Kwanini Mamlaka za Tanzania hadi sasa hazijatangaza kuwa Mama Maria Nyerere ameugua ghafla na kalazwa Uganda?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,554
108,895
Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni leo amelazimika kukatisha Ziara yake alipokuwa akihudhuria Sherehe za Kuwakumbuka Mashujaa wa Kiimani nchini humo ( wenyewe mnaita Hija ) na kukimbia Hospitalini kwenda Kumtembelea Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere ambaye ameugua ghafla. Ikumbukwe kuwa Mama Maria Nyerere yupo nchini humo kwa Mwaliko wa Mheshimiwa Rais Museveni ili nae awe sehemu ya hizi Sherehe.

Nasikitika kwamba wenye Mama yetu ( Watanzania ) hadi hivi sasa hatujajulishwa juu ya hili na ' Mamlaka ' husika nazo zipo Kimya tu. Na mpaka Mheshimiwa Rais wa Uganda ameamua Kukatisha Ziara yake na kuwahi Hospitalini inawezekana Mjane Mama Maria Nyerere labda hali yake si nzuri kiasi hasa ukizingatia ya kwamba kwa muda sasa amekuwa akiuguaugua japo inafanywa Siri na sijui ni kwanini.

Nawasilisha.

Chanzo Taarifa: NTV Uganda.
 
huyo mama wa Makongoro na Madaraka
we anakuhusu nini

Ninachojua ni Mama wa Watanzania wote wenye ' Akili ' timamu na hasa wale wanaoelewa dhana nzima ya ' First Lady ' na ukizingatia huyu ana Historia yake Kubwa na ya ' Kutukuka ' hapa nchini Tanzania, ila Kwako Wewe ' Mpumbavu / Popoma Mwandamizi ' hawezi kuwa na wala huwezi Kuelewa chochote. Kisiasa hata Mama yako Mzazi akiwa ' First Lady ' wa nchi hii basi ' automatically ' katika dhania ya Kisiasa na Kiitifaki atakuwa ni Mama wa Watanzania haijalishi kama ametuzaa au hapana.
 
Shekh msamehe waTZ wengi akili zao wakati huu haziko sawa kabisa namba wamezielewa vyema, Eid Mubarak hii kwa watu woote.
 
Kapigania taifa hili kwa namna yake
Angalieni mataifa ya wenzenu wanavojua kuwaenzi watu walioleta mabadiliko kweny mataifa yao.

Mkuu huyo ' Mpumbavu ' na wengineo wengi watakaojitokeza wakiwa na hizo hizo ' Fikra ' kamwe hawawezi Kuelewa umuhimu wa Mjane Mama Maria Nyerere hasa katika Historia nzima ya nchi hii. Sasa kama Mtu hadi hivi leo akiwa anajiita kabisa Msomi lakini hajui maana au dhana pana ya ' First Lady ' katika nchi huyo akifananishwa na ' Taahira / Mwendawazimu ' atakuwa anaonewa?
 
Shekh msamehe waTZ wengi akili zao wakati huu haziko sawa kabisa namba wamezielewa vyema, Eid Mubarak hii kwa watu woote.

Bahati mbaya sana Mkuu kwa Mimi ' Wapumbavu Waandamizi ' kama hawa huwa sipendi ' Kuwachelewesha ' katika kuwapa ' Dawa / Dozi ' zao Kamili ili ziweze ' Kuwatibu ' vyema ' Akili ' zao ambazo nyingi huwa ni mbovu mbovu na za ' hovyo hovyo ' tupu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom