Kwanini kuna Njaa Tanzania kama wakati wa Nyerere? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini kuna Njaa Tanzania kama wakati wa Nyerere?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 5, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 5, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  [​IMG][​IMG][​IMG][​IMG]  Mojawapo ya ukosoaji mkubwa wa wakati wa Nyerere ni kuwa "watu walikufa na njaa" na kuwa tulilazimika "kula yanga" na kupanga mistari kusubiri mgao - the infamous "duka la kaya". Ukiwasikiliza wanaozungumzia hayo ni watu ambao wanaamini kabisa kuwa Tanzania sasa hivi kuna neema ya chakula na hakuna watu wanaohangaika na njaa na ambao bila msaada wa serikali watakufa njaa. Na kama wengine wanakumbuka miaka michache tu iliyopita (wakati wa Kikwete huu huu) kuna watu huko Pwani walikuwa wakiishi kwa kula mizizi, na sehemu nyingine kwa kula matunda pori - Yaani hata siyo Yanga!!

  Tuangalie mifano michache:

  Februari 11 - Zanzibar - 7000 wakabiliwa na upungufu wa chakula:

  7OOO WAKABILIWA NA UPUNGUFU WA CHAKULA MICHEWENI
  Balozi Seif azitaka Kilimo, Fedha kutafuta ufumbuzi haraka


  Na Mwantanga Ame, Pemba


  TATIZO la uhaba wa chakula limejitokeza tena katika wilaya ya Michweni na kusababisha wananchi zaidi ya 7,000 wa maeneo hayo kukumbwa na upungufu mkubwa wa chakula cha mazao.


  Hali hiyo imejitokeza kwa muda wa miezi mitano sasa baada ya eneo kubwa la mashamba ya wakulima kutokuwa na uzalishaji wa chakula cha aina yoyote.

  Juni 2011 - Ngorongoro uhaba wa Chakula


  TARAFA za Ngorongoro, Sale na Loliondo zilizopo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha zinakabiliwa na baa la njaa. Mpaka sasa taarifa zinaonesha kuwa Tarafa ya Ngorongoro inahitaji zaidi ya tani 1500 za mahindi, tarafa ya Sale na Loliondo zinahitaji zaidi ya tani 1000 .
  Kutokana na kilio hicho cha msaada wa chakula, kamati maalumu imelazimika kuundwa ili kukutana na Rais Jakaya Kikwete kumueleza juu ya tatizo hilo. Mkutano huo uliofanyika jana juu ya majadiliano ya upatikanaji wa uhakika wa chakula uliwashirikisha wadau wa maendeleo na jamii inayoishi ndani ya hifadhi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA).
  Akizungumza katika mkutano huo Mbunge wa Jimbo hilo, Saning'o Ole Telele alisema, tatizo la chakula wilayani humo kwa ujumla limesababishwa na ukame mkubwa. "Wananchi wanahitaji chakula kwa sasa kitakacho watosheleza hadi Januari 2012,"alisema Telele.

  Mei 2011 - Serikali yasababisha upungufu mkubwa wa chakula mikoa ya Kaskazini


  MIKOA ya Kanda ya Kaskazini na Kati inakabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula kutokana na Serikali kutotoa vibali vya kununua chakula kwa kampuni mbalimbali.

  Mwenyekiti wa Bodi ya Mazao Mchanganyiko, Kanda ya Kaskazini, Philemoni Mollel alisema licha ya maombi kuwasilishwa Februari mwaka huu kutaka kununua vyakula kutoka kwenye maghala ya Serikali yaliyoko Arusha, Serikali haijatoa vibali.

  Mollel alisema kutokana na urasimu huo, kampuni husika zimekosa mahindi ambayo walikuwa wakiyanunua kutoka kwenye maghala ya Hifadhi ya Chakula ya Taifa (SGR) na kusaga unga kwa ajili ya kuuza.

  Watoto 43,000 wanakufa kila Mwaka TZ kwa Utapiamlo (Malnutrition) 2010

  Utapiamlo
  Je, Tanzania inaweza kupuuzia vifo 43,000 vya watoto
  na upotevu wa Sh bilioni 700 kila mwaka?

