Kwanini MO Dewji anataka kufunga kiwanda chake cha chai Nchini Tanzania? Bashe amgomea!

Nchi nyingine Viwanda vikisuasua Serikali huingilia kati kuviokoa ili kuokoa Ajira za Wananchi wake.

Shout out to Bashe huyu Jamaa namkubali sana.
 

MeTL Group ina mashamba matatu ya chai katika mikoa miwili tofauti yenye hekta 2,350 za chai iliyopandwa na hekta 1,200 chini ya kilimo cha mkataba kwa wakulima wadogo.

Asilimia 95 ya chai inayozalishwa inauzwa nje ya nchi moja kwa moja au kupitia Mnada wa Mombasa katika nchi jirani ya Kenya, na iliyobaki huuzwa kwa wachanganyaji wa ndani.

Viwanda vipya 3 vya chai vyenye laini 5 za mashine za CTC na laini 1 ya mashine ya chai ya asili yenye uwezo wa kusindika wa kilo 250,000 za majani mabichi kwa siku. Viwanda hivyo ni: Mlima wa Arc na Dindira wilayani Korogwe na Chivanjee wilayani Rungwe. Uzalishaji wa chai ya ubora wa hali ya juu kutoka kwa majani mabichi yaliyovunwa kama inavyopendelewa na wachanganyaji na wapakiaji wengi wakuu kote ulimwenguni wanywaji chai katika viwanda vyetu vitatu, hapo juu.

Chai inayozalishwa katika viwanda hivi hupandwa kwenye udongo wenye madini mengi kwenye mwinuko. Mvua za misimu miwili kwa mwaka hunyesha kwa kipindi cha karibia miezi yote na kuwezesha uzalishaji wa majani mabichi mwaka mzima katika mashamba yetu ya chai.

Zahanati za Kikundi za matibabu zina wafanyikazi wa matibabu waliofunzwa, ambao hutoa huduma ya afya kwa familia za wafanyikazi na jamii za jirani, ambazo zinaishi katika maeneo ya mbali. Mpango wa Mama na Mtoto ni msingi wa utunzaji wa afya ya familia.

Mashamba ya chai huwapa wanawake katika jamii jirani vyanzo salama, visivyobagua, vya mara kwa mara na endelevu vya mapato, pamoja na vituo vya kulelea watoto mchana na shule za msingi kwa watoto wao.

More info :
Tanzania’s largest home-grown company, with a presence in 11 countries in Africa, such as Uganda, Ethiopia Kenya, Rwanda, Burundi, Zambia, Mozambique, Malawi, DR Congo and Tanzania. LG Room Air Conditioners (RAC) External Training – MeTL Group


More info on Tanzanian tea :


View: https://m.youtube.com/watch?v=7Cq1NlwdwjA
 
Unambembeleza mtu wakati ameshahamia U.A.E. Ninashangaa serikali inahangaika na waarabu na kukopa nje wakati kuna watanzania kibao wanauwezo wa kuwekeza. Kipi bora kumpa mtanzania ambaye anaishi hapa nchni au kumpa mtu wa nje. Tanzania tuna matajiri kibao ambao hata sio maarufu kuanzia Iringa,Niombe, Kahama, Mbeya, Kilimanjaro na Arusha. Dola haipatikani kwa sababu nchi imeshikiliwa na watu wasio watanzania. Na cha kushangaza wenye mamlaka hawataki kuwapa fursa watanzania.
 
Hapo ni dili inachezwa mkuu
Inawezekana ikawa dili inachezwa, inawezekana isiwe dili.

Ni muhimu kuhakiki na kuandika vitu vyenye ushahidi ili kuepuka speculations zisizo na ushahidi wala uthibitisho. Hizi zipo nyingi sana.

Just because Mo ni mtu wa deal na kashafanya deal huko nyuma, hilo halimaanishi kila anachofanya ni deal.
 
Yes. Morogoro kuna kiwanda Mweshimiwa Rais Aliongea na Wamiliki wake wakarudi na kukifunguwa hicho kiwanda na mpaka sasa kipo kinafanya uzalishaji.
Kuna tofauti kati ya mtu kulazimishwa asifunge kiwanda na serikali kumuomba mtu asifunge kiwanda, wakafanya mazungumzo kiwanda kisifungwe.

Tanzania tofauti hii inaeleweka?
 
MO angeuza tu kiwanda kama labda hapati faida. Hana haja ya kukifunga coz economically wananchi watauza wapi chai yao?
Kwani lazima chai anunue Mo?

Mo akisema anataka kujikita kwenye biashara ya madini, biashara ya chai haina faida kubwa, mtamlazimisha anunue chai wakati hataki?
 
Wewe unajua unachokiongelea mpaka unajua mashine za CTC yaani CURL TEAR & CUT.
Hiki Cha mlima wa Arc ndio Ambangulu ambacho nacho Kiko Korogwe au ni Balangai wilayani Lushoto?
Thanks.
 
Kuna tofauti kati ya mtu kulazimishwa asifunge kiwanda na serikali kumuomba mtu asifunge kiwanda, wakafanya mazungumzo kiwanda kisifungwe.

