Kwanini mikutano ya CHADEMA kwa sasa haina MVUTO?

Kwanini mikutano ya CHADEMA kwa sasa haina MVUTO?

heshima mbele wana bodi.

Nitajikita katika mikoa miwili ambayo nimeishi kwa muda sasa yaani mikoa ya mbeya , iringa , dar na mwanza.

Hapo nyuma mikutano ya chadema ilikuwa na mvuto na hamasa kubwa sana, maandamo na mikutano yalivuta hisia za watu wengi na mahudhurio yalikuwa makubwa sana, kuanzia watoto, vijana , kinamama na hata wazee.

Jambo linalonisukuma kuanzisha uzi huu ni kuuliza kwa nini mahudhurio yamepungua sana, kwa nini mvuto wa maandamo na mikutano ya chadema umepungua kwa kasi sana, nini chanzo cha yote hayo, kwa nini wananchi walewale waliokuwa wakijitokeza kwa wingi kwenye mikutano ya chadema sasa hivi hawajitokezi tena.

Je wananchi :-

1. Wamepoteza imani na chadema?
2. Wamekata tamaa ya vuguvugu la mabadiliko?
3. Wanamaisha duni na sasa wameamua kuachana na siasa na kujikita katika shughuli za kuwaongezea kipato
4. Wanaelimu ya kutosha ya uraia

naomba kuwasilisha.

wameanza kuuelewa utapeli na ulaghai wa saccos ya kanda.
 
Tatizo huwa ukisikia ngurumo ya Chopa unajificha halafu unapenda kuhadithiwa
 
Kama CDM haina mvuto ni kwa nini hizi takataka zinapigwa kiberiti?

522080_510251082372224_138549568_n.jpg

Hizo si za kutengenezwa tu asiyejua nani
 
kama kwa hii post unalipwa basi, sccm haina watu, kwa hiyo ile ya kinana kuendesha kigari cha watoto ndo mvuto unaoutaka?
 
Heshima mbele wana bodi.

Nitajikita katika mikoa miwili ambayo nimeishi kwa muda sasa yaani mikoa ya Mbeya , Iringa , Dar na Mwanza.

Hapo nyuma mikutano ya CHADEMA ilikuwa na mvuto na hamasa kubwa sana, maandamo na mikutano yalivuta hisia za watu wengi na mahudhurio yalikuwa makubwa sana, kuanzia watoto, vijana , kinamama na hata wazee.

Jambo linalonisukuma kuanzisha uzi huu ni kuuliza kwa nini mahudhurio yamepungua sana, kwa nini mvuto wa maandamo na mikutano ya CHADEMA umepungua kwa kasi sana, nini chanzo cha yote hayo, kwa nini wananchi walewale waliokuwa wakijitokeza kwa wingi kwenye mikutano ya CHADEMA sasa hivi hawajitokezi tena.

Je wananchi :-

1. Wamepoteza imani na CHADEMA?
2. Wamekata tamaa ya vuguvugu la mabadiliko?
3. Wanamaisha duni na sasa wameamua kuachana na siasa na kujikita katika shughuli za kuwaongezea kipato
4. Wanaelimu ya kutosha ya uraia

Naomba kuwasilisha.

dada nafikiri umeamua kujidanganya na kutufahamisha tu kua kuna kipindi wewe huwa unajidanganya na kujidhihaki.unasema mikutano ya chadema haina mvuto? ipi yenye mvuto,ya ccm?maana ilibidi uonyeshe unaifananisha na nini chenye mvuto, au kwako neno mvuto lina maana gani? au unamaanisha mvuto wa mapenzi ya chumbani? hivi chama kisicho na mvuto huwa kinafuatwa na watu kiasi hicho kweli!? usirudie tena kuja na maada za kijinga namna hii,hangaikieni kuwafukuza wale mizigo na kuokoa uhai wa tembo wetu kwanza.msalimie Kinana
 
Back
Top Bottom