Ujana ule na mwingine, uajuza uulete kwa nani?Na wakishapata jeuri hayo maneno yake sasa. Mara oo..kwenda zako kikongwe wewe!! Mara ooh..acha nikatanue na vijana wenzangu we mzee nakupeleka wapi!!!
Eclat is an old French word meaning brilliance of success or reputation- the meaning of the whole name is Anga Angavu
I'm reflecting Anga Angavu.
Kwa culture ya Kiafrika hii haijakaa sawa, unless huyo mwanamke awe na figure yenye kuficha umri na awe tayari kudanganya hivyo.
lakini yote hayo ya nini hadi ukaoe mwanamke mwenye umri mkubwa zaidi yako, maana nijuavyo mimi mtoto wa kike hukomaa/hupevuka mapema zaidi kuliko mtoto wa kiume na hivyo kuanza kujihusisha vile vile na mambo makubwa kama mapenzi nk, ili hali huyu wa kiume wa umri sawa akiwa bado, sasa inapokuja swala la kutaka kuoa mke anayekuzidi umri tena mkubwa kama 10 yrs, kama ambavyo nimeona kwenye mifano huyo sasa mke ama mama ?
Ni kweli unaweza kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke anayekuzidi umri usiwe mkubwa, lakini swala la kuishi kama mume na mke ni haipendezi hata kidogo japo inatokea. N a mara nyingi mahusiano ya watu hawa basi walau mmoja wao hasa mwanamke awe mtu huru mfano, mjane, ama hakuwahi kuolewa nk.
Lisemwalo lipo vipi dada Sky Eclat, kuna watu wanakuwekea kikwazo sehemu kisa umri ama mwananao anataka kukuletea mukwe anayekuzidi, ila Kongosho anasema hawezi kulea mtoto then aleta mkwe/mkamwana wa kuamkiwa, kazi kwelikweli.
Hapo hakuna cha kufahia katika kuoa mwanamke aliyekuzidi umri! Wakati mwingine hutakiwi hata kuoa mnayelingana umri. Sababu kubwa niionayo mimi ni ukweli kwamba katika mazingira yetu ya kiafrika mwanamke kuwa mwanamke kunaambatana na majukumu mengi mazito (baadhi ya asili kama kubeba mimba na kuzaa) pamoja na mengine ya kiutamaduni/ya kimaisha.
Hivyo kwa asili binadamu yeyote kadiri umri unavyokuwa mkubwa huonekana ni mzee, ukiongeza majuku kama hayo itakuwaje? sasa
Simkatazi ila wakaishi huko Unyanyembe waniache mie niishi huku Daslama
Mambo ya wao kuja kunitembelea sitaki, kisa cha kuwa naamka asubuhi na kusema "Shikamoo mkawana" siyataki kwa kweli. Afu ukute kaoa kizee kimepinda na mapenzi yake ya kisasa wanashikana shikana pale siting rum, no way.
In case wakizaa, wananitumia wajukuu waje kunitembelea.
Kuna vitu vingine vizuri tu havijaandikwa kwenye makaratasi kama sheria ila mioyoni vimeandikwa, hata wahusika wenyewe huwa hawoko huru hata kidogo, so hata usipowafukuza wenyewe tu watajifukuza na kutokomea wanapojua wenyewe mbali na jamii yao.
Inaelekea katika culture za Kiafrika wazazi wana say kubwa katika maamuzi ya vijana wao, tatizo hawa vijana wenyewe wanapenda kuwashobokea waliowazidi umri, na wakati wanakuja wanakwambia 'age is just a number'. Ukweli ukifika, baba akija kumsalimia anamkaribisha kwa rafiki yake ambae hajaoa au anamke 'anaekubalika', baada ya muda unagundua kuwa ulikuwa unalea na kufunga nappy wakati akisubiri akue akaoe!
Inamaana kuoa mke aliyekuzidi umri jamii itakunyanyapaa?
Sio wazazi tu, bali hata wahusika wenyewe lazima mmoja wao ama wote huwa hayuko huru, unaweza kukuta hayo mahusiano yalianza kwa sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wa mmoja wapo, mfano sababu za kiuchumi, na mara nyingi kwa mwanaume kuwa na uchumi mdogo nk, na ndani ya mapenzi yanakolea anaishia kuahidi each and every thing.
Sio kweli kwamba age is just a number kama wanavyosema ila hayo ni maneno tu ili mtu apate kile anachokitaka kwa muda huo, sema ndio hivyo tena on the way anaweza kukolea na kusahau kila kitu, lakini hakika moyoni nafsi daima huwa inaendelea kumsumbua juu ya hayo mahusiano aliyonayo na mwenzake, na hata kwa upande wa mwanamke pia, sema mapenzi bhana yakisha kolea huwezi kuyapa definition sahihi.
Sio jamii kukunyanyapaa tu, bali hata ninyi wenyewe mnajinyanyapaa kwa kujitenga na jamii hasa pale age different inapokuwa kubwa sana kiasi cha kila mtu kuitambua hadi mtoto mdogo, hakika hata wahusika hawawezi kuwa huru hata kutambulishana kwa uwazi kwenye jamii zetu.