Kwanini Mke wa pili huwa mkorofi?

Kwanini Mke wa pili huwa mkorofi?

NIMPENDENANI

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2014
Posts
6,114
Reaction score
5,398
Hi MMU,
Nina Shogangu mumewe ameoa mke wa pili lakini yule mdada ni mkorofi utadhani yeye ndio mke wa kwanza, wakati mke wa kwanza ndio alokula dhiki na yule mume sasaivi mambo safi kiasi mume ndio kaongeza mke wa pili.

Wake jamani mnapoingia kwenye ndoa kama mke wa pili au wa 3 hebu muheshimu mwenzio, ujue na yeye ana moyo na sio rahisi kama mnavyodhania.

Na wanaume mkiongeza wake ebu msimsugue roho yule wa mwanzo ni mama wa watoto wako. Mtetee inapobidi na mpe priority kama mke wa kwanza sio kila kitu iwe kosa lake tuu.

Inshallah Mwenyezi Mungu awape Subra manake si mtihani mdogo, naona huruma mtu mumewe akioa. Mwenyezi Mungu aninusuru manake huyu wangu akioa sijui itakuwaje.
 
Mume anatakiwa kuwa muadilifu anapooa mke wa pili, asimpendelee sana mke wa kwanza kisa ametoka nae mbali huyu wa pili atajisikia vibaya atakapogundua. Kama mwanaume huna uwezo na uadilifu baki na mmoja
Still lakini wa Awali ni awali heshima yake kama mke mkubwa apewe...
 
Mke wa pili hajui uchungu wa mume kama mke wa kwanza. Na pia mara nyingi ni katika kutaka kumpindua wa kwanza..
Hapo ndio wanaponiacha hoi mie,mwenzio amemtunza huyo mume akavumilia shidaaa mpaka mambo yakawa sawa baada ya kuingia kwa adabu ndio unajifanya weye ndio mwanamke mwenzio Taka taka,umkute na mume nae ameshawekwa katikati ya miguu ndio dunia utaiona chungu...
 
Kwanza hakuna mwanaume timamu anayeweza kuoa mke wa pili pasipo sababu ya msingi. Pili: Mwanamke mdogo (mke) wa pili kuwa mkorofi kwa mke mkubwa chanzo ni madhaifu ya mwanaume (mme). Tatu: Namna unvyomheshimu mke wako mkubwa ndivyo mke mdogo atakavyomheshimu na atamdharau mke mkubwa (ukorofi) kwa namna wewe mme unavyomdharau mke wako mkubwa.
 
Back
Top Bottom