  Bagamoyo wapewa msaada wa chakula kukabiliana na njaa


  Serikali imetoa jumla ya tani 372.4 za chakula kwa wilaya ya Bagamoyo ili kuweza kukabiliana na tatizo la Njaa
  Na Anna Nkinda – Maelezo, Bagamoyo - 05/10/2009

  Serikali imetoa jumla ya tani 372.4 za chakula kwa wilaya ya Bagamoyo ili kuweza kukabiliana na tatizo la njaa linaloikabili wilaya hiyo.

  Hayo yamesemwa jana na Mkuu wa wilaya hiyo Magessa Mulongo wakati akieleza hali ya chakula kwa mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja katika wilaya hiyo .

  Mulongo alifafanua kuwa tani 186.2 ziligawiwa bure kwa wananchi na tani 186.2 zilitolewa kwa utaratibu wa kuuza ambapo kilo moja iliuzwa Tshs.50.

  "Vijiji 64 kutoka katika kata 16 zenye jumla ya watu 132,703 wameombewa msaada wa chakula kupitia TASAF kwa mradi wake wa uhakika wa chakula (FOOD Security)", alisema.

  [​IMG]

  Simanjiro wahitaji tani 3000 za chakula- Mei 2011


  Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Khalid Mandia, ameiomba serikali kupeleka zaidi ya tani 3,000 za chakula ili kukabiliana na uhaba mkubwa wa chakula ulioikumba wilaya hiyo.Alisema wilaya hiyo ilipata tani 600 za nafaka wiki iliyopita lakini bado hazikithi haja ya wakazi wa wilaya hiyo ambao wengi wao ni wafugaji.
  Alisema tani hizo zilipelekwa maeneo yanayokabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula, lakini kwa maeneo yenye nafuu kidogo hayakupelekewa. Akizungumza upungufu huo, diwani wa Kata ya Langai, Jackson Sipitek, alisema hali si shwari kutokana na mahindi yaliyolimwa kukauka kwa jua.

  Watu 80,000 Longido wahitaji msaada wa chakula - Januari 2010


  Zaidi ya watu 80,000 wa Wilaya ya Longido, mkoani Arusha, wanahitaji msaada wa haraka wa chakula ili kukabiliana na njaa iliyosababishwa na ukosefu wa mvua kwa miaka miwili mfululizo.
  Wilaya hiyo inahitaji takriban tani 5,770 za chakula kwa wananchi wasiokuwa na chakula.
  Hayo yalisemwa jana wakati wa ziara ya siku mbili na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Aggrey Mwanri.
  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Longido, James ole Millya, zaidi ya tani 6,145 za chakula, ndizo zilizofikishwa na serikali katika wilaya hiyo ambazo zimegawiwa katika kaya tofauti.
  Mkuu huyo wa Wilaya alisema hali ya chakula ni mbaya hasa maeneo ya vijijini na kwamba imesababisha mahudhurio katika shule za msingi kushuka kwa wastani wa asilimia 45 kulingana na utafiti uliofanywa na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) katika vijiji mbalimbali vya wilaya hiyo.

  Lissu - Singida wakabiliwa na Njaa Machi 2011

  Wito huo umetolewa jana na mbunge wa jimbo hilo mhe Tundu Lisu kwenye sherehe
  ya kuwashukuru wananchi wa tarafa ya Mungaa kwa kumchagua kuwashika wadhifa huo
  katika uchaguzi mkuu ulipita.Mhe Lisu amesema kuwa wakati wananchi katika jimbo wanakabiliwa na upungufu
  mkubwa wa chakula, taarifa zilizopo serikali zinaonesha kuwa kwa mkoa wa Singida
  ni wilaya ya Manyoni pekee ndio yenye uhaba wa chakula na inatakiwa kupelekewa
  msaada.
  Kutokana na hali hiyo mbunge huyo amezitaka Serikali za Vijiji katika jimbo lake
  kufanya tathimini haraka kwa kila kaya ili kujua hali halisi ya upungufu wa
  chakula na kupeleka taarifa wilayani kwa ajili ya kuchukua hatua za kuomba
  chakula serikali mapema.


  Watu 372,000 Arusha wakabiliwa na njaa - 2009


  ZAIDI ya watu 372,980 katika vijiji mbalimbali vya mkoa wa Arusha wanakabiliwa na tatizo kubwa la chakula.
  Hali mbaya ya hewa iliyosababisha kukosekana kwa mvua za vuli na masika imetajwa kama ndiyo sababu kubwa ya wananchi hao kukabiliwa na uhaba wa chakula.
  Kutokana na hali hii mkoa wa Arusha unahitaji zaidi ya tani 13, 431 za nafaka kwa ajili ya kuwasaidia waathirika hao.
  Mkuu wa mkoa wa Arusha Isdori Shirima alisema idadi ya watu wanaokabiliwa na upungufu wa chakula mkoani humo ni kubwa ukilinganisha na miaka mingine ya nyuma.

