Kwanini Marekani ameshindwa kuimaliza Iran haraka?

Mfano wako uliotumua wa Vietnam hiyo nchi imekuwa ya kibepari na kuna uwekezaji wa Wamarekani wenyewe na Wachina wanawekeza kwa wingi. Chanzo cha vita ile ni Marekani kutetea ubepari ambao ndio upo kwa sasa, kwahiyo mwisho wa yote sera ya Marekani ndio imeshinda.

Mimi siungi mkono Marekani kuishambulia Iran, ila kulinganisha failure ya Urusi kwa miaka minne dhidi ya mafanikio ya Marekani ndani ya mwezi ni makosa.
 
Marekani ana military base ngapi ? Na urusi anazo ngapi na utaje location zake.

Acha ushabiki maandazi mkuu..
 
Marekani hawezi pigana na China kwa vita yoyote ile full stop nimefuta mtazamo wangu wa awali juu ya nguvu na uwezo wa Marekani.
Hongera sana...

Ila ukweli haubadiliki kwamba Marekani ndiyo taifa lenye nguvu kijeshi duniani tangu historia ya binadamu ianze. Kiukweli Marekani lina nguvu mno hasahasa kwenye kipimo cha CONVENTIONAL WARFARE. Tatizo linakuja kwamba vita inategemea mambo mengi sana kushinda, siyo tu silaha na uwezo wa kiuchumi. Marekani wakati anavamia Vietnam mwaka 1964 alikuwa na jeshi linalotisha kuliko hili la leo, na bado akashindwa vita. War is a tool of state politics.

Vita inaweza ikapiganwa vizuri lakini siasa za nchi au dunia zikachangia vita kuisha vibaya. Huu mfano ndiyo aliwahi kusema Albert Einstein "You win the war,but lose the peace". Marekani Vietnam aliua watu milioni 4, huku Vietnam ikiua Wamarekani elfu 60. Ukiwa na akili ya Kibabazi na Kidunya unaweza kusema Marekani ndiyo kashinda vita, bila kuangalia madhara ya kisiasa nchini kwake na duniani kote.

Hili ndilo linasababisha vita zitegemee sana PROPAGANDA ili PUBLIC OPINION iwe upande wao. Bahati mbaya Donald Trump na Netanyahu hawakusoma alama za nyakati. Wamarekani wengi hasa MAGA walimchagua Trump kwa ahadi ya kukomesha vita na kutojihusisha kabisa na Middle-East. Ilikuwa ni America First. Sasa MAGA imevurugika, hadi Tucker Carlson na Candace Owens wanamponda Trump, hivi unadhani hii vita ikiendelea hivi na watu wakaanza kuona mfumuko wa bei na maiti za watoto wao, wataelewa chochote hata kama Marekani anaua viongozi wa Iran kila siku ???

Leo hii ukimchukua Mwakinyo akapigana na Wema Sepetu, halafu Mwakinyo akamchapa kweli Wema Sepetu ngumi za kichwa, ila baadaye Wema Sepetu akafanikiwa kumpiga ngumi moja tu ya pua, na Mwakinyo damu zikaanza kutoka, wewe unadhani watu watazingatia ngumi za kichwa alizopigwa Wema Sepetu ??? A Bleeding Nose, is enough to make Mwakinyo flinch and lose the entire fight...
 
Teh teh 😃 😃 nyie wabongo bhana .

Acheni kujidharau kiwango hicho.
 
Marekani hakwenda Vietnam kupeleka Ubepari bali alikwenda kutengeneza koloni akashindwa. Vietnam (Indochina) lilikuwa koloni la Mfaransa na alivyotoka Marekani akataka kwenda yeye ila bahati mbaya kina Stalin walikuwa washamuwahi. Kafika kakuta Wakomunisti wako tokea mwaka 1930 na wamesoma Urusi, huku wengine wakiwa veterans wa WW2.

Pili, Vietnam siyo taifa la Kibepari (A Capitalist Economy) ni taifa la Kikomunisti (A Communist State) ambalo limeruhusu mfumo wa masoko uliodhibitiwa (Controlled Market) kama Uchina. Kilichobadilika Vietnam ni umiliki wa mali tu na masoko. Siasa na Utawala ni uleule tokea 1930 chini ya Comrade Ho Chi Minh.
 
Marekani ana military base ngapi ? Na urusi anazo ngapi na utaje location zake.

Acha ushabiki maandazi mkuu..
Suala la Urusi kutokuwa na military bases za kutosha kuweza kupigana na jirani Ukraine ndio uvivu wenyewe ninaosema hapa. Mbona unaniunga mkono kwa kunipinga mkuu.

