Kwanini Mozambique tunaiita Msumbiji?

Kwanini Mozambique tunaiita Msumbiji?

Young african = YANGA

Sunderland = SIMBA

Mzizima = DAR-ES-SALAAM

Idodomya = DODOMA

Buba = UKIMWI
 
Ongeza:
Portugal = Ureno
Congo = Zaire
Britain = Uingereza
Netherlands = Uholanzi

1.Portugal nafikiri lilikuwa derived kutoka kwenye neno "REINO do Portugal" ( Kingdom of portugal)
2.Congo nafikiri utakuwa umeghafilika Congo kwa Kiswahili ni Kongo, Zaire lilikuwa ni jina la hii nchi ambayo sasa ni DRC
3. Britain sijui
4. Uholanzi nafikiri ipo wazi ilitokana na "Holland"
 
Young african = YANGA

Sunderland = SIMBA

Mzizima = DAR-ES-SALAAM

Idodomya = DODOMA

Buba = UKIMWI


Mzizima to Dar es salaam na Sunderland to Simba si ni mabadiliko ya jina tu hayo? au sijakuelewa? yaani hiyo iliyokuwa ikiitwa mzizima ilibadilishwa na kuwa Dar es salaam hali kadhalika Sunderland kuwa Simba.

Hilo la mwisho ndiyo nalisikia leo!
 
na kwanini hiyo Portugal tunaiita ureno?


Kila kitu kipo unapaswa tu kusoma, na kama ukisoma wala huwezi kuuliza swali la kipuuzi na kijinga kama hilo ngoja basi nikusadie ,, Jina La Kiswahili la Ureno limetokana na neno la Kireno O reino linalomaanisha Ufalme, Wapelelezi Wareno kama akina Vaso Dagama walijitambulisha kama wawakilishi wa Reino de Portugal (Ufalme wa Ureno)''

Ureno - Wikipedia, kamusi elezo huru
 
Niliwahi kuwa Mozambique kule kuna watu walishangaa nilipowaambia kuwa nchi yao tunaiita Msumbiji japo kuna wamakonde wa Msumbiji wale wa mpakani na Tanzania wanalijua jina hili ila majority hawalijui wao wanajua Mozambique.

Sasa hili jina Msumbiji lilitoka wapi?

Misri - Egypty

Marekani - USA

yalitoka wapi?

Unaweza ukanijib ni kwa nini Petro tunamwita Peter (Pita), Raheli tunamwita Rachel (Recho),...nk?
 
Niliwahi kuwa Mozambique kule kuna watu walishangaa nilipowaambia kuwa nchi yao tunaiita Msumbiji japo kuna wamakonde wa Msumbiji wale wa mpakani na Tanzania wanalijua jina hili ila majority hawalijui wao wanajua Mozambique.

Sasa hili jina Msumbiji lilitoka wapi?

Misri - Egypty

Marekani - USA

yalitoka wapi?
hapo USA ni rahisi
 
Ama kweli uwezo wa watanzania kufikiri uko chini mno mno! Hujui kila lugha ina maneno yake? Ungeuliza basi na kwanini oil inaitwa mafuta au mountain unaitwa mlima au a human anaitwa mtu! Huu ni upuuzi uliopindukia!

kwahiyo mkuu egypt kwa kiswahili ni misri?..kama jibu ni ndiyo basi nitakubali kuwa niko slow more
 
Europa-ulaya,italiano-roma,Pope-papa,jesus-jeisut-yesu,science-sayansi.
 
Hizo mbwembwe tu za kiswahili za kujiongezea misamiati isiyo na mantiki. mi kwa mtazamo wangu kama kitu si chako asilia ama hujakiumba ama kukitengeneza wewe ni bora tu ukubali lile jina ulilotambulishwa na kama ni gumu kwa matamshi ya lugha yako basi rahisisha silabi ili litamkike na si kujitungia jina jipya hapo unaturudisha zero. hebu imagine leo unafundisha types of computer. unasema kuna aina mbili za mashine dadavuzi za kielektroniki ambazo ni dadavuzi meza na dadavuzi mpakato. thats eeeewww!!
 
Misri inatokana na jina lake halisi kwa kiarabu inaitwa MASR.
Msumbiji inatokana na wabantu kushindwa pronounciation ya neno mozambique wakarahisisha Mouzambij(kunja mdomo kama unataka kupiga mluzi) badae Msumbiji.
Nedherland ndio holland sisi tunaita Uholanzi kwaajili ya ile Holand.
 
Misri inatokana na jina lake halisi kwa kiarabu inaitwa MASR.
Msumbiji inatokana na wabantu kushindwa pronounciation ya neno mozambique wakarahisisha Mouzambij(kunja mdomo kama unataka kupiga mluzi) badae Msumbiji.
Nedherland ndio holland sisi tunaita Uholanzi kwaajili ya ile Holand.

Haya ni maoni yako.
 
Back
Top Bottom