungu yupo ili kusimamia wanadamu wakae kwenye mstari, ni kama wazazi wanavyosimamia watoto wao wasiharibike.
Kwahyo unachoniambia ni kwamba bila binadamu kuwepo duniani Mungu asingekuwepo...Maana angekosa binadamu wa kuwasimaia...Hivyo kusingekiwa na haja ya Mungu kuwepo?

Kama kazi yake kuu ni kutusimamia Wanadamu, kama ilivyo kazi ya madaktari ni kutibu wagonjwa, kusingekuwa na magonjwa kungekuwa na madaktari??
Kusingekuwa na Wanadamu wa kusimamiwa kusingekuwa na Mungu?
 
Mungu alikuwepo kabla ya uwepo wa wanadamu.
 
Back
Top Bottom