Kwanini mnakubali kuoa/kuolewa na wasiowapenda?

Beesmom

JF-Expert Member
May 30, 2016
17,221
28,666
Hivi siku ile unamwoa huyo mwanamke ulijua kabisa kuwa hakupendi ila ukamwoa hivyohiyvo? Kwa sababu zako zipi sijui?

Mfano kwa mwanamke, wengi huingia hawajampenda mwanaume ila sababu zake ni Kuogopa kuchachia home, kuolewa kama mashost zake walio ndoani, kufuata Mali za mwanaume na wengine Ili tu akapate watoto ndani ya ndoa nk.

Mnakaa mnalalamika hapa Wanawake wabinafsi, wachoyo ndugu zangu, tatizo lilianzia kwako. Kuforce mapenzi, kuoa asiyekupenda kwa sababu zako binafsi. MWANAMKE ASIPOKUPENDA USITEGEMEE KUSHIRIKIANA NAWE KWA CHOCHOTE NDANI, Never

Zaidi ataishia kukutesa tu(Swalha&Said) mwisho kuchinjana Kwa usaliti. Pendaneni kwanza tafadhali
 
Ulichosema ni kweli wanawake wengi wanaingia kwenye ndoa kwa sababu
1. Wamechoka kukaa nyumbani
2. Kuiga mkumbo wa wenzao waliolewa
3. Kupata mtu wa kubeba majukumu ya mzazi wake
4. Wengi wao huwa awajui wajibu wao ni nini kwenye ndoa.

Alitengeneza mfumo wa ndoa KILA mmoja alimpa wajibu na mipaka yake isiyofaa kuingiliwa na mwingine Ili kuzuia mikwaruzano.
 
Hivi siku Ile unamwoa huyo mwanamke ulijua kabisa kuwa hakupendi ila ukamwoa IVoivo? Kwa sababu zako zipi Sijui?😳🙌
Mfano Kwa mwanamke wengi huingia hawajampenda mwanaume ila sababu zake ni Kuogopa kuchachia home,kuolewa kama mashost zake walio ndoani,kufuata Mali za mwanaume na wengine Ili tu akapate watoto ndani ya ndoa nk..
Mnakaa mnalalamika hapa Wanawake wabinafsi,wachoyo🙄ndugu zangu, tatizo lilianzia kwako...kuforce mapenzi,kuoa asiyekupenda Kwa sababu zako binafsi...MWANAMKE ASIPOKUPENDA USITEGEMEE KUSHIRIKIANA NAWE KWA CHOCHOTE NDANI,Never ...zaidi ataishia kukutesa tu(Swalha&Said) mwisho kuchinjana Kwa usaliti.Pendaneni kwanza tafadhali
Tatizo sio kwamba wanaume tunalazimisha...semeni kuwa wanawake mnaangalia maisha na sio kiwa mna upendo wa kweli.
 
Tatizo sio kwamba wanaume tunalazimisha...semeni kuwa wanawake mnaangalia maisha na sio kiwa mna upendo wa kweli.
Je wewe unakuwa hujui kuwa huyu hanipendi ila ana pretend?
 
Vijana wa kike na kiume kulazimisha mapenzi au mahusiano ni moja ya alama za kutojiamini, kutojithamini, kutojitambua na kuwa na uwezo mdogo wa akili na ukomavu......

Kwa lugha nyepesi ni kuwa mtu huyo ni mlemavu wa fikra na hisia na ameshindwa kujidhibiti msukumo wa hisia zake ili kuwiana na uwezo wa akili yake kufanya maamuzi.......

Watu kama hao Wana madhara makubwa na ni hatari kuishi katika jamii ya watu WALIOSTAARABIKA......

Makundi hayo ya watu ndio huzaa madikteta kama wakibahatika kuwa viongozi.....ndio huzaa mahusiano yanayoendeshwa kikatili.....na ndio hao hao wanaoua wapenzi wao......

Mwanadamu anaposhindwa kujidhibiti anakuwa hana tofauti na wanyama wa mwituni......



Ukiweka hisia pembeni dalili za mwanamke asiyekupenda zipo kwani mwanadamu kamwe hawezi kuongopea nafsi yake na ndipo unapozaliwa unafiki.....
 
Back
Top Bottom