  Dewji asaidia wenye upungufu wa chakula Singida Mjini - Aprili 2011


  MBUNGE wa Jimbo la Singida Mjini (CCM), Mohammed Dewji ametoa msaada wa chakula
  wa zaidi ya tani 100 wenye thamani ya Sh milioni 40 kwa wananchi wanaokabiliwa na upungufu wa chakula katika jimbo hilo.

  Dewji alitoa msaada huo wakati wa ziara ya kukabidhi chakula hicho Jumanne kwenye kata za Mtamaa, Mwankoko, Mandewa na Uhamaka ambako alitoa magunia kadhaa ya mahindi.

  Mbunge huyo alisema kuwa amefikia uamuzi huo, baada ya kupewa taarifa na madiwani wa
  kata hizo kuwa maeneo hayo yanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.

  Mpwapwa watu waishi kwa kula mbogamboga na matunda pori, njaa kali - Januari 2010

  HOFU kubwa imetanda kwa ndugu, jamaa na majirani wa wananchi wanaokabiliwa na njaa kali katika baadhi ya maeneo wilayani Mpwapwa, mkoani Dodoma.
  Hofu hiyo inatokana na kuweko kwa hali mbaya ya upungufu wa chakula, hali inayosababisha baadhi ya familia kuishi kwa kula mbogamboga na matunda ya porini.
  Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima katika baadhi ya maeneo ya wilaya ya Mpwapwa umebaini kuwepo kwa njaa kali hali ambayo kama itaendelea upo uwezekano wa wananchi kupoteza maisha kutokana na kukosa chakula.
  Maeneo mbalimbali yaliyofanyiwa uchunguzi yamebainika kuwa na upungufu mkubwa wa chakula huku hali mbaya zaidi ikiwa katika tarafa za Kibakwe na Mima katika kijiji cha Berege.
  Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, wananchi wa kijiji cha Kibakwe pamoja na viongozi wao walisema hali ni mbaya na baadhi ya watu tayari wameelemewa na kuvimba miguu kutokana na kukosa chakula kwa muda mrefu.

  Watu wapoteza matumaini Isimani Iringa, Njaa!! Mei 2011

  NI balaa hili kwani unapofika katika vijiji mbalimbali vya tarafa ya Isimani wilaya ya Iringa unapokewa na nyuso za watu waliopoteza matumaini na vilio vyao karibu wote ni maombi ya msaada wa chakula kutoka serikalini.
  Ukijikumbusha historia ya maisha katika maeneo hayo hasa wakati kama huu wa mwaka , haikuwa rahisi kuwasikia wananchi wa huko wakilia njaa.

  Hii ni kutokana na ukweli kwamba, huu ndio msimu wa mavuno ya mahindi. Lakini, sasa kilio cha njaa kwa wananchi wengi wa wilaya ya Iringa kimekuwa kawaida! Karibu kila nyumba unayobisha hodi kilio chao kikuu, ni njaa.

  Kwa asili, wananchi wa maeneo hayo ni wakarimu, lakini kwa kipindi hiki ukarimu huo haupo tena kwa sababu kila wakisikia hodi, lazima wapatwe na mawazo jinsi gani wataweza kumhudumia mgeni, kutokana uhaba wa chakula uliopo.

  My Take and Questions:

  a. Yawezekana wale wanaolalamikia kula Yanga au dona wakati wa Mwalimu na kupewa mafuta yale ya misaada kutoka kwa USAID hawajui kinachoendelea nchini, au hawataki kujua. Yawezekana tuliokula Yanga hali haikuwa mbaya kama ilivyo baadhi ya sehemu nchini kwa miaka kadhaa sasa. Yanga oyee!!

  b. Tatizo la njaa ni mojawapo ya matatizo mengine ambayo yanawasumbua Watanzania kama ilivyo nishati lakini ni tatizo ambalo linadhalilisha utu wa mwanadamu kuliko tatizo jingine lolote lile, hata magonjwa hayadhalilishi utu wa mwanadamu kama kufa njaa. Kwanini tatizo hili haliangaliwi kwa ukaribu na uzito wake unaostahili? Kwanini bado kuna watanzania ambao wanahangaikia mlo wa siku moja tu?