Tanzania tofauti hii inaeleweka?
Serikali aiwezi lazimisha Mtu ! Ni lazima kuwe na mazungumzo ya pande zotr husika based on win win Sitaution.Kwa hiyo MO atatoa Sababu na Serikali ikazisikiliza na kuja na majibu.Then The Govwrnment can Give MO an Offer Which He cant refuse😁
 
Wafanyabiashara mara zote wanataka kuoperate kwa faida tu.

Hawataki kushare profit kwa namna yeyote ile.
 

Hakuna mwekezaji anaeogopa kuja Tanzania kwa kauli za waziri. Mwekezaji wa maana anajijuza sheria na sera za biashara wakati anafikiria kuwekeza, na anafunga mikataba. Tumekuwa wahanga wa kudumu wa mikataba, na mpaka juzi kuna kampuni ya gesi imeibembeleza Tanzania ianze mradi haraka maana inanusa harufu ya ulaji kwenye machimbo au mahakamani.

Hatubembelezi wakekezaji, na hatupaswi, not least the Dewji cabal.

Kampuni hii haiwezi kufanya maamuzi kivyakevyake, ina wiwa, ina deni na taifa. Everything from conditioned grants of sisal plantations in Tanga, MUTEX apparel factory in Lake Zone, tea industry in Mbeya and Iringa, and massive swathes of real estate in Lindi, which all belonged to the state, and were used as collateral to secure critical loans to erect the Dewji Conglomerate, this company owes the state. And yes, they breached all the conditions attached to the state assets privation sweetheart deals.

They simply can not make unilateral decisions about the future of the company. Dewji and his son did not singlehandedly build this business behemoth. The state is going to have a say as well.
 
Nchi nyingine Viwanda vikisuasua Serikali huingilia kati kuviokoa ili kuokoa Ajira za Wananchi wake.

Shout out to Bashe huyu Jamaa namkubali sana.
Kwamba Viwanda vya Private visipopata faida Serikali inaingilia kuviokoa kwa kutumia pesa ya mlipa Kodi vikipata faida mlipa Kodi kivyake....!!

Na hilo unaona ni sustainable ? Kwanini from day one hivi viwanda taasisi ambazo ni nguzo ya Taifa na UMMA serikali isiwe na kiwanda chao na Private pia vya kwao wote wapambane kwenye Soko..... ?

Na kama hailipi kwanini tusifanye vitu ambavyo vinalipa kulingana na advantages tulizonazo.... (Na kwanini isilipe iwapo tunalima Chai na wanywaji wa Chai) ?

It is the maxim of a every prudent master of a family, never to attempt to make at home what it will cost him more to make than to buy. The taylor does not attempt to make his own shoes, but buys them of the shoemaker. The shoemaker does not attempt to make his own cloths, but employs a tailor.
 
Serikali aiwezi lazimisha Mtu ! Ni lazima kuwe na mazungumzo ya pande zotr husika based on win win Sitaution.Kwa hiyo MO atatoa Sababu na Serikali ikazisikiliza na kuja na majibu.Then The Govwrnment can Give MO an Offer Which He cant refuse😁
Serikali kuanza ku negotiate na Mo tayari inaonesha uchumi mbovu.

Katika uchumi mzuri ilitakiwa Mo hata kama hataki kufanya biashara, kabla hajaamua kufunga kuwe na wafanyabiashara kibao wanaomsumbua wakitaka kununua biashara yake.

Mo angeweza kuuza biashara watu wengine waendelee na uzalishaji, hata kama yeye hataki kufanya biashara.

Sasa hivi serikali kuanza kumbembeleza Mo asifunge biashara ni kama vile hakuna mtu mwingine yeyote anayeitaka biashara hiyo.
 
MO angeuza tu kiwanda kama labda hapati faida. Hana haja ya kukifunga coz economically wananchi watauza wapi chai yao?
Haya mambo ya kuuza Chai kuna Ukiritimba wa hali ya Juu..., Jaribu ku-export chai utasikia utitiri wa vibali yaani kuna Bodi ya Chai na yenyewe lazima uwasiliane nao ni balaa bin balaa katika hii songombingo yote mkulima sio mfaidika....., kwahio hata hio Chai akiuza Bongo ni kwa bei ya kutupa..., akitaka apeleke nje atapewa utitiri wa vibali itabidi ashindwe kabla hajaanza

Cheki hapo chini steps 38
 
Kwamba Viwanda vya Private visipopata faida Serikali inaingilia kuviokoa kwa kutumia pesa ya mlipa Kodi vikipata faida m
Sio Financial tu Serikali inaweza kuvipunguzia Ushindani kwa kuvilinda na Bidhaa zilizoruzukiwa kutokea Nje kwa mfano Chai kutoka Kenya na Uganda inayoingia kiholela kwa njia za Panya kuongeza Kodi kwenye Chai inayotoka nje nk.
 
Kwa hiyo mtu anaweza kulazimishwa kuendesha viwanda hata kama yeye anataka kufunga viwanda vyake?
Sababu ni ajira alizozitengeneza lakini pia mapato Kwa maana ya Kodi.
Hata hivyo inaweza kuwa ni sindicate ya kuongeza bei ya bidhaa kwa visingizio vya mwenye kiwanda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…