Kwanini mazishi ya waliokufa na ndege huko Bukoba yanagharamiwa na Serikali? Wanaokufaga na mabasi?

😂😂😂😂😂Swali ni zuri ila sina jibu sahihi zaidi ya kuotea tu.
MAONI:
Serikali iwe inagharamia mazishi ya kila raia bila kujali amekufaje.Na iingizwe kwenye katiba.
NB:Maombi mengine ni uwendawazimu sana.🤔🤔🤔😂😂😂😂
 
Wadau naomba kujua kwanini waliokufa kwa ajali ya ndege huko Bukoba jana, mazishi yao yanagharamiwa na Serikali. Mbona wanaokufa na treni, mabasi, boti hayagharamiwagi na Serikali?

Mwenye ujuzi atujuze...
Ikitokea majeneza yao hutengenezwa kwa reject wood
 
Hata ajali ya MV ukara mazishi yaligharamikiwa na serikali lakini majeneza yalikua na quality ndogo ukilinganisha na ya leo.

Nikirudi kwenye swali lako: SIASA ni kujua kwenda na upepo
 
Na tena huwa wanatangaza kana kwamba ni kitu kikubwa wanafanya.
Mpaka kulikuwa na salamu za chama CCM
IMG-20221107-WA0052.jpg
 
wamejishtukia namna walivyofeli ila kibongobongo wanasema tuko pamoja.!

ivyo tyu yaani..."kulikuwa hamna namna;tusameheane"
 
Hata ajali ya MV ukara mazishi yaligharamikiwa na serikali lakini majeneza yalikua na quality ndogo ukilinganisha na ya leo.

Nikirudi kwenye swali lako: SIASA ni kujua kwenda na upepo
hapo utasikia wale wa ajali ya ndege kuna walipakodi wengi wazuri,halafu wale Mv Ukara utasikia si walipa kodi wazuri wa serikali,nawaza lakini
 
Wadau naomba kujua kwanini waliokufa kwa ajali ya ndege huko Bukoba jana, mazishi yao yanagharamiwa na Serikali. Mbona wanaokufa na treni, mabasi, boti hayagharamiwagi na Serikali?

Mwenye ujuzi atujuze...
Hiyo ajali imeivua nguo serikali kimataifa kwenye nyanja ya uokozi, hapo wanafunika kombe mwanaharamu apite
 
Back
Top Bottom