  c. Walioshiba yawezekana kweli hawamjui mwenye njaa, mifano mingi ambayo nimeitoa hapa (mingine hata sijaigusa) ingetosha kabisa kutuambia kuwa Tanzania kuna tatizo la njaa, lakini ni wangapi wanaokula na kusaza huko Dar, nyama choma kila jioni, n.k wanajua kinachoendelea sehemu nyingine ya nchi? Je wabunge wetu (niliangalia zile sherehe ambazo Waziri Mkuu aliandaa nyumbani kwake Dodoma na zile za wapinzani katika kupongezana) wanajua kuna tatizo kubwa sana la njaa nchini?

  d. Kama hali ilikuwa mbaya wakati wa Mwalimu na watu wanatukumbushia hivyo, hivi hawa wa leo ambao nimewadokeza ukiwaambia utawala wa Kikwete watu walikuwa wanashiba na kusaza watakuelewa? Wananchi wa Mpwapwa kwa mfano ambao hata unga wa yanga hawakupata na kujikuta wanakula matunda mwitu wanaweza kusema kuwa "hali ilikuwa nzuri" wakati wao?

  Ninachoweza kuona ni kuwa yawezekana pasipo kuangalia jambo kubwa zaidi ambalo lingehitaji kumalizwa "once and for all" ni hiki kitu tunachokiita "usalama wa chakula". Je, Tanzania inaweza kweli kufikia "usalama wa chakula", itakuwaje kama hatuwezi kufikia?

  e. Je mikataba ya hivi karibuni ya kugawa maeneo makubwa ya ardhi nchini kwa ajili ya kilimo cha makampuni makubwa na kutumia GMF (Genetically Modified food) vitatuleta kwenye usalama wa chakula? Mikataba ambayo baadhi ya makampuni yatazalisha chakula nchini kwa AJILI YA nchi zao, yatatusaidia sisi vipi? Je, tukija kujisikia kuwa tunaexport chakula na nafaka zaidi wakati watu wetu wanakufa njaa tutashangaa?

  Lakini swali la msingi ambalo nalipendekeza kwenu ni KWANINI BADO TUNA TATIZO LA UPUNGUFU WA CHAKULA NCHINI, KITU AMBACHO NYERERE ALIONEKANA AMESHINDWA NA KUBEZWA NA KUBEBESHWA LAWAMA? Kwanini mtazamo huo wa upungufu wa chakula wakati wa Mwalimu hauonekani wakati huu? au hadi kitokee nini?
   
 2. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #2
  Jul 5, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,999
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  handeni pia kulikuwa na njaa kali sana mwaka jana, tena binadamu walikuwa wanagombania maji na mifugo, bado njaa ipo sana tu, tatizo serikali inaogopa kusema ukweli, ajabu maghala yaliyojengwa enzi za nyerere kukiwa na idadi ndogo ya watu ndo hayo hayo hadi leo.
   
 3. Sn2139

  Sn2139 JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 827
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  M/Kijiji, swali lako hapo chini jibu lake ni rahisi mbona?
  Upungufu wa chakula unaoendelea kuonekana nchini kwetu unasababishwa na utawala wa kwanza wa Mwl. Nyerere. Huyo ndio anayesababisha shida zote zikiwemo njaa na umasikini wetu
   
 4. Sn2139

  Sn2139 JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 827
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kama M/Kijiji anazeeka kwa umri wewe umezeekea kwenye iakili zako.

  Wengi tulikula yanga na mimi ni mmoja wapo wa waliokula yanga ya Nyerere, nilipiga foleni kwenye maduka ya kaya, kama wengine, lakini kulikuwa na assurence kubwa kuwa serikali ina uwezo wa kutosha kusaidia watu wake wasife na njaa. Sasa hivi ni maneno tu, "hakuna mtu atakae kufa na njaa" lakini watu wanakufa kweli huko vijijini. Hata huko Zanzibar kwenu hali ni mbaya sehemu yote ya Micheweni na sehemu zingine jirani.

