Rock City
JF-Expert Member
- Feb 11, 2012
- 1,266
- 505
KASI YA MSAFARA WA RAIS:
Sababu kubwa duniani kwa viongozi wakuu wa nchi huwa ni USALAMA. Kwa nchi zetu hizi za dunia ya tatu, misafara inakuwa na kasi zaidi shauri hatuna teknolojia nzuri katika usalama popote viongozi wakuu wapitapo.
Zipo barabara ambazo upo ulinzi toshelezi na baadhi ya nyakati hukuti misafara mikali, waila kiujumla wa nchi yetu lazima misafara iwe na kasi kuepusha jaribio lolote kujiri kwa kiongozi mkuu wa nchi.
Ukiwa Kampala ndio utashangaa ukiona msafara wa M7, pale ipo gari maalum ya kurusha makombora katika msafara wa Rais.
Kwa njia zetu na miundombinu iliyopo, msafara wa Rais au kiongozi yeyote mkuu wa nchi ukivamiwa, ni taabu sana kuokoa (shauri ya miundombinu). Ndio maana njia zote apitazo kiongozi mkuu wa nchi hutanda wanausalama wengi (wanaoonekana dhahiri na wasioonekana kwa sare zao).
Japo awapo Rais popote vipo vyombo maalum vinavyoonyesha usalama na vihatarishi vyake kuzunguka eneo hilo au eneo analotrajia kwenda, bado yapasa kuwa na kasi ya ulinzi kwa mkulu ikiwemo kasi ya misafara.
Wenzetu America na Europe, zipo barabara maalum kutumiwa na viongozi na mara nyingi viongozi wakuu hutumia helikopta.