GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,044
- 119,619
Nimekuwa nikilifuatilia kwa umakini mkubwa sana hili suala la wapi Bomba la Mafuta lipite huku Ndugu zetu Wakenya WAKIJITUTUMUA kama kawaida yao kutaka KUMILIKI kila kitu hapa Afrika ya Mashariki kana kwamba Mwenyezi Mungu aliwabariki wao tu wakati si kweli.
Rais wa Kenya Kenyatta pamoja na team wake wamejitahidi na kwa taarifa nilizonazo zinasema kuwa mpaka jana Jumamosi bado Kenya ilikuwa inaendelea na lobbying kwa Rais wa Uganda Mzee Museveni ili apitishe Bomba hilo kwao na Tanzania tuambulie patupu.
Ila Wakenya na hasa Rais wao Uhuru Kenyatta wamesahau historia ya KUTUKUKA ya Rais Yoweri Kaguta Museveni na nchi yetu hii ya Tanzania. Hakuna ubishi kuwa Rais wa Uganda Mzee Museveni bila jitihada za Tanzania leo hii asingekuwa hapo alipo.
Ukianzia zile harakari zake za kuiokomboa nchi ya Uganda akiwa anatokea huku huku Tanzania na wakati huo huo makazi ya familia yake hasa mkewe Janet na Watoto wao wawili wa kwanza wa Kiume Muhoozi Kainerugaba na wa Kike Natasha Nankuunda ambao waliishi vizuri sana pale Upanga mkabala kabisa na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili huku.
Baada ya Mzee Museveni kumaliza masomo yake UDSM alianza kazi ya kufundisha Chuoni huko Mkoani Kilimanjaro lakini hapo hapo tena akiendeleza harakati zake za kupambana vita ya msituni kuuondoa Uongozi wa Milton Obote akishirikiana na wenzie kama Jemedari Serwanga Lwanga ( R.I.P ), mdogo wake Caleb Akandwabaho ( Salim Salehe ), Kahinda Otafiire, Paul Kagame ( Rais wa Rwanda ), Samson Mande aliyekuwa Ugandan Millitary Attache to Tanzania 1995 - 1998 na wengineo wengi tu ambao kwa msaada wa Tanzania waliweza kufanikisha Wapiganaji wa NRA waliokuwa wakiongozwa na Mzee Museveni kuiteka Uganda na kuwa Watawala mpaka leo japo kuna waliotangulia mbele za haki huku wengine wakitofautiana Kisiasa na Mzee Museveni.
Leo nataka tu niwapashe Wakenya kuwa walikuwa wanapoteza tu muda kufanya USHAWISHI wao kwa Mzee Museveni Rais wa Uganda kwani kwa aina ya Marafiki wa KUFA na KUZIKANA hawa Wafuatao wa Rais Museveni asingeitosa Tanzania yetu hata iweje. Nitawagawa hawa Marafiki wa karibu wa Museveni kwa makundi ili Wakenya mfahamu kuwa mlikuwa ( Wakwere wanasema MNAZOZA ) mnapiga tu soga na kupoteza muda wenu.
MARAFIKI WA KARIBU wa Rais Museveni wa KUFA na KUZIKANA ni:
- Hayati Baba wa Taifa Nyerere na sasa Familia yake nzima.
- Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere Mzee Joseph Butiku.
- Balozi Mstaafu na aliyekuwa Mshauri wa Masuala ya Nje na NYETI Mzee Adam Marwa.
- Hayati Brigadier Hashim Mbita.
- Mkurugenzi Mtendaji wa MKUKI Publishers Mzee Walter Bgoya.
- Aliyekuwa Mbunge wa Karatu Hayati Mzee Patrick Qorro.
- Mkuu wa Majeshi Mstaafu Mzee David Bugozi Musuguri.
- Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ally Hassan Mwinyi.
- Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mzee Benjamin William Mkapa.
- Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mzee Jakaya Mrisho Kikwete.
- Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Joseph Sinde Warioba.
- Balozi Mstaafu wa Tanzania nchini Uganda Mzee Tambwe.
- Naibu Balozi Mstaafu wa Tanzania nchini Uganda Hayati Mzee Mufungo Mujaya.
- Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ )
- Wananchi wote wa Tanzania hasa hasa Wakazi wa Dar es salaam, Kilimanjaro na Kagera.
Hata hivyo najua na nikiri pia kuwa zipo sababu nyingi na tena muhimu pengine hata nje ya hii au hizi ambazo pia zimewezeshesha Uganda kukubali kupitisha Bomba lake nchini Tanzania badala ya Kenya lakini ni ukweli usiopingika kuwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni ana UPENDO WA DHATI na ULIOTUKUKA kwa Nchi ya Tanzania na ANATUHESHIMU pengine hata kuliko Waganda anaowaongoza. Sababu hizo KUU za kihistoria na kirafiki ndizo zimekuwa HUKUMU kwa nchi ya Kenya.
Poleni sana Wakenya ila msihofu FURSA bado zipo nyingi tu tutawashirikisheni na zingine pia ila acheni MAJUNGU na WIVU wenu kwetu Watanzania.
Akhsante Rais Yoweri Kaguta Museveni kwa kuwaonyesha Wakenya kuwa Tanzania ndiyo kila kitu kwako na kwa Waganda wote na usichoke kutupa fursa zingine.