  Mimi nakupongeza kwa kufanya kazi ya kustarehesha watu na vituko vyako, lakini tukija kwenye ukweli jasho litakutoka ukitaka kuosha nguruwe walio karibu na matope. Endelea kuosha nguruwe zako, huenda ujira unaopewa utakusaidia kununua sembe watoto wako na wazazi wako wapate mlo wa siku. Najua unashinda hapa JF kwasababu huna kazi nyingine, shamba huna na kazi huna zaidi ya hii uliyotumwa kuifanya hapa JF
   
 5. W

  WildCard JF-Expert Member

  #5
  Jul 5, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Watawala wetu wa sasa NCHI ni Dar Es Salaam tu na pengine Bunge linapokuwa Dodoma. Ziara za viongozi wetu mikoani sio kuangalia hali halisi za Watanzania zilivyo. Hakuna kiongozi anayethubutu kulala kijijini sasa hivi. Mwalimu alilala vijijini. Alikuwa akiongea na watu wa kawaida kabisa vijijini. Aliijua nchi sio kupitia kwa wapambe wake tu. Mazingira vijijini sasa hivi yameharibika mno. Mkaa umemaliza misitu yote ya mvua. mito na vijito vyote vimekauka. Njaa tunayo tu kila mwaka kama tatizo la umeme lilivyo sasa mijini.
  Ukimaliza njaa utakuwa umemaliza utegemezi wa watu wetu kwa serikali. Watu wakijitegemea CCM itapata taabu.
   
 6. Makame

  Makame JF-Expert Member

  #6
  Jul 5, 2011
  Joined: Jan 3, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NI HIVI:-

  1. NYERERE ALIKUWA NA MAPUNGUFU NA ALITUWEKA KWENYE UJAMAA, JAMBO AMBALO LIMEATHIRI USHINDANI WETU, HASA KWENYE HUDUMA. NENDA BAR AU HOTELI, WANAJIVUTAVUTA NA KUSUASUA; YOTE HIYO NI BAKAA ZA MFUMO SHINDWA WA SAINT JKN.

  2. Mpaka leo tumeshindwa kuji - adjust to the pace of watani wetu wa jadi kwa kuwa hatujaweza kuwa na ushindani.

  3. MATATIZO YA LEO; UMEME WA DHARURA, CHAKULA, MIUNDOMBINU DUNI, na huduma nyengine za jamii, tusimtwishe NYERERE; kweli alituwacha pabaya; lakini tumuangalie Kagame tiu hapo Rwanda anachofanya. Labda ni hii demokrasia ndio tatizo; mara watu wanagoma; mara wanachoma mali na kuunguza magari; nisaidieni hapo wana jamii
   
 7. S

  Stephen Buloya Verified User

  #7
  Jul 5, 2011
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Namkumbuka mwalimu wangu wa historia, Mwalimu Libaba, alivyo kuwa ana laani kitendo cha Nyerere kunyanganya ardhi wakulima wakubwa na kuviingilia kiutendaji vyama vya ushirika, ambavyo miaka ile vilikuwa vyama vikubwa barani Afrika. Vyama vililazimishwa kuwa na viongozi ambao ni makada wa chama. Unjaua ili kilimo kiwe na tija, ni lazima kifanywe kibiashara. Kilimo si kazii rahisi, na ili mkulima ashawishike kulima, ni lazima awe na matarajio ya kupata faida. Ili kilimo kiwe na faida lazima kuwepo na miundombinu kuwezesha uzalishaji. Kuna mtafiti mmoja wa sokoine alisha wahi aandika makala kwenye gazeti la raia mwema kuhusu namna ya kuwezesha kilimo kiweze kuwa na faida, kiasi cha kuweza kushawishi wananchi wawekeze rasilimali zao kuzalisha bidhaa za kilimo, hasa mazao ya chakula. Tatizo la kilimo nchini ni tatizo la uzalishaji, hatuzalishi chakula cha kutosha. Hata sehemu moja ya nchi ikizalisha ziada, kwa mfano huko Rukwa, miundombinu ya kuhifadhi, kusafirisha na kusambaza nchini hakuna. Nadhani ni mwaka jana tu chakula kilioza shambani kule Rukwa, kwa sababu serikali haikutoa pesa kwa SGR kununua mahindi, halafu barabara kutoka huko kwenda mikoa jirani zilikuwa mbovu. On top of that wakulima wakanyimwa vibali vya kuuza mahindi nchi ya jirani. Mpaka leo serikali ina ingilia sekta ya kilimo, kwa namna ambayo ina mkandamiza mkulima. Matokeo yake ni kwamba watu wana aacha kulima mazao ya chakula kama mahindi, na kuanza kufanya shughuli nyingine, kama kuchoma mkaa.