Kama Urusi ilijua haina bases za kutosha ingeacha, yanini kuanzisha mwenyewe kurusha ngumi alafu mkipigana unalamika huna nguvu za kutosha. Tangu mwanzo si ungeacha sasa.
 
Jmn kama haupo vizuri kichwan kwenye huu uzi usichangie...mnakula za uso vibaya mno 🤣

Wacheni mihemko ya umarekan wa buza.

MALCOM...Tuendee baba.
Endelea kudanganywa sasa yaani mtu mwenye akili timamu unaweza kukubali kabisa kuwa Iran ameiwin hii vita? Iran leo wanasema Marekani imeua askari wake wadogo kwenye meli ya kijeshi bahari ya hindi hivyo itaenda mahakamani? Aseeee
 
Kweli waliokukashifu wapo sahihi!!
Urusi iliivamia Ukraine October 2026!
Kweli wewe ni kilaza mkuu!!
 
Jmn kama haupo vizuri kichwan kwenye huu uzi usichangie...mnakula za uso vibaya mno 🤣

Wacheni mihemko ya umarekan wa buza.

MALCOM...Tuendee baba.
Kuna hili lifala linaitwa let the caged bird sings ni moja kati ya Mabazazi na Madunya ya humu ndani. Limetoka shimoni baada ya maumivu makali ya moyo, likaharisha ujinga halafu likaenda kuvimbiwa futari ya Kwaresma.

Lenyewe na wenzake wengi humu ndani niliwahi kuwaambia mwaka 2022 kwamba muda ni mwalimu mzuri sana, wekeni akiba ya maneno. Katika wooote ambaye huwa hajawahi kunivunjia heshima kwenye mijadala ni mdogo wangu T14 Armata , atabishana na mimi vikali ila hajawahi kubisha kitu bila walau kuweka hoja. Katika hili namheshimu sana sanaaa.

Mengine sasa hivi yanachungulia yanapita kimyakimya kama mapepo yakitegemea walau CNN watangaze chochote kibaya kilichowakuta Iran ili wakilete hapa, lakini wapiiiiii. Mimi niko nao tu hawaa Weekend yote hiiiii
 
Jmn kama haupo vizuri kichwan kwenye huu uzi usichangie...mnakula za uso vibaya mno 🤣

Wacheni mihemko ya umarekan wa buza.

MALCOM...Tuendee baba.
Hii vita haipaswi kuwa ya kishabiki ukitaka kuona athari zake angalia tangazo la EWURA hata wiki halina just image vita hii iende mpaka one month,hakika nakuambia hakuna rangi tutaacha kuona hapa nchini.

Ndo maana Mleta Uzi amewaita Mabazazi na Madunya kwamba hawaoni kwamba hili ni tatizo kubwa,bali wao ni ushabiki kama wa Simba na Yanga.
 
Marekani ilienda Vietnam kuzuia domino theory na kuisaidia serikali ya South Vietnam chini ya Rais Ngo Dinh Diem. Same way na Marekani ilivyoamini kwenye domino theory ikapeleka majeshi South Korea kuisaidia kupigana na North Korea iliyoungwa mkono na China na USSR.

Hilo la Marekani kutaka kuanzisha ukoloni Vietnam hongera kwa kulijua, hata Wamarekani wenyewe hawalijui.
Kwahiyo na kule South Korea, Marekani ilianzisha ukoloni?
 
Kwa hiyo mkuu Iran na Marekani wangekuwa wanashea mpaka kama ilivyo kwa Urusi na Ukraine makombora na drone za Iran zisingekuwa zinapiga kwenye miji ya Marekani?
Ila ni kweli hatakiwi kulinganisha maana Ukraine ilivamiwa na Urusi peke yake lakini Iran kavamiwa na mataifa mawili.
 
America is not the Universal Munificent Santa Clause....

Joe Biden na Donald Trump wamekuwa na sifa moja inayofanana tofauti na maraisi wengine wa Marekani waliotangulia. Wamejisemea ukweli kwamba Marekani iko Ukraine kwasababu ya rasilimali na Marekani ilitengeneza Israel na inailinda kwasababu ni uwekezaji wao mkubwa....

Sasa ndugu yangu Armata, nikuulize swali kama lengo la Marekani lingekuwa ni kupambana na Ukomunisti, kwanini Marekani huyohuyo alikuwa anawaunga mkono madikteta wa kikomunisti kama Pol-Pot wa Cambodia, au Tito wa Yugoslavia ???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…