  Bila kuwekeza kwenye miundombinu ya vijijini na kutunga, pamoja na kutekeleza sera ambazo zita chochoea watu wawekeze rasilimali nyingi zaidi kwenye kilimo, njaa haitakwisha.
   
 8. Makame

  Makame JF-Expert Member

  #8
  Jul 5, 2011
  Joined: Jan 3, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  SAFI SANA GURU, Hapo tuko pamoja. Nyerere ana mapungufu yake, ingawa alishamaliza Urais. Kwa sababu aliendelea kuingilia utendaji wa Serikali hadi 1999 alipostaafu dunia. lakini hawa viongozi wengine wana mapungufu yao kwa kushindwa kusimamia dhamana zao.

  Hivi kweli, sisi ile Rada tuliihitaji?

  Tungejenga madaraja na barabara ngapi kwa hela ile?

  We need to know our priorities and act.

   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Jul 5, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Nyerere kaondoka miaka zaidi ya 25 iliyopita, leo kwanini wameshindwa kufanya mabadiliko. Leo hii mashamba mangapi makubwa yako mikononi mwa wafanyabiashara wakubwa? Mbona kwenye simu wameweza kuwekeza kwa kiasi kikubwa na kugombania hadi kugombana, kwenye chakula vipi?
   
 10. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #10
  Jul 5, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  We need a 'KAGAME' to get things going!
   
 11. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #11
  Jul 5, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,999
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  chakula hakilipi km madini, na huu ndo upofu wa viongozi wengi wa kiafrika, uchumi upo kwenye minerals, pesa pesa pesa, pesa imepofusha watu, kweli uwekezaji ktk mazo ya chakula ni muhimu sna, hapo kinachohitajika ni sera tu, sera ya kuwapa ruzuku wakulima wa mazao ya chakula na kuwahakikishia soko kabla walanguzi hawajawarubuni.
   
 12. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #12
  Jul 5, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Yes shirika la chakula duninia limeshatagaza alert ya hali ya kutihs hhuko ETHIOPIA na SOMALIA. Kuna watu wameshakufa njaa. Chanzo ukame.

  Kwa tanzania ni just a mattertr of time kusikia pia wanyama na watu wanakufa njaa kwani Alert waliyotoa TANESCO ya mabwawa kutokuwa na maji ni uthibitisho tosha kwamba wanasiasa wanasubiri deadline kuanza kuwa wawazi kuhuus hali ya chakula.

  Tungekuwa tunawatendea haki wakulima basi tungeruhusu wauze mazao yao Huko kwenye kambi a wakimbizi kenya kwani bei watayolipwa ni nzuri. Lakini kwa kuwa wakulima hawana mtetezi mhhhhh politician kama awada nikupiga marufuku uuzaji wa mazao nje ya nchi.

  Naishauri serikali siku ikipiga marufuku officially wakulima kuuza mazao nje ya nchi itoe ruzuku ya kwa kila kilo hata kama ni shilingi 10.
   
 13. F

  FJM JF-Expert Member

  #13
  Jul 5, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwa nini watu wa hiki 'kijisehemu' cha micheweni wana njaa?
  Malaria Sugu ili argument ya kwamba wakati wa Nyerere watu walikufaa njaa, inabidi kusiwepo na habari za kufa njaa kwa sasa. Yaani kusiwepi na hata 'mtu mmoja' mahala popote ndani ya mipaka ya Tanzania anayekufa kwa sababu ya njaa.
   
 14. S

  Stephen Buloya Verified User

  #14
  Jul 5, 2011
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  "Nyerere kaondoka miaka zaidi ya 25 iliyopita, leo kwanini wameshindwa kufanya mabadiliko. Leo hii mashamba mangapi makubwa yako mikononi mwa wafanyabiashara wakubwa? Mbona kwenye simu wameweza kuwekeza kwa kiasi kikubwa na kugombania hadi kugombana, kwenye chakula vipi?"


  Nyerere ameondoka, lakini utamaduni kwa kutatua matatizo kisiasa bado umejikita kwenye mfumo mzima wa uendeshaji wa serikali. Kufa wa ushirika, athari zake ni kubwa mno, kwa sababu sasa mkulima hana mtetezi mwenye "clout" ya kuweza kuinfluence political decisions in their favor. Katika mfumo ambao maamuzi ya kisiasa yana nguvu kuliko yale ya kitalaamu, the ordinary farmer is losing out. Lakini tatizo la msingi liko kwenye miundo mbinu vijijini, ambao itaweza kufungua fursa za uwekezaji huko, ili wananchi wenyewe waweze kuvutiwa kuweza zaidi kwenye kilimo. Lakini ngoja nimalizie kwa kusema kilimo ni complex problem. Sekta hii inafaa wana siasa waachia watalaamu wetu wa kilimo watafiti matatizo, walewe matatizo na waje na suluhisho mbali mbali kutatua matatizo, na kuzitekeleza. Agriculture is 95% knowledge, 5% work......huu ni msemo wa kiIsraeli sina hakika kama ni sahihi. Na matatizo kwenye kilimo ni sawa na matatizo kwenye sekta mbali mbali. Profit margins in the telecommunications sector are way higher than in the agricultural sector, and there are less risks in telecommunications, that is probably why investment in telecommunications is higher than in agriculture.
   
 15. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #15
  Jul 5, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,682
  Likes Received: 637
  Trophy Points: 280
  Kwanini serikali iliuza mashamba ya NAFCO badala ya kuanzisha mengine? Kilimo cha mazao ya chakula huwa ni kilimo kisicho na faida,mara nyingi wakulima huwa subsidized na serikali zao ili walime vyakula,na serikali nyingi huwa zina discourage export ya vyakula......we had government owned farms,instead of expanding them we sold them.....privatisation is a b**ch!!
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Jul 5, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  NAFCO,? Kobello mbona unataka ugomvi? Sasa WM Pinda ametudokeza kuwa tunaini letu ni wawekezaji wakubwa.
   
 17. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #17
  Jul 5, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,682
  Likes Received: 637
  Trophy Points: 280
 18. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #18
  Jul 5, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mi kinachonisiitisha zaidi ni pale tunaposema soko huru lakini wakulima hawarusiwi kuuza mazao yao nje kuzuzia njaa ya watanzania. Hili kundi la wakulima ni kundi linalonyayasika sana Tanzania. Alfu tunasema kilimo kwanza na hawapewi ruzuku..... Mikopo yenywe shida sababu hawana asset

  Tasisi kama JKT zingekuwa na Tija zaidi kamazingekuwa na mshamba makubw ya mifano mikoani na wilayani. Inawezeaanguvu zote ziko kwenye kuzalisha magari ya nyumbu......
   
 19. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #19
  Jul 5, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  UK katika protocol za cabinet na hta mishahara yao inaendaba na umuhimu wa kisekta
  • UK ni - PM, Chancellor of exchquer, Wazii wa ulinzi( i guess) na mambo ya nje etc

  Sasa Tujiulize Tanzania NI Wizara gani muhimu sana ? Tuzipange kwa mpangilio?
  • Ulinzi, Mambo ya nje, Wizara ya fedha...........( Am i right?)
  Wizara ya kilimo machoni pa wanasiasa wengi ni kama kukomolewa. Tunaona hata mtu alifanya kazi wizara ya mambo ya nje ndio anafaaa kuwa rais( May be uzoefu wa kuomba misaada)

  Mwanakiji swali lako gumu ila moja ya vikwazo vya mwalimu ilikuwa ni profeesional man power. Lakini Leo hii wataalamu wote wa SUA sijui wanaishia wapi? Kama tunavyombebesha lawama mwalimu kwa kuleta njaa wakati kukiwa na wataalamu wa kilimo wachache basi kwa sasa inabidi iwe zaidi ya Lawama.

  Otheriwse labda tumbiwe Kilimo kwanza ini kwa ajili ya mazao ya mibuni, mikorosho na minazi amabyo inachukuwa miaka kuanza kuzalisha.
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Jul 6, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Leo hii tuna wataalamu wengi, tuna taasisi kadha wa kadha za "kilimo" au watu wameshasahu "Uyole" au "Ukiliguru".. Watu wametudokeza sababu ya kwanini kuna tatizo la upungufu wa nishati na maelezo elfu moja na moja, lakini kwanini kuna tatizo la upungufu wa chakula?
   
Loading...